Matokeo ya uchunguzi wa Benki ya Dunia yaliotolewa Jumatatu yanaiorodesha nchi hii kuwa ya tatu maskini zaidi miongoni mwa mataifa yenye mapato ya kadiri kote ulimwenguni.
Ripoti hiyo Ripoti hiyo ya Benki ya Dunia kuhusu Ujumuishaji wa Uchumi inaonyesha kuwa zaidi ya asili-mia 40 ya Wakenya kwa sasa wanaishi katika ufukara uliokithiri.
Kiwango cha umaskini ni takriban mara 10 zaidi kuliko nchini Pakistan na Misri ambazo pia zinaorodeshwa chumi za pato la kadiri zilizoko kwenye daraja la chini.
Zambia ni masikini zaidi huku asilimia 61 ya raia wake wakiishi katika ufukara ikifuatiwa na Nigeria kwa asilimia 58 huku Côte d’Ivoire ikiwa ya nne kwa asilimia 30.
Zimbabwe ina kiwango cha chini cha umaskini wa asilimia 23 lakini ina idadi kubwa ya umaskini huku karibu asilimia 80 ya idadi ya watu wake wakiwa maskini.
Matatizo ya kiuchumi na ya kijamii yanayosababishwa na janga la Covid-19 yameathiri harakati za kupunguza umaskini humu nchini