Categories
Habari

Rais Kenyatta ataka vijana wapewe kipaumbele kwenye mipango ya afya kwa wote Barani Afrika

Rais Uhuru Kenyatta ametoa wito kwa mataifa ya Bara Afrika kutilia maanani zaidi vijana kwenye mipango yao ya afya kwa wote, akisema vijana wana nguvu, uhamasisho na ujuzi wa kuendesha ajenda za nchi zao.

Rais Kenyatta, ameongea leo katika Ikulu ya Nairobi alipotoa hotuba ya ufunguzi wa mkutano wa mwaka huu wa kimataifa kuhusu ajenda ya sekta ya afya, ulioandaliwa kupitia mtandaoni.

Amesema vijana ni muhimu katika kuendeleza ajenda ya mipango ya afya kwa wote na hawapaswi kutengwa.

Rais ameongeza kussema kuwa changamoto za afya zinazowakumba vijana wa Afrika kama vile maambukizi ya virusi vya HIV na ugonjwa wa ukimwi, matatizo ya afya ya kiakili na matumizi ya mihadarati zimefanywa kuwa mbaya zaidi kufuatia chamko la janga la COVID-19.

Ili kufanikisha azma ya mpango wa afya kwa wote, rais amesema mataifa ya Afrika yapasa kuzingatia zaidi upanuzi wa mipango ya afya ya kimsingi, kuimarisha upatikanaji huduma za afya, kufanya huduma za afya kuwa za gharama nafuu na kuzingatia uvumbuzi miongoni mwa vijana wa Bara la Afrika.

Kiongozi wa nchi pia amehimiza kuwepo ushirikiano zaidi miongoni mwa wadau wa sekta ya afya, kuimarishwa usalama wa kiafya na kuwepo ari zaidi ya kisiasa ili kuendeleza ajenda ya mpango wa afya kwa wote.

Kuhusu huduma za afya ya kimsingi, rais amesema mbali na kutoa huduma za matibabu umuhimu zaidi, wito wapasa kutolewa wa kuzuia maambukizi ya magonjwa kwa kina mama na watoto, sekta ya maji na huduma za usafi.

Categories
Habari

Rais Kenyatta azindua hazina ya kufadhili uchumi wa vijana wa MbeleNaBiz

Rais Uhuru Kenyatta amezindua mpango wa kibiashara wa MbeleNaBiz wa kuwatuza wajasiria mali chipukizi na uzinduzi wa mpango makhsusi wa hazina ya vijana wa mwaka 2020-2024.

Akisimamia uzinduzi huo katika Uwanja wa Michezo wa Moi Kasarani Jijini Nairobi, Rais Kenyatta amesema serikali itatenga shilingi bilioni 1.3 za kufadhili uchumi wa vijana wa taifa hili.

Kulingana na Rais, kati ya pesa hizo, shilingi milioni 900 zitatolewa kwa wajasiriamali 250 kama ruzuku.

“Jumla ya shilingi milioni 900 zitapewa

Rais pia ametumia fursa hiyo kuhimiza vijana kuunga mkono mpango wa maridhiano wa BBI ambao tayari umeungwa mkono na mabunge 40 ya kaunti.

Amesema kupitishwa kwa mpango huo kutawawezesha vijana kupata pesa na kuhakikisha rasili mali zaidi zinawasilishwa katika maeneo ya magatuzi ili kufadhili maendeleo.

Categories
Habari

Rais Kenyatta awahimiza vijana wachangamkie maswala ya kitaifa

Rais Uhuru Kenyatta ametoa wito kwa vijana kushiriki ipasavyo katika maswala muhimu ya kitaifa.

Rais Kenyatta amesema kuwa wakati umewadia kwa vijana kuchukua ushukani wa maswala ya humu nchini.

Rais amesema kuwa licha ya vijana kuwa zaidi ya asilimia 70 ya idadi ya Wakenya, hawajashiriki ipasavyo katika uongozi wa taifa hili.

Kiongozi wa taifa amesema hayo katika ukumbi wa Bomas, Jijini Nairobi wakati alipozindua rasmi mjadala wa kitaifa wa vijana kwa jina ‘Kenya ni Mimi’.

Rais ameongeza kuwa vijana wanahitaji kutumia idadi yao kuwania nyadhifa za uongozi nchini.

Amekariri kwamba vijana lazima wawe katika msitari wa mbele kuboresha maisha yao na taifa hili kwa jumla.

“Lazima muwe ndani ya uwanja wala sin je ya uwanja. Lazima mshiriki katika mjadala wa nchi hii kama mtaamua kwamba mnataka kushika usukani wa hatma ya nchi. Mko na nafasi kubwa,” amesema Rais.

Kuhusu mizozo ya kijinsia na tamaduni nyingine zilizopitwa na wakati kama vile ukeketaji na ndoa za mapema, Rais Kenyatta amewahakikishia vijana kuwa serikali haitalegeza juhudi za kukabiliana na maovu hayo.

Aliongeza kwamba serikali yake itaendelea kushirikiana kwa karibu na wanawake pamoja na vijana katika nyanja zote za kimaendeleo.

Categories
Habari

Viongozi wa vijana Nairobi waapa kuandamana wakipinga kubanduliwa mamlakani kwa Sonko

Baadhi ya vijana wa Kaunti ya Nairobi wameshtumu vikali hatua ya kubanduliwa mamlakani kwa Gavana Mike Mbuvi Sonko.

Sonko aliondolewa afisini na wanachama wa Bunge la Kaunti hiyo siku ya Alhamisi kwa madai ya utumuzi mbaya wa mamlaka, utovu wa nidhamu na kukosa uwezo wa kimwili na kiakili kuendesha maswala ya Kaunti hiyo.

Kupitia kwenye mwavuli wa mashirika ya mashinani ya kutetea haki za binadamu, viongozi wa vijana wameapa kukaidi hatua ya kumbandua Sonko uongozini wakisema ilitekelezwa bila kuzingatia sheria.

Vijana hao wametangaza mpango wa kufanya maandamani hadi katika makao makuu ya kaunti hiyo na pia Bunge la Seneti wiki ijayo ili kuonyesha gadhabu yao kutokana na hatua ya kubanduliwa kwa Sonko.

Gavana huyo wa Nairobi anayekabiliwa na matatizo anatarajiwa kufika mahakamani kesho kupinga utaratibu uliotumiwa kumwondoa afisini, akisema ulikuwa na kasoro chungu nzima.

Aidha, Sonko angependa kuwataja Katibu na Spika wa Bunge la Kaunti hiyo Ben Mutura, kwa kudharau maagizo ya mahakama, waliporuhusu kujadiliwa kwa hoja ya kumwondoa mamlakani ilhali  kulikuwa na maagizo ya kusitisha utaratibu huo.

Siku ya Alhamisi, wanachama 88 wa Bunge la Kaunti ya Nairobi walipiga kura na kupitisha mswaada wa kumuondoa Sonko mamlakani.

Categories
Habari

Vijana wahimizwa kuunga mkono BBI kwa manufaa yao ya kiuchumi

Vijana kote nchini wamehimizwa kusoma na kuelewa ripoti ya Mpango wa Maridhiano, BBI, kabla ya kufanya maamuzi yoyote kuhusu.

Chama cha wabunge vijana nchini kinasema ripoti hiyo ina uwezo mkubwa wa kunufaisha vijana nchini lakini lazima wajizindue na kushinikiza ajenda zao.

Kundi hilo lilizungumza wakati ambapo kuna maoni tofauti kuhusu ripoti hiyo huku baadhi ya vijana katika Kaunti ya Kitui wakitaka eneo la Mwingi liwe kaunti kiviake.

Wakati uo huo, Mbunge wa Butere, Tindi Mwale ameanza kuwaongoza baadhi ya vijana wa eneo la Magharibi mwa nchi kuunga mkono ripoti ya BBI.

Mbunge huyo anasema ripoti hiyo ni njia bora ya kujumuisha vijana kikamilifu katika maswala ya  utawala.

Katika Kaunti ya Kakamega, baadhi ya vijana wa eneo hilo wameapa kuunga mkono ripoti ya BBI wakisema inashughulikia uwezeshaji wa kijamii na kiuchumi wa kizazi kipya nchini.

Hata hivyo, kundi hilo linawalaumu wale wanaopinga ripoti hiyo, likiwarai Wakenya kujitenga na watu wachache wanaotumia mchakato huo kuigawanya nchi hii.

Categories
Habari

Balozi wa Marekani ashtumu hatua ya kutumia vijana kuzua vurugu humu nchini

Balozi wa Marekani humu nchini Kyle McCarter amesema nchi yake haitabakia kimya na kutazama vijana wakiendelea kuchochewa na wanasiasa kuzua vurugu humu nchini.

Wakati uo huo, Kyle amekanusha madai kwamba nchi yake inapanga kufutilia mbali hati za Visa za maafisa wa ngazi za juu serikalini, kwa kukatiza uhuru wa kujieleza, kutangamana na kujikusanya pamoja humu nchini.

Balozi huyo ambaye alikuwa akiongea wakati wa ziara ya kutoa mchango wa barakoa kwa utawala wa Kaunti ya Kirinyaga, amesema hafahamu lolote kuhusu habari hizo huku akitaja madai hayo kuwa ya uongo.

Akiwa ameandamana na Gavana wa Kirinyaga Ann Mumbi Waiguru, Kyle pasipo kutoa maelezo zaidi amesema hakuna uamuzi wowote kama huo ambao umeafikiwa na nchi yake, na akahimiza WaKenya kupuuza uvumi wa aina hiyo.

Pia amesema kwamba wale watakaopatikana na hatia kufuatia kupotea kwa fedha za kupambana na janga la COVID-19, watakabiliwa na hatua kali kutoka kwa serikali yake.

Kuhusu usalama, Kyle amesema kwamba serikali za Marekani na Kenya zinashirikiana kwa karibu ili kushinda kundi la kigaidi la Al-Shabaab.

Categories
Habari

Vijana wa ODM huko Pwani waapa kupambana na waasi wa chama hicho

Viongozi wa vijana katika chama cha ODM Ukanda wa Pwani, wamepinga vikali wito wa kuundwa kwa chama cha kisiasa cha Pwani unaotolewa na viongozi wanaoegemea upande wa Naibu Rais William Ruto.

Vijana hao wamesema eneo hilo ni ngome ya ODM na wakaapa kulilinda kutokana na wenye nia ya kulivamia na kugawanya wakazi kisiasa.

Wamesema haya kwenye mkutano na wajumbe wa ODM kutoka eneo zima la Pwani uliofanyika katika Ukumbi wa Arabuko Sokoke Jamii Villas, Kaunti ya Kilifi.

Wamewakashifu wabunge Owen Baya wa Kilifi Kaskazini na Aisha Jumwa wa Malindi kwa kampeni zao za kushinikiza kuundwa kwa chama kipya cha Pwani na pia wakaapa kutwaa ushindi kwenye chaguzi tatu ndogo zijazo katika eneo hilo.

Chaguzi hizo ni ule wa Ubunge wa Msambweni Kaunti ya Kwale na Uwakilishi Wodi za Dabaso na Wundanyi katika Kaunti za Kilifi na Taita Taveta mtawalia, ambazo zimeratibiwa kufanyika tarehe 15 Desemba mwaka huu.

Wamemsihi kinara wa ODM Raila Odinga na naibu wake Ali Hassan Joho watulie na kuwapa nafasi vijana hao wadhihirishe ubabe wao wa kisiasa katika chaguzi hizo tatu ndogo.

Kwenye taarifa kwa vyombo vya habari iliyosomwa naye Mwenyekiti wa Vijana wa ODM Kaunti ya Taita Taveta Patricia Mwashighadi, vijana hao wameamua kuwa katika msitari wa mbele kwenye chaguzi hizo.

“Chama cha ODM kimekita mizizi katika eneo la Pwani, kinaazimia kuleta mafanikio kwa wananchi na kimestahimili changamoto za kutetea haki zao,” amesema Mwashighadi katika taarifa hiyo.

Mwashighadi ameongeza kuwa vijana hao wameazimia kuzuru nyanjani kwa zoezi la kusajili wakazi na kuuza sera za chama hicho ili kutimiza ajenda ya demokrasia na maendeleo.

Categories
Vipindi

Marwa amesisitiza fedha billion 8.5 zilizotolewa na serikali kwa wazee na walemavu zitawifikia

Katibu wa Huduma za Jamii Nelson Marwa amesisitiza fedha billion 8.5 zilizotolewa na serikali kwa wazee na walemavu zitawifikia hivi karibuni.

Akizungumza na Wanahabari wa Radio Taifa Bernard Maranga na Cynthia Anyango, Marwa aliongeza kuwa wizara ya Leba itakabiliana na wale wanaotumia walemavu au watoto kujinufaisha.

https://podcasts.kbc.co.ke/wp-content/uploads/2020/04/PS-SOCIAL-PROTECTION-NELSON-MARWA-RADIO-TAIFA-23RD-APRIL-2020.mp3
Categories
Habari

Ruto asema hatakoma kusaidi makundi ya Kidini na kuinua vijana

Naibu Rais William Ruto amesema hatashurutishwa kukoma kusaidia makundi ya kidini na shughuli za kuwainua vijana.

Akihutubia viongozi wa makanisa waliomtembelea nyumbani kwake Sugoi, Kaunti ya Uasin Gishu, hapo jana, naibu rais alisema haoni aibu kumtumikia Mungu na wala hajutii imani yake.

Aidha alisema imani yake ndiyo ya kwanza mbele ya mamlaka ya kisiasa na akawataka wale wanaotatizika na shughuli zake za kusaidia makanisa, makundi ya kiislamu na juhudi za kuwainua vijana na wanawake kutafuta shughuli za kufanya.

Alisema viongozi walichaguliwa kuwapa uwezo wakenya miongoni mwa sababu nyingine akiongeza kuwa ni kupitia kwa miradi kama ile anayounga mkono ambapo maisha ya wakenya wa kawaida yanaweza kuimarishwa.