Categories
Michezo

Kenya Morans yarejea nyumbani kwa madaha baada ya kufuzu kwa mashindano ya Afrika

Timu ya taifa ya Kenya Morans imerejea nyumbani mapema Jumatano kutoka Yaounde Cameroon ilikoshiriki michuano ya kundi B na kufuzu kwa mashindano ya kuwania kombe la Afrika baian ya Agosti na Septemba mwaka huu nchini Rwanda.

Morans iliandikisha historia kwa kuipiku Angola pointi 74-73 wiki iliyopita katika mchuano wa pili wa kundi B na kujikatia tiketi kwa mashindano hayo ya Afrika kwa mara ya wkanza baada ya miaka 28.

Timu hiyo chini ya ukufunzi wa kocha Liz Mils ililakiwa katika anga tua ya kimataifa ya Jomo Kenyatta muda mfupi baada ya saa nane usiku wa manane na kulakiwa na Rais wa shiriksiho la mpira wa kikapu nchini KBF Paul Otula na Kamishna wa michezo Japson Gitonga.

Hata hivyo ni wachezaji 7 pekee waliorejea nchini huku wengine 6 wakiabiri ndege kurejea ulaya wanakocheza wakiwmeo Tyler Ongwae,Preston Bungei na Joel Awich ,wakati Ariel Okal akisafiri kwenda Oman naye nahodha Griffin Ligare na Victor Ochieng walikuwa wamewasili nchini Jumatatu.

Punde baada ya kuwasilin kocha wa Kenya Liz Mils amesema kuwa alijua Angola ingempa ukinzani mkali baada ya kuchuana nao awalia katika michuano ya zone 6 lakini anajivuni mchezo wa vijana wake na kushukuru KBF kwa kuwa na imani naye licha ya kuwa mwanamke.

“Nilijua Angola watanitatiza kwa kuwa ni timu nzuri baada ya kupambana nao awali katika michuano ya zone 6 lakini najivuni ushindi huo na pia nashukuru shirikisho kwa kuniamini licha ya kuwa mwanamke kuingoza Morans akasema “Mils

Tyler Ongwae alifunga pointi hiyo muhimu huku Kenya ikisajili ushindi wa 74-73 katika sekunde za mwisho kuhakikisha Kenya inajikatia tiketi kwa mashindano hayo ambayo pia yatakuwa ya kufuzu kwa kombe la dunia mwaka 2023.

Timu hiyo inatarajiwa kulakiwa rasmi baadae Jumatano na wizara ya michezo.

Categories
Michezo

Kenya yalenga kufanya vyema FIBA Afrobasket asema kocha Milz

Kocha wa timu ya Kenya ya mpira wa kikapu kwa wanaume Liz Mils amesema analenga kusajili matokeo mazuri kwenye mashindano ya kombe la bara Afrika mjini Kigali Rwanda mwezi Agosti mwaka huu.

Mils ambaye ndiye kocha wa kwanza wa kike kuifuzisha timu ya wanaume kwa mashindano ya FIBA Afrobasket ,amekiri kuwa vijana wake walishindwa na Msumbiji katika mchuano wa mwisho wa kundi B Jumapili kutokana na uchovu baada ya kustahimili ukinzani mkali kabla ya kuilemea Angola pointi 74-73 mjini Yaounde Cameroon na kutinga michuano ya Afrika kwa mara ya kwanza baada ya ya miaka 28.

“Katika mechi ya leo dhidi ya Msumbiji vijana wangu walikuwa wamechoka kufuatia ushindi dhidi ya Angola timu ambayo naiheshimu sana,kikubwa kwetu sasa ni kujitayarisha vizuri ili tusajili matokeo bora mjini Kigali Rwanda”akasema Milz

Milz amesema wanawake wana uwezo wa kufanya vyema na wanapaswa kupewa fursa kuziongoza timu za wanaume.
“Ni wakati mwakafak ambapo pia wanawake wanastahili kupewa nafasi ya kuongoza timu za wanaume,na sisi kama wanawake tunaondoa vikwazo”akaongeza Milz

Kenya ilimaliza ya tatu katika kundi B baada ya kupoteza kwa Senegal na Msumbiji na kuishinda Angola .

Makala ya 30 ya mashindano ya FIBA Afrobasket yataandaliwa Kigali Rwanda baina ya Agosti 24 na Septemba 5 mwaka huu.

Categories
Michezo

Morans wapakatwa na Angola michuano ya kufuzu kwa Fiba Afrobasket

Matumaini ya timu ya taifa ya Kenya katika mpira wa kikapu almaarufu the Morans  kufuzu kwa mashindano ya Fiba Afrobasket mwaka ujao yalididimia baada ya kuambulia kichapo cha pointi 66-83 kutoka kwa Angola katika mechi ya pili ya kundi B  ya  kufuzu, iliyosakatwa Alhamisi Alasiri  katika uwanja wa Kigali  Rwanda.

Morans walipoteza robo ya kwanza ya mchezo pointi 10-18 na ya pili 15-21, lakini wakanyong’oyea zaidi katika robo ya tatu walipocharazwa alama 13-29.

Mabadiliko kadhaa  ya kiufundi kutoka kwa kocha Cliff Owuor yaliimarisha mchezo wa Wakenya  waliojizatiti na kunyakua ushindi katika kwota ya mwisho ya mchezo alama 28-15 ingawa tayari maji yalikuwa yamezidi unga.

Reuben Mutoro na Tyler Ongwae walikuwa wafungaji bora wa pointi kwa Kenya ,kila mmoja akizoa alama 18 .

Nahodha wa kenya Mutoro amesema walicheza vizuri dhidi ya Angola kuliko dhidi ya Senegal huku akiahidi kwamba wataimarisha mchezo wao zaidi dhidi ya Msumbiji Ijumaa “Tulicheza vyema katika mechi ya leo kinyume na  mechi ya Jumatano ,naamini kuwa  tutarudi kufanya utafiti na kujitayarisha vyema dhidi ya Msumbiji  ambao nina imani tutaimarika zaidi na kupata ushindi”akasema Mutoro

“Kwetu sisi mechi ya Msumbiji ni kama fainali tutajituma kwa asilimia 100 kwani hatuna kingine cha kuhofia au kutuzuia na baada ya hapo tutangoja raundi ya pili mwaka ujao”akaongeza Mutoro

Kwa upande wake kocha Owuor amesema kuwa alijaribu kurekebisha makosa mengi waliyofanya dhidi ya Senegal ,walipochuana na Angola na ameahidi kwamba analenga ushindi katika mechi ya mwisho Ijumaa dhidi ya Msumbiji kabla ya kurejea kwa raundi ya pili Februari mwaka ujao.

”Tumekuwa na makosa mengi uwanjani ,ukiangalia tumekuwa tukipoteza mpira kwa urahisi na pia walinzi wetu hawajamakinika ipasavyo,lakini nafurahia mchuano wetu wa leo umekuwa bora kuliko ule dhidi ya Senegal.Kwa sasa tunajiandaa kucheza na Msumbiji tutafute matokeo bora halafu turejee tena Februari mwaka ujao kwa raundi ya pili”akasema kocha Owour

Ushinde wa Morans  dhidi ya Angola ulikuwa wa pili mtawalia katika kundi B kwenye mashindano hayo ,baada ya kulazwa pointi 54-97 katika pambano la ufunguzi siku ya Jumatano.

Hii ina  maana kuwa Kenya ni sharti waishinde Msumbiji katika mchuano wa mwisho Ijumaa hii kuanzia saa kumi na mbili jioni ,ili kuwa na fursa ya kutinga mashindano ya Fiba Afrobasket mwakani nchini Rwanda.

Angola wanaongoza kundi hilo baada ya kushinda mechi ya pili walipowaangusha  Msumbiji Jumatano usiku katika mechi ya kwanza.

Katika mechi ya pili Alhamisi Nigeria imeibwaga Sudan Kusini pointi 76-56  katika kundi D.

Mkondo wa kwanza wa mechi za makundi   utakamilika Jumapili ijayo kabla ya mkondo wa pili kuanza Februari 19 mwaka ujao.

Timu tatu bora kutoka kila kundi baada ya mechi 6 za makundi zitafuzu kwa mashindano ya Fiba Afrobasket mwaka ujao nchini Rwanda.

Categories
Michezo

Morans wanyanyaswa na Senegal 54-92 Fiba Afrobasket nchini Rwanda

Timu ya taifa ya Kenya ya mpira wa kikapu, ilianza vibaya mechi za kufuzu kwa mashindano ya Fiba Afrobasket mjini Kigali Rwanda baada ya kucharazwa pointi 92 -54 katika mchuano uliosakatwa katika uwanja wa Kigali Arena Jumatano jioni.

Kenya maarufu kama Morans walianza vyema pambano hilo ,huku wakilazimisha sare ya alama 19-19 katika robo ya kwanza ya mchezo ,kabla ya kulegea katika robo ya pili walipopoteza alama  14-28  na kisha Morans wakasajili ushindi wa pointi  19-14 katika robo ya tatu ikiwa robo pekee ya mechi iliyoshindwa na Kenya.

Hata hivyo  Morans wanaofunzwa na kocha Cliff Owuor walizidiwa maarifa kwenye robo ya mwisho walipozabwa alama 2-34 wakiwa na makosa mengi ya safu ya ulinzi huku pia wakikosa kumakinika wakati wa kufunga na pia zikiwa alama za chini zaidi walizosajili katika robo moja na pia kufungwa pointi nyingi zaidi .

Licha  ya kocha Owuor kuitisha muda wa mapumziko ili kujaribu kuimarisha mchezo, dau la Kenya lilionekana kuzama kila wakati haswa wakipoteza nafasi nyingi za kufunga alama tatu maarufu kama 3 pointer na pia alama 2.

Katika mchuano huo uliorushwa mbashara na runinga ya Kbc Channel 1 , Tyler Ongwae aliibuka mfungaji bora wa Kenya kwa kuzoa pointi 13 huku Ibrahim Faye akiizolea Senegal alama za juu zikiwa 19.

Vijana wa Morans sasa watakuwa na muda wa chini ya saa 24 kujitayarisha na kurekebisha makosa yao, kabla ya kurejea uwanjani kukabiliana na miamba wa Afrika Angola Alhamisi alasiri na  kufunga ratiba dhidi ya Msumbiji Ijumaa.

Kenya hawana budi kushinda angaa mechi moja ili kuwa na nafasi ya kufuzu kwa fainali za mwaka ujao, ambapo timu tatu bora kutoka kila kundi zitacheza kipute cha Fiba Afrobasket.

Categories
Michezo

Morans wa kenya kufungua kipute cha Fiba Afrobasket dhidi ya Senegal Jumatano

Timu ya taifa ya  mpira wa kikapu  ‘Morans’  itachuana na Senegal Jumatano kuanzia saa kumi na mbili jioni katika mechi ya ufunguzi ya kundi B kwenye michuano ya  kufuzu kwa mashindano ya  kombe la bara Afrika mwaka ujao  maarufu kama Fiba Afrobasket  mjini  Kigali, Rwanda.

Katika mchuano mwingine wa pili wa kundi B  Jumatano ,Msumbiji watashuka uwanjani saa tatu usiku kupambana na Angola.

Morans baade watachuana na Angola Alhamisi na  kisha kuhitimisha ratiba ya  kundi B Ijumaa dhidi ya Msumbiji.

Morans wakicheza na Sudan Kusini katika mechi ya awali uwanjani Nyayo

Kenya ilifuzu kwa mechi hizo baada ya kuwashinda Sudan Kusini  kwenye mechi ya mwisho ya  kufuzu mwaka jana hapa Nairobi.

Morans   inayonolewa na mwalimu  Cliff Owuor ilikuwa imesajili ushindi wa wa pointi 68-66 dhidi Sudan Kusini katika pambano la kujipiga msasa lililoandaliwa Jumanne mjini Kigali.

Mataifa 20 yaliyotengwa katika makundi matano yanashiriki  mashindano hayo huku mabingwa watetezi  Tunisia wakijumuishwa kundi  A pamoja na Jamhuri ya Afrika ya kati, Madagascar na Jamhuri ya Demokrasia ya Congo.

Wenyeji Rwanda wamerundikwa kundi C pamoja na  Nigeria, Mali na Algeria, ilihali kundi E linashirikisha Misri, Morocco, Uganda na Cape Verde.

Mataifa matatu bora kutoka kila kundi yatafuzu kwa mashindano ya kuwania kombe la bara Afrika mwaka ujao mjini Kigali Rwanda .

Ratiba ya kundi B

Kufikia sasa mataifa ya Cameroon, Kodivaa na Equatorial Guinea yamejikatia tiketi kwa kipute cha mwakani  .

Pata uhondo wote wa mechi za Morans kupitia runinga ya taifa KBC Channel one baina ya Jumatatno na Ijumaa hii.

Categories
Michezo

KBC Channel 1 kupeperusha mbashara Fiba Afrobasket

Runinga ya Taifa KBC Channel 1 itapeperusha mechi za makundi za timu ya Taifa ya mpira wa kikapu kwa wanaume al-maarufu Morans kwenye mashindano ya kufuzu kwa michuano ya FIBA Afro Basket mwakani mjini Kigali Rwanda kati ya Novemba 25 na 29 mwaka huu.

Kenya ilishiriki mashindano hayo mara ya mwisho mwaka 1993 jijini Nairobi ikiwa mwenyeji na inalenga kufuzu kwa mara ya pili baada ya kuyakosa kwa takriban mwongo mmoja.

Hata hivyo, ili ifuzu ni sharti imalize miongoni mwa timu tatu bora kutoka kundi B linaloshirikisha Angola, Senegal na Msumbiji.

Morans  watafungua  ratiba ya kundi B dhidi ya Senegal Jumatano hii kuanzia saa kumi na mbili jioni kabla  kurejea uwanjani Kigali Alhamisi  dhidi ya miamba Angola kuanzia saa tisa  na kufunga ratiba dhidi ya Msumbiji Ijumaa kuanzia saa kumi na mbili jioni.

Timu 20 zinashiriki mashindano hayo huku mataifa matatu bora kutoka kila kundi yakifuzu kwa mashindano ya Fiba Afrobasket mwaka  ujao  .

Categories
Michezo

Morans kuondoka nchini kesho kwenda Kigali kwa mashindano ya FIBA Afrobasket

Kikosi cha wachezaji 12 wa timu ya taifa ya mpira wa kikapu maarufu kama Morans  kitakachoshiriki mashindano ya Fiba Afrobasket mjini Kgalia Rwanda kuanzia wiki ijayo  , kimetajwa  huku  mahodha  Griffin Ligare  akitemwa .

Ligare ambaye amekuwa mfungaji wa kutegemewa katika timu ya Morans amelazimika kuachwa nje kutokana na majukumu ya  kikazi huku nafasi yake ikitwaliwa na  mchezaji wa timu ya  Kenya Ports Authority  Victor Odendo.

Kikosi kilicotajwa kinawajumuisha:-

Point guard

Victor Bosire (Ulinzi Warriors)

Eric Mutoro (Ulinzi Warriors)

Shooting guards

Tylor Okari (Bakkan Bears-Denmark)

Fahim Juma (Thunder)

Victor Odendo (KPA)

Small forwards

Valentine Nyakinda  (KPA)

Airel Okal (Algeria)

Fidel Owuor ( Strathmore)

Forwards

Desmond Blacio Owili (Australia)

Preston Bungei (unattached)

Ronnie Gundo( unattached)

Bush Wamukota ( Patriots Rwanda)

Morans itaondoka nchini Jumapili kuelekea Kigali huku wakifungua ratiba ya kundi B  dhidi ya Senegal Jumatano ijayo kabla ya kukabana koo na Angola na kisha Msumbiji.

 

 

 

Categories
Michezo

Morans wanoa makali ya mwisho kwa mashindano ya FIBA Afrobasket nchini Rwanda wiki ijayo

Timu ya taifa ya mpira wa kikapu maarufu kama Morans itafungua kampeini za kuwania kufuzu kwa  mashindano ya AfroBasket dhidi ya Senegal Novemba 25  mjini Kigali Rwanda katika kundi B .

Baadae Morans watamenyana na  Angola Alhmisi ijayo  na kukam,ilisja ratiba dhidi ya Msumbiji tarehe 27 mwezi huu.

Wachezaji wa kulipwa na wale wa humu nchini wamekuwa kwenye kambi ya mazoezi katika uwanja wa Nyayo  kwa Zaidi ya majuma mawili yaliyopita .

Timu hiyo inayoongozwa na kocha mkuu Cliff Owuor  itapunguzwa hadi kusalia wachezaji  12 watakaosafiri kwa mashindano hayo ya Rwanda .

Baadhi ya wanandinga wa kulipwa walio kambini ni  Desmond Owili wa kutoka Australia, Bush Wamukota  aliye Rwanda  na Tyler Okari kutoka  Denmark .

Hata hivyo kwa mjibu wa Rais wa shirikisho la basketiboli nchini KBF  Paul Otula wanakabiliwa na changamoto ya kifedha swala ambalo litatatuliwa na  kamati ya watu 10 iliyoundwa kuchangisha fedha za kuisaidia timu.

“Hii kamati tumeunda  ya watu  10 ambayo ina majukumu ya kuchangisha na kukusanya takriban shilingili milioni 15 zinazohitajika kwa timu hiyo”akasema Otula

Mataifa 20 yaliyotengwa katika makundi 5 ya timu nne kila moja yatashiriki mashindano ya kufuzu ya Fibaafrobasketball nchini Rwanda kati ya Novemba 24 na 29 mwaka huu.

Timu tatu bora kutoka kila kundi zitajikatia tiketi kwa mashindano ya FIBA Afrobasketball mwaka ujao nchini Rwanda.