Categories
Michezo

Onyango kucheza hatua ya makundi ya klabu bingwa Afrika kwa mara ya kwanza

Beki Kisiki Joash Abong’o  Onyango wa Kenya alijiunga na mabingwa wa Tanzania klabu ya Simba na ndani ya msimu wake wa kwanza ameifuzisha timu hiyo kucheza hatua ya makundi kuwania kombe la ligi ya mabingwa Afrika .

Onyango aliye na umri wa miaka 27 aliichezea Western Stima kati ya mwaka 2015 na 2016 kabla ya kujiunga na Gor Mahia tokea mwaka 2017 hadi 2019.

Akiwa Gor Onyango alicheza mechi za mchujo za klabu bingwa lakini kwa miaka yote miwili Gor walishindwa kufua dafu  kucheza hatua ya makundi ya klabu bingwa   wakibanduliwa na baade kufaulu kucheza hatua ya makundi ya kombe la shirikisho.

Onyango alipiga dakika zote 90 katika uwanja wa Benjamin Mkappa jijini Daresalaam Jumatano jioni  na kuisaidia Simba Sc kuikung’uta  Platinum ya Zimbabwe mabao 4-0 huku wakifuzu  hatua ya makundi kwa mara ya pili  na ya kwanza tangia mwaka 2003.

Ishara moja iliyo bayana ni kuwa kuna vitu majirani zetu wamenya sahihi kuinua kiwango cha ligi yao na hata timu ya taifa,Simba pia ndicho klabu pekee kutoka East Afrika kutinga hatua hiyo msimu huu.

Angesalia Kenya kutokana na viwango vya mchezo vilivyo chini ,huenda Onyango angestaafu bila kucheza soka katika kiwango hicho .

Wakenya wengine waliofuzu kucheza hatua hiyo ya makundi ya klabu bingwa Afrika ni Brian Onyango Mandela akiwa na Mamelodi Sundowns ya Afrika Kusini na  Athony Akumu aliye Kaizer Chiefs pia ya Afrika Kusini.