Categories
Kimataifa

Ufaransa kulegeza masharti ya COVID-19 msimu wa Krismasi

Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron amesema nchi yake itaanza kulegeza masharti yaliyowekwa katika kuzuia kuenea kwa ugonjwa wa Corona, kwa kuruhusu baadhi ya maduka kuendelea na biashara zao, kuanzia mwishoni mwa juma hili.

Macron ametangaza kuwa watu wataruhusiwa pia kutangamana na familia zao msimu ujao wa sherehe za Krismasi.

Hata hivyo, rais huyo amesema baa na migahawa zitaendelea kufungwa hadi tarehe 20 Januari mwaka ujao.

Ufaransa imeripoti zaidi ya visa milioni 2.2 vya watu walioambukizwa Corona na vifo vya zaidi ya watu elfu 50 tangu kuripotiwa kwa kisa cha kwanza cha ugonjwa wa COVID-19 nchini humo.

Kupitia hotuba ya televisheni, Macron amesema nchi yake imepita kilele cha wimbi la pili la maambukizi ya Corona.

Amesema kwamba masharti mengi yaliyotangazwa kuzuia kuenea kwa ugonjwa huo yatalegezwa kaunzia tarehe 15 Desemba kwa ajili ya sherehe za Krismasi, ambapo kumbi za sinema zitafunguliwa na masharti yaliyowekewa shughuli za usafiri kuondolewa iwapo kiwango cha maambukizi mapya kitakuwa chini ya visa 5,000 kwa siku.

Mnamo siku ya Jumatatu, Ufaransa ilitangaza visa vya watu 4,452 walioambukizwa ugonjwa wa COVID-19 katika muda wa masaa 24, hiyo ikiwa idadi ya chini zaidi nchini humo tangu tarehe 28 Septemba.

Kiwango cha wastani cha maambukizi ya Corona kwa siku kilikuwa visa 21,918 ambapo kilele chake kilikuwa visa 54,440 mnamo tarehe 7 mwezi huu.

Categories
Kimataifa

Angela Merkel ashinikiza kufungwa kwa shughuli nchini Ujerumani kudhibiti Covid-19

Kansella Angela Merkel wa Ujerumani ameonya kuhusu kipindi kigumu na kirefu cha majira ya baridi,huku akitetea  kurejelewa tena kwa sheria za kufunga shughuli nchini humo kuzuia kusambaa kwa ugonjwa wa Covid-19.

Merkel alionywa  na wabunge wa mrengo wa kulia alipotangaza kurejelewa kwa sheria hizo katika bunge.

Maafisa wa afya wamesema kuwa takriban watu 89 walifariki  nchini humo siku ya alhamisi kutokana na ugonjwa huo,huku wengine 16,774 wakiambukizwa virusi vya ugonjwa huo.

Hata hivyo sheria hizo si kali kuliko zile zilizotangazwa na taifa la Ufaransa ambalo lilifunga baa,migahawa na majumba ya mazoezi ya misuli na ya wasanii.

Ongezeko la maambukizi ya ugonjwa huo barani ulaya limesababisha mataifa husika kutangaza sheria kali zaidi.

Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron alitangaza sheria mpya za kukabiliana na janga hilo baada ya vifo kutokana na ugonjwa huo kuongezeka kwa kiwango kikubwa tangu mwezi Aprili.

Siku ya Alhamisi  taifa hilo lilirekodi visa 47,637 vipya vya ugonjwa huo,ikilinganishwa na visa 36,437 vya siku iliotangulia na vifo vya watu  235 siku ya jumatano.

 

 

Categories
Kimataifa

Ufaransa yaapa kuimarisha juhudi za kupambana na Corona hadi mwaka ujao

Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron amesema taifa hilo litaendelea kupambana na janga la korona hadi katikati ya mwaka ujao.

Tangazo hilo limetolewa huku visa vya maambukizi nchini humo vikipita watu milioni moja.

Siku ya Ijumaa Ufaransa ilirekodi zaidi ya visa 40,000 vipya vya maambukizi ya ugonjwa wa COVID-19 na jumla ya vifo 298.

Mataifa mengine ambayo yamerekodi ongezeko la visa vipya vya ugonjwa huo ni Urusi, Poland, Italia na Uswizi.

Shirika la Afya duniani WHO limesema huu ni wakati muhimu kwa mataifa ya Ulaya kuimarisha mbinu za kuzuia msambao wa ugonjwa huo na kuhakikisha kuwa mitandao ya huduma za afya inakabiliana vilivyo na janga hilo.

Idadi ya wastani ya kila siku ya maambukizi ya ugonjwa huo imeongezeka mara dufu katika muda wa siku kumi zilizopita.

Bara la Ulaya sasa limerekodi visa  milioni 7.8 vya ugonjwa huo na karibu  vifo vya watu 247,000.

Kimataifa, jumla ya visa milioni 42 vya mambukizi ya ugonjwa huo vimerekodiwa na vifo milioni 1.1.

Akiongea katika hospitali moja jijini Paris, Rais Macron amesema kwamba kwa mujibu wa ripoti ya wataalamu wa magonjwa nchini humo, ugonjwa huo huenda ukasalia nchini humo hadi katikati ya mwaka ujao.

Ufaransa imeongeza tena muda wa makataa ya kutotoka nje usiku kwa majuma sita.

Categories
Kimataifa

Mauaji ya mwalimu mmoja nchini Ufaransa yatajwa kuwa kisa cha ugaidi

Rais wa Ufaransa  Emmanuel Macron ametaja kisa cha kukatwa kichwa kwa mwalimu mmoja katika eneo la Kaskazini Mashariki ya mji wa Paris kuwa shambulizi la kundi la kigaidi la kiislamu.

Imesemekana mwalimu huyo alikuwa  amewaonyesha wanafunzi wake  katuni ya mtume Muhammad.

Macron amesema mwalimu huyo ambaye jina lake halijatajwa aliuawa kwa sababu alifundisha kuhusu uhuru wa kujieleza.

Maafisa wa mashtaka wa kukabiliana na ugaidi wanachunguza kisa hicho.

Mshambuliaji huyo aliyekuwa na kisu alipigwa risasi wakati maafisa walipokuwa wakijaribu kumkamata baada ya kumshambulia mwalimu huyo.

Polisi hawajatoa maelezo yoyote kumhusu lakini vyombo vya habari vya nchi hiyo vimesema ni mwanamme wa umri wa miaka 18 wa asili ya  Chechen ambaye alizaliwa huko  Moscow.

Kesi inaendelea kwa sasa mjini Paris kutokana na shambulizi la kigaidi la mwaka 2015 dhidi ya kampuni ya jarida la kifaransa la Charlie Hebdo, ambayo ilishamgbuliwa kwa kuchapisha katuni.

Wiki tatu zilizopita , mwanamme mmoja aliwahssmabulia na kuwajeruhi watu wawili nje ya afisi za zamani za kampuni hiyo.

Categories
Habari

Rais Kenyatta awarai wawekazi wa Ufaransa kuchagua Kenya kwa uwekezaji wao

Rais Uhuru Kenyatta amewahimiza wawekezaji wa Ufaransa kuchagua Kenya kwa uwekezaji wao barani Afrika na kuwahakikishia usaidizi wa serikali ya Kenya.

Wakati huo huo rais ametambua ongezeko la biashara za Ufaransa zinazoanzishwa jijini Nairobi akisema biashara hizo zimeongezeka kutoka chini ya 30 hadi zaidi ya 100 katika muda wa chini ya mwongo mmoja.

Rais  Kenyatta alikuwa akiongea Jumamosi Jijini  Paris wakati wa kongamano la kibiashara kati ya Ufaransa na Kenya lililoandaliwa na kundi la kibiashara la MEDEF.

Kiongozi wa nchi alisema serikali yake inatekeleza sera kadhaa na mageuzi ya masoko ambayo yameboresha pakubwa  uorodheshaji wa Kenya na Benki ya dunia katika kurahisisha shughuli za kibiashara katika miaka ya hivi majuzi.

Rais  Kenyatta alitambua kuwa kukithiri kwa ufisadi ni pigo kubwa katika juhudi za Kenya za kujiweka katika nafasi bora zaidi ya kuvutia wawekezaji barani Afrika na kuwahakikishia wafanyabiashara wa Ufaransa kuwa serikali yake inaweka mikakati ya kukabiliana na uovu huo.

Rais wa Ufaransa  Emmanuel Macron aliwakilishwa kwenye kongamano hilo na waziri wake wa masuala ya Ulaya na nchi za kigeni Franck Riester, alihimiza kampuni za nchi hiyo kuwekeza zaidi nchini Kenya akisema Ufaransa inalenga kuimarisha uhusiano wake wa kiuchumi na Kenya.

 

Categories
Habari

Rais Kenyatta: Rasilimali kubwa zaidi Afrika ni idadi kubwa ya vijana

Rais Uhuru Kenyatta amekariri kwamba rasilmali kubwa zaidi barani Afrika ni idadi kubwa ya vijana wala sio mali yake asili.

Alisema kuwa ilhali bara hili lina rasilmali nyingi zikiwemo dhahabu, almasi, mafuta na gesi, vijana ndio wenye uwezo wa kujenga ulimwengu bora zaidi kwa wote.

Rais aliyasema hayo Alhamisi alipotoa hotuba kuu kwenye kongamano la sita la kibiashara la BPI france Inno Generation, kwenye ukumbi wa Accor jijini Paris, nchini ufaransa ambapo alikuwa mgeni rasmi.

” Rasilimali mkubwa  barani Afrika ni vijana wetu na uwezo wao wa kushiriki katika kujenga ulimwengu bora kwa sisi sote,” alisema Rais

Alisema kuwa ukosefu wa fursa barani humu ndio huwafanya vijana wa bara hili kuwa changamoto barani ulaya na kwenye maeneo mengine duniani kutokana na juhudi zao za kutafuta riziki hasa kupitia uhamiaji haramu.

“Tunafahamu kuwa tatizo kubwa kuhusu swala la uhamiaji  lilasababisha dhana kwamba kile ambacho bara Afrika linaweza kutoa ni wahamiaji pekee,” aliongeza rais.

Na kuhusiana na fursa za uwekezaji nchini Kenya na barani Afrika, Rais Kenyatta alitaja teknolojia, muundomsingi na utengenezaji bidhaa kuwa sekta tatu kuu zinazoweza kuwavutia zaidi wawekezaji kutoka ufaransa.

Rais Emmanuel Macron wa ufaransa alimpongeza rais Kenyatta kutokana na sifa zake za uongozi unaoleta maendeleo. Rais Uhuru Kenyatta yuko nchini ufaransa kwa ziara rasmi.

Categories
Habari

Rais Kenyatta afanya ziara rasmi nchini Ufaransa

Rais  Uhuru Kenyatta alianza ziara  rasmi  nchini  Ufaransa Jumatano jioni  kwenye   Ikulu  ya    Elysee,    ambapo alikaribishwa  na  mwenyeji wake, Rais wa  Ufaransa, Emmanuel Macron.  

Baada ya kuwasili  muda mfupi baada ya  saa tatu  jioni, Rais  alikagaua gwaride la  lililoandaliwa na  wanajeshi wa Ufaransa  mnamo mwanzoni mwa sherehe ya kufana  ya kitaifa ya  makarabisho.

Viongozi hao hatimaye  walishuhudia   kutiwa saini kwa  mikataba kati ya    mataifa  haya mawili  kabla ya kuongoza jumbe zao kwenye  difa  iliyoandaliwa kwa heshima  ya Rais  Kenyatta.

Hatimaye viongozi hao walielekea kwa mashauriano ya    faragha.

Miongoni mwa  mikataba  iliyoafikiwa ni  mpango wa ufadhili wa serikali na  sekta  ya kibnafasi wa ujenzi wa  barabara kuu ya Nairobi-Nakuru-Mau, ulioatiwa saini kati ya   halmashauri ya Barabara Kuu Nchini na  kampuni ya Vinci Concessions.

Miradi mingine ni ujenzi wa reli  kutoka katikati  ya  jiji la Nairobi hadi  uwanja wa  ndege wa Kimataifa wa Jomo Kenyatta na  mkataba wa utekelezaji wa mpango wa usambazaji wa umeme wa kiwango cha Kilo Watt 400 kutoka Menengai hadi Rongai.

Rais  atatoa hotuba muhimu  Alhamisi kwenye kongamano la kibiashara la mwaka huu la  BPI France Inno Generation

Ijumaa Rais ataongoza mkutano wa wafanyabiashara wa humu nchini na wenzao wa Ufaransa  ambao  unaandaliwa na   shirikisho la   wafanyabiashara nchini Ufaransa.