Categories
Michezo

Stars kucheza mechi tatu za kujipiga msasa kabla ya kuikabili Misri

Timu ya taifa Harambee Stars imeratibiwa kucheza mechi tatu za kirafiki kunoa makali kabla ya kukabiliana na Misri katika pambo la kundi G kufuzu dimba la Afcon tarehe 22 mwezi ujao katika uwanja wa kimataifa wa Kasarani.

Stars watapambana na Sudan Kusini tarehe 13 mwezi ujao hapa Nairobi ,kabla ya kuwaalika Tanzania siku mbili baadae na kuzuru Tanzania tarehe 18 .

Kenya itawaalika Pharoes ya Misri katika pambano la tano kundi G Machi 22 kabla ya kusafiri kwenda Lome Togo kwa mkwangurano wa mwisho tarehe 30 mwezi ujao.

Mechi hizo zitakuwa za kuhitimisha tu ratiba kwa Kenya ambayo haina fursa ya kuzipiku Misri na Comoros zilizo kileleni pa kundi hilo, ili kufuzu kwenda AFCON kwa mara ya pili mtawalia kwa mara ya kwanza ,baada ya kushiriki mwaka 2019 nchini Misri.

Comoros inaongoza kund F kwa pointi 8 sawia na Misri huku timu hizo mbili zikimenyana katika mchuano wa mwisho tarehe 30 mjini Cairo Misri ,mataifa yote yakihitaji kwenda sare ili kutwaa nafasi hizo mbili.

Kabla ya hapo Comoros watakuwa na fursa ya kufuzu watakapowaalika Togo tarehe 22 mwezi Machi wakiwania tu sare ili kujikatia tiketi kwa mara ya kwanza.

Kenya ni ya tatu kundini G kwa alama 3 wakati Togo ikiwa imezoa pointi 1.

Wakati uo huo wachezaji 28 wa humu nchini wameitwa kambini kujiandaa kwa mtihani huo.

Categories
Michezo

Musa Otieno ana imani ya Kenya kufuzu AFCON 2022

Aliyekuwa nahodha wa muda mrefu zaidi wa Harambee Stars Musa Otieno ana imani kuwa timu hiyo itashinda mechi mbili za kufuzu za mwezi ujao na kujikatia tiketi kwa kipute cha AFCON mwaka ujao nchini Cameroon.

Otieno ambaye ni mmoja wa washauri wa kiufundi wa FKF amesema ana imani na mbinu za ukufunzi za kocha Jacob Ghost Mulee baada ya kuiongoza timu hiyo katika makala ya mwaka 2004 nchini Tunisia akiwa nahodha.

“Katika soka kila kitu kinawezekana,nina imani na kocha Mulee,cha mhimu ni kujiamini na kupata matokeo katika mechi dhidi ya Misri hapa Nairobi na pia tushinde Togo ugenini “akasema Otieno

Kenya ni ya tatu katika G la kufuzu kwa pointi 3 wakati Comoros na Misri zikiaongoza kwa alama 8 kila moja na ili kujikatia tiketi kwenda Afcon kwa mara ya pili mtawalia Harambee Stars hawana budi kushinda mechi zote mbili zilizosalia dhidi ya Misri Machi 22 mwaka huu uwanjani Kasarani ,na kuilaza Togo tarehe 30 mwezi ujao na kutarajia kuwa Misri na Togo hawatazoa hata pointi moja katika mechi zao mbili zilizosalia.

Otieno amelitaka shirikisho la FKF kuweka mikakati ifaayo kuanzia kwa mashindano ya shule za sekondari kuhakikisha kuwa Harambee Stars inafuzu kwa fainali za kombe la dunia mwaka ujao nchini Qatar.

“majirani zetu wametilia maanani mashindano ya shule za sekondari na pia FKF inapaswa kuyazingatia mashindano hayo na tutengeze timu thabiti za chipukizi,cha mhimu pia ni benchi ya ukufunzi kuhakikisha Kenya inashinda mechi zote za nyumbani na kutafuta sare kadhaa ugenini au hata ushindi ili kufuzu”akaongeza Otieno

Kenya imejumuishwa kundi E la kufuzu kwenda Qatar pamoja na miamba Mali,Uganda na Rwanda huku mechi hizo zikianza mweiz Juni mwaka huu ambapo timu bora kutoka kundi hilo itatinga hatua ya mwondoano.

Categories
Michezo

FKF yaidhinisha shule ya St Athony Kitale kuwa kituo cha kukuza talanta

Shirikisho la soka nchini FKF limezindua shule ya wa wavulana ya St Athony Boys Kitale kuwa kituo cha kitaifa cha kukuza talanta .

Kulingana na mktaba uliotiwa saini baina ya FKF na shule hiyo ya upili hadi mwaka 2026 ,utashuhudia shule hiyo ikipewa msaada wa kiufundi kutoka kwa shirikisho litakalobuni mipango ya mafunzo ya soka kwa shule hiyo kwa wachezaji soka na wanafunzi wengine na kuoa mafunzo kwa makocha na wakufunzi wa timu hiyo.

FFK pia itatoa vifaa vya kufanyia mazoezi huku shule hiyo ikiwa na jukumu la kuwachuchukua wanafunzi 20 watakaopata msaada wa masomo kikamilifu katika mwaka wa kwanza na wengine watano kila mwaka utakaofuatia huku wanafunzi hao wakiteuliwa kupitia kw ampango maalum wa kukuza chipukizi.

Kwa mjibu wa katibu mkuu wa FKF Barry Otieno wanafunzi na wachezaji watakaojiunga na kituo hicho cha kukuza talanta watachaguliwa kila wakati wa likizo huku maskauti wakiteua wale watakaojiunga na timu za taifa .

Categories
Michezo

Leopards kukabana koo Rangers wakati Ulinzi wakipambana na Sofapaka Betway Cup

Vigogo AFC Leopards  wameratibiwa kuwaalika  Posta Rangers katika mechi za awamu ya 32 bora kuwania kombe la Bet way kwa mjibu wa droo iliyoandaliwa mapema Ijumaa.

Kwenye ratiba nyingine itakayoshirikisha vilabu kutoka ligi kuu Ulinzi stars watakuwa na miadi dhidi ya Sofapaka huku mechi hizo zikichezwa baina ya April 17 an 18.

Mabingwa wa mwisho wa kombe hilo Bandari fc wamepangwa dhidi ya Dimba Patriots ,Tusker wachuane dhidi Marafiki FC  nayo timu ya kaunti ya Tranz Nzoia Transfoc FC iwe mgeni wa Kenya Commercial Bank.

Timu itakayotwaa kombe hilo itatuzwa shilingi milioni 2 na nafasi ya kuiwakilisha Kenya katika mashindnao ya kombe la Shirikisho Afrika msimu ujao.

Ratiba kamili ya mechi za raundi ya 32 bora

 1. Fortune Sacco vs Nairobi City Stars
 2. Congo Boys / Gor Mahia vs CUSCO
 3. Marafiki vs Tusker
 4. Sofapaka vs Ulinzi Stars
 5. AFC Leopards vs Posta Rangers
 6. Malindi Progressive vs Luanda Villa
 7. Bandari vs Dimba Patriots
 8. Bungoma Superstars vs Nation FC
 9. KCB vs Transfoc
 10. Kariobangi Sharks vs Tandaza
 11. Kajiado North vs Sigalagala TTI
 12. Equity vs Keroka TTI
 13. Twomoc vs Vegpro
 14. Bidco United vs Twyford
 15. Egerton vs Administration Police
 16. Mara Sugar vs NYSA
Categories
Michezo

Uwanja Gusii kuitwa Simeon Nyachae Stadium

Rais Uhuru Kenya ametangaza kuwa serikali itatumia shilingi milioni 150 kuukarabati uwanja wa Gusii katika kaunti ya Kisii.

Akizungumza kwenye mazishi ya aliyekuwa waziri wa Fedha na kiongozi wa jamii ya Abagusii ,Simenon Nyachae Jumatatu adhuhuri ,Rais Kenyatta ametangaza kuwa serikali itaongeza shilingi milioni 150 zaidi kwa shughuli ya ukarabati inayoendelea na kusema kuwa kama nji moja ya kumuenzi marehemu Nyachae uwanja huo utabadilishwa jina na kuitwa Simeon Nyachae Stadium.

Uwanja wa Gusii hutumiwa na klabu ya Shabana Fc kwa mechi za ligi kuu NSL na pia ulitumika Disemba mwaka jana kuandaa hafla za siku kuu ya Mashujaa.

Categories
Michezo

Mganda William Oloya kuzihukumu Gor Mahia na NAPSA Stars kombe la shirikisho

Mwamuzi wa Uganda William Oloya   atakuwa refa wa katikati ya uwanja katika mkondo wa kwanza wa mechi ya mchujo kuwania kombe la shirikisho la soka Afrika baina ya  Gor Mahia na  NAPSA Stars ya  Zambia Jumapili Februari 14 katika uwanja wa Taifa wa Nyayo.

Oloya atasaidiwa na Waganda wenza  Lee Okello atakayekuwa msaidizi wa kwanza, Isa Masembe msaidizi wa pili   Chelanget Ali Sabila ambaye atakuwa afisa wa nne.

Alexis Redamptus Nshimiyimana wa  Rwanda atakuwa kamisaaa wa mechi hiyo  huku Wycliffe Makanga,ambaye ni tabibu wa Harambee Dtars akiwa afisa wa afya kuhusu Covid 19.

NAPSA Stars  ambayo ni timu wafanyikazi wa mamlaka ya malipo ya uzeeni inatarajiwa kuwasili nchini Jumatano alasiri tayari kwa mkwangurano huo.

Kogalo watamenyana na NAPSA stars anayoichezea difenda wa Harambee Stars  David Owino Februari 14 kuanzia saa tisa katika uwanja wa nyayo kabla ya mechi ya marudio kupigwa nchini Zambia huku mshindi wa jumla akitinga hatua ya makundi ya kombe la shirikisho.

Categories
Michezo

Kocha Auseems ahudhuria mazoezi ya kwanza ya Ingwe

Kocha mpya wa AFC Leopards Patrick Auseems alihudhuria mazoezi ya  kwanza  ya timu hiyo Jumanne asubuhi saa chache baada ya kusaini mkataba wa kuifunza timu hiyo .

Mbelgiji huyo ambaye zamani alitwaa ubingwa wa ligi kuu  Tanzania akiwa  na  Simba SC  msimu wa mwaka 2018/2019  na  kufikia robo fainali ya ligi ya mabingwa Afrika ,ana leseni ya  EUFA PRO na anatwaa mikoba  ya ukufunzi kutoka kwa  Antony Kimani.

Kocha huyo aliye na umri wa miaka 55 pia amewahizifunza timu za Al Hilal ya Sudan akishinda kombe la Super na kunyakua ligi kuu nchini Congo na AC Leopards mwaka 2014 na amefanya ukufunzi kwa miaka 30 barani ualaua na Afrika.

Kocha Patrick Auseems akiongoza mazoezi ya AFC Leopards

Kibarua cha kwanza kwa kocha huyo akiwa usukani ni mechi ya raundi ya 64 bora kuwania kombe la FKF Jumapili ijayo mjini Wundanyi dhidi ya Taita Taveta Stars.

Auseems alikuwa difenda wa zamani wa klabu cha Stadard Liege nchini Ubelgiji.

 

Categories
Michezo

Mulee awajumuisha limbukeni katika kikosi cha Harambee Stars kwa mechi za kufuzu AFCON

Kocha wa Harambee Stars Jacob Ghost  Mulee ametaja kikosi cha wachezaji 28 wanaopiga soka humu nchini kujiandaa kwa mechi mbili za mwisho za kundi  G mwezi ujao  kufuzu kwa mashindano ya kombe la AFCON mwaka ujao nchini Cameroon.

Miongoni mwa wachezaji walioitwa kikosini kwa mara ya kwanza ni kipa wa KCB Joseph Okoth na mchezaji mwenza Nahashon Alembi pamoja na  kiungo wa AFC Leopards  Collins Shichenje huku pia kiungo wa Wazito FC kevin Kimani akijumuishwa kikosini kwa mara ya kwanza.

Henry Mejja ambaye ni mshambulizi kutoka Tukser Fc aliyefanya vyema katika mashindnao ya CECAFA kwa chipukizi walio chini ya umri wa miaka 20 mwaka jana pia amejumuishwa kikosini huku wakitarajiwa kuripoti kwa mazoezi ya kambi Jumatatu ijayo.

Kikosi kilichotajwa kinawajumuisha:-

Makipa

Brian Bwire (Kariobangi Sharks), James Saruni (Ulinzi Stars), Joseph Okoth (KCB), Peter Odhiambo (Wazito)

Mabeki

Johnstone Omurwa (Wazito), Michael Kibwage (Sofapaka), Samuel Olwande (Kariobangi Sharks), Nahashon Alambi (KCB), Bonface Onyango (Kariobangi Sharks), David Owino (KCB), Daniel Sakari (Kariobangi Sharks), Baraka Badi (KCB)

Viungo

Lawrence Juma (Sofapaka), Kenneth Muguna (Gor Mahia), Collins Shichenje (AFC Leopards), Micheal Mutinda (KCB), Musa Masika (Wazito), John Macharia (Gor Mahia), Reagan Otieno (KCB), James Mazembe (Kariobangi Sharks), Oliver Maloba (Nairobi City Stars), Bonface Muchiri (Tusker), Kevin Kimani (Wazito), Abdalla Hassan (Bandari)

Washambulizi

Erick Kapaito (Kariobangi Sharks), Elvis Rupia (AFC Leopards), Henry Meja (Tusker), Benson Omalla (Gor Mahia)

Stars iliyo ya tatu kundi G kwa pointi 3 baada ya mechi 4 itawaalika Misri tarehe 22  mwezi ujao kabla ya kuhitimisha ratiba ugenini tarehe 30 mjini Lome Togo.

Misri na Comoros wanaongoza kundi hilo kwa alama 8 kila moja wakisaka alama 1 kutoka kwa mechi mbili zilizosalia ili kufuzu kwenda AFCON mwakani.

 

Categories
Michezo

FKF kubuni mbinu ya kuteua mwakilishi wa CAF Confed Cup

Shirikisho la kandanda nchini FKF limebuni mbinu ya kutafuta mwakilishi wa Kenya kwa mashindano ya kombe la shirikisho endapo mashindano hayo yataahirishwa kama ilivyokuwa mwaka jana.

Akizungumza Alhamisi na wanahabari jijini Nairobi  katibu wa FKF  Barry Otieno ambaye anatumikia marufuku ya mwaka mmoja kutoka kwa CAF ,amefichua kuwa hawakuteua mwakilishi wa Kenya kwa mashindano hayo kutokana na kuahirishwa kwa mashindano ya kombe la FKF mwaka uliopita kutokan na janga la Covid 19.

“Fkf inaoperate na regulations lakini sasa we have a criteria of choosing a Winner if covid doesnt allow for the tournament to be played to the end”akasema Otieno.

Otieno amesisitiza kuwa shirikisho hilo halitaruhusu mashabiki uwanjani hivi karibuni kwani serikali haitoa ruhusa kutokana na msambao wa Covid 19.

Otieno alisema hayo baada ya kuongoza droo ya mchujo  wa kwanza wa mechi za kombe la FKF ,mechi zilizoratibiwa kuanza Februari 13 .

Kulingana na droo ya mechi hizo mabingwa watetezi Bandari Fc watafungua kibarua ugenini dhidi ya Murang’a Seal wakati Gor Mahia wakipangwa dhidi ya Congo Boys ya Mombasa mechi itakayoratibiwa upya kutokana na Gor kuwa na majukumu ya kombe la shirikisho.

AFC Leopards nao watamenyana na  Taita Taveta Allstars nao Sofapaka wazuru Kitale kutoana jasho na Kitale All Stars .

Mshindi wa kombe hilo atafuzu kuiwakilisha Kenya katika mashindano ya kombe la shirikisho la soka Afrika maarufu kama CAF Confed .

Ratiba ya mechi za raundi ya 64 bora kuwania kombe la FKF 

1.KSG Ogopa vs Dimba Patriots  2.Marafiki FC vs JKUAT FC  3.Taita Taveta Allstars vs AFC Leopards;

4.Alphonse FC vs Administration Police FC 5. Flamingo FC vs Kariobangi Sharks 6.Uprising FC vs Progressive FC

7.MYSA vs Machakos United 8.FC Shells vs Fortune Sacco 9.Mutono Tigers vs Nairobi City Stars

10.Tandaza FC vs MCF 11.Rware vs Posta Rangers FC 12. Muranga Seal vs Bandari FC 13. Congo Boys vs Gor Mahia FC 14. Kajiado North vs Nkanas FC

15. Mwatate United vs Twyford FC 16. Vegpro FC vs SS Assad FC 17.Bungoma Superstars vs Zetech Titans

18. Elim vs Ulinzi Stars 19. Sigalagala vs Dero 20 .MMUST vs Bidco United 21. Kiandege Jets vs KCB

22. Twomoc vs Naivas FC 23 .Luanda Villa vs GDC 24.Black Diamond Rangers vs Sindo United

25.Vihiga Spotiff vs Nation FC 26.Kobare United vs Egerton FC 27. Nax Fussball vs Mara Sugar

28.Mihuu United vs Tusker 29. Transfoc vs Migori Youth 30. Nyabururu Sportiff vs Keroka TTI 31. Blessings FC vs Equity FC 32. Kitale Allstars vs Sofapaka FC.

 

 

Categories
Michezo

Katibu mkuu wa FKF Barry Otieno apigwa marufuku ya miezi 6 na CAF kwa utundu

Sherikisho la kandanda barani Afrika Caf limempiga marufuku ya miezi 6 katibu mkuu wa shirikisho la soka nchini Kenya FKF Barry Otieno kwa utundu na ukaidi wakati wa mechi ya marudio ya kundi F kufuzu kwa fainali za AFCON dhidi ya Comoros mjini Moroni mwezi Novemba mwaka jana ambapo Kenya ilishindwa mabao 1-2.

Imebainika kuwa Otieno wakiwa na Team Manager wa Kenya Ronny Oyando walichelewesha na kukataa kutoa matokeo ya uchunguzi wa COVID 19 maarufu kama PCR tests ya wachezaji  wa Harambee Stars na kuchelewesha matokeo hayo kwa takriban saa tatu na kuyatoa muda mchache kabla ya kuanza kwa mechi.

Kamisaa wa mechi hiyo hakupata fursa ya kuangalia matokeo hayo baada ya Otieno na Oyando kumpokonya karatasi hiyo na kuirarua wakipinga matokeo ambapo wachezaji wane  wa Harambee Stars walikuwa wamepatikana na  COVID 19.

Uchunguzi wa matokeo hayo baada ya mechi uliashiria Kenya ilichezesha wachezaji 4 waliokuwa na virusi vya korona hivyo kuhatarisha maisha ya wachezaji na maafisa wengine waliokuwa katika mechi hiyo na kukiuka sheria za CAF kuhusu COVID 19.

Kufuatia kosa hilo FKF imepigwa faini ya shilingi milioni 2  huku Barry Otieno na Ronny Oyando wakifungiwa kujihusisha na mechi wala mashindano yoyote ya CAF kwa kipindi cha miezi 6.