Categories
Michezo

Uingereza kutuma ombi la kuandaa kombe la dunia mwaka 2030

Uingereza imepanga kuwasiliasha ombi rasmi la kuandaa fainali za kombe la dunia mwaka 2030 wakishirikiana na Jamhuri ya Ireland.

Kulingana na waziri mkuu wa Uingereza Boris Johnson watawasilisha ombi hilo  kirasmi Jumatano hii huku wakiahidi kutenga bajeti ya pauni milioni 2 nukta 8 .

FIFA itafungua kuchuku maombi ya maandalizi ya dimba la kombe la dunia mwaka 2030,mapema mwaka ujao.

Uwanja wa Wemley utaandaa mechi 7 za kombe la Euro kwa mataifa ya ulaya baina ya  Juni na Julai mwaka huu ikiwemo nusu fainali na fainali huku miji ya Dublin na Glasgow  ikiandaa mechi mbili.

Uingereza tayari imepata uungwaji mkono kutoka kwa mataifa yake kama vile Jamhuri ya Irelenda,Scotland na Wales.

Uingereza iliandaa fainali za kombe la dunia kwa mara ya kwanza na ya pekee mwaka 1966 na ilishindwa na Urusi kwenye maombi ya kuandaa kipute cha mwaka 2018.

Chile,Argentina,Paraguay na Uruguay wanatarajiwa kutuma ombi la pamoja kuandaa kombe la dunia wmaka 2030 sawa na Moroko,Ureno na Uhispania ambao pia wanapanga kutuma ombi la pamoja kwa fainali hizo pia.

Fainali za kombe la dunia kuanzia mwaka 2026 zitashirikisha mataifa 48 zikiandaliwa kwa  pamoja na mataifa ya  ,USA,Canada na Mexico.

Qatar itakuwa mwenyeji wa fainali za mwaka ujao kati ya Novemba na Disemba.

Categories
Michezo

Gor na Wazito FC wafungiwa kusajili wachezaji kwa mwaka mmoja kwa kushindwa kuwalipa wachezaji

ShirikIsho la soka ulimwenguni FIFA   limezipiga marufuku timu za  Gor Mahia  na  Wazito Fc kusaini wachezaji wapya kuanzia msimu huu  wa uhamisho wachezaji kwa kushindwa kuwalipa wachezaji  Dickson Ambudo na   Augustin Otu  mtawalia.

Yamkini gor walishindwa kumlipa wing’a wa Tanzania Ambudo shilingi milioni 1 nukta 2 alipowachezea  yakiwa malimbikizi ya mshahara na marupurupu huku Wazito wakikosa kumlipa  Otu kutoka Liberia shilingi milioni 1 baada ya kukatiza kandarasi yake kwa njia isiyofaa kinyume na kandarasi.

Ambudo na  Otu walikuwa wamewasilisha kesi yao kwa jopo la kutatua mizozo kwenye shirikisho la FIFA  disemba 16 na 26 mtawalia.

Vilabu hivyo vilipewa makataa ya siku 45 kuwalipa wachezaji hao au vipigwe marufuku .

Hata hivyo inasubiriwa kuona hatua ambayo FKF itazichukulia timu hizo mbili kwani kogalo walikuwa wamekamilisha usajili wa mshmabulizi wa Brazil Wilson Silva Fonseca, nahodha wa zamani Harun Shakava  na  Abdul Karim Nikiema Zoko  kutoka Burkina Fasso kwa kandarasi ya miaka miwili kila mmoja.

Upande mwingine , Wazito walimsajili kiungo wa Sopaka  Eli Asieche.

Endapo zitawalipa wachezaji hao ,timu hizo mbili ziko huru kusajili wachezaji wapya kuanzia Agosti mwaka ujao.

Ambudo,ambaye kwa sasa anachezea timu ya  Dodoma Jiji  katika ligi kuu ya Tanzania bara aliondoka Gor Julai mwaka jana baada ya kukamilika kwa mkataba wake  wa mkopo wakati Otu akiwa kati ya wanandinga 12 waliotimuliwa na usimamizi wa Wazito Fc Julai mwaka jana.

 

 

 

Categories
Michezo

Olunga apiga dakika 46 huku ndoto yake ya kucheza na Bayern Munich ikizimwa na Al Ahly

Mshambulizi wa Harambee Stars Michael Olunga alicheza dakika 46 kabla ya kuondolewa uwanjani katika ushinde wa timu yake  ya Al Duhail Sc wa bao  1 na mabingwa wa Afrika Al Ahly katika kwota fainali ya kombe la dunia baina ya vilabu  katika uwanja wa Education City Stadium mjini  Al Rayyan nchini Qatar Alhamisi usiku.

Ilikuwa mechi ya kwanza kwa Olunga kucheza katika fainali hizo za kombe la dunia akiwakilisha mabingwa hao watetezi wa ligi kuu nchini Qatar tangu ajiunge  nao mwezi uliopita kutoka kashiwa Reysol ya Japan.

Tobwe la Hussein El Shahat kunako dakika ya 30 liliotosha kuwapa Ahly maarufu Red Devils kutoka Misri ushindi huo ambao uliwafuzisha kwa nusu fainali watakapochuana na mabingwa wa ulaya Bayern Munich Februari 8 wakilenga kuwa timu ya pili ya Afrika kucheza fainali ya kombe hilo baada ya TP Mazembe ya Jamhuri ya demokrasia ya Congo.

Katika mechi nyingi ya robo fainali mabingwa wa Marekani Kaskazini  Tigres UNL ya Mexico waliibandua Ulsan Hyundai ya Korea Kusini mabao 2-1 na kufuzu kwa nusu fainali kuchuana na mabingwa wa Amerika Kusini  Palmeiras ya Brazil .

Al Duhail watarejea uwanjani dhidi ya mabingwa wa Asia Ulsan kuwania nafasi ya 5 na 6 tarehe 7 kabla ya fainali ya tarehe  11 mwezi huu.

Mashindano hayo hushirikisha  mabingwa wa kila bara na huandaliwa kila mwaka .

 

Categories
Michezo

Timu ya Olunga Duhail yaangukia Ahly Droo ya kombe la dunia kwa vilabu mwezi ujao

Timu ya Al Duhail Sc  ya Qatar anakocheza Michael Olunga imeratibiwa kuchuana na mabingwa wa Afrika mara 9 Al Ahly  kutoka Misri katika mchuano wa pili wa fainali za kombe la dunia baina ya vilabu mwezi ujao nchini Qatar.

Kwa mjibu wa droo iliyoandaliwa Jumanne jioni mjini Zurich Uswizi mabingwa wa bara Asia Ulsan Hyundai ya Korea Kusini watapiga mechi ya kwanza dhidi ya Tigres ya Mexico Februari 4 mwaka huu katika uwanja wa Ahmad Bin Ali , kabla ya mabingwa wa Qatar Al Duhail Sc kumenyana  Al Ahly katika mechi ya pili  dhidi ya Ahly katika kiwara cha Education City.

Mshindi wa pambano kati ya Ulsan na Tigres atakutana na mabingwa wa Amerika kusini ambao watabainika katika fainali ya kuwania kombe la Libertadores baina ya Santos Fc na Palmeiras zote za Brazil ,nusu fainali hiyo ikichezwa Januari 30 .

Atakayeshinda robo fainali baina ya Ahly na Duhail atapimana nguvu na mabingwa wa Ulaya Bayern Munich kwenye nusu fainali ya pili kisha washindi watoane jasho tarehe 11 mwezi ujao katika fainali.

Mashindano ya kombe la dunia baina ya vilabu hushirikisha timu 6 mabingwa wa kila bara ,wakati bara wenyeji wakiwakilishwa  na timu  2 .

 

Categories
Michezo

Rais wa FIFA Infantino atua Cameroon kufungua CHAN

Rais wa FIFA Gianni Infantino  amewasili mjini Younde  Cameroon mapema ijumaa tayari kufungua rasmi makala ya 6 ya fainali za kombe la CHAN Jumamosi jioni.

Kaimu Rais wa CAF  Constant Omari  na nyota wa soka Afrika Samuel Etoo walimpokea Infantino punde alipowasili .

Infantino anatarajiwa kuongoza  kikao na baraza kuu la CAF Ijumaa ambapo atamtawaza kinara wa zamani wa CAF  Issa Hayatou  .

Mechi ya Ufunguzi ya CHAN itapigwa Jumamosi saa moja usiku wenyeji Indomitable Lions wakivaana na Zimbabwe katika uwanja wa  Ahmadou Ahidjo .

Mechi 32 za kipute hicho zitachezwa katika viwanja vinne katika miji mitatu ya Yaounde,Limbe na Doula.

Mataifa 16 yanayowashirikisha wachezaji wanaocheza katika ligi za nyumbani pekee watashiriki mashindano hayo ya wiki tatu huku fainali yake ikipigwa Februari 7.

Categories
Michezo

Taswira ya vifo vya wanaspoti mwaka 2020

Mwaka 2020 umeshuhudia magwiji wengi wa michezo wakiaga dunia kutokana na sababu mbalimbali.

Miongoni mwa nyota wa michezo waliofariki ni mchezaji  wa zamani wa Senegal  Pope Diouf  ambaye alihudumu kama Rais wa klabu ya  Olympiaue Marseille aliaga dunia mwezi April akiwa na umri wa miaka 68 kutokana na ugonjwa wa Covid 19 .

Akiwa Rais wa Marseille kati ya mwaka 2005 na 2009  timu hiyo ilimaliza ya pili, mara mbili katika ligi kuu Ufaransa  na kucheza fainali mbili za kombe la Ufaransa .

Pope Diouf

Paolo Rossi, mchezaji aliyekuwa katika kikosi cha Italia kilichotwaa kombe la dunia mwaka 1982 pia alifariki mapema Disemba mwaka huu akiwa na umri  wa  miaka 64.

Paolo Rosi

Gerard Houllier wa Ufaransa ambaye pia alikuwa meneja wa zamani wa Liverpool aliaga dunia akiwa na umri wa miaka 73 ,na kiwa meneja wa Liverpool kati ya mwaka 1998 na 2004 alitwaa mataji matatu.

Gerrard Houlier

Nahodha wa Cameroon miaka ya 90 Stephen Tataw pia alifariki ,na atakumbukwa  wakiwa pamoja na  Roger Milla na Francois Omam-Biyik,kwenye fainali za kombela dunia Indomitable Lions ikicheza hadi robo fainali .

Stephen Tataw

Mchezaji wa zamani wa  timu Afrika Kusini  Anele Ngongca pia alifariki kupitia ajali ya barabarani.

Ulimwengu pia uliomboleza kifo cha  nyota wa mpira wa kikapu  Kobe Bryant  aliyekuwa na umri wa miaka 41 ,aliyeangamia kwenye ajali ya ndege akiwa na binti yake .

Kobe Bryant

Mwezi Novemba pia kiungo mkabaji  wa Senegal kwenye kombe la dunia mwaka 2002 Papa Bouba Dioup alifariki akiwa na umri wa miaka 42.

Pia Disemba beki wa kati wa klabu ya Mamelodi Sundowns Motjeka Madisha alifariki kupitia ajali ya barabarani akiwa na umri wa miaka 25.

Diop baada ya kufunga bao mwaka 2002  dhidi ya Ufaransa

Nyota wa Argentina  Diego Maradona  alifariki   Novemba 25 akiwa na umri wa miaka 60 baada ya kuugua kwa muda kutokana na sababu kadhaa.

Maradona anakumbukwa kwa bao alilofunga kwa mkono katika robo fainali ya kombe la dunia dhidi ya Uingereza mwaka 1986 akiwa nahodha na pia kusaidia kuishinda Ujerumani Magharibi kwenye fainli.

Diego Maradona

Nchini Kenya nyota wa michezo walioangamia ni kama:-

Beki  Tonny Onyango mchezaji raga wa kilabu cha KCB  alifariki akiwa na umri wa miaka 28 baada ya kuanguka na kufariki akiwa nyumbani kwake Ngong mapema mwezi Machi mwaka huu .

Hadi kifo chake Onyango alichezea timu za taifa kwa chipukizi kabla ya kuteuliwa kuichezea timu ya taifa kwa wachezaji 15 kila upande Simbas mwaka 2012.

Tonny Onyango

Charles Oguk mchezaji hoki wa timu ya taifa  aliyeshiriki Olimpiki mwaka 1988 alifariki akiwa na umri wa miaka 56 .

Uguk pia alishiriki michezo ya bara Afrika mwaka 1987 jijini Naiorobi na kuisaidia timu hiyo kutwaa medali ya fedha.

Taifa pia lilimpoteza kocha wa soka  Henry Omino mara ya mwisho akiifunza Western Stima , aliyefarifiki mwezi Machi akiwa na umri wa miaka  71 kutokana na saratani na alikuwa amefanya ukufunzi tangu mwaka  1975.

Henry Omino

Mshambulizi wa zamani wa Harambee Stars  na Gor Mahia ,Martin Ouma maarufu kama Ogwanjo alifariki mwezi Mei akiwa na umri wa miaka  71 kutoka na kiharusi,akiwa kwenye timu iliyoshiriki fainali za Afcon mwaka 1972 nchini Cameroon.

Pia sekta ya Soka ilimpoteza Suleiman Khamisi Shamba, beki wa zamani wa Harambee Stars akiwa na umri wa miaka 62 kutokana na matatizo ya figo .

Alikuwa kwenye kikosi cha Kenya kilichonyakua kombe la Cecafa miaka 1981,83 na 85.

Katika Mwezi Agosti pia Kevin Oliech kakake mdogo Dennis Oliech alifariki nchini Ujerumani kutokana na saratani akiwa na umri wa miaka 31.

Katika enzi zake alichezea timu za Mathare United,Tusker Fc,Nairobi City Stars,Thika United,Ushuru Fc,Nakumatta Fc  na Gor Mahia huku akichukua ubingwa wa ligi na mathare mwaka 2008.

Kevin Oliech

Raga pia ilimpoteza Allan Makaka, akiwa na umri wa miaka 38 baada ya wing’a huyo kuhusika katika ajali barabarani .

Hadi kifo chake alikuwa amechezea timu za Ulinzi na Herlequins na pia timu ya wachezaji iliyoshiriki kombe la dunia mwaka 2005 na michezo ya jumuiya ya madola ,mwaka 2006.

Allan Makaka

Dickson Wamwiri, mchezaji Taekwondo aliyeshiriki michezo ya Olimpiki mwaka 2008  na kunyakua dhahabu katika michezo ya Afrika mwaka 2007 aliaga dunia akiwa na umri wa miaka 35

Ben Jipcho gwiji wa riadha alifariki Julai 24 katika Hospitali ya Fountain mjini Eldoret kutoka na viungo vyake vingi mwilini kudinda kufanya kazi.

Ben Jipcho

Jipcho alianza riadha mapema miaka ya 60 na aliishindia Kenya dhahabu katika mita  5000 michezo ya Afrika mwaka 1973  na dhahabu katika michezo ya jumuiya ya madola mwa 74 mbio za mita 5000 na mita 3000 kuruka viunzi na maji na shaba ya mita 1500.

Rosemary “Mara” Aluoch, kipa wa zamani wa timu ya soka ya wanawake ya Kenya aliaga akiwa na umri wa miaka  44 na anakumbukwa kuichezea Harambee starlets baina ya mwaka 1995 na 2012.

Rosemary Aluoch Mara

Mshindi mara 4 wa mashindano ya gofu ya Kenya Open Edward Legei, alifariki Novemba akiwa na umri wa miaka  56.

Mohammed  Hatimy aliyekuwa Rais wa shirikisho la soka nchini baina ya mwaka 2005 na 2011 alifariki Novemba 14 kutokana na ugonjwa wa Covid 19 .

Mohammed Hatimy

Meneja wa muda mrefu wa klabu ya Nairobi City Stars Neville Pudo,alifariki akiwa na umri wa miaka  63 akiwa nyumbani kwake .

Nevile Pudo

Kwa jumla mwaka 2020 tumewapoteza wanamichezo wengi kwa sababu mbalimbali lakini pia gonjwa la Covid 19 limechangia kwa idadi ya vifo hivyo.

Kunao nyota wengine wa michezo ambao sijawataja lakini kwa familia za wanamichezo wa Kenya waliotuacha mwaka 2020 ,,,,,,,Makiwa.

 

 

Categories
Michezo

Taswira ya matukio makuu ya soka 2020

Mwaka 2020 umekuwa na matukio machache ya soka kuliko ilivyotarajiwa kutokana na kuzuka kwa ugonjwa wa Covid 19 .

Barani Afrika  mashindano ya kombe la CHAN yalipaswa kuandaliwa mwezi April nchini Cameroon,pia fainali za kombe la Euro barani Ulaya  na mashindano mengine makuu yakiahirishwa hadi mwaka ujao.

Sadio Mane wa Senegal na Liverpool ,alitawazwa mwanasoka bora Afrika kwa mara ya kwanza mapema Januari.

Hata hivyo Ligi nyingi za bara Afrika na mabara mengine zilifutiliwa mbali huku chache zikiahirishwa .

Nchini Kenya msimu wa ligi kuu ulifutiliwa mbali huku Gor Mahia wakitawazwa mabingwa baada ya mechi 23 pekee  wakiwa na  alama 54.

Pia mechi za Harambee Stars za Kundi  G kufuzu kombe la AFCON zilizokuwa zichezwe mwezi Machi dhidi ya Comoros nyumbani na ugenini zilisongezwa mbele hadi Novemba mwaka huu  Kenya wakipoteza nafasi ya kufuzu baada ya kutoka sare  ya 1-1 nyumbani kabla ya kushindwa 1-2 ugenini .

Mechi mbili za mwisho kuchezwa Machi mwaka ujao Kenya ikihitaji kushinda mechi zote na kutarajia kuwa Misri na Comoros wanaongoza kundi hilo  watakosa kuzoa pointi.

Kenya inasalia kuanza kujipanga kwa mechi za kufuzu kwenda Afcon ,mwaka 2023 kwani hawana fursa ya kufuzu kwenda Cameroon mwaka 2022.

Ligi kuu ya Soka  msimu wa mwaka 2020/2021 hatimaye  ilianza Novemba 28 ikifuatwa na ligi ya Nsl wiki moja baadae na ligi kuu ya Wanawake.

Soka ya bara Afrika ilishuhudia klabu ya RS Berkane ya Moroko ikitawazwa mabingwa wa kombe la shirikisho kwa mara ya kwanza kwa kuwashinda Pyramids kutoka Misri  bao 1-0  mwezi Oktoba wakati Al Ahly  ya Misri ikiwazidia maarifa Zamalek  2-1 na kunyakua kombe la ligi ya mbingwa Afrika  kwa mara ya 9 .

Barani Ulaya Bayern Munich walishinda kombe la ligi ya mabingwa kwa mara ya 6 ,baada ya kuwaangusha PSG bao  1-0 wakati Seville wakishinda Europa League kwa kuinyuka Intermilan  3-2 na kushinda kombe hilo kwa mara ya 6.

Rais wa CAF Ahmad Ahmad alipigwa marufuku ya miaka mitano  na kitengo cha maadili cha FIFA  mwezi Novemba kwa makosa kadhaa ya ufisadi na matumizi mabaya ya Afisi.

Ligi mbalimbali za mabara yote hatimaye zilirejelewa au kuanza upya huku  pia bara Amerika kusini likicheza mechi nne za kufuzu kwa kombe la dunia mwaka 2022 baina ya Oktoba na Novemba.

 

 

Categories
Michezo

Uwanja wa Bin Ali utakaondaa kipute cha kombe la dunia mwaka 2022 wazinduliwa

Uwanja wa Ahmad Bin Ali ulizinduliwa rasmi  Ijumaa nchini Qatar  sherehe hiyo pia ikiadhimisha miaka 2 kabla ya mechi  ya fainali kuwania kombe la dunia mwaka 2022  kuchezwa.

Uzinduzi wa uwanja huo unaomudu mashabiki 40,000 uliambatana na sherehe za kitaifa nchini Qatar huku ukiwa wa hivi punde  na wa nne kuwa tayari kwa  kindumbwendumbwe cha kombe la dunia baada ya ya   Khalifa International, Al Janoub na  Education City .

Sherehe hiyo ilihudhuriwa na Rais wa FIFA  Gianni Infantino, Rais wa shirikisho la soka barani Asia  Shaikh Salman bin Ebrahim Al Khalifa, kinara wa CONMEBOL Alejandro Domínguez na mwenzake wa  UEFA Aleksander Čeferin.

Dimba la kombe la dunia litaandaliwa  kati ya Novemba 18 na Disemba 18 mwaka 2022.

  
Categories
Michezo

Lewandowski avunja ukiritimba wa Ronaldo na Messi na kushinda tuzo ya FIFA ya mwanasoka bora

Mshambulizi wa Poland  na klabu ya Bayern Munich Rober Lewandowski alitawazwa mwanasoka bora wa mwaka katika tuzo za Fifa  Alhamisi usiku.

Lewendowksi aliye na umri wa miaka 32 aliongoza Bayern Munich kunyakua kombe la ligi ya mabingwa Ulaya kando na kushinda ligi kuu Ujerumani na kombe la Ujerumani  na kuibuka mfungaji bora nchini ujerumani na katika ligi ya mabingwa  Ulaya.

Mshambulizi huyo wa Poland ndiye mwanasoka wa kwanza kuvunja utawala wa  Cristiano Ronaldo na Lionell Messi  katika tuzo za FIFA tangu Ronadhino Gauto mwaka 2005 ni kwa mwaka wa pili ndani ya miaka mitano ambapo Ronaldo na Messi wanapigwa kumbo katika tuzo hiyo.

Orodha ya mwisho ya tatu bora ilikuwa na Lewandowski Roaldo na Messi huku mshambulizi huyo wa Poland akiwa mchezaji wa kwanza anayepiga soka ya kulipwa nchini Ujerumani kunyakua tuzo huyo.

Lewandowski alipata kura 52 akifuatwa na Ronaldo kwa kura 38 ,tatu zaidi ya Messi.

Kwa Jumla Ronaldo amenyakua tuzo hiyo ya FIFA mara mbili mwaka  2016,2017 ,Messi akainyakua  mwaka 2019 naye Luka Modric akitawazwa mshindi mwaka  2018.

Tuzo ya mchezaji bora kwa wanawake ilinyakuliwa na  beki wa Uingereza Lucky Bronze baada ya kuwapiku Wendie Renard wa Ufaransa na Parnille Hander wa Norway.

Jurgen Klopp aliibuka kocha bora wa mwaka kwa wanaume kwa mwaka wa pili mtawalia kwa kuiongoza  the reds kushinda  taji ya ligi kuu  Uingereza kwa mara ya kwanza baada ya subira ya miaka 30 na kuzoa alama 99 .

Klopp aliwashinda Marcelo Bielsa wa Leeds United na Hans Dieter Flick wa Bayern Munich.

Sarina Wiegman wa Uholanzi alinyakua tuzo ya kocha bora wa mwaka kwa wanawake .

 

Categories
Michezo

Safari ya kwenda Qatar kutoka Ulaya kuanza Machi 2021

Mataiafa ya Ulaya 55 yataanza mechi za makundi kufuzu kwa dimba la kombe la dunia nchini Qatar baina ya Machi na Novmber mwaka ujao.

Kwa mjibu wa droo iliyoandaliwa Jumatatu usiku mjini Zurich Uswizi mataifa hayo 55 yametengwa katika makundi 10 huku timu itakayoongoza kila kundi baada ya mechi za makundi zikifuzu kwenda kombe la dunia .

Mataifa 10 bora katika nafasi za pili kutoka kila kundi na timu 2 bora kutoka mashindano ya UEFA Nations League yatajumuishwa pamoja kwenye droo kila timu ikicheza mchujo  na wapinzake wake wawili huku timu 3 bora zitakazoshinda pia zikijikatia tiketi kupiga kombe la dunia nchini Qatar kati ya Novemba na Disemba mwaka 2022.

Michuano ya mchujo itapigwa Machi mwaka 2022.

Bara ulaya litawakilishwa na mataifa 13  kwenye fainali za kombe la dunia mwaka 2022,wakati Afrika ikitengewa nafasi 5,Asia nafasi 4,Marekani Kusini nafasi 4 ,

eneo la Conacaf nafasi 3,Oceania nafasi 1 au 0,waandalizi Qatar huku nafasi nyingine  zikijazwa kupitia michujo baina ya mabara.

Tayari bara Amerika Kusini limecheza mechi nne   za makundi za kufuzu kwa kombe la dunia huku bara Afrika ikipanga kuanza michuano yake mwezi Juni mwaka ujao.