Tamasha la kutuza washindi wa AFRIMMA

Washindi wa mwaka huu wa tuzo za “Africa Muzik Magazine Awards, AFRIMMA” watatuzwa jumapili tarehe 15 mwezi huu wa Novemba mwaka 2020.

Tofauti na maonyesho ya awali ya tuzo hizo, mwaka huu onyesho litapeperushwa kupitia mitandao ya kijamii.

Kwa kawaida wanamuziki walioteuliwa kuwania tuzo katika vitengo mbali mbali husafiri hadi marekani ambapo wanajumuika kwa tamasha.

Mwaka huu mambo ni tofauti kidogo kutokana na janga la ulimwengu mzima la virusi vya Corona. Wawaniaji wa mwaka huu wa 2020 walitangazwa mwanzo wa mwezi Septemba mwaka huu wa 2020.

Wanamuziki kadhaa wamethibitisha kwamba watatumbuiza kwenye onyesho hilo ambalo litapeperushwa kupitia mtandao wa “You Tube” kwenye akaunti ya “AFRICANMUZIKMAG”.
Mwanamuziki wa Kenya Nadia Mukami na Fally Ipupa wa Congo ni kati ya wale ambao watatumbuiza kwenye tamasha hilo litakaloanza zaa tatu usiku saa za Afrika mashariki.

Wakenya wengi wameteuliwa kuwania tuzo kadhaa za AFRIMMA kama vile Jamal Gaddafi ambaye anawania tuzo la mtangazaji bora wa redio na televisheni, Sauti Sol na wimbo wao Suzana ambao unawania video bora ya mwaka, DJ Fully Focus na Dj Shinski wanaoishi Marekani ambao wanawania tuzo la Dj bora wa Africa nchini Marekani, Dj Moh Spice anawania tuzo la Dj bora wa Africa, Enos Olik anawania tuzo la mwelekezi bora wa video, Khaligraph Jones anawania tuzo ya mwanamuziki bora wa rap kitengo cha wanaume kati ya wengine.

Shughuli ya kupiga kura inaendelea.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *