Categories
Michezo

Kenya yailemea Sudan katika mechi ya kirafiki

Timu ya Kenya kwa chipukizi wasiozidi umri wa miaka 20 maarufu kama Rising Stars,  ilikuwa na wakati mgumu kabla ya kuishinda Sudan mabao 2-1 katika mchuano wa kujipima nguvu uliochezwa Alhamisi jioni katika uwanja wa taifa wa Nyayo.

Kenya walianza kwa uzembe huku Sudan walichukua uongozi katika dakika ya 4 kabla ya mshambulizi  Brian Wanyama kusawazisha  wenyeji kunako dakika ya 35.

Licha ya mashambulizi kutoka kwa pande zote kipindi cha kwanza kilimalizika kwa sare ya bao 1-1 .

Wachezaji wa Kenya wakimiliki Mpira  Uwanjani Nyayo                        picha @Mnyamwezi

Katika kipindi cha pili  timu zote zilicheza kwa tahadhari kubwa lakini utepetevu wa Sudan katika dakika ya 78 kulimpa  Matthew Mwendwa  nafasi ya kupachika bao la ushindi  kwa Rising Stars.

Ulikuwa ushindi wa pili kwa Kenya dhidi ya Sudan baada ya kuwapiga mabao 3-1 tarehe 2 mwezi huu katika uwanja wa kimataifa wa Kasarani katika pambano jingine la kirafiki.

Kenya chini ya ukufunzi wa Stanley Okumbi sasa wanajipanga kuelekea Arusha Tanzania kushiriki mashindano ya CECAFA baina ya Novemba 22 na Desemba 6 ambapo wamejumuishwa kundi C pamoja na Ethiopia na Sudan.

Risinga Stars wakisherehekea bao                                                                                picha @Mnyamwezi

Kundi A linajumuisha mabingwa watetezi na wenyeji  Tanzania, Rwanda, Somalia, na  Djibouti, wakati kundi B likiwa na  Burundi, Eritrea, South Sudan na Uganda.

Timu bora kutoka kila kundi pamoja na timu bora ya pili kutoka makundi yote matatu ,zitafuzu kwa nusu fainali huku timu mbili zitakazotinga fainali zikifuzu kwa mashindano ya Afcon mwaka ujao.

Rising Stars walipoteza bao 1-0 kwa Serengeti Boys ya Tanzania katika fainali ya mwaka jana ya CECAFA  nchini Uganda.

Categories
Michezo

Rising Stars ya Kenya yaipakata Sudan Kasarani

Rising Stars ya Kenya imeipakataka Sudan mabao 3-1 katika mchuano wa kirafiki uliopigwa Jumatatu alasiri  katika uwanja wa kimataifa wa Moi Kasarani.

Wageni Sudan walipata bao la uongozi katika dakika ya 8  kupitia kwa Nogh Hussein  huku Kenya wakirejea mchezoni kwa bao la kusawazisha la  dakika ya 21  kupitia kwa  Sellasie Otieno na kipindi cha kwanza kumalizika kwa sare ya bao 1.

Ronald Reagan na  Mathew Mwendwa walipachika kimiani mabao ya Kenya kunako dakika za  58 na 85 na  huku wenyeji wakiibuka kidedea katika mchuano huo.

Timu hiyo ya Kenya itasafiri kuelekea Arusha baadae mwezi huu kwa mashindano ya kuwania kombe la Cecafa yatakayoandaliwa nchini Tanzania kuanzia Novemba 22 hadi Desemba 6 ambayo ni kutawafuta waakilishi wawili wa kanda hii kwenye michuano ya Afcon kwa vijana wasiozidi umri wa miaka 20 nchini Moroko mwakani.

Katika mashindano hayo ya Cecafa Kenya imejumuishwa kundi C pamoja na Sudan na Ethiopia, huku timu bora kutoka kila kundi ikifuzu kwa hatua ya nusu fainali .

Categories
Kimataifa

Vikwazo viliyowekewa Sudan vyaondolewa na Marekani

Serikali ya Marekani imeondoa vikwazo vya muda wa miaka 23 vilivyowekewa Sudan baada ya nchi hiyo kutoa hakikisho kwamba haitaunga mkono vitendo vya ugaidi wa kimataifa siku za usoni.

Rais Donald Trump kwenye taarifa alisema hatua hii inajiri baada ya Sudan kulipa fidia ya dolla milioni 325 kwa waathiriwa wa mashambulizi ya kigaidi.

Vikwazo hivyo vilizuia shughuli zozote kutekelezwa kwa kutumia sarafu ya Marekani.

Hii ilimaanisha kwamba kampuni yoyote ya kibiashara iliyokuwa nchini Marekani haingelifanya biashara na Sudan.

Kutokana na hatua hii, Sudan sasa iko huru kuafikia mikataba ya kibiashara na Marekani na makampuni makubwa ya mataifa ya magharibi tangu mwaka wa 1997 wakati ilipowekewa vikwazo hivyo.

Hatua hii pia inamaanisha kuwa Sudan sasa inaweza kutafuta mikopo kutoka mashirika ya kimataifa ya utoaji mikopo, kuwaalika wawekezaji nchini humo na kununua vipuri vya kukarabati viwanda na ndege zake za kale za shirika lake la kitaifa la ndege.

Sudan chini ya serikali ya mseto ya waziri mkuu Abdalla Hamdok ililazimika kulegeza msimamo wake ili kuafikia maridhiano na serikali ya Marekani.

Categories
Kimataifa

Trump atoa masharti ya kuiondoa Sudan katika orodha ya wanaofadhili ugaidi

Rais wa Marekani Donald Trump amesema ataoindoa Sudan kwenye orodha ya mataifa yanayofadhili ugaidi ikiwa taifa hilo litakubali kulipa fidia ya dola milioni 335 kwa familia za raia wa Marekani walioathiriwa na mashambulizi ya kigaidi.

Hatua hii pia inatarajiwa kuanzisha utaratibu wa kurejesha uhusiano wa kidiplomasia kati ya Sudan na Israel kufuatia makubaliano sawia kati ya taifa hilo na Muungano wa Milki za Kiarabu na Bahrain.

Hata hivyo mazungumzo hayo bado yanaendelea kuhusu mkataba huo.

Sudan iliorodheshwa miongoni mwa mataifa yanayofadhili vitendo vya kigaidi wakati wa enzi ya aliyekuwa rais Omar al- Bashir aliyeondolewa mamlakani.

Hatua hiyo bado inainyima serikali ya sasa ya mpito ruzuku na ufadhili wa kigeni inayohitaji kuendeleza shughuli zake.

Categories
Kimataifa

Serikali ya Sudan yatia saini mkataba wa Amani na viongozi wa Waasi

Serikali ya Sudan na viongozi wa waasi wametia saini mkataba wa kihistoria wa amani unaolenga kukomesha vita vilivyodumu kwa miongo mingi ambavyo vimesababisha vifo vya maelfu ya watu.

Mkataba huo wa amani uliotiwa saini leo jijini Juba nchini Sudan kusini ulipatanishwa na nchi kadhaa zikiwemo Kenya, misri na Sudan kusini.

Kiongozi wa chama cha Wiper Kalonzo Musyoka aliyeakilisha Kenya alisema kuwa mikataba ya amani inahitaji kujitolea ili itekelezwe.

Alisema kuwa wakati umewadia kwa bara Afrika kukomesha vita na kuungana ili kuliendelea bara hili.

Katibu mkuu mwandamizi katika wizara ya mashauri ya nchi za kigeni Ababu Namwamba alisema kuwa amani katika eneo hili italeta ukuaji na maendeleo.

Rais Salva Kiir  wa Sudan kusini alisema kuwa uthabiti nchini Sudan utanufaisha nchi yake pia.

Makundi saba ya waasi kutoka Darfur na Sudan magharibi yalisema yatasitisha vita na kuleta umoja kwenye mkataba wa amani uliopatanishwa na serikali za kanda hii.

Kukomeshwa mizozo ya ndani nchini Sudan kumepewa umuhimu na serikali ya mpito nchini humo iliyotwaa mamlaka mara tubaada ya kung’atuliwa kwa kiongozi wa muda mrefu Omar al-Bashir. Mkataba huo wa amani nchini Sudan umesifiwa na viongozi mbalimbali duniani kuwa wenye manufaa kwa umoja ulimwenguni.

 

Categories
Kimataifa

Zaidi ya watu 100 wafariki kutokana na mafuriko nchini Sudan

Shirika la chakula na kilimo la umoja wa mataifa-FAO limesema mafuriko makubwa yanayoshuhudiwa nchini Sudan yameathiri takriban thuluthi moja ya ardhi iliyolimwa na familia zipatazo laki-6.

Zaidi ya tani milioni moja za nafaka zimeharibiwa hasa mtama ambao ndilo zao kuu na familia nyingi sasa zimelazimika kutumia chakula kidogo kidogo kwa siku.

Mafuriko hayo yamesababisha vifo vya zaidi ya watu 100.

Mapato yameathiriwa pia huku mimea ya kibiashara ikiwemo migomba ya ndizi na miembe pia ikiathiriwa vibaya.

Shirika la FAO limesema kwamba nzige ambao wameathiri mimea katika eneo hilo la upembe wa Afrika, bado ni tishio kwa nchi hiyo.