Categories
Michezo

Charles Okere ateuliwa kocha wa Harambee Stars

Naibu kocha wa Tusker Fc Charles Okere ameteuliwa  kuwa kocha mkuu wa timu ya taifa ya wanawake Harambee Starlets.

Okere anatwaa mikoba ya ukufunzi kutoka kwa Daivid Ouma ambaye alijiuzulu kwa maafikiano.

Okere atasaidiwa na  naibu kocha wa KCB  Godfrey Oduor  na Mildred  Cheche ambaye pia amekuwa katika benchi ya ukufunzi wa timu ya KCB.

Kocha huyo mpya na wasaidizi wake wataiandaa Starlets kwa mechi ya kirafiki dhidi ya Zambia tarehe 24 mwezi huu mjini Lusaka na pia mechi za kufuzu kombe la mataifa ya Afrika na michuano ya CECAFA.

Categories
Michezo

Kikosi cha awali cha Harambee Starlets kwa mechi ya Zambia chatajwa

Kocha mkuu wa timu ya taifa ya soka ya wanawake Harambee Starlets , David Ouma ametangaza kikosi cha awali kwa mech ya kirafiki dhidi ya  Zambia tarehe 24 mwezi huu.

Martha Amnyolet aliyeshiriki mashindano ya CECAFA mwaka 2018 nchini Rwanda amerejeshwa kikosini wakati pia mabeki

Dorcas Shikobe  wa Thika Queens na  Foscah Nashivanga wakiwania nafasi ya beki kisiki.

Timu hiyo itaingia kambini tarehe 15 mwezi huu kwa maandalizi kwa mechi ya kirafiki dhidi ya Zambia maarufu kama Shepolopolo mjini Lusaka April 24.

Kikosi cha awali kilichotajwa kinawajumuisha:-

Makipa

Annette Kundu (AEL Champions) , Valentine Khwaka (Mathare United Ladies), Pauline Muthakye (Kibera Soccer Ladies), Judith Osimbo

Mabeki

Ruth Ingosi (AEL Champions), Quinter Owiti, Dorcas Shikobe (Thika Queens), Foscah Nashivanga, Nelly Sawe (Thika Queens), Leah, Vivian Nasaka (Vihiga Queens), Juliet Andipo (Kayole Starlet), Lucy

Viungo

Lillian Mmboga(Kibera Soccer Ladies), Vivian Corazone Aquino (Gaspo Women), Sheryl Angachi (Gaspo Women), Lydia Akoth (Thika Queens), Laventine Lihemo (Kibera Soccer Ladies), Topister Situma (Vihiga Queens), Puren Alukwe (Zetech Sparks), Diana Wacera (Gaspo Women), Rael Kamanda (Makolanders), Janet Bundi (Vihiga Queens), Siliya Rasoha (Ulinzi Starlets), Rachael Muema (Thika Queens), Martha Amnyolet

Washambulizi

Mwanahalima Adam (Thika Queens), Mercy Airo (Gaspo Women), Gily Okumu, Faith

Categories
Michezo

Harambee Stars yapanda nafasi mbili msimamo wa FIFA

Timu ya Harambee Stars imepanda kwa nafasi mbili kwenye msimamo wa dunia wa FIFA wa mwezi Machi uliotangazwa Jumatano.

Stars imechupa kutoka nafasi ya 104 duniani hadi ya 102 kufuatia ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya Togo katika mechi ya kufuzu AFCON na kutoka sare ya 1-1 dhidi ya Misri katika mchuano mwingine.

Kenya ni ya 23 barani Afrika kwa mjibu wa msimamo huo.

Senegal ingali kuongoza Afrika katika nafasi ya 22 ,licha ya kuteremka nafasi 2,ikifuatwa na Tunisia iliyosalia ya 26 wakati Super Eagles ya Nigeria ikikwea nafasi 4 hadi nambari 32 ,wakifuatwa na mabingwa wa Afrika Algeria katika nafasi ya 33.

Atlas Lions ya Moroko ni ya 34 na ya 5 Afrika ,Misri ikapanda nafasi 3 hadi nambari 46,wakifuatwa na Black Stars ya Ghana iliyo ya 49.

Cameroon,Mali na Ivory Coast zinaambatana katika nafasi za 55,57 na 59 katika usanjari huo katika nambari za 8 ,9 na 10 Afrika kwenye usanjari huo.

Uganda Cranes ingali ya kwanza Afrika Mashariki ikiwa ya 84 ikifuatwa na Kenya ,Rwanda na Tanzania katika nafasi za 102,129 na 137 mtawalia.

Nafasi 6 za kwanza ulimwenguni hazibadilika,Ubelgiji,Ufaransa na Brazil zikishikia nafasi za 1,2 na 3 mtawalia.

Uingereza ,Ureno na  Uhispania zimo katika nafasi za 4,5 na 6 kwenye usanjari huo wakati Italia ikipanda kwa nafasi 3 hadi nambari 7,nazo Argentina,Uruguay na Denmark zikiambatana katika nafasi za 8,9 na 10 katika usanjari huo.

Categories
Michezo

Harambee Stars kufungua mechi za kufuzu kombe la dunia dhidi ya Uganda mwezi Juni

Harambee Stars itaanza mechi za kundi E kufuzu kwa kombe la dunia mwaka ujao nchini Qatar dhidi ya majirani Uganda Cranes baina ya Juni 5 na 6  mwaka huu katika uwanja wa Kasarani .

Baadae Kenya watazuru Kigali kumenyana na Amavubi ya Rwanda aidha tarehe 12 au 13 Juni.

Kenya itacheza mechi ya tatu mjini Bamako dhidi ya Flying Eagles ya Mali kati ya Septemba 3 na 4  na kuialika Mali siku tatu baade.

Stars itazuru Kampala kwa mchuano wa tano utakaopigwa baina ya tarehe 6 na 7 Oktoba ,kabla ya kuhitimisha ratiba nyumbani dhidi ya Rwanda baina ya Oktoba 11 na 12 mwaka huu.

Timu itakayoongoza kundi hilo itafuzu kwa mchujo wa mechi za nyumbani na ugenini kisha mshindi wa jumla ajikatie tiketi kwenda Qatar kwa fainali za kombe la dunia kati ya Novemba na Disemba mwaka ujao.

Ratiba ya mechi za Kenya

Kenya vs Uganda – 5th/6th June

Rwanda vs Kenya – 12th/13th June

Mali vs Kenya – 3rd/4th Sept

Uganda vs Kenya – 6th/7th Oct

Kenya vs Rwanda – 11th/12th Oct

Categories
Michezo

Harambee Stars tayari kukamilisha kibarua cha Togo Jumatatu usiku mjini Lome

Timu ya taifa Harambee Stars itashuka uwanjani Keg’ue mjini Lome kupambana na wenyeji Sparrow Hawks ya Togo katika mechi ya mwisho ya kundi G kufuzu kwa fainali za kombe la AFCON mwakani nchini Cameroon.

Kenya iliyowasili Togo Jumamosi usiku ilifanya mazoezi ya kwanza katika uga wa Keg’ue Jumapili jioni inavyohitajika kujiandaa kwa mkwangurano huo.

Katika mechi ya Jumatatu usiku Kenya itakosa huduma za beki Samuel Olwande aliyelishwa kadi nyekundu katika sare ya 1-1 dhidi ya Misri wiki jana  na kiungo wa Gor Mahia Kenneth Muguna anayeuguza jeraha.

Stars na sparrow Hawks watatumia pambano hilo kujitayarisha kwa michuano ya kufuzu kwa kombe la dunia kuanzia mwezi  Juni baada ya timu zote kubanduliwa katika safari ya kufuzu kwenda AFCON.

Mshindi wa mechi hiyo atamaliza katika nafasi ya tatu ,Kenya ikiwa imezoa pointi 4 kutokana na mechi 5 huku Togo wakiwa na alama  2.

Kenya imejumuishwa kundi E  katika mechi za kufuzu kwa kombe la dunia kuanzia Juni mwaka huu pamoja na Mali,Rwanda na Uganda  wakati Togo wakiwa kundi E pamoja na Senegal,Namibia na Congo Brazaville.

 

Categories
Michezo

Harambee Stars yawasili Lome kwa mechi ya AFCON Jumatatu jioni

Timu ya Harambee Stars imewasili mjini Lome Togo mapama Jumapili tayari kwa pambano la mwisho la kundi G kufuzu kwenda fainali za AFCON mwaka ujao dhidi ya wenyeji Sparrow Hawks ya Togo Jumatatu jioni.

Wachezaji wa Stars wanatarajiwa kufanya mazoezi Jumapili jioni saa 24 kabla ya mechi ya Jumatatu kwa mjibu wa sheria za FIFA/CAF.

Timu zote zitatumia mchuano huo kujitayarisha kwa mechi za makundi kufuzu kwenda kombe la dunia mwaka ujao nchini Qatar ,baada ya kubanduliwa katika harakati za kufuzu kwa AFCON.

Mchuao huo utang’oa nanga saa moja usiku Jumatatu.

Hata hivyo Stars itakosa huduma za Kenneth Muguna anayeuguza jeraha.

Kikosi kamili cha Kenya kilichosafiri ni kama kifuatavyo:_

Makipa

Ian Otieno, James Saruni, Joseph Okoth

Mabeki

Eric Ouma, Joash Onyango, Clyde Senaji, Nahashon Alembi, Harun Mwale, Daniel Sakari,  Baraka Badi.

Viungo

Duke Abuya, Cliff Nyakeya, Lawrence Juma, Kevin Simiyu, Duncan Otieno, James Mazembe, David Owino, Kevin Kimani, Abdallah Hassan, Cliffton Miheso.

Washambulizi

Masud Juma, Michael Olunga ©, Elvis Rupia

Categories
Michezo

Michezo yafungwa kote nchini

Shughuli zote za michezo kote nchini  zimefungwa kutokana na ongezeko  la maambukizi  ya virusi vya Korona.

Kwenye hotuba yake kwa taifa Ijumaa Rais Uhuru Kenyatta amesema kuwa ,shughuli za michezo na mikusanyiko yote inayohusiana na michezo itafungwa hadi April 27 .

Hatua hii ina maana kuwa ligi kuu za soka,voliboli,mashindano ya magari,mashindano ya raga ya Kenya Cup  na riadha ambayo imekuwa ikiendelea itasitishwa hivyo basi kusongeza mbele muda wa kumalizika kwa michezo hiyo.

 

Categories
Michezo

Harambee Stars kuondoka kwenda Togo kwa mechi ya mwisho kufuzu AFCON kwa ndege ya kukodi

Timu ya taifa  Harambee Stars  itaondoka  nchini mapema Jumamosi kwa ndege ya kukodi  kwenda Lome Togo kwa mchuano wa mwisho wa kundi G kufuzu kwa fainali za kombe la  AFCON mwaka 2022 dhidi ya wenyeji Sparrow Hawks Jumatatu.

Kulingana na kinara wa FKF  Nick Mwendwa  ,ndege hiyo ya kukodi imewasaidia kukabiliana na changamoto za usafiri  kuelekea Afrika magharibi jinsi ambayo imekuwa.

“Timu itaondoka nchini Jumamosi kwa kutumia ndege ya kukodi kwenda Lome ,hivyo hatutakuwa na changamoto za usafiri kuelekea Afrika magharibi  jinisi imekuewa awali.

Kwa sasa tunajenga timu ya siku za usoni miaka kama 5 ,7 ijayo ndio maana tunatumia wachezaji chipukizi “akasema Mwendwa .

Togo na Kenya watakuwa wakicheza mechi ya kukamilisha ratiba baada wote kubanduliwa kwenda makala ya 33 ya fainali  AFCON siku ya Alhamisi Kenya wakiambulia sare ya 1-1 na Misri wakato Togo wakitoka sare kapa wenyeji Comoros.

Kenya sasa  itaanza maandalizi kwa mechi za makundi kufuzu kwa kombe la dunia kuanzia Juni mwaka huu wakiwa kundi moja na miamba wa Afrika magharibi Mali,na majirani Uganda na Rwanda.

Categories
Michezo

Misri yafuzu kwenda AFCON 2022 licha ya sare ya 1-1 na Kenya

Misri imejikatia tiketi kwa fainali za AFCON mwaka ujao nchini Cameroon ,licha ya kutoka sare ya bao 1-1 na Harambee Stars ya Kenya katika mchuano wa kundi G uliopigwa katika uga wa Kasarani Alhamisi usiku.

Kenya walianza mchuano huo kwa uzembe na kumruhusu kiungo wa Al Ahly Mohamed Magdi Kafsha kupachika bao la kwanza katika dakika ya pili ya mchezo.

Harambee Stars walijiszatiti lakini wakakosa kutumia vyema nafasi zao walizopata na kipindi cha kwanza kuishia  kwa uongozi wa Misri wa bao 1-0.

Stars waliendelea kujituma kipindi cha pili ndiposa beki Hamisi Abdala akasawazisha kunako dakika ya 65 na kukawa na matumaini ya ya kupata ushindi.

Hata hivyo kulishwa kadi nyekundu kwa difenda Jonstone Omurwa kulizima ndoto ya Kenya kupata bao la ushindi huku mechi ikiishia sare ya 1-1.

Matokeo hayo yana maana kuwa Misri na Comoros zimefuzu kwenda AFCON kutoka kundi G baada ya Comoros pia kutoka sare ya 0-0 na Togo,zikiwa na pointi sawa 9 wakifuatwa na Kenya kwa alama 4 huku Togo wakiburura mkia kwa alama 2.

Kenya itasafiri Jumamosi kwenda Togo kupiga mchuano wa mwisho wa kuhitimisha tu ratiba wakati Misri ikikamilishia kibarua nyumbani dhidi ya Comoros.

Categories
Michezo

Mashabiki hawataruhisiwa uwanjani Kasarani mechi ya Kenya na Misri

Mashabiki hawataruhiswa kuingia uwanjani Kasarani Alhamisi usiku  katika mechi ya kufuzu kwa kombe la AFCON baina ya Kenya na Misri kuanzia saa moja usiku.

Kulingana na taarifa kutoka kwa waziri wa michezo DKT Amina Mohammed ,mashabiki bado wamefungiwa kuingia uwanjani.

Hata hivyo Mashabiki watapata afueni kutazama pambano hilo kupitia runinga ya KBC Channel 1 ambayo itarusha mechi hiyo mbashara.

Hali ya usalama pia umeimarishwa   huku washika doria wakipelekwa Kasarani kabla,wakati na baada ya mechi.