Chipolopolo ya Zambia watafungua ratiba ya kundi D ya michuano ya Chan Jumanne usiku dhidi ya Taifa Stars ya Tanzania saa moja usiku katika uwanja wa Limbe Omnisport mjini Limbe Cameroon.
Tanzania wanashiriki michuano ya CHAN kwa mara ya 2 baada kushiriki kwa mara ya kwanza mwaka 2009 walipotoka sare moja ,kushinda mchuano mmoja na kupoteza mmoja.
Upande wao Chipolopolo wanacheza CHAN kwa mara ya 4 na ya 3 mtawalia baada ya kushiriki miaka ya 2016 na 2018 ambapo waliibuka wa tatu mwaka 2009 huku wakicheza hadi robo fainali mwaka 2016 na 2018.
Baadae saa nne usiku Brave Warriors ya Namibia watashuka uwanjani Limbe Omnisport dhidi ya Syli Nationale ya Guinea .
Guinea wanacheza CHAN kwa mara ta tatu mtawalia baada ya kukosa makala matatu ya wkanza na waliibuka wa nne mwaka 2016 kabla ya kuyaaga mashindano katika hatua ya makundi mwaka 2018.
Namibia wanashiriki CHAN kwa mara ya pili baada ya kubanduliwa na wenyeji Moroko katika robo fainali mwaka 2018 mabao 2-0.
Mechi 6 zimepigwa kufikia sasa na mabao 4 kufungwa nazo mechi mbili kuishia sare tasa.
Mechi za mzunguko wa pili hatua ya makundi kuanza Jumatano ambapo watakaosonga mbele na wale watakaoanza kufunganya virago wakianza kubainika.