Categories
Michezo

Misri yafuzu kwenda AFCON 2022 licha ya sare ya 1-1 na Kenya

Misri imejikatia tiketi kwa fainali za AFCON mwaka ujao nchini Cameroon ,licha ya kutoka sare ya bao 1-1 na Harambee Stars ya Kenya katika mchuano wa kundi G uliopigwa katika uga wa Kasarani Alhamisi usiku.

Kenya walianza mchuano huo kwa uzembe na kumruhusu kiungo wa Al Ahly Mohamed Magdi Kafsha kupachika bao la kwanza katika dakika ya pili ya mchezo.

Harambee Stars walijiszatiti lakini wakakosa kutumia vyema nafasi zao walizopata na kipindi cha kwanza kuishia  kwa uongozi wa Misri wa bao 1-0.

Stars waliendelea kujituma kipindi cha pili ndiposa beki Hamisi Abdala akasawazisha kunako dakika ya 65 na kukawa na matumaini ya ya kupata ushindi.

Hata hivyo kulishwa kadi nyekundu kwa difenda Jonstone Omurwa kulizima ndoto ya Kenya kupata bao la ushindi huku mechi ikiishia sare ya 1-1.

Matokeo hayo yana maana kuwa Misri na Comoros zimefuzu kwenda AFCON kutoka kundi G baada ya Comoros pia kutoka sare ya 0-0 na Togo,zikiwa na pointi sawa 9 wakifuatwa na Kenya kwa alama 4 huku Togo wakiburura mkia kwa alama 2.

Kenya itasafiri Jumamosi kwenda Togo kupiga mchuano wa mwisho wa kuhitimisha tu ratiba wakati Misri ikikamilishia kibarua nyumbani dhidi ya Comoros.

Categories
Michezo

Stars kukabiliana Misri Kasarani katika mechi ya kufa kupona

Timu ya taifa Harambee Stars itashuka uwanjani Kasarani Alhamisi  jioni kwa mechi ya 5 ya kundi G kufuzu kwa kombe la AFCON mwaka ujao nchini Cameroon.

Kulingana na kocha Jacob Mulee wanalenga ushindi katika pambano hilo ili kufufua matumaini ya kufuzu kwenda AFCON na pia watakuwa wakilenga kuondoa nuksi ya kutoishinda Misri katika mechi zote walizokutana .

Upande wake nahodha wa Kenya Michael Olunga anayesakata soka ya kulipwa nchini Qatar ,itakuwa kazi ngumu kupambana na Misri lakini anatarajia kuwa watajituma na kupata matokeo bora.

Itakuwa mechi ya kwanza kwa Olunga kuichezea Stars baada ya kukosa mechi mbili dhidi ya Comoros kutokana na vikwazo vya usafiri alivyowekewa akiwa  Japan   .

Beki wa Simba SC Joash Onyango atakuwa na mtihani mgumu kumthibiti mshambulizi wa Misri Mo Salah ,lakini anasema pia yuko tayari kwa kibarua hicho huku akijivunia kucheza na wachezaji wengi wa Misri wakati klabu ya Simba ilipowashinda Al Ahly  ya Misri a mwezi uliopita jijini Daresalaam.

Kenya itakosa huduma za wachezaji lvis Rupia ,beki David Owino ,na beki Brian Mandela wa Mamelodi  Sundowns ya Afrika Kusini.

Misri inajivunia kurejea kwa wachezaji wote nyota wakiwemo Mo Salah ,David Trezeguet na Mohammed El Nenny miongoni mwa wengine waliokosa mkondo wa kwanza wakati timu hizo zilipotoka sare mjini Cairo.

Wachezaji wa Misri wakiwa mazoezini Kasarani

Ushindi pekee ndio utafufua matumaini ya Kenya kufuzu wakishikilia nafasi ya tatu kwa pointi 3 ,huku wageni Misri wakihitaji sare, ili kufuzu kwa makala ya 33 ya AFCON baina ya Januari na Februari mwaka ujao wakiongoza kundi hilo kwa alama 8 sawia na Comoros.

Comoros pia itakuwa nyumbani dhidi  ya Togo katika mechi nyingine itakayochezwa sambamba Alhamisi.

Categories
Michezo

Harambee Stars yafungua Kambi ya mazoezi kujiandaa kuikabili Misri Alhamisi

Timu ya taifa Harambee Stars imeanza kambi ya mazoezi mapema Jumatatu kujiandaa kwa mechi ya kufuzu kwa kombe la AFCON kundi G dhidi ya Misri tarehe 25 mwezi huu.

Wachezaji wanaopiga soka humu nchini waliripoti kambini Jumapili jioni baada ya mechi za ligi kuu na kufanyiwa vipimo vya COVID 19 kabla ya kuanza mazoezi.

Wachezaji wa kulipwa wanatarajiwa kuwasili nchini kuanzia baade Jumatatu usiku na kuingia kambini kuanzia Jumanne.

Harambee Stars itawaalika Misi Alhamisi hii saa moja usiku katika uwanja wa Kasarani ,kabla ya kuondoka nchini wikendi hii kwenda Togo kwa mchuano wa mwisho wa kundi G dhidi ya Togo tarehe 30 mwezi huu.

Misri na Comoros wanaongoza kundi hilo kwa pointi 8 kila moja ,wakifuatwa na Kenya kwa umbali kwa alama 3 huku Togo ikiwa na alama 1.

Tayari Stars wamecheza mechi mbili za kujipiga msasa wakisajili ushindi dhidi ya Sudan Kusini goli 1-0 na kuwalemea  Tanzania mabao 2-1.

 

Categories
Michezo

Misri waibwaga Togo na kuhatarisha maisha ya Kenya kwenda AFCON

Mabingwa mara 7 wa kombe la AFCON ,Misri walifufua matumaini ya kushiriki kipute cha mwaka 2022 nchini Cameroon baada ya kusajili ushindi wa kwanza katika kundi G wa bao 1-0 dhidi ya Togo Jumamosi usiku.

The Pharoes walijipatia bao la pekee na la ushindi katika kipindi cha pili kupitia kwa bao la kichwa la Mahmoud Hamdy akiunganisha free kick ya dakika ya 54.

Matokeo hayo yanawaweka Misri uongozini mw akundi G kwa pointi 5 sawia na Comoros watakaoikaribisha Kenya Jumapili kuanzia saa moja usiku mjini Moroni.

Ilivyo kwa sasa Kenya hawana budi kuepuka kushindwa Jumapili usiku ugenini kwa Comoros ili kuwa na mataumaini ya kufuzu kwa dimba la AFCON wakiwa na pointi 3 kutokana na mechi tatu.

Comoros nao wanahitaji ushindi dhidi ya kenya ili kuwa na uhakika wa kufuzu kwa fainali za AFCON kwa mara ya kwanza .

Katika matokeo mengine ya Jumamosi Benin wakicheza nyumbani waliwaangusha Lesotho bao 1-0 huku Jamhuri ya Demokrasia ya Congo ikilazimishwa kwenda sare kapa nyumbani dhidi ya Angola.

 

Categories
Michezo

Ahly watawazwa mabingwa wa Misri

Al Ahly walinyakua ubingwa wa  ligi kuu nchini Misri kwa mara ya 42 mwishoni mwa wiki iliyopita huku msimu ukikamilika .

Kocha wa Ahly Pitso Mosimane  aliendeleza matokeo bora  katika majukumu yake mapya na miamba hao wakiipiga  Talaea El Geish mabao 3-0 na kufunga msimu kwa pointi 89.

Walid Soliman , Geraldo na Mahmoud Kahraba walipachika mabao hayo ya Ahly  ambao wameshinda mechi 28 kati ya 34 walizocheza huku wakipiga sare  tano na kushindwa mchuano mmoja pekee.

Kwa jumla Ahly maarufu kama Red Devils wamefungwa mabao manane  na kuandikisha rekodi ya kuzoa pointi nyingi zaidi ndani ya msimu mmoja zikiwa 89.

Tanta, FC Masr na  Haras El Hodood  zimeshushwa kucheza ligi ya daraja ya kwanza huku mabingwa wa msimu wa mwaka 1972 na 1973  Ghazl El Mahalla  wakipandishwa ngazi pamoja na Bank Al Ahly na Ceramica Cleopatra.

Categories
Michezo

Wachezaji watano wa kulipwa waitwa katika kikosi cha Misri

Kocha wa timu ya taifa ya Misri Hossam El-Badry amewaita kikosini wachezaji watano wa kulipwa kwa mechi za mwezi Novemba  kufuzu kwa kombe la Afcon mwaka 20121.

Misri ambao ni mabingwa mara 7 wa kombe hilo la Afcon wameanza vibaya harakati za kufuzu kutoka kundi  G wakiwa na  pointi 2 baada ya kutoka sare dhidi ya Kenya na Comoros.

Wanandinga wa kulipwa walijumuishwa kikosini ni Mohamed Salah wa Liverpool , Mohamed Elneny wa Arsenal, Ahmed Hegazi wa Westbromwich Albion, Mahmoud Trezeguet wa Aston Villa, na  Ahmed Hassan Kouka  wa Olympiacos ya Ugiriki.

Misri watapambana na  Togo nyumbani na ugenini mwezi ujao kuwania tiketi ya kwenda Afcon mwaka ujao.