Categories
Michezo

Kocha wa Uganda Cranes Jonathan Mckinstry atimuliwa

Shirikisho la soka nchini Uganda FUFA limetamatisha kanadarasi ya kocha wa timu ya taifa The Cranes Jonathan Mckinstry kwa maafikiano.

Makinstry amekuwa akiiongoza Uganda kwa kipindi cha miezi 18 iliyopita kwenye mkataba wake wa miaka mitatu , huku akiwasaidia kutwaa kombe la CECAFA mwaka 2019.

Hata hivyo mambo yamemwendea tenge Mwingereza huyo wa Ireland Kaskazini  ,huku akipigwa marufuku katika mechi mbili za mwisho za Uganda kufuzu kwa kombe la AFCON mwakani dhidi ya Burkina Faso na Malawi, huku wakikosa kufuzu kwa kuibuka nafasi ya tatu.

Mckinstry awali amezinoa timu za Rwanda na Sierra Leona na FUFA inatarajiwa kutangaza mkufunzi mpya kabla ya kuanza kwa mechi za kufuzu kwa kombe la dunia mwezi Juni mwaka huu,timu hiyo ikiwa kundi moja na Kenya,Rwanda na Mali.

Categories
Michezo

Nahodha wa Uganda Dennis Onyango astaafu soka kimataifa

Nahodha wa muda mrefu wa timu taifa ya Uganda Dennis Onyango amestaafu soka ya kimataifa.

Onyango ambaye amekuwa kipa chaguo la kwanza wa Uganda Cranes aliandika waraka kwa shirikisho la Uganda FUFA  kustaafu akitaja kuwa aliafikia uamuzi huo mgumu kufuatia ushauri wa familia yake.

“Nimechukua uamuzi huu mgumu baada ya kushauriwa na familia yangu ,nichukue fursa hii kuishukuru familia yangu,meneja wangu na wote waliochangia ufanisi wangu”akasema Onyango

Kwa jumla Onyango ambaye pia anaichezea klabu ya Mamelodi Sundowns ya Afrika Kusini, aliichezea Cranes mechi 79  za kimataifa tangu mwaka  2005 dhidi ya Cape Verde.

Kustaafu kwa Onyango aliye na umri wa miaka 35 kunatokea wiki moja baada ya kiungo  Hassan Waswa pia kutangaza kustaafu soka ya kimataifa.

 

Categories
Michezo

Uganda Hippos waing’ata Burkina Faso na kutinga nusu fainali AFCON U 20

Uganda Hippos waliandikisha historia Alhamisi usiku walipoibwaga Burkina Faso penati 5-4 na kufuzu kwa nusu fainali ya kombe la bara Afrika kwa chipukizi wasiozidi umri wa miaka 20 mjini Nouakchott Mauritania.

Burkina Faso maarufu kama Young Stallions walianza vyema mechi kwa mashambulizi mengi lakini kipa wa Uganda Komakach alikuwa mwiba na kupangua matobwe yote.
Ugand pia walishuhudia mikwaju yao kupitia kwa Steven Sserwadda ,Ivan Bogere na Isma Mugulusi ikipanguliwa.

Mechi ilimalizikia kwa sare tasa baada ya dakika 120 na kuamuliwa kupitia matuta ya penati Uganda wakiunganisha zote 5 huku kipa wa Hippos Komakach akipangua

penati ya kwanza iliyochongwa na Naser Djiga Yacouba .

Uganda wanaoshiriki michuano hiyo kwa mara ya kwanza watacheza nusu fainali na mshindi kati ya Tunisia na Moroko watakaomenyana kwenye robo fainali ya Ijumaa.

Ghana wakimenyana na Cameroon

Ghana waliibandua Cameroon pia kupitia penati 5-3 kufuatia sare tasa dakika 120 katika kwota fainali ya kwanza.

Ghana ukipenda Black Satelites watamenyana na mshindi wa robo fainali ya Ijumaa baina ya Afrika ya kati na Gambia katika hatua ya nusu fainali.

Categories
Michezo

Uganda yaipakata Msumbiji AFCON U 20

Timu ya Uganda maarufu kama Hippos imeanza vyema mechi za kundi A katika mashindano ya kuwania kombe la AFCON kwa chipukizi walio chini ya umri wa miaka 20 baada ya kuwacharaza Msumbiji mabao 2-0 katika mechi iliyochezwa Jumatatu alasiri nchini Mauritania .

Mshambulizi wa klabu ya Police Derrick Kakooza alipachika bao la kwanza dakika ya 57 kupitia penati kabla ya kiungo wa KCCA Steven Serrwada dakika 4 kabla ya kipenga cha mwisho huku ushindi huo ukiwaweka katika nafais nzuri ya kutinga robo fainali wakiongoza kundi hilo kwa alama 3 sawa na Cameroon kuelekea kwa mechi kati ya timu hizo mbili Jumatano hiii.

Mashindano hayo yanashirikisha mataifa 12 huku fainali yake ikipigwa tarehe 6 mwezi ujao.

 

Categories
Michezo

East Afrika Derby Uganda kukabana koo na Rwanda CHAN

Miamba wa Afrika Mashariki Amavubi ya Rwanda na Uganda Cranes watamenyana jumatatu usiku  katika mchuano wa pili wa kundi C kuwania kombe la CHAN  uwanjani Reunification mjini Doula.

Kocha wa Rwanda Johnny McKinstry aliyeiongoza Rwanda kucheza hadi robo fainali mwaka 2016 wakiwa nyumbani ataiongoza Uganda Cranes katika mechi ya Jumatatu  dhidi ya msaidizi wake mwaka 2016  Vincent Mashami  ambaye ndiye kocha mkuu wa Rwanda katika makala ya mwaka huu.

Rwanda itamtegemea sana mshambulizi Jaques Tuyisenge wa APR  huku Uganda ikitegemea huduma za mshambulizi wa KCCA  Brian Aheebwa.

Waganda pia wamekuwa na matayarisho mazuri baada ya kuibuka mabingwa wa  mashindano yaliyotangulia fainali hizo za CHAN mapema mwezi huu nchini Cameroon kwa kushinda mechi mbili dhidi ya Zambia na Niger na kutoka sare na wenyeji Cameroon.

Uganda inashiriki CHA N kwa mara ya 5 huku Rwanda wakipiga kwa mara ya pili.

Kundi hilo pia linajumuisha mabingwa watetezi Moroko na Togo wanaoshiriki kwa mara ya kwanza.

Mechi zote mbili zitarushwa mbashara na runinga ya taifa KBC Channel 1.

Moroko dhidi ya Togo saa moja usiku na Uganda dhidi ya Rwanda 10pm

Categories
Michezo

Uganda Cranes yaikwaruza Zambia mechi ya kujinoa kwa CHAN

Uganda Cranes iliibwaga Chipopolo ya Zambaia mabao 2-0 Jumatatu jioni katika mechi ya pili ya mashindano ya kutangulia makala ya 6 ya michuano ya CHAN nchini Cameroon,mechi iliyosakatwa katika uwnaja wa Annex Omnisports mjini Younde.

Vianne Sekajugo na Steven Mukwala waliifungia Cranes mabao hayo katika dakika ya 25 na 60 mtawalia ,Waganda wakiendeleza msururu wa matokeo mazuri baada ya kwenda sare ya 1-1 na wenyeji Cameroon katika mechi ya kwanza ya  ya mashindano hayo yanayotangulia michuano ya CHAN.

Uganda watafungua ratiba ya kundi C katka makala ya 6 ya michuano ya Chan dhidi ya Amavubi ya Rwanda Tarehe 18 mwezi huu kabla ya kumenyana na Zimbabwe Januari 22 na kukamilisha ratiba dhidi ya Togo Januari 26.

Michuano ya Chan ambayo hushirikisha wachezaji wanaopiga soka katika ligi za nyumbani yataanza Januari 16 na kukamilika Februari 7 huku mataifa 16 yakiwania kombe hilo linaloshikiliwa na Moroko.

Runinga ya taifa KBC Channel 1   itakuletea mechi zote live kutoka Cameroon.

Categories
Michezo

Uganda Cranes yadunda Cameroon kuwania kombe la CHAN

Timu ya taifa ya Uganda Cranes iliwasili Cameroon Jumanne tayari kushiriki michuano ya kombe la Chan kuanzia tarehe 16 mwezi ujao.

Uganda Cranes imekuwa mazoezini kwa kipindi cha mwezi mmoja uliopita mjini Kampala kabla ya kuabiri ndege kwenda Cameroon.

Timu hiyo itakita kambi katika uwanja wa Omnisport mjini Younde  na inatarajiwa kuanza mazoezi  Jumatano alasiri kabla ya kuhsiriki  mashindano ya mataifa mane  yatakayotangulia michuano ya CHAN  ambapo wenyeji Cameroon,Niger ,uganda na Zambia kati ya Januari 1 na 7 mwaka ujao.

Kikosi cha Uganda kilichotua Uganda kinawajumuisha:-

Makipa: Tom Ikara (Police), Joel Mutakubwa (Kyetume), Nafian Alionzi (URA)

Mabeki: Halid Lwaliwa (Vipers), Musitafa Mujuzi (Kyetume), Patrick Mbowa (URA),Eric Ssenjobe (Police), Aziz Kayondo (Vipers), Paul Willa (Vipers), Ashraf Mandela (URA), Hassan Muhammad (Police)

Viungo: Tonny Mawejje (Police), Bobosi Byaruhanga (Vipers), Shafiq Kagimu (URA), Karim Watambala (Vipers), Saidi Kyeyune (URA), Hassan Ssenyonjo (Wakiso Giants)

Washambulizi: Mohamed Shaban (Vipers), Joseph Ssemujju (BUL), Joackim Ojera (URA), Milton Karisa (Vipers), Stephen Mukwala (URA),Ben Ocen (Police), Ibrahim Orit (Vipers), Vianne Ssekajjugo (Wakiso Giants)

Maafisa

 • Leader of Delegation: Hamid Juma
 • Head Coach: Johnathan McKinstry
 • Assistant Coaches: Abdallah Mubiru Charles Livingstone Mbabazi
 • Performance Coach: Alexander McCarthy
 • Goalkeeping Coach: Sadiq Wassa
 • Sports Scientist: Felix Ayobo
 • Doctors: Dr. Emmanuel Nakabago and Dr. Opika Opoka
 • Media: Hussein Marsha Ahmed
 • Team manager: Geoffrey Massa
 • Equipment managers: Samuel Hassan Mulondo & Ayub Balyejusa
 • Team Coordinator: Paul Mukatabala

Uganda itafungua kampeini ya kundi C tarehe 18 mwezi ujao dhidi ya majirani Rwanda kabla ya kukabiliana na Togo Januari 22 na kuhitimisha ratiba dhidi ya Moroko tarehe 26.

Uganda watakuwa wakicheza CHAN kwa mara ya 5 mwaka ujao baada ya kushiriki  mwaka 2011,2014,2016 na 2018 huku wakilenga kufuzu kwa hatua ya mwondoano kwa mara ya kwanza kulingana na kocha Johnny McKinstry.

Mataifa 16 yatashiriki fainali hizo zitakazokuwa za makala ya 6  kuanzia Januari 16 na Februari 7.

 

Categories
Michezo

Uganda yaipakata Kenya 5-0 na kutinga nusu fainali CECAFA U 17

Mabingwa watetezi Uganda wamefuzu kwa nusu fainali ya michuano ya kombe la CECAFA kwa chipukizi wasiozidi umri wa miaka 17  nchini Rwanda baada ya kuigaragaza Kenya mabao 5-0 katika mechi ya mwisho ya kundi A  iliyopigwa Jumatano adhuhuri uwanjani Umuganda mjini Rubavu .

Oscar Mawa  aliwaweka Uganda maarufu kama Cubs kifua mbele kwa bao la dakika ya 7 lililodumu hadi mapumzikoni.

Waganda waliondelea kucheza mchezo wa kuonana vyema kunako kipindi cha pili huku safu ya ulinzi ya Kenya ikionekana kuishiwa nguvu nao washambulizi wakikosa makali  na ilichukua dakika 9 pekee kabla ya Mawa kuongeza mabao mawili ya haraka dakika ya 50 na 54 na kukamilisha Hat trick yake katika mchezo huo.

Travis Mutyaba na Ronald Madoi waliongeza goli moja kila mmoja katika dakika za 78 na 88 na kudidimiza matumaini ya Kenya kufuzu kwa nusu fainali kwani itawalazimu Ethiopia ambao pia wamo kundi A na Kenya ,wapoteze kwa mabao 6-0  katika mchuano wa Ijumaa dhidi ya uganda  ili Kenya inayofunzwa na kocha  Oliver Page  ifuzu nusu fainali.

Timu ya Uganda kwa chipukizi walio chini ya umri wa miaka 17

Kenya ni ya mwisho katika kundi A kwa alama 1 baada ya kukamilisha mechi zake kufuatia kutoka sare ya 2-2 dhidi ya Ethiopia  katika pambano la ufunguzi Jumapili iliyopita .

Timu ya Kenya kwa chipukizi walio chini ya umri wa miaka 17

Uganda waliocheza mechi moja wanaongoza kundi hilo kwa alama 3 na wanahitaji tu sare dhidi ya Ethiopia katika mechi ya mwisho ili kumaliza ya kwanza.

Tanzania ilikuwa ya kwanza kufuzu kwa nusu fainali kutoka kundi B  siku ya Jumanne  baada ya kuwazabua wenyeji Rwanda mabao 3-1.

Michuano hiyo ya Cecafa itaingia hatua ya nusu fainali tarehe 20 nayo fainali isakatwe Disemba 22 ambapo mataifa mawili bora yatafuzu kucheza fainali za kombe la AFCON kwa vijana wasiozidi umri wa miaka  17 mwezi Juni mwaka ujao nchini Moroko.

 

Categories
Michezo

Viboko wa Uganda waitafuna Tanzania na kunyakua kombe la CECAFA 2020

Timu ya Uganda kwa Chipukizi walio chini ya umri wa miaka 20 maarufu kama Hippos ,ndio mabingwa wa mwaka huu wa kombe la Cecafa  baada ya kuwadhalilisha wenyeji Tanzania mabao 4-1 katika fainali iliyosakatwa Jumatano jioni katika uwanja wa Black Rhino Academy eneo la Karatu mjini Arusha Tanzania.

Richard Basangwa, Steven Sserwadda,  Ivan Bogere na  Kenneth Semakula waliiwajibikia Uganda kwa bao moja kila mmoja ,huku Abdul Suleiman akifunga bao la maliwazo kwa Ngorongoro Heroes kupitia penati.

Viboko hao wa Uganda wangeongoza mabao 3-1 kufikai mapumziko lakini mshmabulizi mwiba Ivan Bogere  akapaishia penati ya dakika ya 45 .

Ilikuwa  mechi ya kulipiza baada ya Tanzania kunyakua kombe la Cecafa mwaka jana ,michuano hiyo ilipoandaliwa nchini Uganda.

Hata Hivyo  timu zote mbili za Uganda na Tanzania zimejikatia tiketi kucheza fainali za Afcon mwaka ujao nchini Mauritania katika mala ya 15.

Kuelekea fainali Uganda iliikomoa Kenya mabao 3-1 katika semi fainali wakati Tanzania wakiwaadhibu Sudan Kusini magoli 2-1 pia katika nusu fainali.

Iilikuwa kombe la 4 la Cecafa kwa uganda tangu mashindano hayo yatangulizwe mwaka 1971,wakiibuka mabingwa miaka ya 1973,2006,2010 na 2020 na kuwa taifa lenye ufanisi mkubwa katika michuano hiyo.

Uganda pia kwa mara ya kwanza wanashikilia vyokombe vyote vya Cecafa kwa wakati mmoja vikiwa nia:-Cecafa kwa wavulana wasiozidi umri wa miaka 15 ,Wasichana walio chini ya umri wa miaka 17,Wavulana walio chuini ya miaka 17 ,wanaume walio chini ya umri wa miaka 20,kombe la Cecafa Kagame linaloshikiliwa na KCCA na kombe la Cecafa senior challenge cup wanaloshikilia Ugand Cranes.

 

 

 

 

Categories
Michezo

Viboko wa Uganda kukabiliana na Ngorongoro Heroes ya Tanzania fainali ya CECAFA

Fainali ya kuwania  kombe la Cecafa kwa vijana  chipukizi wasiozidi umri wa miaka 20 itapigwa Jumatano  alasiri baina ya mabingwa watetezi Tanzania dhidi ya Uganda katika uwanja wa Black Rhino Academy eneo la Karatu mjini Arusha Tanzania.

Wenyeji Tanzania maarufu kama Ngorongoro Heroes  walianza safari ya michuano  hiyo katika kundi A  kwa kuipakata  Djibouti magoli 6-1 ,kabla ya kuimenya Somalia mabao 8-1 katika pambano la mwisho na hatimaye  kuibandua Sudan Kusini bao 1-0 kwenye nusu fainali.

Upande mwingine  Viboko wa Uganda au Hippos walianza kundi B kwa kutoka sare tasa dhidi ya Sudan Kusini kabla ya kuigaragaza  Burundi mabao 6-1 katika mechi ya mwisho na kuitema kenya mabao 3-1 kwenye nusu fainali.

Uganda na Tanzania tayari zimejikatia tiketi kupiga fainali za 15 za kuwania kombe la Afcon mwaka ujao nchini Mauritania kwa kufika fainali.

Tanzania wakipiga fainali ya mwaka jana dhidi ya Kenya

Fainali ya Jumatano  itashuhudia Tanzania wakilenga kuhifadhi ubingwa wa mwaka uliopita wakati Waganda pia wakipania kulipiza kisasi kwa kukosa kunyakua kombe hilo wakiwa nyumbani mwaka uliopita.

Kenya na Sudan Kusini zitamenyana kuanzia saa sita adhuhuri katika mechi ya kuwania nafasi ya tatu na nne katika uwanja wa Black Rhino Academy eneo la Karatu mjini Arusha.