Categories
Burudani

Sukari, Zuchu

Zuchu mwanamuziki anayeangaziwa zaidi katika kampuni ya WCB nchini Tanzania ana kibao kipya kwa jina “Sukari” ambacho alikiachia rasmi kwenye You Tube tarehe 20 mwezi Januari mwaka 2021.

Wimbo huo ulikuwa umesubiriwa kwa hamu na ghamu kutokana na namna alikuwa amefanya matayarisho ya ujio wake kwenye mitandao ya kijamii hasa Instagram.

Alitafuta usaidizi wa watu kadhaa maarufu nchini Tanzania ambao wana umuhimu kwenye jamii kwa jumla ambao walirekodi video fupi kuhusu wasifu wao na mwisho wote wanamalizia kujirejelea kama sukari.

Mamake mzazi ambaye pia ni msanii kwa jina Khadija Omar Kopa ni kati ya waliosaidia kutangaza ujio wa kibao hicho cha Sukari. Kwenye video yake, Khadija anasifia burudani yake ambayo anasema ikosekanapo watu hutaharuki na watu huwa tayari kuigharamia wakati wowote. Onyesho zuri la usaidizi wa mama kwa mwanawe hasa katika kuendeleza talanta.

Mwingine kati ya watu hao mashuhuri ni muigizaji Wema Sepetu ambaye alisema kwamba urembo wake ndio ulimjengea jukwaa analosimamia kwa sasa tangu mwaka 2006 baada ya kushinda shindano la ulimbwende wakati huo na kutawazwa “Miss Tanzania”.

Aligusia pia kipaji chake cha uigizaji ambacho anasema ni cha hali ya juu zaidi na kwamba yeye ni sukari.

Kabla ya kuachilia kibao hicho, Zuchu naye alitoa video akisema kwamba anaamini kila mwanadamu ana umuhimu wake katika jamii. Umuhimu huo ndio anafananisha na ladha ya sukari huku akijirejelea kama sukari ya Zanzibar alikozaliwa.

Zuchu alikwenda kuhojiwa katika kituo cha redio cha Wasafi Fm katika kipindi cha jioni kwa jina Mgahawa ambapo alionyesha waliokuwepo jinsi ya kuuchezea wimbo huo.

Ikumbukwe kwamba alipoingia WCB alimhusisha mkubwa wake Diamond kwenye nyimbo kadhaa ambazo zilisababisha minong’ono kwamba wana uhusiano wa kimapenzi.

Walikuwa wakiandamana kwenye maonyesho kadhaa lakini zamu hii Zuchu alikuwa peke yake alipokwenda kuhojiwa. Alisema Diamond alimpa ahadi ya kumshika mkono alipokuwa akianza lakini pia alimwambia kwamba kuna wakati atamwachilia afanye kazi peke yake.

Kama ilivyo mazoea nchini Tanzania, wengi wamerekodi video wakichezea wimbo huo mpya wa Zuchu kwa jina sukari na amechapisha hizo video kwenye akaunti yake ya Instagram.

Categories
Burudani

Nilidhani nitakufa, Wema Sepetu

Mwanamitindo na muigizaji maarufu nchini Tanzania Bi. Wema Sepetu amezungumzia maradhi aliyougua kwa mara ya kwanza kabisa kwenye mahojiano na gazeti moja nchini Tanzania.

Wema ambaye pia hujiita “The Tanzanian Sweetheart” alifichua kwamba amekuwa akiugua homa ya mapafu au ukipenda “Pneumonia” ambayo ilisababisha kifua chake kijae na ikawa vigumu kwake kupumua.

Alisema kwa wakati mmoja alikuwa na maumivu makali mpaka akadhani kwamba ni kifo kinamjia. Wema ambaye anaendelea kupona anasema akipona kabisa atasema dua kwa mwenyezi Mungu kumshukuru kwa kulinda maisha yake.

Afya ya muigizaji huyo ambaye kwa wakati mmoja alikuwa mpenzi wa Diamond Platnumz imekuwa ikitiliwa shaka na mashabiki wake ndani na nje ya Tanzania hasa baada yake kupunguza kwa kiasi kikubwa uzani wa mwili.

Ombi lake kwa mashabiki wake kwa sasa ni kwamba waendelee kumwombea ili apone kabisa kwani ugonjwa huo wake huwa unajirudia mara kwa mara.

Anaonekana kujikaza sana maanake kupitia Instagram, ametangaza kwamba amechapisha kipindi kipya cha upishi kwenye “App” yake kwa jina ‘Wema App’.

Sio siri kwamba binti huyo ambaye wakati mmoja alishinda shindano la ulimbwende na kuiwakilisha Tanzania kama “Miss Tanzania” amekuwa akitaka sana kupata mtoto lakini tatizo la afya ambalo hakufichua limemzuia.

Maajuzi amezua minong’ono kwenye mitandao ya kijamii baada ya kununua mbwa wa rangi nyeupe akampa jina, “Vanilla Nunu” na akamfungulia akaunti ya Instagram ambayo kufikia sasa ina wafuasi zaidi ya elfu 12.

Maelezo kwenye akaunti ya Vanilla Nunu yanasema, “Mimi ndiye mbwa mwenye raha kabisa unayemjua. Mamangu ni mpenzi wa Tanzania Wema Sepetu. Karibu kwa ulimwengu wangu. Na ndio mimi nimeharibiwa sana angalau hilo ndilo mamangu hunifanyia.”

Categories
Burudani

Nandy akiri kuandikiwa wimbo

Mwanadada Nandy ana kibao kipya kwa jina “Nibakishie” ambacho amemshirikisha Ali Kiba ambaye amekuwa kwenye ulingo wa muziki nchini Tanzania kwa muda mrefu.

Wimbo huo ni wa mapenzi na wawili hao wanaonyeshana mapenzi kwenye video ya wimbo wao mpya ambayo ni ya uzuri wa hali ya juu.

Wawili hao kwanza walizindua sauti ya wimbo pekee kwenye majukwaa kadhaa ya muziki mitandaoni ambapo ulisikilizwa kwa wingi na baadaye wakaweka video yake kwenye youtube ambapo pia kufikia sasa umetazamwa zaidi ya mara laki sita.

Binti huyo ambaye pia hujiita “The African Princess” amemshukuru mwanamuziki na mwandishi wa nyimbo kwa jina “Kusah” kwa kumwandikia wimbo huo. Kulingana naye, wimbo huo umemletea mafanikio mengi hadi sasa.

Alisema hakuna ubaya kwa mwanamuziki aliyeendelea kuandikiwa nyimbo kwani waandishi wa nyimbo pia wanahitaji kupata riziki.

Aliwaalika waandishi wengine wa nyimbo ambao wana kazi ambazo wanaonelea zitamfaa kwamba yuko tayari kwa biashara. Haijulikani kama Kusah aliandika maneno yote ya wimbo huo hata sehemu ambayo inaimbwa na Ali kiba.

Nandy amekuwa pia akionyesha picha za matukio wakati wakirekodi video ya wimbo huo na kwa wakati mmoja anakaribia kulia kwa woga kwamba angezama majini kwenye kidimbwo kimoja ambapo walikuwa.

Wanamuziki wenza wamempongeza kwa kazi hiyo huku wakimtania kama vile Ommy Dimpoz ambaye aliweka sehemu ya video ya wimbo huo kwenye Instagram na kuandika,

“Sema Hakuna mtu Mvumilivu na Mwenye Moyo Wa Chuma Kama billnass. Ndo Maisha kaka uzuri ulikuwepo location. Anyway tuendelee kuenjoy mziki mzuri kutoka kwa officialalikiba na officialnandy. Nibakishie. link on their bio”

Alikuwa akimtania mpenzi wa Nandy kwa jina Billnass ambaye pia ni mwanamuziki. Wema Sepetu ambaye ni muigizaji aliandika, “yaani nyie mngekuwa wapenzi, nasema tu.” kwenye picha ya Nandy na Ali Kiba.

Categories
Burudani

Walinitishia maisha! Van Vicker

Muigizaji mzaliwa wa nchi ya Ghana Van Vicker amefunguka kuhusu ushindani ulioko katika sekta ya filamu nchini Nigeria almaarufu Nollywood.

Wengi walipata kumfahamu Vicker kutokana na filamu alizoigiza za Nigeria wasijue yeye ni mzaliwa wa Ghana na sio Nigeria.

Akizungumza maajuzi katika kipindi kimoja cha mahojiano nchini Ghana, Vicker alifichua kwamba kuna wakati waigizaji nyota wa kiume nchini Nigeria walimtishia maisha.

Kisa na maana alikuwa anapata kazi nyingi za uigizaji nchini Nigeria na kuwa mhusika mkuu jambo ambalo hawakufurahia.

“Unajua mtayarishaji filamu akikuangazia inakuwa kwamba ni wewe tu kila mara. Na ikiwa ni wewe basi yule mwingine anakosa.” Alisema Van.

Joseph Van Vicker alizaliwa tarehe mosi mwezi Agosti mwaka 1977, mamake ana asili ya Ghana na Liberia na babake ni mjerumani na aliaga dunia Van akiwa na umri wa miaka sita tu. Van ana mke kwa jina “Adjoa” na walifunga ndoa mwaka 2003 na wana watoto watatu.

Anampenda sana mamake na kwake yeye ndiye shujaa wa maisha yake. Alianza na utangazaji katika vituo mbali mbali vya redio nchini Ghana kabla ya kuingilia utangazaji wa Televisheni na baadaye uigizaji.

Muigizaji huyo hakutaja majina ya waigizaji maarufu wa Nigeria ambao walimtishia maisha kwa kuchukua nafasi zao za kazi.

Mwaka 2014 Van Vicker aliigiza kwenye filamu kwa jina ‘Day After Death’ na muigizaji wa nchi ya Tanzania Wema Sepetu.

Wema Sepetu na Van Vicker
Categories
Burudani

Happy Birthday Wema Sepetu!

Ni siku ya kuzaliwa ya muigizaji, mwanamitindo na mfanyibiashara wa nchi ya Tanzania Bi. Wema Sepetu. Kupitia akaunti yake ya instagram hii leo kidogo amewachezea mashabiki wake pale alipodanganya kuhusu mwaka wake wa kuzaliwa.

Wema ameachia picha yake nzuri na maneno,

” 30 years old Queen … I promised to say the truth on my exact day … September 28th 1990, i was delivered from the womb of Mariam Athmann Sumbe … I am happy am i’m celebtaring 30 years of my life …”

Yaani ” Malkia wa miaka 30 … Niliahidi kusema tarehe kamili …Septemba tarehe 28 mwaka 1990, siku nilizaliwa toka kwa tumbo la Mariam Athmann Sumbe … Nafurahia kusherehekea miaka 30 ya maisha.”

Baada ya hapo ameacha nafasi kidogo na kuongeza maneno, ” Sorry I lied” kwa kiswahili “Pole nilidanganya.”

 

Ukweli ni kwamba Wema Sepetu alizaliwa mwaka 1988 tarehe kama ya leo hivyo ana miaka 32.

Alipata kujulikana sana nchini Tanzania na nje ya nchi hiyo baada ya kushiriki shindano la mwanamke mrembo zaidi nchini Tanzania mwaka 2006 akaibuka mshindi na akawakilisha taifa hilo kwa shindano sawia la ulimwengu mzima huko Poland mwaka 2006.

Kutoka hapo Wema aliingilia uigizaji na ni jambo ambalo alijifunza kwa mpenzi wake wa wakati huo marehemu Stephen Kanumba.

Wema na Kanumba wakiwa kazini kuigiza

 

Kufikia sasa Wema ameshiriki filamu nyingi ambazo zinahusisha watanzania na zingine zina wasanii wa kimataifa. Amepata kuteuliwa kwa tuzo kadhaa za uigizaji na kushinda baadhi yazo.

Wema pia aliwahi kuwa na uhusiano wa kimapenzi na Diamond Platinumz mwanamuziki tajika.

 

Diamond na Wema

 

La hivi maajuzi ambalo amelizungumzia wazi ni uwezo wa kupata watoto.

Mara kwa mara amesikika akisema anatami mtoto ila ana tatizo linalozuia hilo. Wema anamiliki kampuni kwa jina “Endless fame Production” ambayo inajihusisha na kutayarisha filamu na usimamizi wa wasanii.