Categories
Michezo

Al Ahly wamteua Pitso Mosimane kuwa kocha mpya kwa miaka miwili

Miamba wa soka nchini Misri Al Ahly wametangaza uteuzi wa Pitso Mosimane kuwa kocha mpya kutwaa mikoba ya ukufunzi kutoka kwa Rene Weiler.

Kwa mjibu wa vyanzo vya habari nchini Misri Mosimane anatarajiwa kutua Cairo Oktoba 2 kusaini mkataba na miamba hao wa Afrika maarufu kama the Red Devils, huku akiwachagua wasaidizi wake watatu.

Mosimane akiwa na Rais wa Al Ahly

Rais wa Ahly Mahmoud El-Khatib amekuwa mfuasi mkuu wa kocha Mosimane aliyeisaidia Mamelodi kunyakua taji ya tano mtawalia ya ligi kuu nchini Afrika kusini ingawa alikuwa amesalia na miaka minne kwenye kondrati yake na the Brazilians ukipenda Mamelodi na kombe moja la ligi ya mabingwa Afrika mwaka 2016.

Mosimane akibeba kombe la ligi kuu Afrika Kuisni na Mamelodi

Duru kutoka Cairo zaarifu kuwa Mosimane ameahidiwa donge nono na Ahly waliotwaa kombe la ligi ya mabingwa afrika mara 8 ambapo atakuwa akilipwa shilingi milioni 12 za Kenya sawa na dola 120,000 kwa mwezi ambazo ni mara dufu ya kiwango alichokuwa akilipwa akiwa Mamelodi.

Kwa jumla Mosimane ambaye ni kocha wa zamani wa timu ya taifa ya Afrika kusini atakuwa akilipwa dola 270,000 kwa mwezi ukiongezea na kwa mwezi bila marupurupu ya kushinda mechi.

Mosimane

Mosimane amekubali kuandikisha mkataba wa miaka miwili na ataandamana na msaidizi wake Rhulani Mokwena, mkufunzi wa viungo Kabelo Rangoaga na mdadisi wa ubora wa uchezaji Musi Matlaba katika timu ya Ahly ,baada ya kuhudumu nao pamoja katika timu ya Mamelodi.