Categories
Michezo

Olunga alenga kuandikisha historia kucheza FIFA World Cup

Mshambulizi  wa Harambee Stars Michale Olunga anatarajiwa kuingia kwenye madaftari ya kumbukumbu kuwa Mkenya wa kwanza kucheza mashindano ya kombe la dunia baina ya vilabu yatakayoanza  Alhamisi hii nchini Qatar.

Olunga aliye na umri wa miaka 26 amejumuishwa kwenye kikosi cha klabu ya Al Duhail Sc  huku wakicheza mchuano wa ufunguzi Alhamisi Februari 4 dhidi ya mabingwa wa Afrika Al Ahly kutoka Misri.

Awali Mc Donald Mariga alikuwa kwenye kikosi cha Inter Milan ya Italia kilichonyakua kombe la dunia mwaka 2010 katika muungano wa Milki za kiarabu.

Olunga ambaye aliibuka mfungaji na mchezaji bora katika ligi kuu ya Japan mwaka jana akiwa na klabu ya Kashiwa Reysol alijiunga na mabingwa hao wa Qatar kwa kima cha shilingi milioni 933 ambapo anakisiwa kulipwa mara dufu ya mshahara aliokuwa akilipwa akiwa Japan .

Mshambulizi huyo wa Kenya anatarajiwa kuichezea Al Duhail katika mechi ya robo fainali ya kombe la dunia Alhamisi dhidi ya mabingwa mara 9 wa Afrika Al Ahly baada ya kujumuishwa kwenye kikosi cha wanandinga 23 wa mabingwa hao watetezi wa ligi kuu Qatar zamani wakifahamika kama Lakhwiya.

Katika mechi nyingine ya robo fainali ya Alhamisi mabingwa wa Marekani kaskazini Tigres UNL  ya Mexico itapambana na mabingwa wa bara Asia Ulsan Hyundai.

Mashindano ya kombe la dunia kati ya vilabu yanajumuisha mabingwa wa kila bara ,Ulaya ikiwakilishwa na Bayern munich na Palmeiras wakiwakilisha Marekani Kusini  huku fainali yake ikisakatwa Februari 11.

 

 

 

Categories
Michezo

Olunga afungua akaunti za magoli Qatar kwa Hatrick

Mshambulizi wa Harambee Stars Michael Olunga alifungua ukurasa wa kupachika mabao katika klabu yake mpya ya Al Duhail Sc   Jumatatu usiku nchini Qatar alipopiga magoli matatu na kuipa timu yake ushindi wa mabao 6-0  na kufuzu kwa kwota fainali ya kombe la Amir.

Olunga aliyejiunga  na klabu hiyo mapem mwezi akitokea Kashiwa Reysol ya Japan alipachika mabao 2 kunako kipindi cha kwanza ,dakika ya 6 kupitia mkwaju wa penati  baada ya mshambulizi Dudu kutoka Brazil kuangushwa katika eneo la hatari.

Edmilson alimpokeza Olunga pasi ya dakika ya 43  akiunganisha kwa kichwa mkwaju wa kona na kupiga goli la 2 .

Olunga alipachika goli la tatu dakika  ya  69  huku timu yake ikisajili ushindi wa jumla wa mabao 37-7 katika mechi hiyo ya mikondo miwili na kufuzu wka robo fainali.

Mshambulizi huyo aliibuka mfungaji bora katika ligi kuu ya Japan msimu jana pamoja na kutawazwa mchezaji bora kabla ya kuhamia Qatar anakolipwa msahara mara dufu.

Categories
Michezo

Olunga ajiuanga Al Dhuhail Fc ya Qatar

Mshambulizi wa Harambee Stars Michael Olunga amejiunga na Al Dhuhail Sports Club ya Qatar akitokea  Kashiwa Reysol ya Japan aliyoichezea kwa miaka miwili.

Olunga aliye na umri wa miaka 26  aliibuka mfungaji bora msimu jana katika ligi kuu ya Japan akipachika mabao 28 na pia kutawazwa mchezaji bora kwenye ligi hiyo ya J1 league.

Yamkini Olunga atakuwa akilipwa  mara mbili ya mshahara wa shilingi milioni 8 aliokuwa akilipwa kwa mwezi katika timu ya Kashiwa  huku mkataba huo ukigharimu takriban shilingi bilioni 1.

Hii ina maana kuwa Olunga ambaye zamani alikuwa na vilabu vya  Thika United,Tusker Fc na Gor Mahia kwa mkopo atakuwa akitia kibindoni shilingi milioni 16 za Kenya  kwa mwezi.

Al Dhuhail ndio mabingwa watetezi wa ligi kuu nchini Qatar zamani wakifahamika  kama Al Lakwiya na kwa sasa wanashikilia nafasi ya pili kwa pointi 27 kufuatia mechi 13 nyuma ya viongozi Al Saad walio na alama 35.

Olunga  anafuata mkondo wa wachezaji wengi nyota wanaoichezea Al Duhail wakiwemo nahodha wa zamani wa Moroko Mehdhi Benatia ,Dudu wa Brazil ,mshambulizi wa Tunisia Yousef Msakni na wa hivi punde kuichezea akiwa Mario Mandzukic kabla ya kutamatisha kandarasi yake .

 

Categories
Michezo

Olunga aibuka mchezaji bora MVP ligi kuu Japan

Mshambulizi wa Kenya Michael Olunga ametawazwa mchezaji bora katika ligi kuu ya Japan  kwenye tuzo za ligi hiyo maarufu kama J1  league zilizoandaliwa mapema leo .

Olunga ameshinda tuzo hiyo ya mwanasoka bora wa  mwaka maarufu kama MVP baada ya kuisaidia Kashiwa Reysol kumaliza katika nafasi ya 7 ligini katika msimu wa kwanza baada ya kupandihswa ngazi kutoka J 2 league msimu jana  .

Mshambulizi huyo wa Harambee Stars pia ameshinda tuzo ya mfungaji bora kwa magoli 28 kando na kuchangia mabao 4 kufungwa  na hali kadhalika amejumuishwa katika kikosi cha wachezaji 11 bora wa ligi hiyo msimu huu.

Olunga ndiye  mchezaji wa kwanza asiye wa Japan kutawazwa mchezaji bora baada ya wenyeji kuinyakua  mtawalia tangu mwaka 2012  na anajiunga na wachezaji 8 wa Brazil waliotawazwa mabingwa  awali na mmoja wa Yugoslavia .

Olunga amekiri kujituma msimu huu akiongoza safu ya mashambulizi na pia katika difensi.

“Naamini msimu huu niliweza kutumia nguvu zangu na kasi kujaribu kutumia mianya  iliyokuwa kwenye safu za ulinzi za timu pinzani  na pia nikatumia nguvu zangu kujaribu  kusaidia timu yangu  haswa wakati wa kujihami dhidi ya mikwaju ya  set pieces imenisadia sana”akasema Olunga

Timu ya Kashiwa Reysol ilifunga jumla ya mabao 60 huku Olunga ambaye zamani alikuwa na timu za Tusker Fc,Thika United na Gor Mahia akichangia takriban nusu ya idadi ya magoli hayo yote .

Sadfa ni kuwa Leandro Dominquez wa Brazil ndiye mchezaji wa mwisho wa Kashiwa  Reysol kunyakua tuzo hiyo mwaka 2012 na pia ndiye alikuwa mwanasoka wa mwisho kutoka nje ya Japan kushinda tuzo hiyo kabla ya Olunga kuondoa ukiritimba huo wa Wajapani msimu huu.

 

Categories
Michezo

Olunga aibuka mfungaji bora ligi kuu Japan kwa mabao 28

Michael Olunga Ogada ametawazwa mfungaji bora ligi kuu nchini Japan huku msimu wa ligi hiyo ukifikia tamati mapema Jumamosi akifunga jumla ya mabao 28 ,magoli 10 zaidi Everaldo wa Kashima Antlers .

Olunga alifunga bao lake la 28 katika mechi ya kufunga msimu wakati timu yake ya Kashiwa ilipopoteza mabao 3-2 nyumbani na mabingwa wa ligi Kawasaki Frontale.

Kwa Jumla mshambulizi huyo wa Harambee Stars amefunga bao moja zaidi ya  27 aliyofunga msimu uliopita akiisaidia Kashiwa kupandishwa ngazi hadi ligi kuu kutoka J League 2 .

Kilabu ya Kashiwa ilifunga jumla ya mabao 60 ,na kufungwa  46.

Frontale wametwaa ubingwa wa ligi hiyo kwa pointi 83 wakifuatwa na Gamba Osaka kwa alama 65  wakati Nagoya Grampus ikiibuka ya 3 kwa pointi 63 .

Kashiwa Reysol imemaliza katika nafasi ya 7 kwa alama 52 kutokana na mechi 34 ,wakishinda 15 kutoka sare 7 na kushindwa mechi 12 .

 

Categories
Michezo

Olunga atawazwa mfungaji bora ligi kuu Japan kwa kupiga bao la 27

Mshambulizi wa Harambee Stars Michael   Olunga  amejihakikishia kunyakua tuzo ya mfungaji bora katika ligi kuu  nchini Japan  msimu huu, baada ya kupachika bao la 27 Jumatano adhuhuri na kuisaidia timu yake ya Kashiwa Reysol kuibwaga Sanfrece Hiroshima bao 1-0 ugenini .

Olunga alipachika bao hilo katika dakika ya 17 baada ya kuunganisha pasi ya mshambulizi Hiroto Gaya  na kufyatua tobwe la chini pembeni kulia kutoka ndani ya hatua ya miguu 18 na matokeo hayo kusimama hadi kipenga cha mwisho.

Bao hilo lilimwezesha Engieneer Olunga kusawazisha rekodi ya mabao 27 aliyofunga msimu jana akiwa na timu hiyo katika ligi ya daraja ya kwanza nchini Japan na kumaliza wa pili katika ufungaji mabao,ingawa msimu huu tayari ametwaa tuzo hiyo ya kiatu cha dhahabu kwani  amemwacha mfungaji wa pili bora Everaldo kutoka Kashima Antlers  kwa magoli 10 ikisalia mechi moja msimu ukamilike  .

Kwa jumla Kashiwa imefunga mabao 58 msimu huu katika ligi kuu ,27 kati yake yakifungwa na Olunga ambaye amekuwa na msimu wa kwanza wa  kufana .

Ligi hiyo itakamilika Jumamosi Disemba 19 kwa michuano ya awamu ya 34 ambapo  Kashiwa yake Olunga itakuwa nyumbani dhidi ya mabingwa Kawasaki Frontale.

Hata hivyo Kashiwa tayari imepoteza nafasi ya kufuzu kwa ligi ya mabingwa barani Asia ikiwa ya 7 kwa pointi 52.

 

Categories
Michezo

Olunga anusia taji ya mfungaji bora Japan

Mshambulizi wa Harambee Stars Michael olunga aliendeleza harakati zake za kuwania tuzo ya mfungaji bora katika ligi kuu nchini Japan alipofunga mabao 2 huku akiisaidia timu yake ya Kashiwa Reysol kuicharaza  Vissel kobe mabao 4-3 mapema Jumamosi.

Olunga aliye na umri wa miaka 26 alipachika bao la kwanza katika dajkika 20 kufuatia pasi ya kiungo Cristiano na kuongeza la pili muda mfupi kabla ya mapumziko.

Mshambulizi Ataru Esaka alipachika mabao mengine  mawili  katika kipindi cha pili.

Olunga anaongoza chati ya ufungaji mabao kwa magoli 21 akifautwa na Everaldo wa Kashima na Yu Kobayashi walio na mabao 12 kila mmoja.

Mshambulizi huyo pia liibuka mfungaji bora msimu jana katika ligi ya daraja ya pili nchini Japan akiisaidia  Kashiwa kupandishwa daraja hadi ligi kuu.

Licha ya ushindi wa Jumamosi Kashiwa ingali ya 6 ligini kwa pointi 36 kutokana na mechi 21.

 

 

Categories
Michezo

Wakenya wanaosakata soka ya kulipwa ugaibuni wasajili matokeo mseto wikendi

Nahodha wa Kenya Victor Wanyama amecheza dakika zote 90 mapema leo ,huku timu yake ya Montreal Impact ikiandikisha ushindi wa mabao 4-2 ugenini dhidi ya Vancouver Whitecaps  ligi kuu ya MLS huko Marekani.

Wanyama alicheza dakika zote 90 huku Montreal ikipanda hadi nafasi ya tano ligini katika Eastern Conference wakiwa wamezoa alama 16  kutokana na mechi 10.

Montreal watarejea kuchuana na Vancouver whitecups tarehe 17 mwezi huu.

Wanyama wakisherehekea bao na wenzake mapema leo

Awali hapo jana mshambulizi Michael Olunga alipachika bao la 16 huku timu yake ya Kashiwa Reysol ikiambulia  kichapo cha mabao 2-1 ugenini .

Olunga ndiye mfungaji bora katika ligi kuu nchini Japan kwa mabao 16 kutokana na mechi 16 huku timu yake ikiwa ya 7 ligini kwa pointi 26.

Olunga na Timu yake ya Kashiwa watawaalika Hiroshima jumamosi hii Septemba 19 katika raundi ya 17 ya ligi hiyo

Ligi hiyo inaongozwa na Kawasaki Frontale walio na alama 44.

Olunga baada ya kufunga bao jana

Nchini Misri Ijumaa iliyopita kiungo wa Kenya Cliff Nyakeya alifunga bao la lake la kwanza tangu ajiunge na kilabu ya Fc Masr iliyotoka sare ya mabao 2-2 dhidi ya Al Itihad .

Nyakenya zamani akiwa na Mathare united alicheza dakika 63 kabla ya kupumishwa, na timu yake ingali ya 17 ligini kati ya timu 18 kwa pointi 19 kutokana na mechi 25.

kikosi cha kwanza cha Fc Masr

Fc Masr watarejea uwanjani kesho kwa kuizuru Misri Lel Makassa katika mchuano mwingine wa ligi kuu.

Hatimaye nchini Tanzania Simba sports club ilitoka sare ya bao 1-1 dhidi ya Mtibwa Sugar katika pambano la ligi kuu huku difenda wa Kenya Joash Onyango akicheza dakika zote 90.

 

Categories
Michezo

Olunga afunga lakini wazidiwa nguvu

Fowadi matata wa Harambee Stars Michael Olunga alifunga bao la pekee la kipindi cha kwanza kwa timu yake ya Kashiwa Reysol ,lakini halikutosha huku wakipoteza mabao 1-2 ugenini kwa Sagan Tosu katika mchuano wa ligi kuu Japan ,J1 uliosakatwa mapema leo.

Olunga aliunganisha mkwaju wake Shunki Takahashi katika dakika ya 25 alipofyatua tobwe la chini kwa chini pembeni kulia na kuwaweka Kashiwa Uongozini .

Hata hivyo  Tosu walisawazisha kupitia penati kabla ya mapumziko ,naye Rikki Harakawa akafunga bao la ushindi kwa  wenyeji.

Bao la leo lilikuwa la 16 kwa Oulunga ,ambaye bado anaongoza chati ya ufungaji mabao huku timu yake ikishuka hadi nafasi ya 7 kwa pointi 26 kufuatia michuano 16 ,akiwa na wastani wa kufunga bao moja katika kila mechi.

Kawasaki Frontale wangali kuongoza jedwali kwa alama 44 wakifuatwa na Cerezo Osaka kwa pointi 36 wakati Fc Tokyo ikihitimisha tatu bora kwa alama 32.

Olunga na Timu yake ya Kashiwa watawaalika Hiroshima jumamosi hii Septemba 19 katika raundi ya 17 ya ligi hiyo.

Categories
Michezo

Olunga ashinda tuzo ya mwanasoka bora Japan mwezi Agosti

Mshambulizi wa Harambee stars Michael Olunga ametawazwa mwanasoka bora wa wmezi uliopita katika ligi kuu ya Japan J1.

Olunga alitamba sana akiwa na timu yake ya Kashiwa Reysol  akiwa mbioni kuwania tuzo ya mfungaji bora baada ya kupachika kimiani mabao 15 kutokana michuano 14.

Nyota huyo wa Kenya akipokea tuzo hiyo jana maarufu kama Meijji Yassuda Konami ,aliwashukuru wachezaji wenzake katika timu ya Kashiwa Reysol,na wasimamizi wa timu waliochangia ufanisi huo.

Olunga ambaye zamani alikuwa na Thika United na Tusker Fc  alifungua mwezi Agosti 5 kwa kufunga bao dhidi ya Nagoya Grampus ,na kufunga tena Agosti 8 kwa bao dhidi ya Yokohama  Marinos.

Mshmabulizi huyo pia alifunga bao katika ushinde wa mabao 3-1 nyumbani dhidi ya  Cerezo Osaka na dhidi ya Vissel Kobe  na kisha akafunga mabao mawili wakati timu yake ikipigwa na Kashima Antlers.