Categories
Michezo

Simba yanusia robo fainali ya ligi mabingwa baada ya kumng’ata mwarabu mweusi 3-0

Miamba wa soka Afrika mashariki Simba SC imeendelea kuongoza kundi A la michuano kuwania kombe la ligi ya mabingwa Afrika na kujiweka katika hali nzuri ya kutinga kwota fainali kwa mara ya kwanza baada ya kuifyatua Al Merreikh ya Sudan magoli 3-0 katika mechi iliyosakatwa uwanja wa Benjamin Mkapa jijini Daresalaam Tanzania Jumanne alasiri.

Luis Miquissone aliyepachika bao lilomwadhibu mwarabu wa Misri,alifungua ukurasa wa magoli kwa bao la dakika ya 18 kabla ya Mohamed Hussien kuongeza la pili dakika ya 38 huku vijana wa msimbazi wakiongoza 2-0 kufikia mapumzikoni.

Kipindi cha pili Mnyama aliendelea na gonga gonga zake na kubisha mlango wa wakwasi wa mafuta ,Merreikh na dakika ya 49 Chris kope Mugalu akacheka na nyavu kwa bao la tatu na kutoka hapo wajukuu wa Mkapa wakaendelea na mazoezi hadi kipenga cha mwisho wakipata alama tatu muhimu na magoli matatu bila jawabu.

Ushindi huo unaiweka Simba mguu mmoja ndani ya robo fainali ya kombe hilo kwa mara ya kwanza wakihitaji pointi moja pekee kutokana na mechi zilizosalia mbili wakiwaalika AS Vita Club ya Jamhuri ya demokrasia ya Congo na mwaliko mjini Cairo dhidi ya mabingwa mara 9 Al Ahly April 9.

Ahly pia wamesajili ushindi wa pili baada ya kuwanyuka Vita 3-0 katika mji wa Kinsasha na kufufua matumaini yao ya kufuzu kwa robo fainali.

Simba wanaongoza kundi A kwa pointi 10 ,3 zaidi ya Ahly huku Vita ikiwa na alama 4 nayo Merreikh inashika nanga kwa alama 1

Categories
Michezo

Yanga yamnyatia kocha Auseems wa Leopards

Miamba wa soka nchini Tanzania  Young Africans   maarufu kama  vijana wa Jangwani  wameanza kumnyemelea  kocha  wa AFC Leopards Patrick Aussems .
Auseems ambaye ni raia wa Ubelgiji angali na kandarasi ya miezi 6 na Leopards  huku ikiyakinika kuwa Yanga wako tayari  kufanya kila juhudi kumsajili  kocha huyo  kutwaa mikoba ya Mrundi Cedric Kae aliyepigwa kalamu Jumapili iliyopita kwa matokeo mabovu.
Endapo ataondoka Ingwe itakuwa mara ya pili kwa Auseems kurejea  Tanzania baada ya awali kuwa na timu ya Simba SC mwaka 2018 hadi 2019.
Yanga ingali kuongoza ligi kuu Tanzania bara kwa  pointi 50 kutoka na michuano 23,pointi tano zaidi ya watani wao Simba SC lakini matokeo yao yamedorora wakiwa wameshinda pambano moja pekee kati ya tano za mwisho.

 

Categories
Michezo

Wakenya Joash Onyango na Francis Kahata wazidi kuandikisha historia na Simba SC

Beki kisiki wa Kenya Joash Onyango  na  kiungo Francis Kahata waliendelea kutamba na miamba wa Tanzania klabu ya Simba huku ikilazimisha sare tasa ugenini Jumamosi jioni mjini Khartoum Sudan katika mkwangurano wa tatu wa kundi A kuwania kombe la ligi ya mabingwa Afrika.

Kama desturi Onyango alipiga dakika zote 90 za mechi huku Kahata akiingia uwanjani dakika ya 77 kumpumzisha Cletus Chama ,wakiwa wakenya pekee waliocheza mechi hizo za ligi ya mabingwa Jumamosi,baada ya Brian Mandela wa Mamelodi Sundowns na Athony Teddy Akumu wa Kaizer Chiefs  wakikosa kujumuishwa kwenye vikosi vya timu zao.

Joash Onyango akiwasili Darsalaam mapema Jumapili na wenzake kutoka Sudan

Simba wangali kuongoza kundi A kwa pointi 7 wakifuatwa na AS Vita Club ya DR Congo kwa alama 4 sawa na mabingwa watetezi Al Ahly ya Misri huku Al Merreikh ikishika nanga bila alama.

Simba itawaalika Al Merreikh katika uwanja wa Benjamin Mkapa Daresalaam tarehe 16 mwezi huu,wekundu wa msimbazi wakihitaji ushindi ili kuweka hai matumaini ya kutinga robo fainali kwa mara ya kwanza.

Categories
Michezo

Simba amrarua mwarabu na kuongoza kundi A ligi ya mabingwa

Simba Sports club wameweka hai matumaini ya kutinga robo fainali ya kombe la ligi ya mabingwa Afrika baada ya kuwachuna mabingwa watetzi Al Ahly bao 1-0 katika mkwangurano uliosakatwa Jumanne alasiri katika uwanja wa Benjamin Mkapa jijini Daresalaam Tanzania.

Bao la pekee na la ushindi kwa mnyama simba lilipachikwa kimiani na kiungo wa Msumbiji Luis Muquissone kunako dakika ya 39 na kudumu hadi kipenga cha mwisho.

Kichapo cha Al Ahly kilikuwa cha kwanza katika ligi ya mabingwa Afrika baada ya zaidi ya msimu mmoja .

Uwanja wa Mkapa ulifurika hadi pomoni wakati wa mechi hiyo baada ya tiketi zote za mechi kuuzwa .

Ushindi huo unaweweka Simba uongozini pa kundi A kwa alama 6 baada ya mechi 2 kufuatia ushindi wa goli 1-0 ugenini mjini Kinsasha dhidi ya As Vita katika pambano la ufunguzi .

Mnyama Simba ataanza matayarisho kwa ziara ya Khartoum mwishoni mwa juma hili dhidi ya El Merreikh ya Sudan huku wakihitaji angaa ushindi katika mechi mbili kati ya 4 zilisozalia ili kutinga kwota fainali kwa mara ya kwanza.

Categories
Michezo

Simba yaitafuna Vita hadharani

Miamba wa soka nchini Tanzania,klabu ya Simba Sports club walianza vyema mechi za makundi za kuwania kombe la ligi ya mabingwa Afrika baada ya kuwaangusha AS Vita Club ya Jamhuri ya Demokrasia ya Congo bao 1 bila jawabu katika pambano la kundi A lililopigwa Ijumaa usiku katika uwanja wa Kinsasha.

Bao la mnyama Simba lilitiwa kimiani na mshambulizi Mutshimba Lugalu kupitia mkwaju wa penati  kunako dakika ya 60 na kudumu hadi kipenga cha mwisho.

beki kisi wa Kenya Joash Onyango alipiga dakika zote 90 huku kiungo Francis Kahata akiingia uwanjani kipindi cha pili.

Simba wanaongoza kundi hilo kwa alama 3 ,wakishiriki hatua ya makundi  kwa mara ya pili na ya kwanza  tangu mwaka 2013.

Wekundu wa msimbazi Simba watarejea Dar kujiandaa kwa mkwangurano wa pili watakapowaalika mabingwa watetezi na washindi mara 9 wa kombe hilo Al Ahly  kutoka Misri Februari 23.

Katika pambano la kundi D lililochezwa Cairo,Zamalek walilazimishwa kutoka sare kapa nyumbani dhidi ya MC Alger kutoka Algeria.

Categories
Michezo

Simba SC tayari kumvaa Vita Club huko Kinsasha

Mabingwa wa ligi kuu ya Tanzania bara Simba Sc wameanza mazoezi mjini Kinsasha  Alhamisi jioni  katika jamhuri ya Demokrasia ya Congo kujitayarisha kwa mechi ya kwanza ya makundi kuwania kombe la ligi ya mabingwa Afrika Ijumaa hii dhidi ya wenyeji As Vita Club.

Wekundu wa Msimbazi ambao ni mabingwa mara 21 wa ligi kuu ya kwao wamefuzu kucheza hatua ya makundi ya kombe hilo kwa mara ya pili katika historia na mara ya kwanza tangu mwaka 2003.

Kikosi cha Simba kilicho DRC kinawajumuisha wakenya Francis Kahata na beki kisiki Joash Onyango huku timu hiyo ikiwa ya pekee kutoka ukanda wa East Afrika iliyotinga hatua ya makundi katika kombe hilo .

Baadae tarehe 23 mwezi huu Simba watawaalika mabingwa watetzi na mabingwa mara 9 wa kombe hilo Al Ahly ya Misri,kabla ya kuzuru sudan Machi  5 kuvaana na Al Merreikh na kurudiana nao jijini daresalaam tarehe 16 mwezi uja.

Michuano ya ufunguzi hatua ya nakundi kuwania kombe la ligi ya mabingwa kusakatwa kati ya Ijumaa na Jumamosi.

Categories
Michezo

Onyango kucheza hatua ya makundi ya klabu bingwa Afrika kwa mara ya kwanza

Beki Kisiki Joash Abong’o  Onyango wa Kenya alijiunga na mabingwa wa Tanzania klabu ya Simba na ndani ya msimu wake wa kwanza ameifuzisha timu hiyo kucheza hatua ya makundi kuwania kombe la ligi ya mabingwa Afrika .

Onyango aliye na umri wa miaka 27 aliichezea Western Stima kati ya mwaka 2015 na 2016 kabla ya kujiunga na Gor Mahia tokea mwaka 2017 hadi 2019.

Akiwa Gor Onyango alicheza mechi za mchujo za klabu bingwa lakini kwa miaka yote miwili Gor walishindwa kufua dafu  kucheza hatua ya makundi ya klabu bingwa   wakibanduliwa na baade kufaulu kucheza hatua ya makundi ya kombe la shirikisho.

Onyango alipiga dakika zote 90 katika uwanja wa Benjamin Mkappa jijini Daresalaam Jumatano jioni  na kuisaidia Simba Sc kuikung’uta  Platinum ya Zimbabwe mabao 4-0 huku wakifuzu  hatua ya makundi kwa mara ya pili  na ya kwanza tangia mwaka 2003.

Ishara moja iliyo bayana ni kuwa kuna vitu majirani zetu wamenya sahihi kuinua kiwango cha ligi yao na hata timu ya taifa,Simba pia ndicho klabu pekee kutoka East Afrika kutinga hatua hiyo msimu huu.

Angesalia Kenya kutokana na viwango vya mchezo vilivyo chini ,huenda Onyango angestaafu bila kucheza soka katika kiwango hicho .

Wakenya wengine waliofuzu kucheza hatua hiyo ya makundi ya klabu bingwa Afrika ni Brian Onyango Mandela akiwa na Mamelodi Sundowns ya Afrika Kusini na  Athony Akumu aliye Kaizer Chiefs pia ya Afrika Kusini.

 

 

Categories
Michezo

Simba anguruma na kuweka historia ya kutinga makundi ya ligi ya mabingwa

Klabu ya Simba imeandikisha historia baada ya kusajili wa ushindi wa mabao 4-0 dhidi ya Platinum Fc ya Zimbabwe  na kufuzu hatua ya makundi ya kombe la ligi ya mabingwa Afrika katika mchuano wa marudio uliosakatwa Jumatano jioni katika uwanja wa Benjamin Mkapa jijini Dar.

Difenda Erasto Nyoni aliwanyanyua mashabiki  takriban 30,000 wa wekundu wa msimbazi waliofurika uwanjani   kwa bao la kwanza kupitia mkwaju wa penati wa dakika ya 40  huku wakienda mapumziko kwa uongozi huo.

Kipindi cha pili Mnyama Simba alirejea kwa uchu wa mashambulizi yaliyozalisha goli la pili lililopachikwa kimiani na beki Shomari Kapombe katika dakika ya 61 naye Juma Bocco akapiga bao la tatu dakika ya 91 huku Cletus Chama akifunga karamu kwa bao la nne dakika ya 94.

Simba watakuwa wakipiga hatua ya makundi ya kombe hilo lenye donge nono  kwa mara ya pili na ya kwanza tangu mwaka 2003 ikiwa pia timu ya pekee kutoka Afrika Mashariki kucheza hatua hiyo.

Simba walikuwa wamepoteza duru ya kwanza bao 1-0 ugenini hivyo basi wapiga delji hadi hatua ya makundi kwa ushindi wa jumla wa mabao 4-1 dhidi ya Platinum.

Categories
Michezo

Simba alenga kurudia Historia na kutinga makundi ya Ligi ya mabingwa

Timu ya Simba Sports  Club ya Tanzania inaazimia kufuzu kwa  hatua ya makundi ya ligi ya mabingwa Afrika Jumatano jioni   katika uwanja wa Benjamin Mkapa nchini Tanzania itakapowaalika Platinums kutoka Zimbabwe.

Simba walipoteza bao 1-0 kutokana na mkumbo wa kwanza mjini Harare wanahitaji ushindi wa mabao 2-0 ili kuingia hatua ya makundi ya kombe hilo yenye donge nono.

Beki kisiki wa Kenya Joash Onyango ameenza pambano hilo akilenga kupiga soka hatua ya makundi baada  ya kujaribu mara kadhaa biloa mafanikio akiwa na Gor Mahia ya Kenya.

Wekundu wa Msimbazi wanalenga kufuzu kwa hatua ya makundi kwa mara ya pili katika historia yao baada ya kucheza hatua hiyo kwa mara ya kwanza mwaka 2003.

 

 

Categories
Michezo

Joash Onyango awanusuru Simba kutafunwa na Yanga Derby ya Kariakoo

Beki kisiki wa Kenya Joash Onyango aliwanusuru wekundu wa Msimbazi Simba Sports club ,alipoachika bao la dakika ya 86 na kulazimisha Derby ya Kariakoo kuishia sare ya bao 1-1 dhidi ya Young Africans ukipenda YANGA katika pambano la ligi kuu Tanzania Bara VPL ,Jumamosi alasiri katika uchanjaa wa Benjamin Mkapa.

Mashabiki    wa    Simba uwanjani Benjamin Mkapa Jumamosi
Mashabiki wa YANGA uwanjani Benjamin Mkapa Jumamosi

Wenyeji Yanga walitamalaki kipindi cha kwanza huku wakidhihirisha mchezo wa hali ya juu kwa pasi kamilifu na mashambulizi ya uhakika yaliyozaa matunda baada ya  mshambulizi wa kutokea Ghana Michael Sarpong kuwanyanyua mashabiki kwa bao la ufunguzi la dakika ya 32 kupitia mkwaju wa penati iliyotakana na mshambulizi wao kuangushwa na beki wa Simba .

Bao hilo lilidumu hadi mapumzikoni huku mashabiki wa Simba wakilazimika kufyata ndimi kwa muda mrefu uwanjani kutokana na  mashambulizi mengi yaliyoelekezwa katika lango lao.

Hata hivyo kuondolewa uwanjani kwa mshambulizi Sarpong kuliwapa mabeki wa Simba fusra ya kupumua na kupunguza kasi ya Yanga na kosa la dakika ya 86 kutoka

kwa madifenda wa Yanga kukampa Joash Onyango beki kisiki wa Kenya nafasi ya kuirejesha Simba mchezoni huku timu zote zikitoka sare ya bao 1-1 katika derby hiyo na kuzidisha ubabe wa Simba dhidi ya YANGA kwenye Derby hiyo.

Mashabiki zaidi ya elfu 40 waliujaza uwanja wa Benjamin Mkapa hadi pomoni wakivalia jezi za timu zao wakiwa na mirindimo ya nyimbo,magoma na densi uwanjani.

Matokeo hayo yanawaacha Vijana wa jangwani Yanga katika nafasi ya pili kwa pointi 24  kutokana na michuano 10 na ikiwa timu pekee ambayo haijapoteza mchuano katika ligi kuu ya VPL,pointi 1 nyumba ya Azam United fc huku Simba ikishikilia nafasi ya tatu kwa alama 20.