Categories
Burudani

Zari atetea mwanawe huku akitetewa na Mange Kimambi

Mwanamitindo na mfanyibiashara mzaliwa wa Uganda anayeishi Afrika Kusini Zari Hassan ametetea mtoto wake kujitokeza na kutangaza kwamba yeye ni shoga.

Mvulana huyo kwa jina Raphael Ssemwanga Junior, aliingia Instagram mubashara jumatano usiku na kupasua mbarika.

Alhamisi mambo yalipochacha kwenye mitandao, Zari alijibu mmoja wa mashabiki kwamba Raphael alifanya vile ili kufukuza wanawake ambao wamekuwa wakimwandama kwenye mitandao.

Zari alisema hata wanawake ambao wanamzidi umri walikuwa wakimfuata mvulana huyo kimapenzi huku wengine wakitaka hela. Kulingana naye, Raphael tayari ana mpenzi wa kike.

Raphael ndiye mtoto wa pili, kati ya watoto watatu wa Zari na marehemu Ivan Ssemwanga na ana wengine wawili wadogo na mwanamuziki wa Tanzania Diamond Platnumz.

Kuhusiana na swala hili la mwanawe kujitangaza kuwa shoga, adui yake mitandaoni Mange Kimambi ameamua kusimama naye.

Mange ni mwanaharakati wa nchi ya Tanzania lakini kwa sasa anaishi Marekani na yeye na Zari huwa hawapatani kwenye mitandao ya kijamii.

Lakini kwa hili amemtetea Zari akimsihi apende mtoto wake hata baada yake kujitokeza kuwa shoga. Kwenye akaunti yake ya Instagram Mange aliweka picha ya kina mama wazungu wenye mabango ya kuonyesha upendo kwa wanao ambao ni mashoga, kisha akaandika,

“Huenda huu ndio wakati pekee nitamtetea Zari. Zari love your son, not just love him but be proud of him, accept him. Huyo mtoto mpaka kuingia live kujitangaza it means anatafuta acceptance ambayo haipati nyumbani so anatafuta acceptance kwa strangers. Muonyeshe acceptance, mkubali, tena mpende kuliko ulivyokuwa unampenda mwanzo. He needs you now more than ever. Na kaamua kufanya hivyo ili akufosi wewe kumkubali. Ile live was about getting your attention.

.
.
Naongea kama mama wa watoto wawili wa kiume, bado ni wadogo sana kiasi cha kwamba bado sijajua watakuwaje huko mbeleni, only thing I know ni kwamba nitawakubali na nitawapenda no matter what, I will be a proud mom. Mungu pushilia mbali niliendie vijana wangu ila kama wakiwa gay mimi ni yule mama ambae nitaandamana barabarani kupigania haki za magay ili mwanangu aishi kwa amani. Mimi ni yule mama wa kutembea kifua mbele tena ntaua mtu atakae mbully mwanangu, yani ntamlinda mpaka ndugu zake wadhani nampenda yeye zaidi ila ni vile yeye atanihitaji zaidi ya wenzie.
.
.
Hakuna mwanamke aliezaa mtoto wa kiume akataka awe gay ila ndo ishatokea, hakuna la kufanya zaidi ya kuwa mama. Zari weka ustaa pembeni, mkumbatie mtoto huyo, muhakikishie mapenzi yako na ya familia nzima la sivyo UTAMPOTEZA. Na umdefend against anyone. Fight for him and stop denying his truth. Yeye amepata nguvu ya kujitangaza wewe unakataa, unamuonyesha picha gani? Hii sio mara ya kwanza, yule gay wa Mombasa tena famous nimemsahau jina na hata nikilikumbuka siliandiki alishawahi kuposti dm zake na mwanao mwaka jana, DM zilikuwa graphic mnooo ila nilipotezea ile story sababu nna watoto wa kiume nikaogopa karma.
.
.
Zari stop worrying about what people think and just accept your son and be proud of him, I know its hard but that’s what being a mother is about.
.
.
Na nyie mnaomposti huyo mtoto kumbukeni he is a minor, hana hata miaka 18, mngekuwa nchi zingine mngefungwa. Kueni na roho za ubinadamu, hili jambo ni zito mnooo kwa mzazi, halibebeki, haswa haswa kwa mzazi wa kiafrica anaeishi Africa. Kama kuna mtihani Zari kawahi kupitia huu utakuwa ndo mtihani mkubwa kuliko.”

Categories
Burudani

“Nashukuru Mungu kwa kunipa mzazi mwenza kama Zari” Diamond

Mwanamuziki wa Tanzania Diamond Platnumz au ukipenda Simba au Chibu Dangote amemsifia sana mzazi mwenza kwa jina Zari Hassan.

Akizungumza jana katika kituo cha redio cha Wasafi Fm kwenye kipindi cha ‘The Switch’, mmiliki huyo wa Wasafi Media alifichua kwamba hana uhusiano wa kimapenzi na Zari mzaliwa wa Uganda anayeishi na kufanya biashara nchini Afrika Kusini.

Diamond alikuwa amekwenda kituoni humo jana kwa ajili ya kuzindua kibao walichoshirikiana na Koffi Olomide.

Alisema wanasaidiana tu katika malezi ya wanao wawili na alikuwa amekuja kumletea watoto kwani hakuwa ameonana nao kwa muda wa miaka miwili.

“Miongoni mwa watu ama wazazi wenzangu ambao ninaweza nikawasifia, yaani nasifia katika namna tunajua namna gani ya kuishi kama wazazi ni Zari.” ndiyo baadhi ya maneno aliyasema Diamond.

Alisema pia kwamba anafarijika kuona kwamba watoto wake wana mama kama Zari na alibahatika kuzaa naye na anashukuru Mungu.

Kuhusu wanawe kulelewa na baba mwingine Diamond alisema hakuna tatizo bora aruhusiwe kutagusana na watoto wake anavyotaka.

Wanawe wakiwa nchini Tanzania, Diamond alipata fursa ya kurekodi kibao na mtoto wake wa kike Tiffah na amesema kibao chenyewe kitazinduliwa kabla ya mwisho wa mwaka.

Zari anasemekana kuwa ana mahusiano mengine ya mapenzi naye Diamond akasema bado yuko peke yake hajapata mpenzi.

Sifa alizomimina Diamond kwa Zari zinafanya wanawake wengine ambao ana watoto nao kuonekana vibaya sana. Bwana huyo ana mtoto wa kiume na mwanamitindo wa Tanzania Hamisa Mobeto na mwingine wa kiume na mwanamuziki wa Kenya Tanasha Donna.

Categories
Burudani

Zari Hassan asuta kakake Diamond

Mwanamitindo Zari Hassan, mzaliwa wa Uganda anayeishi na kufanya biashara nchini Afrika kusini amegadhabishwa na matamshi ya kaka wa kambo wa Diamond Platinumz kwa jina Ricardo Momo. 

Ricardo alihojiwa na hapo ndipo alimwaga mtama kuhusu mahusiano ya Zari na Diamond Platinumz. Kulingana naye, Zari ndiye alianza kumnyemelea Diamond kwa kutaka kufurahia mali yake na umaarufu. 

Lakini Zari anakana hayo akisema kwamba Ricardo anafaa kufanya utafiti kabla ya kusema mambo kwani sio ukweli anaonelea kuwa kaka huyo wa Diamond anatafuta ufuasi kwenye mitandao ya kijamii kwa kutumia jina lake. 

Hata hivyo Zari amekiri kwamba yeye ndiye kwanza alimpigia Diamond simu akitaka huduma zake kama mwanamuziki kwenye sherehe ambayo alikuwa ameandaa, Diamond akamwelekeza kwa meneja wake na ikatokea kwamba hangeweza kuhudhuria na kutumbuiza kwenye sherehe ya Zari kwani alikuwa na kazi kipindi hicho chote.

Baada ya hapo, Zari anasema walikutana tena kwenye ndege wakisafiri na hapo ndipo walibadilishana nambari za simu na Diamond akawa ndiye mwenye kuwasiliana na Zari kwa sana kwa kutuma jumbe kila mara. Mwanadada huyo anasema alikuwa na pesa hata kabla ya kukutana na Diamond. 

Zari na Diamond walikuwa kwenye uhusiano wa kimapenzi ambao una matunda ambayo ni watoto wawili, wa kike Tiffah na wa kiume Nillan.

Walitengana baada ya kile kinachosemekana kuwa uzinzi kwa upande wa Diamond.

Alipohojiwa yapata mwaka mmoja uliopita, Diamond alikiri kwamba yeye ndiye alikuwa na makosa mengi kwenye uhusiano wake na Zari.

Zari pia anakoseshwa kwa kuwa kwenye uhusiano wa kimapenzi na Peter Okoye mwanamuziki wa Nigeria na mwalimu wake wa mazoezi wakati akiwa kwenye uhusiano na Diamond.

Categories
Burudani

Diamond Platinumz kuzuru Kenya

Msanii wa nchi ya Tanzania Diamond Platinumz au ukipenda Chibu Dangote au Simba anatarajiwa kutua nchini Kenya hii leo kwa kile ambacho kinasemekana kuwa ziara ya mapumziko.

Ama kweli miezi michache ambayo imepita imekuwa ya kazi nyingi kwa msanii huyo kiasi cha kwamba sasa anahitaji mapumziko.

Mwezi Septemba alikuwa anajihusisha na kazi ya kutoa muziki na Bi. Zuchu ambaye alikuwa amejiunga na kampuni ya WCB anayomiliki Diamond. Wawili hao walitoa nyimbo kama vile ‘Cheche’ na ‘litawachoma’ ambazo zilizua minong’ono chungu nzima kwenye mitandao ya kijamii.

Swali ambalo wengi walikuwa wanajiuliza ni la uhusiano kati ya wawili hao kwa jinsi walicheza kwenye video za nyimbo na kuandamana karibu kila sehemu.

Baada ya hapo Diamond na wanamuziki wengine wa WCB waliingilia Kampeni ambapo walikuwa wakikipigia debe chama cha CCM na hasa Rais John Pombe Magufuli.

Uchaguzi ulipokamilika alifanya tamasha nchini Sudan Kusini na nchini Malawi. Aliporejea nyumbani Tanzania alitembelewa na mpenzi wake wa zamani Zari Hassan na watoto wao Tiffah na Nillan. Hakuwa ameonana na watoto hao kwa muda wa miaka miwili.

Na sasa ametangaza likizo yake nchini Kenya ila wengi wanaonelea kwamba anakuja kuona mtoto wake na mwanamuziki wa Kenya Tanasha Donna ambaye ni somo wake kwa jina Naseeb Junior.

Ukurasa wa Facebook kwa jina ‘Wasafi News’ unaoaminika kuwa wa Wasafi Media kampuni inayomilikiwa na Diamond Platimumz ndio umetangaza ziara yake ya Kenya na kupachika picha ya awali ya Diamond na Tanasha.