Categories
Michezo

Mkufunzi wa makipa wa Gor Mahia Willis Ochieng ajiuzulu

Mkufunzi wa  makipa katika klabu ya Gor Mahia Willis Ochieng amejiuzuluzu kutoka wadhfa  huo baada ya kuhudumu kwa miaka minne .

Ochieng alitwaa nafasi hiyo kutoka kwa Mathews Otomax na amesema amejiuzulu kwa sababu za kifamilia .

Ochieng ameishukuru Kogalo kwa kumpa fursa ya kuitumikia .

Gor imekuwa ikikumbwa na kashfa za upangaji matokeo ya mechi  hivi maajuzi hatua iliyoilazimu timu hiyo kuanza uchunguzi kuhusu madai hayo.

Ochieng ameitaka Gor Mahia kumlipa mshahara wake wa miezi 14 .

Categories
Michezo

Gor wazidi kutota ligini baada ya kushindwa na Posta Rangers

Mabingwa watetezi wa ligi kuu ya Kenya Gor Mahia waliendeleza msururu wa matokeo duni ligini baada ya kuambulia kichapo cha pili mtawalia walipolazwa na Posta Rangers bao 1-0 katika mojawapo wa mchuano wa ligi uliosakatwa katika uwanja wa Kasarani Jumatano alasiri.

Kiungo Francis Nambute alipachika bao la pekee la ushindi kwa Rangers dakika ya kwanza ya ziada katika kipindi cha kwanza, huku Kogalo wakipoteza nafasi  nyingi za kusawazisha  hadi kipenga cha mwisho.

Ilikuwa mechi ya pili mtawalia kwa Gor kupoteza na ya sita msimu huu baada ya ksuhindwa na  KCB mabao 2-0 mwishoni mwa juma lililopita.

Gor Mahia ingali ya 8 ligini kwa pointi 19  na watarejea uwanjano Machi 21 dhidi ya Bidco United.

Rangers kwa upande wao wamepanda hadi nafasi ya 14 kwa alama 14 kufuatia ushindi huo.

Katika pambano jingine la Jumatano Zoo Fc ya Kericho na Western Stima walitoka sare tasa katika uwanja wa Kericho Green.

Categories
Michezo

Gor Mahia watajilaumu kwa kushindwa kufuzu hatua ya makundi

Mabingwa wa ligi ya Kenya Gor walipoteza uongozi wa mabao 2-1 ugenini katika uwanja wa Heroes mjini Lusaka dhidi ya NAPSA All Stars na kutoka sare ya magoli 2-2 Jumapili jioni matokeo yaliyozima ndoto ya Gor kutinga hatua ya makundi ya kombe la shirikisho la soka Afrika kwa mara ya pili katika historia.

Gor maarufu kama Kogalo walikuwa waliongoza mabao 2-1 kufikia mapumzikoni ,magoli yao yakipachikwa wavuni na Samuel Onyango kunako dakika ya 17 kabla ya Austin

Banda kuwarejesha wenyeji mchezoni dakika moja baadae naye Clifton Miheso akatikisa wavu kwa goli la pili dakika ya 20.

Kipindi cha pili kilisalia kigumu kwa timu zote kabla ya mwamuzi kuwapa wenyeji penati ya dakika ya 96 iliyofungwa na Emmanuel Mayuka na kuwafuzisha Napsa kwa hatua ya makundi huku Gor wakifeli kuingia hatua hiyo.

Kabla ya mchuano huo Kogalo walikumbwa na masaibu si haba ikiwemo mgomo wa wachezaji na kusafiri kuelekea Lusaka wakiwa wamechelewa.

Ni funzo kwa wasimamizi kujaribu kuweka mambo sawa kwenye timu hiyo ili irejelee matokeo mazuri .

Categories
Michezo

Pamzo ateuliwa kocha msaidizi wa Gor Mahia

Sammy ‘Pamzo Omollo’ ameteuliwa kuwa naibu kocha wa mabingwa wa Kenya Gor Mahia .

Omollo, ambaye alikuwa beki wa zamani wa Kogalo anatarajiwa kusafiri na timu hiyo kwa mechi ya marudio kufuzu kwa hatua ya makundi Jumapili dhidi ya NAPSA Stars ya Zambia.

Omollo anatwaa mikoba hiyo ya naibu kocha wa Kogalo  kusaidiana na kocha mkuu  Mreno Carlos Manuel Vaz Pinto na ndiye naibu kocha wa kwanza tangu kuondoka kwa Patrick Odhiambo  aliyehamia Kakamega Homeboyz.

Kocha huyo hajakuwa na kibarua tangu afurushwe Posta Rangers akiwa kocha mkuu kutokana na matokeo mabovu,na ni mara yake ya pili kurejea Gor baada ya kuwa usukani katika mechi za ligi ya mabingwa msimu huu .

Gor Mahia walioshindwa bao 1-0 katika mkumbo wa kwanza wiki jana watawania ushindi wa magoli 2-0 Jumapili ili kufuzu kwa hatua ya makundi ya kombe hilo kwa mara ya pili.

Categories
Michezo

NAPSA Stars wanoa makali kukabiliana na Gor Mahia Jumapili

Klabu ya NAPSA Stars kutoka Zambia  imeendeleza mazoezi  katika uwanja wa Utalii kujianda kwa mkumbo wa kwanza wa mchujo wa kufuzu kwa hatua ya makundi ya kombe la shirkisho dhidi ya Gor Mahia Jumapili ya Februari 14.

NAPSA inayochezewa na wakenya Shaban Odhonji na beki wa zamani wa Gor David Odhiambo Owino aka Calabar iliwasili nchini Jumatano alasiri.

Gor pia walirejea mazoezini Alhamisi baada ya mgomo wakilalama kutolipwa malimbikizi ya mshahara wa miezi 2.

Mkondo wa pili utasakatwa Lusaka Zambia ,huku mshindi wa jumla akifuzu kwa hatua ya makundi ya kombe la shirikisho ambayo Gor wamefuzu mara mbili mtawalia ,mwaka 2018 huku msimu wa mwaka 2018-2019 wakicheza hadi robo fainali.

NAPSA Stars wakiwa maozeizini  uwanja wa Utalii

Gor wanakalia nafasi ya 6  ligini kwa sasa pointi 16 baada ya mechi 9 .

Wageni NAPSA Stars ni klabu iliyobuniwa 1969 lakini ilipandishwa daraja kucheza ligi kuu Zambia mwaka 2012 ikijulikana kama Profund Warriors kabla ya kubadilisha jina ilipotwaliwa na mamlaka ya malipo ya uzeeni  yaani National Pension Scheme Authority Stars huku ikishikilia nafasi ya 13  ligini  kwa alama 18 kutokana na michuano 16 ,alama 10 nyuma ya  viongozi ZANACO.

Mechi ya Jumapili ambayo itakuwa Valentine’s  itaanza saa tisa alasiri katika uwanja wa taifa wa  Nyayo.

Mwamuzi mkuu wa pambano hilo atakuwa Mganda William Oloya na  atasaidiwa na Waganda wenza  Lee Okello atakayekuwa msaidizi wa kwanza, Isa Masembe msaidizi wa pili   huku  Chelanget Ali Sabila aakiwa afisa wa nne.

Alexis Redamptus Nshimiyimana wa  Rwanda atakuwa kamisaaa wa mechi hiyo  huku Wycliffe Makanga,ambaye ni tabibu wa Harambee Dtars akiwa afisa wa afya kuhusu Covid 19.

Categories
Michezo

Wageni NAPSA Stars watua huku wenyeji Gor wakiwa mgomo

Kikosi cha wachezaji na maafisa wa klabu ya mamlaka ya uzeeni nchini Zambia NAPSA Stars kiliwasili jijini Nairobi Jumatano jioni tayari kwa mkumbo wa kwanza wa mechi ya kufuzu kwa hatua ya makundi ya kombe  la shirikisho la soka barani Afrika dhidi ya mabingwa wa Kenya Gor Mahia mchuano utakaopigwa Jumapili hii katika uwanja wa Nyayo.

Kikosi cha NAPSA kilichowasili kinawajumuisha wachezaji wawili wa humu nchini Shaban Odhonji zamani akiwa na Mathare United na Difenda wa zamani wa Gor Mahia David Owino lakini Mkenya mwingine Andrew Tololwa hakusafiri na timu himu hiyo.

Wakati uo huo wenyeji Gor Mahia walikuwa kwenye mgomo baradi na kudinda kuhudhuria mazoezi katika uwanja wa Camp Toyoyo wakiteta kuhusu kutolipwa malimbikizi ya mshara wa miezi miwili.

Wachezaji wa Kogalo wamekuwa wakigoma kabla ya kila mechi ya kimataifa kuanzia mwaka jana .

Kikosi cha NAPSA kilichowasili kinawajumuisha:-

Makipa

Philip Banda, Rabson Muchelenganga and Shabaan Odhonji

Mabeki

David Owino, Luka Banda, Luka Nguni, Aaron Kabwe, Lawrence Chungu, Bornwell Selengo, Amos Simwanza

Viungo

Jacob Ngulube, Daniel Adoko, Simon Nkhata, Dickson Chapa, Danny Silavwe, Enock Sabumukama, Austin Banda, Aaron Banda

Washambulizi

Chanda Mushili,  Laudit Mavugo, Jimmy Mukeya,  Doisy Soko, Tapson Kaseba

NAPSA watakuwa wakifanya mazoezi Alhamisi na Ijumaa katika uwanja wa Kasarani kabla ya kufanya mazoezi kwa mara ya kwanza katika uwanja wa taifa wa Nyayo siku ya Jumamosi.

Categories
Michezo

Mganda William Oloya kuzihukumu Gor Mahia na NAPSA Stars kombe la shirikisho

Mwamuzi wa Uganda William Oloya   atakuwa refa wa katikati ya uwanja katika mkondo wa kwanza wa mechi ya mchujo kuwania kombe la shirikisho la soka Afrika baina ya  Gor Mahia na  NAPSA Stars ya  Zambia Jumapili Februari 14 katika uwanja wa Taifa wa Nyayo.

Oloya atasaidiwa na Waganda wenza  Lee Okello atakayekuwa msaidizi wa kwanza, Isa Masembe msaidizi wa pili   Chelanget Ali Sabila ambaye atakuwa afisa wa nne.

Alexis Redamptus Nshimiyimana wa  Rwanda atakuwa kamisaaa wa mechi hiyo  huku Wycliffe Makanga,ambaye ni tabibu wa Harambee Dtars akiwa afisa wa afya kuhusu Covid 19.

NAPSA Stars  ambayo ni timu wafanyikazi wa mamlaka ya malipo ya uzeeni inatarajiwa kuwasili nchini Jumatano alasiri tayari kwa mkwangurano huo.

Kogalo watamenyana na NAPSA stars anayoichezea difenda wa Harambee Stars  David Owino Februari 14 kuanzia saa tisa katika uwanja wa nyayo kabla ya mechi ya marudio kupigwa nchini Zambia huku mshindi wa jumla akitinga hatua ya makundi ya kombe la shirikisho.

Categories
Michezo

Gor na Wazito FC wafungiwa kusajili wachezaji kwa mwaka mmoja kwa kushindwa kuwalipa wachezaji

ShirikIsho la soka ulimwenguni FIFA   limezipiga marufuku timu za  Gor Mahia  na  Wazito Fc kusaini wachezaji wapya kuanzia msimu huu  wa uhamisho wachezaji kwa kushindwa kuwalipa wachezaji  Dickson Ambudo na   Augustin Otu  mtawalia.

Yamkini gor walishindwa kumlipa wing’a wa Tanzania Ambudo shilingi milioni 1 nukta 2 alipowachezea  yakiwa malimbikizi ya mshahara na marupurupu huku Wazito wakikosa kumlipa  Otu kutoka Liberia shilingi milioni 1 baada ya kukatiza kandarasi yake kwa njia isiyofaa kinyume na kandarasi.

Ambudo na  Otu walikuwa wamewasilisha kesi yao kwa jopo la kutatua mizozo kwenye shirikisho la FIFA  disemba 16 na 26 mtawalia.

Vilabu hivyo vilipewa makataa ya siku 45 kuwalipa wachezaji hao au vipigwe marufuku .

Hata hivyo inasubiriwa kuona hatua ambayo FKF itazichukulia timu hizo mbili kwani kogalo walikuwa wamekamilisha usajili wa mshmabulizi wa Brazil Wilson Silva Fonseca, nahodha wa zamani Harun Shakava  na  Abdul Karim Nikiema Zoko  kutoka Burkina Fasso kwa kandarasi ya miaka miwili kila mmoja.

Upande mwingine , Wazito walimsajili kiungo wa Sopaka  Eli Asieche.

Endapo zitawalipa wachezaji hao ,timu hizo mbili ziko huru kusajili wachezaji wapya kuanzia Agosti mwaka ujao.

Ambudo,ambaye kwa sasa anachezea timu ya  Dodoma Jiji  katika ligi kuu ya Tanzania bara aliondoka Gor Julai mwaka jana baada ya kukamilika kwa mkataba wake  wa mkopo wakati Otu akiwa kati ya wanandinga 12 waliotimuliwa na usimamizi wa Wazito Fc Julai mwaka jana.

 

 

 

Categories
Michezo

Kocha mpya wa Gor Mahia Vaz Pinto asaini mkataba wa miaka miwili

Kocha mpya wa Gor Mahia Carlos Vaz Pinto amesema lengo lake ni kuhakikisha Gor Mahia wanafuzu kwa hatua ya makundi ya kombe la shirikisho mwaka huu.

Pinto ambaye ni rai wa Ureno ,amesema haya mapema Jumapili baada ya kusaini mkataba wa miaka miwili na Kogalo akisisitiza kuwa tajriba pana aliyo nayo kufanya kazi ya ukunzi barani Afrika itamsaidia pakubwa katika majukumu yake mapya.

“Lengo langu kuu ni kuifuzisha Gor Mahia kwa hatua ya makundi ya kombe la shirikisho pamoja na kushinda mechi katika ligi na kuandikisha historia,tuna muda wa kutosha kuwasoma wapinzani wetu NAPSA na pia timu yangu ili kuleta matokeo” ‘akasema Pinto

Mreno huyo ameongeza kuwa atalenga kushinda mataji akiwa na Gor  kwa kuwa ni klabu kubwa .

“Nimefurahia kujiunga na Gor Mahia ambayo ni timu kubwa na nimekuja kuandikisha historia”akaongeza Pinto

Kwa upande wake mwenyekiti wa Gor Ambrose Rachier amesema wamelazimika kumtafuta kocha mpya baada ya kutamatisha kandarasi ya Robertinho kwa maafikiano.

“Imebidi tumtafute kocha mpya miezi minne tangu tumzindue kocha Oliveira kutoka Brazil kuiongoza Gor baada ya Caf kurekebisha vikwazo vya cheti cha kufuzu ili kusimamia mechi za bara Afrika,imekuwa vigumu kumsubiri kocha Oliveira kwa miezi minne ijayo ili aendelee na kazi yake baada ya kwenda kuongeza masomo, na ndio tumeafikiana naye tukatize kandarasi yake na tutafute kocha mpya”akasema Rachier

“Tunamshukuru Pinto kwa kukubali ombi letu na inavyoonekana tunahitaji kuimarisha idara yetu ya tiba maungo ndio maana pia tumemzindua kocha Khamis Juma Musa kuwa physiotherapist wetu,tuna imani ujio wa wawili hawa kutaongeza makali kwenye timu huku pia tukiendelea kumtafuta kocha msaidizi”akaongeza Rachier

 

Categories
Michezo

Carlos Manuel Vaz Pinto ateuliwa kocha mpya wa Gor Mahia

Mabingwa wa ligi ya Kenya Gor Mahia  wamemteua Mreno  Carlos Manuel Vaz Pinto kuwa kocha wa klabu  hicho kwa miaka miwili ijayo.

Vaz Pinto aliwasili nchini Kenya Jumamosi  usiku kutwaa mikoba ya ukufunzi kutoka kwa  Roberto Oliveira wa Brazil ailiyepigwa kalamu mwezi Disemba  mwaka jana kwa kukosa cheti kinachohitajika cha ukufunzi kusimamia mechi za shirikisho la soka Afrika CAF na kuwalazimu Kogalo kumteua Pamzo Omolo kwa mechi zao nne za mchujo kuwnaia kombe la ligi ya mabingwa dhidi ya APR ya Rwanda na CR Belouizdad.

Pinto aliye na umri wa miaka 46 ana leseni ya za ukufunzi za  Uefa Pro na Caf ‘A’  na awali amezifunza timu za  St George ya Ethiopia na  Clube Recreativo Desportivo do Libolo kutoka Angola ,kabla ya kuifunza timu ya chipukizi wasiozidi umri wa miaka 23 ya FC Famalicao nchini Ureno kutoka Septemba 2019 hadi Juni mwaka 2020.

Kibarua cha kwanza kw akocha huyo ni kuingoza Gor kwa mechi mbili za mchujo kufuuz hatua ya kuandi ya kombe la shirikisho la soka dhidi ya National Pension Scheme All stars (NAPSA)ya Zamabia baina ya Februari 14  mjini Nairobi na 21 mwaka huu mjini Lusaka .

Kogalo imekuwa na makocha wengi wa kigeni ndani ya muda mfupi uliopita wakiwemo Frank Nuttal, Dylan Kerr, Zdravcko Logarusic, Jose Marcelo Ferreira , Hassan Oktay  na Steven Polack  wote waliojiuzulu kutokana na kutolipwa huku wa hivi punde akiwa Robertinho.

Hata hivyo timu hiyo haijamtangaza msaidizi wa Pinto.