Categories
Michezo

Bayern Munich watwaa kombe la dunia baada ya kuwazidia maarifa Tigres

Bayern Munich ndio mabingwa wa dunia baina ya vilabu baada ya kuwalemea Tigres UANL kutoka Mexico bao 1-0 katika mechi  fainali iliyosakatwa uwanjani Education City nchini Qatar.

Bao la pekee na la ushindi kwa Munch maarufu kama Bavarians lilipachikwa kimiani na Benjamin Pavard kunako dakika ya 59  .

Kombe hilo lililkuwa la 6 kwa Munich na la pili la dunia  na kusawazisha rekodi ya Pep Guardiola aliyetwaa mataji 6 na Baverians msimu wa mwaka 2009/2010.

Mabingwa wa Afrika Al Ahly walinyakua nishani ya shaba baada ya kuwalemea mabingwa wa Marekani Kusini Palmeiras kutoka Brazil mabao 3-2 kupitia mikiki ya penati kufuatia sare tasa dakika 90.

Categories
Michezo

Bayern Munich kupimana nguvu na U.A.N.LTigres fainali ya kombe la dunia

Mabingwa wa Ulaya Bayern Munich watakuwa wakiwinda taji ya pili ya kombe la dunia baina ya vilabu ulimwenguni watakaposhuka uwanjani Education City nchini Qatar kumenyana na mabingwa wa Amerika Kaskazini U.A.N.L Tigres kutoka Mexico  .

Munich walishinda kombe la dunia kwa mara ya kwanza mwaka 2013  na walifuzu kwa fainali ya Alhamisi baada ya kuwashinda mabingwa wa Afrika Al Ahly mabao 2-0 katika nusu fainali wakati Tigres ikiwabandua mabingwa wa Amerika Kusini Palmeiras bao 1-0 katika nusu fainali nyingine.

Al Ahly ambao ni mabingwa Afrika watashuka uwanjani Education City kukabiliana na  Palmeiras  ya Brazil katika mechi ya kuwania nafasi ya tatu na nne .

Mashindano hayo yalikuwa yaandaliwe Disemba mwaka jana kabla ya kuahirishwa  hadi mwaka huu kutokana na ugonjwa wa Covid 19.

Categories
Michezo

Olunga apiga dakika 46 huku ndoto yake ya kucheza na Bayern Munich ikizimwa na Al Ahly

Mshambulizi wa Harambee Stars Michael Olunga alicheza dakika 46 kabla ya kuondolewa uwanjani katika ushinde wa timu yake  ya Al Duhail Sc wa bao  1 na mabingwa wa Afrika Al Ahly katika kwota fainali ya kombe la dunia baina ya vilabu  katika uwanja wa Education City Stadium mjini  Al Rayyan nchini Qatar Alhamisi usiku.

Ilikuwa mechi ya kwanza kwa Olunga kucheza katika fainali hizo za kombe la dunia akiwakilisha mabingwa hao watetezi wa ligi kuu nchini Qatar tangu ajiunge  nao mwezi uliopita kutoka kashiwa Reysol ya Japan.

Tobwe la Hussein El Shahat kunako dakika ya 30 liliotosha kuwapa Ahly maarufu Red Devils kutoka Misri ushindi huo ambao uliwafuzisha kwa nusu fainali watakapochuana na mabingwa wa ulaya Bayern Munich Februari 8 wakilenga kuwa timu ya pili ya Afrika kucheza fainali ya kombe hilo baada ya TP Mazembe ya Jamhuri ya demokrasia ya Congo.

Katika mechi nyingi ya robo fainali mabingwa wa Marekani Kaskazini  Tigres UNL ya Mexico waliibandua Ulsan Hyundai ya Korea Kusini mabao 2-1 na kufuzu kwa nusu fainali kuchuana na mabingwa wa Amerika Kusini  Palmeiras ya Brazil .

Al Duhail watarejea uwanjani dhidi ya mabingwa wa Asia Ulsan kuwania nafasi ya 5 na 6 tarehe 7 kabla ya fainali ya tarehe  11 mwezi huu.

Mashindano hayo hushirikisha  mabingwa wa kila bara na huandaliwa kila mwaka .

 

Categories
Michezo

Olunga alenga kuandikisha historia kucheza FIFA World Cup

Mshambulizi  wa Harambee Stars Michale Olunga anatarajiwa kuingia kwenye madaftari ya kumbukumbu kuwa Mkenya wa kwanza kucheza mashindano ya kombe la dunia baina ya vilabu yatakayoanza  Alhamisi hii nchini Qatar.

Olunga aliye na umri wa miaka 26 amejumuishwa kwenye kikosi cha klabu ya Al Duhail Sc  huku wakicheza mchuano wa ufunguzi Alhamisi Februari 4 dhidi ya mabingwa wa Afrika Al Ahly kutoka Misri.

Awali Mc Donald Mariga alikuwa kwenye kikosi cha Inter Milan ya Italia kilichonyakua kombe la dunia mwaka 2010 katika muungano wa Milki za kiarabu.

Olunga ambaye aliibuka mfungaji na mchezaji bora katika ligi kuu ya Japan mwaka jana akiwa na klabu ya Kashiwa Reysol alijiunga na mabingwa hao wa Qatar kwa kima cha shilingi milioni 933 ambapo anakisiwa kulipwa mara dufu ya mshahara aliokuwa akilipwa akiwa Japan .

Mshambulizi huyo wa Kenya anatarajiwa kuichezea Al Duhail katika mechi ya robo fainali ya kombe la dunia Alhamisi dhidi ya mabingwa mara 9 wa Afrika Al Ahly baada ya kujumuishwa kwenye kikosi cha wanandinga 23 wa mabingwa hao watetezi wa ligi kuu Qatar zamani wakifahamika kama Lakhwiya.

Katika mechi nyingine ya robo fainali ya Alhamisi mabingwa wa Marekani kaskazini Tigres UNL  ya Mexico itapambana na mabingwa wa bara Asia Ulsan Hyundai.

Mashindano ya kombe la dunia kati ya vilabu yanajumuisha mabingwa wa kila bara ,Ulaya ikiwakilishwa na Bayern munich na Palmeiras wakiwakilisha Marekani Kusini  huku fainali yake ikisakatwa Februari 11.

 

 

 

Categories
Michezo

Timu ya Olunga Duhail yaangukia Ahly Droo ya kombe la dunia kwa vilabu mwezi ujao

Timu ya Al Duhail Sc  ya Qatar anakocheza Michael Olunga imeratibiwa kuchuana na mabingwa wa Afrika mara 9 Al Ahly  kutoka Misri katika mchuano wa pili wa fainali za kombe la dunia baina ya vilabu mwezi ujao nchini Qatar.

Kwa mjibu wa droo iliyoandaliwa Jumanne jioni mjini Zurich Uswizi mabingwa wa bara Asia Ulsan Hyundai ya Korea Kusini watapiga mechi ya kwanza dhidi ya Tigres ya Mexico Februari 4 mwaka huu katika uwanja wa Ahmad Bin Ali , kabla ya mabingwa wa Qatar Al Duhail Sc kumenyana  Al Ahly katika mechi ya pili  dhidi ya Ahly katika kiwara cha Education City.

Mshindi wa pambano kati ya Ulsan na Tigres atakutana na mabingwa wa Amerika kusini ambao watabainika katika fainali ya kuwania kombe la Libertadores baina ya Santos Fc na Palmeiras zote za Brazil ,nusu fainali hiyo ikichezwa Januari 30 .

Atakayeshinda robo fainali baina ya Ahly na Duhail atapimana nguvu na mabingwa wa Ulaya Bayern Munich kwenye nusu fainali ya pili kisha washindi watoane jasho tarehe 11 mwezi ujao katika fainali.

Mashindano ya kombe la dunia baina ya vilabu hushirikisha timu 6 mabingwa wa kila bara ,wakati bara wenyeji wakiwakilishwa  na timu  2 .