Categories
Burudani

Nandy na Billnass wameachana

Wanamuziki Nandy na Billnass wametengana baada ya uhusiano wa kimapenzi wa muda mrefu. Mara ya kwanza kwa watu kukisia kwamba mambo sio mazuri, ni wakati Nandy alijitokeza kutangaza kwamba pete ya uchumba aliyovishwa na Billnass ilikuwa imepotea.

Wengi walihisi kwamba Nandy alivua pete hiyo mwenyewe lakini amekuwa akijitetea akisema kwamba alivuliwa na mashabiki bila kujua kipindi cha kutumbuiza kwenye mikutano ya Kampeni mwaka jana.

Mara nyingine ni wakati alikwenda kumlaki mwanamuziki Koffi Olomide kwenye uwanja wa ndege yapata mwezi mmoja uliopita na alikuwa amemwalika kwa ajili ya kufanya kibao naye.

Nandy hakuwa na Billnass jinsi wengi walitarajia lakini Nandy alisema kwamba mpenzi huyo wake alikuwa naye kwenye mipango yote hata ingawa hakuonekana huko kwenye uwanja wa ndege.

Baadaye Nandy na Koffi walitumbuiza tena kwenye tamasha lililokuwa limeandaliwa na Clouds Media kwa ajili ya siku ya wapendanao lakini Billnass hakuonekana huko. Mamake Nandy alipohojiwa siku hiyo alisema mambo kati ya wanawe yalikuwa sawa na alikuwa anasubiri tu wampe siku ya arusi.

Billnass na Nandy

Siku ya kuzindua kibao chake na Koffi kwa jina “Leo Leo” kwenye kipindi cha “Leo Tena” cha Clouds Tv Billnass pia hakuonekana na Nandy aliendelea tu kumtetea akisema anamuunga mkono kwa kazi yake.

Nandy mwenyewe alitangaza utengano wake na Billnass wakati alikuwa anajibu shabiki mmoja ambaye alimwita mke wa Billnass kwenye picha aliyopachika kwenye Instagram.

Shabiki huyo kwa jina carinamarapachi aliandika “Mrs Billnass love uu more” naye Nandy akamjibu “Single”.

Categories
Burudani

Pete ilipotea!

Mwanamuziki Nandy amelezea sababu kuu ya kukosa kuonekana na pete aliyovishwa na Billnass baada ya kuchumbiwa mwaka jana.

Akihojiwa na runinga ya Clouds nchini Tanzania jana alikokwenda kwa ajili ya kuzindua wimbo wake na Koffi Olomide “Leo Leo” mwanadada huyo alisema kwamba pete hiyo ilipotea.

Kulingana naye, mashabiki walimvua pete hiyo mwaka jana wakati ule wakitumbuiza kwenye kampeni za chama cha CCM. Alihisi akiguswa mkono mashabiki walipokuwa wakiwashangilia wakiondoka jukwaani lakini alipofika kwenye gari ndio aligundua kwa kweli ameipoteza.

Mtangazaji aliyekuwa akimhoji alitaka kujua ni kwa nini asivishwe nyingine au mpaka sherehe ifanyike kama ile ya kwanza ambapo alisema anahisi Billnass anasubiri arusi yao ikikaribia kabisa ndio amvishe nyingine.

Billnass alimvisha Nandy pete ya uchumba mwezi Aprili mwaka 2020 wakati alikuwa jukwaani akiimba kwenye TVE ambapo alimwambia kwamba amekuwa naye muda mrefu, amejua upande wake mzuri na mbaya na amechagua kupenda pande hizo mbili.

Nandy baada ya kuvishwa pete hiyo aliandika, “Sina mengi ya kuandika hapa sababu nimeyamaliza yote mbele ya uso wako! Safari ndio kwanza inaanza MUNGU wetu ni mkuu sana alituvusha na hata hili tutavuka salama! Asanteni wote kwa hongera mlizo nipa na kwa kuangalia pia show ya HOMA tuko pamoja more blessings.”

Mwezi wa nne mwaka 2018 wapenzi hao watiwa mbaroni kwa kile kinachosemekana kuchapicha picha ambazo hazifai kwenye mitandao ya kijamii.

Categories
Uncategorised

Leo Leo – Nandy

Hatimaye mwanamuziki wa Tanzania Nandera maarufu kama Nandy amezindua kibao chake na mwanamuziki wa Congo Koffi Olomide.

Uzinduzi huo ulifanyika jana kupitia runinga ya Clouds Tv kwenye kipindi kwa jina “Leo Tena” ambacho kinakaribia kufananisha jina na kibao hicho, “Leo Leo”.

Kwenye matangazo kabla ya uzinduzi huo kauli mbiu ilikuwa, “Leo leo kwenye leo tena” maneno yaliyoingiana kishairi.
Kwenye wimbo huo, Koffi ameimba ubeti mzima na ameimba maneno aliyotunga kwa ajili ya wimbo huo kinyume na alivyofanya kwenye wimbo wake na Diamond Platnumz kwa jina “Waah”.

Kwenye Waah, alifanya kurudia maneno ambayo tayari alikuwa ameyatumia kwenye nyimbo zake zingine na hata kuyaimba kwa mtindo ule ule.

Kwa kawaida, wanamuziki huenda kwenye vituo vya runinga au redio kuzindua vibao vyao lakini Nandy alifanya tofauti, alialika watangazaji wa runinga hiyo ya clouds nyumbani kwake.

Aliunda eneo kama jukwaa rasmi kwa ajili ya kuzindua kibao hicho chake. Eneo hilo lilikuwa limepambwa kwa rangi ya pinki na picha yake na Koffi ilikuwa nyuma ya walikokuwa wameketi ikiwa na tarehe ya uzinduzi wa kibao chao.

Nandy ameweka wimbo huo kwenye akaunti yake ya You Tube na unaweza kuusikiliza hapa;

.

Categories
Burudani

Idris Sultan atania Nandy na Koffi

Muigizaji na mchekeshaji wa nchi ta Tanzania Idris Sultan ametania wasanii wa muziki Nandy wa Tanzania na Koffi Olomide wa nchi ya Congo.

Alichukua picha ya pamoja ya wasanii hao wawili na kuandika, “Ni wajibu wetu kama watanzania kuhakikisha tunalinda mali zote za kitanzania na hatuziachi katika hali yoyote hatarishi. UZALENDO sio jambo la kuonea aibu kabisa.”

Anajaribu kutetea Nandy mtanzania mwenzake asije akanyakuliwa na Koffi kuelekea Congo ila ni utani tu kwani picha hiyo walipigwa wakitayarisha video ya wimbo wao ambao utazinduliwa wakati wowote kutoka sasa.

Baadaye Idris alipachika picha yake akisinzia huku ameketi na kuongeza utani dhidi ya Koffi. .

Anasema; “Nimeshtuka usiku baada ya kukumbuka kitu “Koffii si anatoka kwenye source ya vumbi la Congo?” Mungu wanguuuuuu… Narudi kulala”

Vumbi la Congo ni dawa fulani ya kuongeza nguvu za kiume.

Idris Sultan wa umri wa miaka 28 alipata umaarufu nchini Tanzania na Afrika baada ya kushinda shindano la Big Brother mwaka 2014.

Baada ya hapo aliingilia uchekeshaji, uigizaji na utangazaji wa redio ambapo aliongoza kipindi kwa jina, “Mji wa Burudani” kwenye kituo cha redio kiitwacho Choice Fm.

Amewahi kujipata pabaya kutokana na maigizo yake kwenye mitandao ya kijamii kiasi cha kutiwa mbaroni kwa kosa la kuharibia watu jina au kuwaonyesha visivyo.

Categories
Burudani

Rhumba la Wapendanao!

Mwanamuziki Koffi Olomide kwa mara nyingine atakuwa nchini Tanzania kwa ajili ya tamasha la kabla ya siku ya wapendanao ulimwenguni almaarufu “Valentine’s day”.

Tangazo la tamasha hilo limetolewa na kampuni ya mawasiliano ya Clouds nchini Tanzania kupitia kwa mtangazaji wake Babu wa Kitaa.

Mtangazaji huyo aliamua kuvaa sketi akifanya tangazo hilo huku akijitetea kwamba hata nchini Scotland wanaume huvalia sketi hasa kwa sherehe kubwa.

Clouds Media ni mshindani wa Wasafi Media na kampuni hizo mbili zinaonekana kufuatana katika kumwalika Koffi nchini Tanzania.

Mwisho wa mwaka jana, Koffi alialikwa nchini Tanzania na Diamond Platnumz mmiliki wa Wasafi Fm ambapo walifanya colabo moja kali kwa jina Waah ambayo imependelewa sana kwenye mitandao.

Wakati huo, Koffi hakutumbuiza kwenye tamasha lolote lililoandaliwa na Wasafi bali alihojiwa tu wakati wakizindua kibao chao.

Maajuzi amerejea Tanzania kwa ajili ya kufanya kazi ya video ya wimbo wake na The African Princess almaarufu Nandy kazi ambayo hawajazindua hadi sasa.

Nandy huwa anahusishwa na Clouds Media na huenda kibao hicho chao kwa jina “Leo” kikazinduliwa kwenye tamasha hilo la Jumamosi tarehe 13 mwezi februari mwaka huu wa 2021 katika eneo la Mlimani City, Jijini Daresalaam nchini Tanzania.

Wawili hao wamekuwa wakichapisha tu picha ambazo zinadhaniwa kutokana na video ya kibao chao.

Kituo cha redio cha Clouds Fm kimetayarisha wasifu wa Koffi Olomide ambapo wanaelezea kwamba hata kama alizaliwa kwa familia yenye uwezo, alipata wakati mgumu kujijenga katika fani ya muziki.

Wanafichua pia kwamba ana majina ya utani 35!

Categories
Burudani

Nandy aangukia ubalozi wa sodo

Mwanamuziki wa Tanzania Nandy ambaye hujiita ‘The African Princess’ sasa ndiye balozi wa sodo za chapa ya “Flowless” ambazo zinapatikana kwa soko la Tanzania.

Tangazo hilo lilitolewa jana alhamisi na kampuni ya kuunda sodo hizo kwa kikao na wanahabari ambapo Nandy alikuwa na akatia saini makubaliano ya kazi hiyo ya ubalozi.

Sio mara ya kwanza kwa Nandy kufanya kazi na kampuni hiyo ya kuunda pedi za Flowless kwani mwaka jana yapata mwezi wa tano, picha yake ilitumika kwenye mabango ya mauzo ya pedi hizo.

Akizungumza baada ya kutia saini makubaliano hayo, Nandy alisifia sodo hizo akisema mwanamke anayezitumia anaweza kufanya jambo lolote bila kuogopa wakati wa hedhi.

Wasimamizi wa kampuni hiyo walisema walimchagua Nandy kwa sababu ni mwanamke ambaye anajiamini, jasiri na ambaye hakati tamaa maishani.

Alijipatia fursa hiyo pia kwa jinsi amekuwa akijulikanisha ujio wa pedi hizo ambazo zilizinduliwa rasmi mwaka jana 2020.

Nandy pia anaendeleza kazi nyingine kama hiyo kwa bidhaa ya sabuni kutoka kwa kampuni inayojulikana kama Azania. Ameonekana kwenye picha za mauzo za sabuni hiyo ya unga kwa jina King Limau.

Nandy ambaye jina halisi ni Faustina Charles Mfinaga, alizaliwa mwezi Novemba mwaka 1992 nchini Tanzania na alianza rasmi kazi ya muziki mwaka 2013.

Kazi hii yake imewadia wakati mashabiki wake wanasubiria kwa hamu kazi ya muziki kutoka kwake kwa ushirikiano na Koffi Olomide wa Congo.

Categories
Burudani

Mgeni Njoo mwenyeji apone!

Ndiyo hali ambayo imejitokeza wazi kwenye ziara ya Koffi Olomide nchini Tanzania ambako alikuwa amealikwa na “The African Princess” Nandy.
Koffi alitua nchini Tanzania usiku wa kuamkia Jumanne tarehe 26 mwezi huu wa Januari mwaka 2021 ambapo alilakiwa na Nandy kwenye uwanja wa ndege.

Baadaye Nandy aliweka video kwenye akaunti yake ya Instagram akiwa kwenye meza ya maankuli pamoja na Mopao na watu wengine huku akimpakulia Mopao chamcha.

Mwanamuziki huyo alisifiwa sana kwa kuonyesha hulka za mke nyumbani lakini akajipata pabaya kutokana na vyombo vyake ambavyo wengi walionelea sio vya mtu wa hadhi yake.

Mfuasi wake mmoja kwa jina Cleo.Doctor anamwandikia, “Kumbe na mastaa mnatumia mapoti kama yetu”. Mwingine anayejiita Selu_Jo akamwandikia, “Ma super star jamani hata table mats hakuna….dah mnaboa sana …table setting ovyo kabisa”.

Lakini hali hiyo imegeuka na kuwa baraka kwake kwani sasa amepatiwa vyombo bure kutoka kwa maduka ya kuuza vyombo nchini Tanzania.

Nandy alipachika video kwenye akaunti yake ya Instagram ikionyesha mpangilio wa baadhi ya vyombo hivyo vipya vya kuvutia, vingine vikiwa vya dhahabu.

Kwenye mojawapo ya video akipokea vyombo hivyo, Nandy anasikika akigusia jinsi amechambwa kwenye mitandao mpaka sasa imebidi awe makini sana. Anasikika akisema anatamani kukimbia chumbani aone kama kitanda kiko sawa kabla kionekane na wote.

Koffi alikwenda Tanzania kwa ajili ya kufanya video ya wimbo wake na Nandy.

Categories
Burudani

Koffi olomide arejea Tanzania

Mwanamuziki tajika mwa nchi ya Congo Koffi Olomide kwa mara nyingine amerejea Tanzania na zamu hii hajakwenda kule kwa ajili ya Diamond Platnumz bali amekwenda kufanya kazi na mwanamuziki wa kike Nandy.

Nandy ambaye wengi humrejelea kama “African Princess” anasemekana kurekodi sauti ya kibao chake pamoja na Koffi awali na sasa kazi iliyosalia ni ya kurekodi video.

Usiku wa kuamkia leo, Nandy na anaofanya kazi nao walimlaki Koffi katika uwanja wa ndege nchini Tanzania, ambapo Koffi alifungua begi na kumkabidhi Nandy zawadi ambayo inaonekana kama marashi japo Mopao alikataa kusema ni nini haswa akisema ni zawadi toka moyoni.

Wawili hao walitangaza kufanya kazi pamoja mwaka jana hata kabla ya kazi ya Diamond na Koffi, na wengi wanahisi imechelewa lakini Nandy ameelezea kwamba walitaka wimbo wao kwa jina “Leo” uwe mzuri zaidi na ndio maana wamechukua muda.
Nandy amesema pia kwamba alitaka kazi iwe ya uzuri wa hali ya juu kwenye video na ndio maana amechukua muda kukusanya fedha za kufadhili kazi hiyo yao.

Alipohojiwa kwenye uwanja wa ndege, Mopao alisema anampenda Nandy kwa sababu anaimba vizuri na ana sauti nzuri.
Wawili hao huenda pia wakaandaa tamasha nchini Tanzania.

Mwaka jana Mopao alikuwa nchini Tanzania kwa ajili ya kufanya kazi pamoja na simba au ukipenda Diamond Platnumz. wimbo wao kwa jina Waaah uliandikisha historia kwa kutizamwa kwa wingi kwenye mtandao wa Youtube ndani ya siku chache tu.

 

Categories
Burudani

Shishi Baby aomba ukuu wa Wilaya

Mwanamuziki na mjasiriamali wa nchi ya Tanzania Zena Yusuf Mohamed maarufu kama Shilole au ukipenda Shishi Baby ametoa ombi kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania John Pombe Magufuli.

Wakenya wanamfahamu dada huyo kutokana na video iliyosambazwa awali kwenye mitandao ya kijamii ambapo alishindwa kutamka neno, “Subscribe”.

Mwanadada huyo ambaye anamiliki mkahawa kwa jina Shishi Food anasema anatamani sana kuwa mbunge lakini kwa sasa anaomba Rais ampe ukuu wa wilaya.

Amewahi kuwa mwenyeji wa watu mashuhuri kwenye mkahawa huo wake, wa hivi punde zaidi akiwa mwanamuziki tajika wa Congo, Koffi Olomide.

Shishi anakubali kwamba hana kisomo, aliachia darasa la saba, lakini ana kipaji cha uongozi na ikiwa Rais ataona vyema ampatie kazi hiyo ya kusimamia wilaya.

Mwanamuziki huyo alitaja Mkuu wa Wilaya ya Kisarawe Bi. Jokate Urban Mwegelo wa miaka 33 ambaye awali alikuwa mtangazaji na mfanyibiashara akisema ikiwa atapatiwa kazi ataifanya kama anavyoifanya Jokate kwa kujitolea.

Siku za hivi karibuni Shilole amekuwa akijitahidi sana kujitafutia yeye na binti zake pale ambapo amekuwa akitangazia kampuni kadhaa biashara zao na inaaminika kampuni hizo zinamlipa vizuri.

Amekuwa pia akihusishwa kwenye tamasha linaloendeshwa na wasafi media ya Diamond Platnumz almaarufu “Tumewasha na Tigo”.

Alijihusisha pia kikamilifu na kampeni za chama cha CCM kabla ya uchaguzi mkuu na sasa inasubiriwa kuona ikiwa Rais Magufuli ataridhia ombi lake.

Categories
Burudani

Sihitaji walinzi nalindwa na Mungu, Koffi Olomide

Mwanamuziki wa muda mrefu wa nchi ya Congo Koffi olomide au ukipenda Le Grand Mopao au Boss ya Mboka amefichua kwamba yeye huwa hatembei na walinzi kwani anaamini kwamba analindwa na Mungu.

Koffi aliyasema hayo kwenye studio ya Wasafi Fm wakati yeye na Diamond Platnumz walikuwa wanazindua kibao chao kwa jina “Waaa”.

Hapo hapo kwenye kipindi cha ‘The Switch’ ilifichuka kwamba Koffi ana ujuzi wa kiwango cha juu katika mchezo wa Karate maanake ana “Black Belt”.

Alisema kwamba akikasirika yeye huwa mbaya na anaweza kuumiza mtu na ndio maana wakati wote anajituliza na kupoesha hasira.

Ama kweli ana ujuzi huo ikikumbukwa teke aliyomrushia mmoja wa wacheza densi wake katika uwanja wa ndege nchini Kenya kitendo kilichosababisha atimuliwe hata kabla ya onyesho lake.

Boss ya Mboka anatarajiwa kuendelea kukaa nchini Tanzania kwa muda kulingana na usemi wa Diamond kwamba ana video nyingine anafaa kuandaa.

Duru za kuaminika zinaarifu kwamba video hiyo ni ya kibao cha Koffi na Nandy au ukipenda African Princess. Wakati wa mahojiano Koffi alifichua kwamba ameshirikiana pia na Nandy kwenye muziki na dada huyo amekuwa akimsukuma wafanye video lakini akampa Diamond nafasi ya kwanza.

Alipoulizwa kuhusu kitu ambacho amependa sana nchini Tanzania, Koffi alisema kwamba ni wanawake ambao kulingana naye ni warembo.

Tukio jingine ambalo linatarajiwa kumweka Koffi nchini Tanzania ni ziara inayofanywa na Wasafi Media kwa ushirikiano na Tigo na Pepsi ambapo Diamond alimwalika kwenye ziara ya mwishi mjini Daressalaam. Jana mwanamuziki huyo alikwenda kwenye mkahawa wa Shilole kwa jina Shishi food kwa chakula cha mchana.