Categories
Michezo

Samatta apiga bao la tatu Fernabahce

Nahodha wa timu ya taifa ya Tanzania Ali Mbwana Samatta alifunga bao lake la tatu katika klabu ya Ferbahce ya Uturuki msimu huu huku akichangia ushindi wa magoli 3-1 nyumbani dhidi ya Ankaragucu Jumatatu usiku.

Sammata  alipachika bao hilo kunako dakika ya 34 ya mchezo alipopokea  pasi katika eneo la D na kumhadaa kipa .

Likuwa bao la tatu msimu huu kwa  Samatta msimu huu ,huku ushindi huo ukiichupisha  Fernabahce hadi nafasi ya pili kwenye jedwali kwa alama  38 sawa na Besiktas.

Mshambulizi huyo alijiunga na Ferbahce  Septemba mwaka jana kwa mkataba wa miaka minne  akitokea Aston Villa kwa kima cha Euro miloni 6 na awali alikuwa na Racing Genk ya Ubelgiji alikosakata mechi 121 na kupachika mabao  76 huku akichangia mengine 20.

Categories
Michezo

Ozil kurejea kucheza nyumbani Fernabahce kwa mkataba wa miaka mitatu unusu

Mesut Ozil  hatimaye  amepata makao mapya ya kupiga soka baada ya kuafikiana  kutia saini mkataba wa miaka mitatu  unus na miamba wa Uturuki Fenerbahce kwa mjibu wa ripoti za kutoka mjini Istanbul.

Ozil, aliye na umri wa miaka 32, yuko tayari kujiunga na vigogo hao  wa Uturuki baada ya kukatalia mbali ofa nono  kutoka kwa klabu ya DC United inayoshiriki ligi kuu ya Marekani MLS.

Ozil ambaye amekuwa na wakati mgumu katika timu ya Arsenal ambako amecheza kwa miaka minane na kunyakua mataji mane ya kombe la FA, amepitia wakati mgumu tangu kuwasili kwa meneja Mikel Arteta ambaye hajakuwa akimjumuisha kikosini.

Kiungo huyo mbunifu aliyetwaa kombe la dunia na Ujerumani, alitemwa kutoka kikosi cha Arsenal cha ligi kuu,ligi ya Europa na mechi zote za klabu hiyo msimu jana na hapajakuwa na dalili ya kurejeshwa kikosini hata msimu huu.

Ozil ambaye alizaliwa Ujerumani pia ana asili ya Uturuki na ana mlahaka mzuri na uhusiano wa karibu na Rais wa Uturuki Recep Tayyip Erdogan .

Ozil anajiunga na mshambulizi wa Tanzania Ali Mbwana Samatta ambaye pia anaichezea timu hiyo ya Istanbul.