Mwanaume ambaye aliwabaka bintize wawili katika kaunti ya Kirinyaga, amehukumiwa kifungo cha miaka 140 gerezani.
Akitoa hukumu hiyo, hakimu mkuu Anthony Mwicigi alidokeza kwamba mshakiwa huyo ameharibu maisha ya wasichana hao wawili pamoja na ya watoto wao akisema anapaswa kuondolewa kabisa katika jamii.
Kwa mujibu wa Mwicigi, wasichana hao wamepokonywa usalama na dhamani yao ya maisha na mtu ambaye alipaswa kuhakikisha siku zao za usoni ni salama.
Mshatikiwa huyo kwa jina John Gichira ambaye ni wa dini ya Akorino kutoka kijiji cha Kathaka, alitiwa nguvuni mwezi uliopita baada ya shangazi mmoja wa wasichana hao wawili kuripoti kisa hicho katika kituo cha polisi cha Sagana.
Mmoja wa wasichana hao ana mtoto wa miezi saba na huyo mwingine ama uja uzito wa miezi sita.
Alipokuwa akijitetea mbele ya mahakama hiyo, mshtakiwa huyo John Gichira Gichini aliomba msamaha kutoka kwa mahakama hiyo pamoja na familia yake kutokana na kitendo hicho, akilaumu shetani kwa kumpotosha.
“Ninasikitika sana kwa jinsi nimekosea familia yangu na ninaomba mahamaka hii inisamehe kwani kila binadamu anaweza kosea,” alisema Gichini.
Awali kiongozi wa mashtaka aliwasilisha fomu ya P3, ripoti za ukaguzi wa kimatibabu na kadi za ubatizo kuunga mkono kesi hiyo.