Categories
Michezo

Kothbiro kutinga nusu fainali Alhamisi

Mashindano ya soka ya kila mwaka ya  Kothbiro yataingia hatua ya nusu fainali  katika uwanja wa Ziwani kaunti ya Nairobi  siku ya Alhamisi .

 

Dallas All Stars kutoka Muthurwa  ilitinga nusu fainali baada ya kuwapachika Kajiado All stars 2-1 kwenye robo fainali,Asec Huruma wakawatema  Biafra Kamaliza ya wadi ya  Kiambio 2-1 robo fainalini.

Kwa mjibu wa mshirikishi wa mashindano hayo Paul Ojenge  licha ya changamoto kadhaa makala ya mwaka huu yamekuwa na ufanisi mkubwa  hususan tangu kupokea ufadhili kutoka kwa kampuni ya Betmoto.
“Licha ya changanoto kdhaa zilizoshuhudiwa hadi sasa mashindano yamekuwa na ufanisi mkubwa  na ningependa kuchukua fursa hii  kuzipongeza timu zilizosalia mashindanoni kwa kudhihirisha ukakamavu na ukomavu.pia niwashukuru wadhamini wetu Betmoto  ambao wamefufua upya mashindano haya “akasema Polosa
Meneja wa mauzo wa Betmoto  ambaye pia ni mchezaji wa zamani wa timu ya taifa ya Charles Cardovillis amesema kuwa maswala tata yaliyokuwepo kwenye mashindano hayo tayari yametatuliwa keulekea kwani fainali ya Jumapili hii.
“Tumekutana na timu zote na ndio maana tulikuwa tumeahirisha mashindano haya .Tunataka kucheza soka na kila mmoja anataka kuendelea na soka ikiwemo timu za mwaka jana .
Tatizo kubwa lilikuwa ni kukatika kwa mawasiliano  kutoka kwa waandalizi  hatua iliyokera timu zilizokosa kutuzwa mwaka jana  ikionekana kuwa walikuwa wakitoa ahadi hewa.
Kama Betmoto tumekubaliana kulipa sehemu ya zawadi ya pesa za mwaka jana huku waandalizi wakilipia gharama itkayosalia  kwa sababu ya maslahi ya mchezo”akasema Cardovillis
Kothbiro ni mashindano ambayo huandaliwa kila mwaka mtaani Ziwani na ni mojawapo wa mashindano makongwe zaidi nchini.
Categories
Michezo

Kothbiro yapata ufadhili wa muda mrefu kutoka Betmoto

Mashindano ya kila mwaka ya kuwania kombe la Koth Biro yataingia hatua ya 16 bora Jumapili Disemba 27 katika uwanja wa Ziwani Nairobi.

Kulingana na mshirikishi wa mashindano hayo Paul Ojenge maarufu kama Polosa  wanatarajia kucheza fainali ifikiapo Januari mosi mwaka ujao.

Kama mashindano mengi humu nchini Kothbiro pia yamekabilia na changamoto ya ufadhili hatua iliyochangia washindi wa mwaka jana kukosa kupewa zawadi ,lakini mwaka huu hali ni tofauti baada ya kampuni ya Betmoto kujitolea kuyapiga jeki.

“Timu zile zilijisajili zilikuwa zaidi ya 40 na Jumapili tunaingia round of 16 pale Ziwani na tumepata changamoto timu zile zilishinda last year hazikupata zawadi yao na wamekuwa wakiingia kwenye pitch na kuwalazimu sponsers kujiondoa ,hata hivyo mwaka huu tunafurahia kupata Betmoto ambao watatoa fedha na uniforms na tutacheza fainali Januari 1 mwaka ujao”akasema Polosa

 

Charles Cardovillis ambaye ni mchezaji wa zamani wa timu ya taifa ya raga amejitosa katika usimamizi wa michezo baada ya kustaafu  na amekuwa katika mstari wa mbele kuhakikisha makala ya mwaka huu ya Kothbiro yanapata ufadhili.

Hata hivyo kulingana na Cardovillis changamoto ya ukosefu wa  ufadhili ni hatua ya waandalizi wengi wa mashindano kutoandaa miswaada mizuri.

“Challenges na sponsership ni discipline vile watu wanatumia pesa na kukosa ile accountability  na pia hatujui kuweka pamoja ile proposal kumshawishi mfadhili kuwa atapata return on investment,lazima tuonyeshe wafadhili watafaidika kupitia mashindano “akasema Cardovillis

 

Betmoto itatoa sare kwa kila timu na pia kutoa pesa zitakazoshindaniwa mwaka huu na gharama ya usalama na marefa  asemavyo Cardovillis .

“Mashindano hayo yana alot of traditions na licha ya Betmoto kuwa itaanza shughuli zake mwaka ujao lakini tumeamua kusaidia kukuza soka ya mashinani ili kukuza vipaji”akasema Cardovillis

Mashindano hayo yatashirikisha kaunti zote 47 kuanzia mwaka ujaoa ambapo timu zitacheza mchujo   huku mabingwa wa kila kaunti wakikutana kwenye mashindano ya kitaifa.

“Lazima tuingie mashinani wacha tusaidie hawa vijana ili wakigrow watawasaidia wengine,tumeingia hapa tutasaidia Kothbiro na tumesaini mktaba wa muda mrefu na tunayapeleka katika kaunti zote 47  na lazima tumalizie Ziwani”akaongeza Cardovillis.

Kama njia moja ya kukuza michezo nchini kiwango cha mashinani kampuni ya Betmoto inanuia kushirikiana na fani zote za michezo nchini viwango vya mashinani.

Kulingana na Joe Kimani ambaye ni Mkurugenzi wa Betmoto  watasaidia mashindano hayo kwa muda mrefu ,huku pia wakiazmia kuangalia ndondi ,Voliboli  na raga.

“lakini kwa hiyo harakati tukaskia kuna Koth Biro na kwa kuwa objective yetu ni kusupport grassroot football na hata tukianza shughuli zetu hapa nchini Mid Next month tutaekezea zaidi katika michezo mashinani”akasema Kimani

Koth Biro ni mashindano ya soka yaliyoanzishwa mwaka 1978 kwa lengo la kutambua na kukuza talanta kwa timu za mitaa ya Nairobi.