Categories
Michezo

Timu ya marathon ya olimpiki yapata ufadhili wa sh Milioni 1

Timu itakayowakilisha Kenya katika mbio za marathon kwenye michezo ya Olimpiki ya Tokyo Japan baina ya julai na Agosti mwaka huu imepokea ufadhili wa shilingi milioni 1 kupiga kambi ya mazoezi kujiandaa kwa mashindano hayo

Timu ya marathon kwa michezo ya Olimpiki inawajumuisha bingwa mtetezi kwa wanaume Eliud Kipchoge, mshindi wa nishani ya shaba ya dunia mwaka 2019 Amos Kipruto, bingwa wa Boston na Chicago Marathon Lawrence Cherono, na bingwa wa Vienna City marathon Vincent Kipchumba .

Wanawake watakaolekea Tokyo Japan ni pamoja na bingwa wa dunia Ruth Chepngetich,bingwa mara mbili wa Londona marathonna mshikikizi wa rekodi dunia Brigid Kosgei, Ruth Chepngetich ,bingwa wa dunia na mshikilizi wa rekodi ya dunia ya nusu marathon Peres Jepchirchir na bingwa wa Olimpiki katika mita 5000 mwaka 2016 Vivian Cheruiyot.

kutoka kushoto , naibu kiongozi wa timu ya Kenya SHoaib Vayani, koingozi wa timu ya kenya Waithaka Kioni, Rais wa NOCK Paul Tergat, Ruth Chepngetich, Meneja wa Kenya Barnaba Korir na meneja wa timu ya riadha ya kenya Ben Njoga

Rais wa kamati ya Olimpiki Kenya Paul Tergat ametoa hakikisho kuwa timu hiyo itapata usaidizi wote na maandalizi wanayohitaji kwa mashindano hayo.

“Kama NOCK tutahakikisha timu inapata mavazi ya kutosha na kwa wakati ufaao ,hatutaki kuwa na vijisababu Olimpiki ni mashidnnao muhimu hata mimi nimekuwa huko kwa wakati mmoja na nafahamu hisia ambazo mwanariadha huwa nazo” akasema Tergat

Categories
Michezo

Mashindano ya Paris kufuzu kwa Olimpiki yafutwa

Mashindano ya mwisho ya ndondi , kufuzu kwa michezo ya Olimpiki ya mwaka huu, yaliyoratibiwa kuandaliwa mwezi Juni mwaka huu  jijini Paris Ufaransa yamefutiliwa mbali.

Tangazo hilo lilitolewa na kamatai ya kimataifa ya Olimpiki IOC ,jopokazi la masumbwi BTF linamaanisha kuwa nafasi 53 zilizokuwa ziwaniwe na mabondia  katika mashindano hayo ya kufuzu sasa zitagawanywa kwa kuzingatia uoredheshaji wa mabondia.

Hatua hii ina maana kuwa bondia anayeorodheshwa bora kutoka kila bara katika kila uzani ndio watapewa tiketi hizo za Olimpiki ambao ni 32 za wanaume na 21 kwa wanawake.

Kwa mjibu wa mkurugenzi wa mawasiliano katika shirikisho la masumbwi nchini Kenya BFK Duncan Kuria  bara la Afrika litapata  nafasi 13 huku Kenya ikinuai kupata angaa nafasi mbili kuelekea Tokyo baina ya mwezi Julai na Agosti.

“Tuna imani kuwa tutapa angaa nafasi 2 katika uzani wa welter kwa wanawake na uzani wa Heavy ambapo naona kuwa Elizabeth Akinyi na Elly Ajowi waliomaliza katika nafasi za tatu kwenye mashidnano ya kufuzu yaliayoandaliwa mwaka mmoja uliopita mjini Dakar Senegal “akasema Kuria

Mabondia 11 wa Kenya walikuwa mazoeizini katika ukumbi Lavington  kujiandaa kwa mashindano hayo ya kufuzu Olimpiki.

kenya iliwakilishwa na mabondia watatu kwenye makala ya mwaka 2016 ya michezo ya olimpiki mjini Rio De Janeiro Brazil.

Tayari mabondia Christine Onagre na Nick Okoth wamefuzu  kwa michezo hiyo itakayoandaliwa kati Julai 23 na Agosti  8 mwaka huu mjini Tokyo Japan.

Categories
Michezo

Timu ya Kenya ya Olimpiki yapigwa jeki na KCS

Timu ya Kenya itakayoshiriki makala  ya 32 ya michezo ya Olimpiki  imepigwa jeki baada ya kamati ya Olimpiki nchini NOCK kusaini mkataba wa miaka mitano na kampuni ya kamari ya Kenya Charity Sweepstake  ,mkataba wa kima cha shilingi milioni 10.

Pesa hizo zitatumika kuiandaa timu ya Kenya kwa michezo ya mwaka huu ya Olimpiki kuanzia Julai 23 mjini Tokyo Japan na Olimpiki ya mwaka 2024  mjini Paris Ufaransa .

Rais wa Nock Paul  Tergat ana imani kuwa pesa hizo zitaiwezesha timu ya Kenya kupata maandalizi bora .

“Kwa miaka  iliyopita,na haswa mwaka huu tumekuwa na matayarisho mazuri kwa michezo ya Olimpiki tukilenga ufanisi . Ndio maana tunawaomba wakenya wote kutuunga mkono  ili tupate  matokeo bora mwaka huu “akasema Tergat

Kulingana na mkataba huo asilimia 10 ya pato kutokana kwa Kenya Charity Sweepstake  itawekwa katika akaunti ya NOCK.

Jumla ya wanamichezo 83 wa Kenya wamefuzu kwa michezo hiyo wakiwemo  wanariadha 17,mchezaji Taekwondo mmoja,mabondia wawili,timu raga kwa wachezaji 7 upande kwa wanaume na wanawake,na timu ya voliboli kwa akina dada kila timu ikiwa na wachezaji 12 kwa jumla wakiwa 36.

Kenya italenga kuboresha matokeo ya  mwaka 2016  mjini Rio De Janeiro ilikozoa dhahabu 6 fedha 6 na shaba 1 na pia matokeo bora zaidi iliyowahikusajili mwaka 2008 mjini Beijing ya dhahabu 6 fedha  4 na shaba 6.

 

 

 

 

 

 

 

 

 

Categories
Michezo

Michezo ya Olimpiki haitaahirishwa kamwe 2021 asema Bach

Rais wa kamati ya kimataifa ya Olimpiki IOC Thomas Bach amesesitiza kuwa kamwe micheoz ya Olimpiki ya mwaka huu haitaahirishwa bali itaanza ilivyopangwa Agosti 23 mwaka huu mjini Tokyo Japan.

Akizungumza mapema Alhamisi  kwenye mahojiano ya runinga na Kydo News ,Bach amesema kuwa IOC haina mpangilio mbadala wa michezo hiyo na hakuna kisuizi chochote kwa michezo hiyo.

“Tumejitolea kwa wakati huu,na hakuna sababu yoyote ya kuamini kuwa michezo hiyo haiytaandaliwa mjini Tokyo Japan kuanzia Agosti 23  katika uwanja wa Olympic mjini Tokyo,” akasema Bach

“Hii ndio maana hatuna mpango mbadala  na tumejitolea  kufanikisha michezo michezo na kuhakikisha imefanyika”akaongeza Bach

Imeabinika kuwa Tokyo wamasimama kidete kuwa hawataahirisha michezo hiyo kutokana na gharama kubwa iliyotumika kwa maandalizi huku pia michezo ya olimpiki ya majira ya baridi mwaka 2022 ikikaribia mjini Beijing.

Michezo ya Olimpiki makala ya 32 ilipaswa kuandaliwa kuanzia Julai 23 mwaka uliopita kabla ya kuahirishwa hadi mwaka huu kutokana na mkurupuko wa ugonjwa wa Covid 19.

Categories
Michezo

Kenya kutuma wanamichezo 100 Olimpiki

Kamati ya Olimpiki nchini Kenya inalenga kutuma takriban wanamichezo 100 kwa makala  ya 32 ya michezo ya Olimpiki  ya mwaka huu mjini Tokyo Japan.

Kulingana na kiongozi wa ujumbe wa Kenya Waithaka Kioni wanamichezo ambao wamefuzu kwa michezo hiyo ni 87 kutoka fani za riadha,Raga kwa wachezaji saba kila upande wanaume na wanawake,ndondi na voliboli wanawake.

Wachezaji watakaofuzu watapiga kambi ya maozezi kabla ya kuelekea Japan huku pia Nock ikiahidiwa usaidizi wa kutosha kutoka kwa serikali.

“Tumekutana na serikali kupitia kwa wizara ya michezo mara kadhaa na wametuhakikishia kutoa usaidizi wote tunaohitaji kuelekea kwa michezo hiyo,hadi sasa tuna wanamichezo 87 waliofuzu huku tukilenga kutuma angaa wanamichezo 100 kwa hiyo michezo”akasema Kioni

Kenya ilimaliza ya 15 katika michezo ya Olimpiki ya  mwaka 2016 mjini Rio De Janeiro kwa dhahabu 6 fedha 6 na shaba 1.

Categories
Michezo

Michezo ya Olimpiki kuendelea ilivyopangwa

Michezo ya Olimpiki ya mwaka huu mjini Tokyo Japan itaendelea mbele ilivyopangwa kwa mjibu wa waziri mkuu wa Japan Yoshihide Suga.

Makala ya 32 ya michezo ya Olimpiki yameratibiwa kuanza Julai 23 mwaka huu ikifuatwa na Olimpiki ya walemavu mwezi mmoja baade .

Hofu ilikuwa imetanda nchini Japan endapo michezo hiyo itaendelea mbele au itaahirishwa kufuatia kuongezeka kwa visa vya ugonjwa wa Covid 19 ambapo kwa mara ya kwanza zaidi ya  visa 1000 vya maambukizi viliripotiwa nchini humo Disemba 31 mwaka jana.

Yoshihide Suga ametoa hakikisho kuwa michezo hiyo itaendelea ilivyopangwa  .

Japan imenakili visa  239,041 vya maambukizi ya coronavirus na vifo  3,337 tangu kuzuka kwa gonjwa hilo sugu.

 

Categories
Michezo

Breakdance kushirikishwa Olimpiki kwa mara ya kwanza mwaka 2024

Kamati ya Olimpiki nchini Nock imepongeza hatua ya kamati ya kimataifa  ya Olimpiki ya kuidhinisha mchezo wa breakdance kujumuishwa katika orodha ya fani za michezo  ya Olimpiki ya mwaka 2024 jijini Paris Ufaransa.

Mchezo huo utafahamika kama Breaking  kinyume na breakdance jinsi wengi wanavyoufahamu.

Breaking ni mmoja wa  fani tatu za michezo zilizopendekezwa na kamati andalizi ya IOC kujumuishwa kwenye olimpiki ya mwaka 2024 ikiwemo  skateboarding, sport climbing na upigaji makasia .

Breaking ilijumuishwa katika michezo ya olimpiki kwa chipukizi mwaka 2018 mjini  Buenos Aires, Argentina, na umeidhinishwa kuwa mchezo wa Olimpiki na baraza kuu la IOC Disemba 7 mwaka huu.

Breakdance imekuwa ikifanyika humu nchini kwa jina la  streetdance ikiendehswa na kundi lijulikanalo  Streetdance Kenya jijini  Nairobi kabla ya kuenea kote nchini ..

Mchezo huo unasimamiwa na shirikisho la dunia la  michezo ya kupiga densi maarufu kama World Dance Sports Federation.

 

 

Categories
Michezo

Nock yazidisha maandalizi kwa michezo ya 32 ya Olimpiki

Matayarisho ya wanaspoti wa Kenya kwa michezo ya Olimpiki yanaendelea vyema licha ya janga la Covid 19.

Kulingana na Rais wa kamati ya Olimpiki nchini Nock Paul Tergat, zaidi ya wanaspoti 80 wamefuzu kwa michezo hiyo ya mwaka ujao mjini Tokyo Japan  huku uteuzi kwa nafasi zilizosalia  ukitarajiwa kuandaliwa mapema mwaka ujao.

“Kufikia sasa tuna takriban wanamichezo 80 waliofuzu wakiwemo wale wa timu za raga kwa wachezaji 7 kila upande  wanuame na wanawake na timu ya akina dada ya Voliboli,na tunatarajia kuteua wanaspoti waliosalia mapema mwaka ujao”akasema Tergat

Kulingana na Tergat janga la Covid 19 limeilazimu kamati ya Olimpiki Nock kuongeza bajeti ya michezo hiyo  kutoka kwa bajeti ya awali.

Hii ni kutokana na baadhi ya mashindano ya  uteuzi  kuahirishwa na pia kwa minaajili ya matayarisho kwa timu zilizofuzu kwa michezo hiyo.

“Kwa sasa itabidi tuongeze kiwango cha bajeti ambayo tumewasilisha kwa Serikali tukisubiri iidhinishwe kwa sababu kila kitu kimebadilika kuliko tulivyopanga awali,kuna uteuzi mwingine ambao tutafanya upya,na pia wanamichezo waliofuzu wanahitaji kujiandaa vyema”akaongeza Tergat

Michezo ya Olimpiki iliyokuwa iandaliwe mwaka huu ,iliahirishwa kutokana na janga la Covid 19 na sasa makala ya 32 ya michezo hiyo yataandaliwa kati ya Julai 23 hadi Agosti 8 mwaka ujao.

Uwanja wa Tokyo utakaondaa michezo ya Olimpiki mwaka ujao

Katika makala yaliyopita ya olimpiki mwaka 2016 huko Rio De Janeiro Brazil  Kenya iliwakilishwa na wanimichezo 89 katika fani 7 za michezo na kuzoa medali 13,dhahabu 6 fedha 6 na shaba 1.

Wanamichezo waliojikatia tiketi kwa michezo hiyo ya mwaka ujao  kufikia sasa ni pamoja na mabondia wawili mshindi wa nishani shaba ya jumuiya ya madola

Christine Ongare  katika uzani wa Fly na Nick Okoth katika uzani wa unyoya  Faith Ogalo, katika  tae kwon-do ,timu za raga kwa wachezaji 7 kila upande kwa wanaume na wanake,timu ya Voliboli ya akina dada pamoja  uogeleaji.

Mabondia Nick Okoth na Cristine Ongare wakipiga zoezi

Tergat pia ameipongeza serikali kwa kuingilia kati na kunusuru jengo la Nock Plaza lililoko Upper Hill  ambalo lilikuwa litwaliwe na wapiga mnada baada ya Nock kushindwa kulipia ada ya ujenzi na gharama nyinginezo.

“Tunafurahia kuwa Serikali iliingilia kati na kunusuru jengo letu la Nock Plaza na kulipa pesa zote  tulizokuwa tunadaiwa ,auctioneers walikuwa wametaka kutwaa jengo hilo mara kadhaa na ingekuwa vibaya kama lingenyakuliwa na waekezaji wa kibinafsi” akasema Tergat

 

 

Categories
Michezo

Viwanja vya Olimpiki ya baridi mwaka 2022 mjini Beijing kukamilika mwishoni mwa mwaka huu

Waaandalizi wa michezo ya Olimpiki ya majira ya baridi mwaka 2022 Beijing wameafikiana  kwa kauli moja kufanya vipimo vya COVID 19 mara kwa mara kwa wachezaji na maafisa wa kamati ya kimataifa ya Olimpiki IOC,kamati ya Olimpiki kwa walemavu IPC na mashirikisho  ya kimataifa ya michezo .

Kamati ya michezo ya Olimpiki ya majira  ya baridi  mwaka 2022  jijini Beijing ,  na IPC kwa kauli moja wamekubaliana kubuni na kuhakisha kuna vipimo ya mara kwa mara kwa kabla ya michezo hiyo .

Hali ya sasa ulimwenguni kuhusu msambao wa Covid 19 imesababisha kufungwa au kuzuiwa kwa safari hali ambayo huenda ikaendelea hadi mwaka 2022 wakati wa michezo ya Beijing .

Viwanja vya Beijing vitakavyotumika kuandaa michezo hiyo vinatarajiwa kukamilika kujengwa ifikiapo mwishoni mw amwaka huu  na imezua haja ya kuwepo kwa vipimo hivyo vya Covid 19 vya mara kwa mara ili kuhakisha michezo hiyo haihatarishwi na  ugonjwa huo.

 

Categories
Kimataifa

Iran yamnyonga Navid Afkari licha ya shinikizo za kimataifa za kutotekeleza adhabu hiyo

Iran imemnyonga mwana mieleka mmoja aliyepatikana na hatia ya mauaji baada ya kuupuza wito wa jamii ya kimataifa wa kutotekeleza adhabu hiyo ya kifo dhidi yake.

Navid Afkari, mwenye umri wa miaka 27, alihukumiwa kifo baada ya kupatikana na hatia ya kumuua mlinzi mmoja wakati wa wimbi la maandamano dhidi ya serikali mwaka wa 2018.

Shirika la habari la Iran lilipeperusha moja kwa moja kukiri kwa Navid kutekeleza mauji hayo.

Hata hivyo Navis alisema aliteswa ili kukiri mauaji ya mlinzi huyo kulingana na wakili na familia yake.

Wakili wake alisema hakukuwa na ushahidi kwamba Navid alitekeleza mauaji hayo.

Idara ya mahakama ya Iran ilipuuzilia mbali madai kwamba Navid aliteswa.

Navid Afkari na ndugu zake walikuwa wameajiriwa katika kampuni moja ya ujenzi eneo la Shiraz kilomita  680 kusini mwa jiji kuu Tehran.

Mahakama ya mkoa wa Shiraz pia iliwahukumu ndugu zake  Navid ambao ni Vahid Afkari na  Habib Afkari kifungo cha miaka  54 na 27  gerezani mtawalia.

Wakili wa Afkari alilaumu utawala kwa kutokubalia familia ya mteja wake kumtembelea kabla ya kumnyonga jinsi inavyohitajika kisheria.

Chama kinachowakilisha wanariadha 85,000 duniani ni miongoni mwa wale waliotaka hukumu hiyo kusitishwa.

Shirika la michezo duniani kwa upande wake limesema Navid alilengwa na serikali ya taifa hilo maksudi kwa kuhusika kwenye maandamano hayo, na limetoa wito taifa hilo lisiruhisiwe kushiriki mashindano yeyote ya kimataifa.

Rais wa Marekani Donald Trump aliitaka Iran kumsamehe mwanamieleka huyo akisema kosa lake lilikuwa tu kushiriki kwenye maandamano dhidi ya serikali.

Kamati ya kimataifa ya olimpiki IOC imetaja kutekelezwa kwa hukumu hiyo ya kifo dhidi ya Navid kama tukio la kuhuzunisha na imeitakia familia yake faraja.