Mshambulizi wa Harambee Stars Michael Olunga alifungua ukurasa wa kupachika mabao katika klabu yake mpya ya Al Duhail Sc Jumatatu usiku nchini Qatar alipopiga magoli matatu na kuipa timu yake ushindi wa mabao 6-0 na kufuzu kwa kwota fainali ya kombe la Amir.
Olunga aliyejiunga na klabu hiyo mapem mwezi akitokea Kashiwa Reysol ya Japan alipachika mabao 2 kunako kipindi cha kwanza ,dakika ya 6 kupitia mkwaju wa penati baada ya mshambulizi Dudu kutoka Brazil kuangushwa katika eneo la hatari.
Edmilson alimpokeza Olunga pasi ya dakika ya 43 akiunganisha kwa kichwa mkwaju wa kona na kupiga goli la 2 .
Olunga alipachika goli la tatu dakika ya 69 huku timu yake ikisajili ushindi wa jumla wa mabao 37-7 katika mechi hiyo ya mikondo miwili na kufuzu wka robo fainali.
Mshambulizi huyo aliibuka mfungaji bora katika ligi kuu ya Japan msimu jana pamoja na kutawazwa mchezaji bora kabla ya kuhamia Qatar anakolipwa msahara mara dufu.