Categories
Michezo

Omolo asajiliwa na Erzrum BB yaUturuki

Kiungo wa Kenya Johanna Omolo amejiunga na klabu ya Buyuksehir Belediye Erzurumspor  inayoshiriki ligi kuu Uturuki  kutoka  Cercle Brugge  ya Ubelgiji ambako amecheza kwa mismu minne  iliyopita.

Omolo anatarajiwa kujumuishwa katika kikosi cha timu yake mpya Alhamisi itakapochuana na  katika kombe la Uturuki dhidi ya Alanyaspor.

Klabu ya Erzrum BB ilitangaza usajili wa kiungo huyo kupitia kwa mtandao wa twitter Jumatano usiku akiwa Mkenya pekee anayesakata soka ya kulipwa nchini Uturuki kwa sasa.

Hata hivyo kiung huyo anakabiliwa na kibarua kigumu cha kuisaidia Erzrum BB kusalia ligini msimu ujao wakiburura mkia kwa alama13 baada ya michuano 18.

Omolo atakuwa mchezaji wa pili kutoka Afrika Mashariki kupiga soka ya kulipwa nchini Uturuki baada ya Ally Mbwana Samatta ambaye ni nahodha wa Tanzania kusajiliwa na Fernabahce mwanzani mwa msimu.