Categories
Kimataifa

Kimbunga Lota chawafurusha wakazi 40,000 nchini Nicaragua

Kimbunga kikali kimesababisha mvua kubwa na upepo katika pwani ya Caribbean huko Nicaragua, wiki mbili baada ya dhoruba nyingine iliyosababisha uharibifu mkubwa.

Kimbunga hicho kwa jina Lota, kiliorodheshwa kuwa dhoruba ya daraja la 4 baada ya kutua karibu na mji wa Puerto Cabezas, ambako ilibidi wagonjwa kuhamishwa kutoka  hospitali za muda baada ya paa kung’oka.

Wakaazi wamejenga makaazi ya muda, huku ikihofiwa kwamba kutakuwa na uhaba wa chakula.

Kituo cha kitaifa cha Marekani kuhusu Vimbunga (NHC) kinasema kimbunga cha Lota sasa kimeorodheshwa katika daraja la 2 lakini kimeonya kuhusu  dhoruba zinazotishia maisha ya watu, mafuriko na pia maporomoko ya ardhi.

Kimbunga cha Lota kilifika Nicaragua Jumatatu jioni huku pepo zake zikivuma kwa kasi ya karibu kilomita 250 kwa saa.

Hakukuwa na ripoti zozote za maafa lakini maafisa wanasema karibu watu elfu-40 wamehamishwa kutoka kwenye njia za kimbunga hicho .