Categories
Michezo

Simba wa Atlas wahifadhi kombe la CHAN baada ya kuwazima Mali

Atlas lions ya Moroko ilifanikiwa kuhifadhi kombe la bara Afrika kwa wachezaji wanaosakata soka katika ligi za Nyumbani maaru kama CHAN baada ya kuwagaragaza Mali mabao 2-0 katika fainali iliyopigwa Jumapili usiku katika uwanja wa Ahmadou Ahidjo mjini Yaounde Cameroon.

Fainli hiyo ilisimamiwa na refarii wa Kenya Dkt Peter Waweru ambaye ni mhadhiri  katika chuo kikuu cha JKUAT akisaidiwa na mwenzake Gilbert Cheruiyot huku pia akiandikisha historia kuwa Mkenya.

Baada ya kipindi cha kwanza kumalizikia sare tasa kipindi cha pili timu zote zilirejea kwa lengo la kusaka magoli lakini kipa Anas Zniti wa Moroko alikuwa ange na kuzima mashambulizi yote ya Mali.

Soufiane Bouftini aliwaweka Moroko uongozini kwa bao la dakika ya 69 akiunganisha mkwaju wa kona naye Ayoub El Kaabi akaongeza la pili dakika ya 79.

Moroko waliokuwa wamenyakua kombe hilo kwa mara ya kwanza mwaka 2018 wakiwa wenyeji, ndiyo timu ya kwanza kuhifadhi kombe hilo huku ikiwa mara ya pili kwa Mali kupoteza katika fainali baada ya kushindwa na DR Congo mwaka 2016 nchini Rwanda.

Soufiane Rahimi wa Moroko aliibuka mfungaji bora kwa mabao 5,lakini Yakoub El Kaabi  pia kutoka Moroko akaweka rekodi ya kuwa mfungaji bora tangu kuanza kwa mashindano ya CHAN  mwaka 2009 akifunga mabao 12 kwa jumla.

Rahimi pia alituzwa kuwa mchezaji bora wa michuano ya mwaka huu nchini Moroko .

Makala ya mwaka 2022 ya CHAN  yataandaliwa nchini Algeria.

Categories
Michezo

Moroko walenga kuhifadhi kombe la CHAN

Moroko inadhamiria kuwa timu ya kwnaza kihifadhi kombe la CHAN  itakaposhuka uwanjani  Ahmadou Ahidjo  mjini Yaounde kwenye  fainali ya makala ya 6 ya kombe hilo dhidi ya Mali.

Timu zote zinajivunia kutopoteza mechi tangu kuaza kwa kinyang’anyoro hicho  wakati Mali wakiwinda kombe la kwanza nao Moroko wakisaka kombe la pili baada ya kutwaa ubingwa mwaka 2018.

Moroko wamekuwa wakitisha tangu mechi ya mwisho ya kundi lao  ikiwemo kuwacharaza Uganda mabao 5-2,kuilima  Cameroon mabao 4-0 katika nusu fainali wakati Mali wakishinda kupitia penati katika robo na nusu fainali.

Mchuano huo utasimamiwa n refarii wa Kenya Dkt Peter Waweru ikiwa fainali ya kwanza ya kombe hilo kusimamia ,na mchuano wa tatu kwenye mashindano ya CHAN mwaka huu.

Waweru atasaidiwa na Mkenya mwenza Gilbert Cheruiyot.

Categories
Michezo

Mali yafuzu fainali ya CHAN baada ya kuwaangusha Guinea penati 5-4

Mali ilijikatia tiketi kwa fainali ya makala ya 6 ya mashindano ya kombe la CHAN nchini Cameroon baada ya kuwazidia nguvu majirani Guinea magoli 5-4 kupitia mikiki ya penati kufuatia sare tasa baada ya dakika 120 katika nusu fainali iliyosakatwa uwanjani  Japoma mjini Doula Jumatano usiku.

Pande zote zilikuwa na nafasi chungu nzima za kupachika magoli huku mikwaju ya Yakhouba Gnagna Barry,Alpha Oumar Sow,Victor Kantabadouno na Morlaye Sylla ikipanguliwa wakati pia Mali wakipoteza nafasi za wazi kupitia kwa Yacouba Doumbia,Moussa Ballo ,Siaka Bagayoko  na  Issaka Samake.

Timu zote zilimaliza sare tasa baada ya dakika 120 huku Guinea wakifunga penati kupitia kwa Yakhouba Gnagna Barry,Ismael Camara,Ousmane Camara  na Mamadouba Bangoura huku ile ya mwisho iliyochongwa na  mmchezaji wao nyota Morlaye Sylla  ikipanguliwa na kipa wa Mali.

Mali waliunganisha mikwaju yote mitano kwa mechi ya pili mtawalia baada pia ya kuibwaga Congo katika robo fainali penati 5-4.

Penati za Mali zilitiwa kimiani na  Issaka Samake ,Moussa Kyabou,Makan Samabaly,Sadio Kanoute na Mamadou Coulibaly.

Guinea ukipenda Syli  Nationale  watacheza mechi ya kuwania nafasi ya tatu na nne Jumamosi usiku .

Categories
Michezo

Mali yatinga nusu fainali ya CHAN baada ya kuilaza Congo 5-4

Mali walijikatia tiketi kwa nusu fainali ya CHAN kwa mara ya pili katika historia baada ya kuwabandua Congo mabao 5-4 kupitia mikwaju ya penati kwenye nusu fainali ya kwanza iliyochezwa Jumamosi usiku uwanjani Ahmad Ahidjo mjini Doual Cameroon.

Timu zote zilishindwa kutumia vyema nafasi zao za kupachika magoli huku makipa wakiwa ange na kuzima mashambulizi na kulazimisha kipindi cha kwanza na cha pili kuishia sare tasa.

Mkenya Dkt Peter Waweru aliyesimamia pambano hilo aliamurisha kupigwa dakika 30 za ziada ambazo pia ziliishia sare ndiposa penati zikapigwa kutenganisha timu hizo.

Mikwaju ya penati ilipigwa huku ile ya Congo ikifungwa na Julfin Ondongo, Hardy Binguila, Yann Mokombo na kipa  Pavelh Ndzila huku Prince Mouandzu Mapata akipiga mkwaju wake nje.

Mali waliunganisha penati zote 5 kupitia kwa Issaka Samake, Moussa Kyabou, Makan Samabali, Mamadou Doumba na  Mamadou Coulibaly  ikiwa mara ya pili kwa timu hiyo kufuzu nusu fainali baada ya kufanya hivyo kw amara ya kwanza mwaka 2016 nchini Rwanda.

Mali watapambana katika nusu fainali na mshindi kati ya Guinea na Rwanda watakaovaana kwenye robo fainali ya mwisho Jumapili usiku.

 

Categories
Michezo

Cameroon na Mali watoshana nguvu huku Burkina Fasso ikiwatimua Zimbabwe CHAN

Wenyeji Cameroon maarufu kama Indomitable Lions na Flying Eagles ya Mali  zilitoka sare  ya bao 1-1   katika uwanja wa Ahidjo Ahmadou mjini Doula,mchuano  wa kundi A uliochezwa Jumatano usiku .

Cameroon walitangulia kufunga bao katika dakika ya 6  kupitia kwa Salomon Bindjeme 2 kabla ya Issaka Samake kuisawazishia Mali kunako dakika 12 na kipindi cha kwanza kumalizika kwa sare ya 1-1.

Timu zote zilicheza kwa tahadhari kuu huku mchuano ukimalizika kwa sare ya bao 1-1.

Matokeo hayo yanamaanisha kuwa timu zote zina fursa ya kufuzu kwa robo fainali zikiwa na alama 4 kila moja huku wakimaliza mechi zao Jumapili ijayo  ambapo Cameroon watacheza na Burkinafasso huku Mali wakihitimisha ratiba dhidi ya  Zimbabwe.

Katika pambano la pili Jana usiku Zimbabwe inayofunzwa na kocha Zdravko Lugarisic ilikuwa timu ya kwanza kubanduliwa katika mashindano ya mwaka huu baada ya kupoteza mabao 3-1 kwa Burkina Fasso  katika uwanja wa Ahidjo Amadou.

Issouf Sosso alifungua ukurasa wa magoli kwa Burkinafasso katika dakika ya 14 kabla ya Partson Jaure kusawazisha katika dakika ya 23 na kipindi cha kwanza kuishia sare ya 1-1.

Claver Kiendrébéogo aliwarejesha Burkinafasso uongozini kwa bao la pili dakika 53 naye Issiaka Ouédraogo kupachika bao la tatu dakika ya 67.

Cameroon wangali kuongoza kundi hilo kwa pointi 4 sawa na Mali wakifuatwa na Burkina Fasso kwa alama 3 wakati Zimbabwe ikiwa bila alama.

Mechi mbili za kundi B kupigwa Alhamisi Libya wakifungua ratiba dhidi ya Congo DR nao Niger wacheze na Congo Brazaville saa nne usiku.

 

 

Categories
Michezo

Cameroon na Mali zawinda nafasi ya robo fainali

Wenyeji Indomitable Lions ya Cameroon na Flying Eagles ya Mali watakuwa wakiwania tiketi ya kwanza kucheza robo fainali ya makala ya 6 ya kombe la CHAN watakapopambana Jumatano usiku katika mchuano wa kwanza wa raundi ya pili uwanjani Ahidjo Amadou  mjini Yaounde Cameroon.

Timu hizo zitakutana katika mechi ya kundi A ikiwa ni mara ya pili katika historia baada ya Cameroon kuwashinda Mali bao 1-0 katika makala ya CHAN mwaka 2011 nchini Sudan.

Mataifa yote yaliafungua makala ya mwaka huu ya CHAN kwa ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Zimbabwe na Burkinafasso Jumamosi iliyopita huku pia ikisadifu magoli yote kufungwa kuanzia dakika za 70  na 72 .

Kocha wa Mali Nahoum Diane’ ambaye ana uzoefu mkubwa atajaribui kutumia vyema safu yake ya ushmabulizi na mabeki ili kupata matokeo huku Indomitable Lions pia wakijivunia safu imara ya nyuma.

Sare pia itafaidi pande zote na kuwafuzisha robo fainali endapo mchuano wa pili kati ya Burkinafasso na Zimbabwe utaishia sare.

Categories
Michezo

Mali waipakata Burkina Fasso 1-0 CHAN

Mali maarufu kama the Flying Eagles walifungua mechi yao ya Chan mwaka 2021 kwa ushindi baada ya kuilaza Burkina Fasso bao 1-0 katika pambano la kundi A lilipoigwa Jumamosi usiku katika uwanja wa Ahmadou Ahidjo mjini Younde Cameroon.

Derby hiyo ya Afrika Magharibi iliishia sare tasa katika kipindi cha kwanza huku pande zote zikibuni nafasi haba za kupachika mabao.

Burkinabe walipoteza nafasi za wazi za kufunga magoli huku mikjwaju ya Soumaila Quattara, Illias Tiendrebeogo na  Clement Pitroipa ikipanguliwa huku  Demba Diallo akipoteza nafasi ya mwaka upande wa  Mali .

Hata hivyo kufuatia bishabisha za muda mrefu kipindi cha pili Mali walipata bao kupitia kwa mshambulizi Siaka Bagayoko  aliyeunganisha mkwaju wa kona kwa kichwa iliyochongwa na Issaka Samake na kumwacha kipa wa Burkibabe  Babayoure Aboubacar Sawadogo akiduwaa.

Bao hilo la dakika ya 70 lilitosha kuwapa Mali ushindi mhimu na alama tatu na kujiongezea matumaini ya kuingia hatua ya nane bora.

Mali watarejea uwanjani Jumatano ijayo dhidi ya wenyeji Cameroon ,pambano ambalo huenda liamue atakayeongoza kundi hilo huku washinde wa Jumamosi Zimbabwe na Burkina Fasso wakichuana katika mechi nyingine ya Kundi A .

Categories
Michezo

Mali washiriki CHAN kwa mara ya 4

Timu ya taifa ya Mali maarufu kama the Eagles inashiriki fainali za 6 za kombe la CHAN zitakazoanda Jumamosi hii nchini Cameroon kwa wakicheza michuano hiyo kwa mara ya 4 wakijivunia kumaliza katika nafasi ya 2  mwaka 2016 nchini Rwanda.

Mali inajivunia wachezaji kadhaa watakaoshiriki CHAN kwa mara ya pili   akiwemo beki Mamadou Doumbia aliye na umri wa miaka 25 aliyecheza fainali ya mwaka 2016 wakipoteza kwa DRC.

Kocha Nouhoum Diane analenga kunyakua kombe hilo kwa mara ya kwanza .

The Eagles waatacheza mechi ya ufunguzi Jumamosi usiku dhidi ya Burkinafasso katika kundi A kabla ya kucheza na wenyeji Cameroon na hatimaye Zimbabwe.

Categories
Michezo

Tunisia na Mali zafuzu AFCON mwaka 2022 nchini Cameroon

Tunisia na  Mali zilifuzu kwa fainali za kombe la AFCON mwaka 2022 nchini Cameroon baada ya mechi za raundi ya 4  hatua ya makundi kukamilika Jumanne usiku.

Tunisia maarufu kama  The Carthage Eagles walijikatia tiketi licha ya kutoka sare ya bao 1-1 ugenini dhidi ya Tanzania jijini Daresalaam.

Saif Eddine aliwaweka Tunisia uongozini katika kipindi  cha kwanza kabla ya Feisal Salum kuwarejesha wenyeji mchezoni kwa bao la kusawazisha huku akiweka hai matumaini ya Tanzania kufuzu wakipanda hadi nafasi ya tatu kwa alama 4.

Sare hiyo iliwaweka Tunisia uongozini pa kundi  J kwa pointi 10 kutokana na mechi 4 .

Mjini Windhoek,The Eagles ya  Mali walijikatia tiketi baada ya kulazimisha ushindi wa mabao 2-1 ugenini dhidi ya Namibia  katika kundi A ,wakiwa na alama 10,pointi mbili Zaidi ya Guinea 9 iliyo ya pili.

Baada ya kukamilika kwa mechi za mzunguko wa nne mataifa yaliyofuzu kwa kinyang’anyiro cha 32 cha kombe la Afcon  ni  wenyeji Cameroon,Teranga Lions ya Senegal ,Desert Foxes kutoka Algeria,Tunisia na Mali huku michuano ya makundi ikikamilika Machi 30 mwakani.

 

 

Categories
Kimataifa

Huenda jumuiya ya ECOWAS ikaiondolea Mali vikwazo

Jumuiya ya kiuchumi ya eneo la Afrika magharibi, ECOWAS imeashiria kwamba huenda vikwazo dhidi ya Mali vikaondolewa hivi karibuni.

Hayo ni kulingana na arafa iliyokuwa kwenye ukurasa wa twitter wa rais wa muda wa Mali.

Jumuiya ya  Ecowas iliiwekea nchi hiyo vikwazo hivyo vya kuiadhibu baada ya jeshi kumng’atua rais  Ibrahim Boubacar Keïta mwezi Agosti mwaka huu.

Ilishinikiza kurejeshwa kwa utawala wa kiraia lakini licha ya rais wa kiraia,  Bah Ndaw, na waziri mkuu, Moctar Ouane, kuteuliwa, vikwazo hivyo bado havijaondolewa.

Mapema juma hili, rais Muhammadu Buhari wa Nigeria alisema kuwa kungali na maswala yanayohitaji kusuluhishwa kabla ya mahusiano kurejea katika hali ya kawaida.