Timu ya taifa ya Kenya Morans imerejea nyumbani mapema Jumatano kutoka Yaounde Cameroon ilikoshiriki michuano ya kundi B na kufuzu kwa mashindano ya kuwania kombe la Afrika baian ya Agosti na Septemba mwaka huu nchini Rwanda.
Morans iliandikisha historia kwa kuipiku Angola pointi 74-73 wiki iliyopita katika mchuano wa pili wa kundi B na kujikatia tiketi kwa mashindano hayo ya Afrika kwa mara ya wkanza baada ya miaka 28.
Timu hiyo chini ya ukufunzi wa kocha Liz Mils ililakiwa katika anga tua ya kimataifa ya Jomo Kenyatta muda mfupi baada ya saa nane usiku wa manane na kulakiwa na Rais wa shiriksiho la mpira wa kikapu nchini KBF Paul Otula na Kamishna wa michezo Japson Gitonga.
Hata hivyo ni wachezaji 7 pekee waliorejea nchini huku wengine 6 wakiabiri ndege kurejea ulaya wanakocheza wakiwmeo Tyler Ongwae,Preston Bungei na Joel Awich ,wakati Ariel Okal akisafiri kwenda Oman naye nahodha Griffin Ligare na Victor Ochieng walikuwa wamewasili nchini Jumatatu.
Punde baada ya kuwasilin kocha wa Kenya Liz Mils amesema kuwa alijua Angola ingempa ukinzani mkali baada ya kuchuana nao awalia katika michuano ya zone 6 lakini anajivuni mchezo wa vijana wake na kushukuru KBF kwa kuwa na imani naye licha ya kuwa mwanamke.
“Nilijua Angola watanitatiza kwa kuwa ni timu nzuri baada ya kupambana nao awali katika michuano ya zone 6 lakini najivuni ushindi huo na pia nashukuru shirikisho kwa kuniamini licha ya kuwa mwanamke kuingoza Morans akasema “Mils
Tyler Ongwae alifunga pointi hiyo muhimu huku Kenya ikisajili ushindi wa 74-73 katika sekunde za mwisho kuhakikisha Kenya inajikatia tiketi kwa mashindano hayo ambayo pia yatakuwa ya kufuzu kwa kombe la dunia mwaka 2023.
Timu hiyo inatarajiwa kulakiwa rasmi baadae Jumatano na wizara ya michezo.