Categories
Burudani

Mwimbaji Letoya Luckett atangaza talaka

Letoya Luckett ni mmoja wa waimbaji wa kundi la zamani la muziki kwa jina Destiny Child na wengine waliokuwa kwenye kundi hilo ni Beyonce Knowles, Kelly Rowland, La Tavia Robertson na Mitchelle Williams.

Wengi wa waimbaji hao sasa wanafanya kazi kama waimbaji huru hasa baada ya kundi hilo kuvunjika mwaka 2006.

Letoya Luckett alitumia akaunti yake ya Instagram kutangaza kwamba yeye na mume wake Tommicus Walker wameamua kutalikiana baada ya miaka mitatu na sasa wana watoto wawili ambapo wa mwisho ana umri wa miezi michache tu.

Aliandika, “Baada ya kufikiria kwa muda na maombi pia, Tommicus nami tumeamua kupata talaka. Ningependa tuwe wazazi wenye upendo tunaposaidiana kulea watoto wetu na kudumishaamani kwa ajili ya heshima kwa watoto wetu. Tafadhali eleweni hitaji letu la usiri. Asanteni kwa maombi, usaidizi na nafasi tunapopitia kipindi hiki kigumu.”

Duru zinaarifu kwamba Tommicus Walker hakuwa mwaminifu katika ndoa yao na ndiyo sababu kuu ya talaka yao.

Tommicus naye alitangaza hayo kwenye akaunti yake ya Instagram huku akiomba mashabiki na wafuasi wawe waangalifu na wanavyowachukulia katika kipindi hiki.

Alirudia maneno ya Letoya kuhusu kuwa wazazi wenye upendo kwa wanao huku wakisaidiana kwa malezi na kwamba watasalia marafiki.

Wakati mmoja, anasemekana kuonyesha tabia ambayo sio mwafaka kwa mwanaume ambaye ameoa wakati alionekana kwa kipindi kwa jina, “Friends and Family hustle” cha runinga ya VH1.

Baadaye Tommicus aliweka picha ya awali yake na Letoya akisema kwamba watatembea safari hii pamoja na kuhakikisha wanakuwa wazazi wazuri kwa wanao.