Categories
Habari

Watu 10 wafariki kutokana na Covid-19 huku visa 780 vipya vikinakiliwa hapa nchini

Watu 780 wamethibitishwa kuambukizwa ugonjwa wa COVID-19 katika kipindi cha saa 24 zilizopita kutokana na sampuli 6,158 zilizopimwa.

Idadi hiyo mpya inafikisha idadi jumla ya visa vya Covid-19 hapa nchini kuwa 80,102.

Kwa ujumla taifa hili limepima sampuli 861,561 tangu mwezi Machi mwaka huu wakati kisa cha kwanza kiliripotiwa.

Kati ya visa hivyo vipya, 754 ni wakenya na 26 ni raia wa kigeni ambapo 460 ni wanaume na 320 ni wanawake.

Aliye na umri mdogo zaidi ni mtoto wa mwaka mmoja na mkubwa zaidi ana umri wa miaka 94.

Watu 10 wameaga dunia kutokana na ugonjwa huo na kufikisha 1,427 jumla ya watu ambao wameaga dunia kutokana na ugonjwa wa COVID-19.

Habari njema ni kwamba watu 552 walipona ugonjwa huo ambapo 468 walikuwa kwenye mpango wa kuwahudumia wagonjwa hao nyumbani na 84 waliondoka kutoka hospitali mbali mbali.

Watu 53,526 wamepona ugonjwa huo kufikia sasa hapa nchini.

Kaunti ya Nairobi ingali inaongoza kwa maambukizi ya visa vipya huku ikinakili visa 273, Kiambu 93, Mombasa 86, Busia 85, Nakuru 40, Turkana 32, Uasin Gishu 20, Kilifi 16, Meru, Kajiado na Kericho visa 13 kila moja na Kisumu visa 11.

Categories
Habari

Watu 810 zaidi waambukizwa Covid-19 huku wengine wanane wakifariki hapa nchini

Wizara ya afya imetangaza visa 810 vipya vya Covid-19 na kufikisha idadi jumla ya maambukizi hapa nchini kuwa 79,322.

Kulingana na wizara ya afya, idadi hiyo mpya imetokana na kupimwa kwa sampuli 7,387 katika muda wa saa 24 zilizopita.

Kati ya visa hivyo vipya , 792 ni wakenya ilhali 18 ni raia ya kigeni. Aliye na umri mdogo Zaidi ni mtoto wa mwaka mmoja ilhali mkongwe Zaidi ana umri wa miaka 87.

Wakati uo huo idadi ya vifo kutokana na Covid-19 imefika 1,417 baada ya wagonjwa 8 zaidi kufariki kutokana na makali ya ugonjwa huo.

Kulingana  na waziri wa afya Mutahi Kagwe, wagonjwa 1,198 wamelazwa katika vituo mbali mbali vya afya humu nchini  huku wagonjwa 7,162 wakiwa katika mpango wa kuwatunza wagonjwa nyumbani.

Aidha wizara hiyo ilitangaza kwamba watu 265 wamepona ugonjwa huo ambapo 210 walikuwa katika mpango wa kuwahudumia wagonjwa hao nyumbani na 55 waliondoka katika hospitali mbali mbali. Jumla ya waliopona sasa ni 52,974.

Kaunti ya Nairobi ilinakili iliongoza katika visa vya maambukizi mapya ikiwa na  252, Mombasa 77, Nakuru 38, Uasin Gishu 36, Siaya 34, Nyandarua 31 huku Kericho  na Busia  zikiwa na visa 30.

Kaunti ya  Nyamira iliandikisha visa 29, Kisumu 22, Kakamega 22, Machakos 21, Murang’a 19, Kimabu 19, Kwale 19, Kajiado na Bungoma  visa 15 kila moja.

Kisii  iliandikisha visa 15 huku  Turkana na Migori zikinakili visa  13 kila moja. Homa Bay 12, Nandi 9, Kilifi 9, Bomet 6, Pokot  magharibi 5, Samburu 4. Vihiga, Tana River na Makueni visa 3 kila moja huku  Nyeri na Lamu zikiwa na visa 2 kila moja.

Narok na Embu zilinakili kisa kimoja kila moja.

 

Categories
Habari

Visa 1,211 vipya vya Covid-19 vyanakiliwa hapa nchini

Watu 1,211 wamebainishwa kuambukizwa virusi vya korona, kutoka kwa sampuli 9,304 zilizopimwa katika saa 24 zilizopita.

Idadi hiyo inafikisha  idadi jumla ya maambukizi hapa nchini ya Covid-19 hadi 76,404, tangu kuthibitishwa kwa kisa cha kwanza mwezi machi mwaka huu.

Idadi ya vifo kutokana na ugonjwa huo, pia imeongezeka hadi 1,366 baada ya wagonjwa 17 zaidi kuaga dunia .

Hata hivyo wagonjwa 368 wamepona, 265 kati yao chini ya mpango wa uuguzi wa nyumbani,huku 103 wakiruhusiwa kuondoka katika vituo mbali mbali vya afya .

Hadi sasa jumla ya wagonjwa 51,352 wamepona virusi hivyo hatari.

Wagonjwa wengine 1,134 wamelazwa katika vituo mbali mbali vya afya ,67 kati yao wamelazwa katika vyumba vya matibabu maalumu ,huku 36 wakiwa kwenye vipumuzi.

Categories
Habari

Asilimia 13 ya biashara hapa nchini zilifungwa kutokana na athari za Covid-19

Utafiti wa chama cha wadau wa sekta ya kibinafsi umebainisha kuwa asilimia 13 ya biashara humu nchini zimefungwa tangu kuzuka kwa ugonjwa wa Korona.

Utafiti huo uliofanywa kati ya mwezi Septemba na Oktoba mwaka huu pia unabaini kuwa biashara nyingi zimechukua muda kurejelea hali ya kawaida licha ya kulegezwa kwa masharti ya kudhibiti msambao wa Korona.

Kwa mujibu wa utafiti huo ulioshirikisha biashara 428 katika sekta mbalimbali, asilimia 50 ya biashara zilifungwa punde tu chamuko la Korona liliporipotiwa humu nchini.

Asilimia 23 ya biashara zilifungwa kwa kipindi cha nusu mwezi, asilimia 50 zikafungwa kwa kati ya mwezi mmoja na miezi mitatu na asilimia 27 zikafungwa kwa kati ya miezi minne na miezi sita.

Ni asilimia 37 pekee ya biashara zilizofunguliwa ambazo zinaendelea na shughuli zao ilhali asilimia 13 ziko katika hatari ya kufungwa tena.

Aidha, watu wengi wamepoteza ajira katika sekta za maduka ya jumla, utalii, elimu na ujenzi.

Categories
Habari

Kenya yanakili visa 1,048 vipya vya Covid-19 huku watu 19 wakiaga dunia

Visa vipya 1,048 vya maambukizi ya korona vimethibitishwa leo hapa nchini kutoka kwa sampuli 8,660 zilizopimwa na kuongeza idadi jumla ya maambukizi hadi 75,193.

Kwenye taarifa,waziri wa afya Mutahi Kagwe, amesema kati ya visa hivyo,1,018  ni Wakenya,ilhali 30 nia raia wa kigeni.

Mgonjwa wa umri wa mdogo ni mtoto wa maka moja ,ilhali mgonjwa wa umri mkubwa ana miaka 90.

Kaunti ya Nairobi  kwa mara nyingine imeongoza katika maambukizi mapya kwa kunakili visa 408 ,ikifwatiwa na Kericho kwa visa 84, Mombasa 80, Kiambu 71, Busia 52, Migori, 36, Uasin Gishu, 35, Kisumu na Machakos visa 25  kila moja na Kajiado visa 23.

Kaunti ya Siaya imenakili visa 18, Bungoma, 15, Kakamega 14, Nakuru, 13, Taita Taveta 12, Bomet, Makueni na Nyeri visa 11 kila moja.

Kaunti za  Kilifi na Laikipia visa 10 kila moja , Baringo, Nandi na Kwale visa 9 kila moja , Meru 8, Vihiga, 6, Murang’a,Pokot Magharibi , Mandera na Kitui visa  5 kila moja.

Kaunti ya Kirinyaga 4, Trans Nzoia na Embu visa 3 kila moja.Kaunti za Elgeyo Marakwet, Narok, Tharaka Nithi, Garissa na Tana River zilikuwa na visa viwili kila moja ,ilhali kaunti za  Homa Bay, Turkana na Nyamira zilikuwa na kisa kimoja kila moja.

Wakati uo huo watu 19 zaidi wameaga dunia kutokana na ugonjwa huo ,na kuongeza idadi jumla ya vifo hadi 1,349.

Wagonjwa wengine 326 wamepona,ambapo 219 walikuwa wakiuguzwa nyumbani na wengine 107 wameruhusiwa kuondoka katika vituo mbali mbali  vya afya .Hadi sasa jumla ya watu 50,984 wamepona.

Categories
Habari

Kenya yanakili visa 925 vipya vya Covid-19 huku watu 15 zaidi wakifariki

Watu 15 zaidi  wamefariki dunia hapa nchini kutokana na ugonjwa wa Covid-19 katika saa 24 zilizopita.

Idadi hiyo inaongeza idadi jumla ya vifo kutokana na ugonjwa huo hadi 1,302.

Hayo yamejiri huku visa vipya 925 vya maambukizi vikinakiliwa kutoka kwa sampuli 5,559 zilizopimwa,na kuongeza idadi jumla ya maambukizi hapa nchini hadi 71,729.

Jumla ya sampuli 798,585 zimepimwa tangu kisa cha kwanza cha ugonjwa huo kilipobainishwa mwezi Machi.

Kwenye taarifa, waziri wa afya Mutahi Kagwe alisema kati ya visa hivyo vipya, 893 ni Wakenya ilhali 32 ni raia wa kigeni,ambapo 556 ni wanaume na 369 ni wanawake.

Mgonjwa wa umri mdogo ni mtoto wa miezi mitano na yule wa umri wa mkubwa ana miaka 92.

Hata hivyo wagonjwa wengine 1,018 wamepona na kuongeza idadi jumla ya waliopona hadi 47,262.

Kulingana na taarifa hiyo,kaunti ya Nairobi imeongoza kwa maambukizi kwa kunakili visa 358,ikifuatiwa na Kiambu kwa visa 102, Mombasa – 59, Nakuru- na Nyeri -39,  ilhali Machakos na Busia zimenakili visa 32 kila moja.

Kisumu imenakili visa 29, Kilifi 28  Kajiado 25, Kericho 2, Trans Nzoia, Kwale ,Pokot magharibi, Garissa, Bomet, Migori na Kirinyaga zilinakili kisa kimoja kila moja .

 

Categories
Habari

Watu 21 zaidi waaga dunia kutokana na Covid-19 hapa nchini

Idadi ya vifo kutokana na virusi vya Covid-19 hapa nchini inaendelea kuongeza  huku wagonjwa wengime 21 wakifariki katika muda wa saa 24 zilizopita.

Miongoni mwa wale walioaga dunia ni madaktari wanne waliofariki walipokuwa wakitekeleza majukumu yao. Hii inafikisha 1,249 jumla ya idadi ya vifo nchini.

Vifo hivyo vimejiri huku watu wengine 1,080 wakithibitishwa kuwa na ugonjwa huo kufuatia upimaji wa sampuli  8,322 na kufikisha 69,273 jumla ya visa vya maambukizi nchini.

Kwa jumla watu 783,304 wamepimwa ugonjwa huo kufikia sasa.

Kati ya visa hivyo vipya, 1,066 ni wakenya huku 14 wakiwa raia wa kigeni.

Mgonjwa mwenye umri mdogo zaidi ana miezi 11 na mongwe zaidi ana miaka 100.

Kaunti ya Nairobi imenakili visa 216, Mombasa visa 163, Nakuru visa 103, Kilifi visa 64 Baringo visa 60, Machakos visa 57, miongoni mwa nyingine.

Wagonjwa  542 wamepona ugonjwa huo ambapo 262 walikuwa kwenye mpango wa utunzaji wa nyumbani na 280 wameruhusiwa kuondoka kwenye hospitali mbalimbali nchini.

Jumla ya wagonjwa 1,185 wamelazwa katika vituo mbalimbali vya afya huku wengine 5,794 wakijitenga nyumbani.

Wagonjwa 58 wako katika vitengo vya wagonjwa mahututi, 23 wanasaidiwa kupumua kwa mitambo, 30 wanapewa hewa ya oksijen, 75 kwenye wadi za kawaida na 15 katika vitengo vya wagonjwa wasiojiweza.

Categories
Habari

Visa 1,470 vipya vya Covid-19 vyanakiliwa huku watu 25 wakifariki hapa nchini

Kenya imenakili visa 1,470  vipya vya Covid-19 kutokana na sampuli 8,072 zilizopimwa katika kipindi cha saa 24 zilizopita.

Idadi hiyo inafikisha 68,193 jumla ya watu ambao wameambukizwa ugonwa huo hapa nchini.

Jumla ya sampuli 774,982 zimepimwa hapa nchini kufikia sasa. Kati ya wagonjwa hao wapya, 1,397 ni wakenya na 73 ni wageni huku 986 wakiwa wanaume na 484 wanawake.

Aliye na umri mdogo zaidi ni mtoto wa miezi miwili huku mkubwa zaidi akiwa na umri wa miaka 88.

Kwenye taarifa, wizara ya afya ilisema watu 791 wamepona ugonjwa huo, 695 kutoka mpango wa kuwahudumia wagonjwa hao nyumbani na 96 walikuwa katika hospitali mbali mbali.

Jumla ya waliopona ugonjwa huo sasa ni 44,872. Aidha watu 25 wameaga dunia kutokana na ugonwa huo na kufikisha idadi ya watu ambao wameaga dunia kufikia sasa kuwa 1,228.

Jumla ya wagonjwa 1,364 wamelazwa katika vituo mbali mbali vya afya hapa nchini huku 5,726 wakihudumiwa nyumbani.

Wagonjwa 54 wamezuiliwa katika kitengo cha kuwahudumia wagonjwa mahututi-ICU, 16 kati yao wakitumia msaada wa vipumuzi, na 32 wanatumia hewa ya oksijeni ya ziada.

Wagonjwa 93 wanapokea huduma za oksijeni ambapo 73 wanahudumiwa kwenye wadi za jumla na 20 wako kwenye kitengo cha huduma maalum cha HDU.

Categories
Habari

Shule ya Msingi ya Lporos huko Samburu yafungwa kwa hofu ya maambukizi ya Corona

Shule ya Msingi ya Lporos katika eneo la Maralal, Kunti ya Samburu imefungwa kwa muda baada ya mwalimu mmoja kuambukizwa virusi vya Corona.

Kwa sasa mwalimu huyo anapokea matibabu katika hospitali moja katika Kaunti ya Nakuru.

Kulingana na Afisa Mkuu wa Elimu katika Kaunti ya Samburu Allan Omondi, shule hiyo imefungwa ili kutoa nafasi ya kupilizwa kemikali ya kuua virusi hivyo.

Omondi amesema kuwa wanafunzi hao wa gredi ya nne na darasa la nane wanatarajiwa kurejea shuleni baada ya siku mbili, kwa ushauri wa maafisa kutoka Wizara ya Afya.

“Baada ya kupulizwa kemikali, tunatarajia kwamba wanafunzi wetu watarudi shuleni baada ya masaa 48,” ameeleza Omondi.

Aidha, walimu tisa na mfanyikazi mwengine mmoja wa shule hiyo wamefanyiwa upimaji wa virusi hivyo na wanasubiri matokeo.

Wazazi wa watoto hao wameitaka serikali kusaidia katika juhudi za kudhibiti maambukizi ya virusi hivyo kwa ajili ya usalama wa wanafunzi shuleni.

“Serikali ichukue hatua ili watoto watakaporudi shuleni wazazi wajue watoto wao wako salama,” amesema mzazi mmoja ambaye pia ni mkazi wa eneo hilo.

Categories
Habari

Watu 24 wafariki kutokana na makali ya Covid-19 huku visa 1,344 vipya vikinakiliwa nchini

Kuongezeka kwa mara ya pili  kwa visa vya maambukizi ya ugonjwa wa COVID-19 kunaendelea kusababisha vifo vingi ikilinganishwa na hapo hawali.

Wagonjwa 24 wamepoteza maisha yao kutokana na ugonjwa huo na kufikisha 1,154 idadi ya watu waliofariki kutokana na ugonjwa huo.

Visa vipya  1,344 vya maambukizi ya ugonjwa huo wa Covid 19 vilirekodiwa humu nchini, katika kipindi cha  saa 24 zilizopita na kufikisha  64,588 idadi ya maambukizi ya ugonjwa huo humu nchini.

Kwenye taarifa, waziri wa afya  Mutahi Kagwe amesema visa hivyo vipya vilibainika kutoka sambuli  7,162.

Hii inafikisha idadi ya jumla ya maambukizi  753,959 humu nchini.  Visa 45 vinawahusisha raia wa nchi za kigeni.

Kuhusiana na jinsia , wanaume  815 walipatikana na maambukizi hayo ikilinganishwa na wanawake 529.

Mwenye umri mdogo zaidi ni mtoto wa mwezi moja huku mzee zaidi akiwa na umri wa miaka 96. Kaunti ya Nairobi imerekodi visa vipya 322, Kiambu na visa  221, Mombasa ikiwa na visa 133.

Laikipia visa  72,  Uasin Gishu ikirekodi visa 66,  Kericho visa 65, Nakuru visa  63, Kajiado visa vya maambukizi  43, Kilifi visa 40, Kisumu ikiwa na visa  36, Kwale na  Migori ikirekodi visa 32 kila moja.

Machakos ilikuwa na visa  30, Baringo visa 20, Bomet ikirekodi visa 19, Nandi ikiwa na visa 16, Meru  visa 13, Nyeri ikirekodi visa  12, Kisii, Embu na Mandera zikiwa na visa vya maambukizi 11 kila moja.

Kakamega, Murang’a na  Naymira vilirekodi visa 8 kila moja, Elgeyo Marakwet na  Turkana  vikiwa na visa 5 kila moja.

Nyandarau, Narok, Kirinyaga na Transnzoia vilirekodi visa 3 kila moja , Tharaka Nithi, Vihiga, Pokot Magharibi, Bungoma Taita Taveta, Wajir, Busia, Makueni, Samburu, Homa Bay na Siaya vilikuwa na visa viwili kila moja huku  Kitui ikirekodi kisa kimoja.