Categories
Michezo

CAF yakubali ombi la Gor na kuahirisha mechi ya ligi ya mabingwa hadi Jumamosi

Mabingwa wa Kenya Gor Mahia wamepata afueni, baada ya shirikisho la kandanda barani Afrika CAF kukubali ombi lao la kutaka mechi ya mkondo wa kwanza awamu ya pili ya mchujo kuwania ligi ya mabingwa  dhidi ya CR Belouizdad ya Algeria  kuahirishwa kutoka Jumatano hadi Jumamosi .

Caf ilikubali ombi la Gor kutokana na changamoto za usafiri walizokumbana nazo   kuelekea Algiers kwa mechio hiyo muhimu.

Gor sasa wanatakiwa kuwa Algeria kufikia Jumatano ili kujitayarisha kwa pambano hilo.

Awali vigogo hao walipaswa kuondoka nchini Jumapili usiku kuelekea Cairo ,safari ambayo ingewachukua saa tano kabla ya kupumzika na baadaye wangesafiri kwa kipindi cha saa tatu unusu hadi Tunis na kwa kuwa anga za Algeria zingali zimefungwa kwa ndege za usafiri wa abiria ili kuzuia msambao wa Covid 19 ,ingewalazimu green Amry kusafiri kwa treni kutoka Tunis hadi Algiers safari ya zaidi ya kilomita 800  kwa takriban saa 6.

Pia safari ya Gor ilikumbwa na ukosefu wa tiketi za kutosha hatua ambayo usimamizi wa timu umekiri kurekebisha na timu hiyo inatazamiwa kuondoka nchini Jumanne kupitia Doha Qatar ambapo wameruhusiwa kutua Algiers na serikali ya nchi hiyo.

Kogalo pia imekumbwa na masaibu  chungu tele kuelekea  kwa ziara  hiyo  huku wachezaji wakisusia mazoezi kwa takriban siku tatu wakidai kulipwa malimbikizi ya mshahara wa miezi miwili.

Mshindi wa mechi ya Gor na Belouizdad baada ya duru ya pili itakayochezwa mapema mwezi ujao jijini Nairobi atafuzu kucheza hatua ya makundi ya kombe hilo ,huku atakayeshindwa akicheza mchujo mmoja wa kufuzu hatua ya makundi ya kombe la shirikisho.

Categories
Michezo

Safari ya Gor kwenda Algeria yakumbwa na misukosuko

Safari ya timu ya Gor Mahia  kuelekea Algeria imekumbwa na utata baada ya kudaiwa kukosekana kwa ndege ya usafiri moja kwa moja kutoka Nairobi hadi Algiers .

Kogalo walitarajiwa kusafiri Jumapili usiku kwenda Algiers kwa  mkumbo wa kwanza wa mechi ya mchujo kuwania ligi ya mabingwa Afrika dhidi ya mabingwa wa Algeria CR  Belouizdad Jumatano jioni ,lakini hadi mapema Jumatatu timu hiyo ilikuwa bado haina uhakika wa kusafiri.

Awali timu hiyo ilikosa tiketi za usafiri kabla ya kampuni Air 748 kutoa shilingi milioni 1 kwa usafiri huku  pia yamkini tiketi zilizonunuliwa hazikutosha kwa wachezaji na maafisa wote wanaohitajika kwenye ziara hiyo.

Pia wachezaji wanadai  kulipwa mishahara yao kabla ya kusafiri na huenda wakosa  kucheza mechi hiyo hatuya ambayo itachangia kupigwa marufuku na kutozwa faini na CAF.

Mkumbo wa pili wa mchuano huo uliratibiwa kuchezwa jijini Nairobi mapema mwezi ujao huku mshindi wa jumla akitinga hatua ya makundi ya ligi ya mabingwa Afrika.

 

Categories
Michezo

Gor Mahia walenga hatua ya makundi ligi ya mabingwa CAF kwa mara ya kwanza

Miamba wa soka nchini Gor Mahia wanalenga kufuzu kwa hatua ya makundi ya kombe la ligi ya mabingwa barani Afrika Caf kwa mara ya kwanza msimu huu.

Kulingana na meneja wa Gor Jolawi Obondo kikosi walicho nacho kwa sasa ni kizuri na pia kina tajriba ya kuweka rekodi kuwa kilabu cha kwanza kutoka humu nchini kucheza hadi hatua ya makundi ya ligi ya mabingwa baada ya majaribio kadhaa bila ufanisi.

“Ni maombi yetu tucheze hadi hatua ya makundi na hata ikiwezekana hadi hatua ya mwondoano ya ligi ya mabingwa barani Afrika”akasema Obondo

Kwa mjibu wa Obondo Kogalo pia ina fursa ya kwenda mbali msimu huu katika kombe  hilo kutokana  na usaidizi wanaopata kutoka kwa Wizara ya michezo na shirikisho la FKF na kukanusha madai kuwa kikosi cha sasa ni hafifu na hakina uwezo wa kwenda mbali..

“Watu wanasema huenda hatuna kikosi kizuri lakini mimi sikubaliani,tuna kikosi kizuri na tuko na usaidizi kutoka kwa serikali,wizara na  hata shirikisho  sioni kwa nini tushindwe kufika hatua ya makundi” akaongeza Obondo

“Ushindi unataegemea na mtazamo,malengo na pia ushirikiano wa wachezaji ,usaidizi wa na maono ya kocha na nadhani tumejianda kwa hayo yote”akasema Obondo

Nahodha wa kilabu hicho Keneth Muguna pia anaazimia kuingoza Kogalo hadi hatua ya makundi licha ya upinzani mkali watakaopata.

“Tunataka tufuzu ,na kila timu pia inataka kufuzu ,tunajua itakuwa ngumu  lakini mwisho wa siku sisi tunajua sisi ndio tutashinda na kufuzu hatua ya makundi ya Caf Champions League”akasema Muguna

Gor Mahia imeratibiwa kuchuana na mabingwa wa Algeria CR Belouizdad ya Algeria  tarehe 22 mwezi huu mjini Algiers kabla ya kuwaalika wageni hao tarehe 5 mwezi ujao kisha mshindi kijumla afuzu kwa hatua ya makundi ya kombe la ligi ya mabingwa Afrika.

Mabingwa hao mara 18 wa ligi ya Kenya walifuzu kwa raundi ya pili ya mchujo wiki jana baada ya kuibandua APR ya Rwanda mabao 4-3 kwa jumla katika raundi ya kwanza ya mchujo.

Kogallo wamekuwa wakibanduliwa katika hatua ya mchujo ya  ligi ya mabingwa  Afrika kwa misimu mitatu mtawalia iliyopita,baadae wakafuzu kwa hatua ya makundi ya kombe la  shirikisho .

Hata hivyo Gor wameshindwa kuingia hatua ya mwondoano ya kombe la shirkisho katika misimu mitatu iliyopita.

Mabingwa hao mara 18 wa ligi ya Kenya walifuzu kwa raundi ya pili ya mchujo wiki jana baada ya kuibandua APR ya Rwanda mabao 4-3 kwa jumla katika raundi ya kwanza ya mchujo.

 

 

Categories
Michezo

Gor kukabiliana na mabingwa wa Algeria Belouizdad

Mabingwa wa ligi kuu ya Kenya Gor Mahia wameratibiwa kuchuana na mabinwga wa Algeria CR Belouizdad  katika mchujo wa pili wa ligi ya mabingwa barani Afrika Caf  Disemba 22 mjini Algiers huku pambano  la marudio likichezwa Nairobi Janauri 5 mwaka ujao.

Gor walitinga hatua hiyo baada ya kuishinda Rwanda Patriotic Army mabao 3-1 Jumamosi iliyopita katika uwanja wa Nyayo na kufuzu kwa ushindi wa jumla wa mabao 4-3 .

Upande wao Beloiuzdad waliishinda  Al Nasr ya Libya magoli 2-0 Jumapili jioni na kufuzu kwa hatua ya mchujo wa pili kwa ushindi wa jumla wa magoli 4-0.

Kogalo wamekuwa na rekodi mbovu wanapocheza ugenini dhidi ya vilabu vya  Algeria baada ya kucharazwa mabao 4-1 na Usm Algers mwaka uliopita mjini Algiers katika hatua ya mchujo wa ligi ya mabingwa kabla ya kupoteza bao moja kwa bila ugenini dhidi ya Na Hussein Dey katika hatua ya makundi ya kombe la shirikisho la soka .

CR Belouizdad

Ili kuwa na matumaini ya kufuzu kwa hatua ya mwisho ya mchujo ni lazima  Gor warekebishe makosa kadhaa haswa ya safu ya ulinzi na pia kujipanga mapema na kusafiri kwa wakati ufaao.

Mshindi wa mchuano kati ya Gor na Belouizdad atacheza  mchujo wa mwisho itakayompa fursa mshindi kuingia hatua ya makundi ya kombe la  ligi ya mabingwa .

Belouizdad wamenyakua taji ya ligi kuu Algeria mara 7 na kombe la shirikisho nchini Algeria mara 8 na ni miongoni mwa timu zilizo na ufanisi mkubwa nchini humo.