Categories
Michezo

Uganda Hippos waing’ata Burkina Faso na kutinga nusu fainali AFCON U 20

Uganda Hippos waliandikisha historia Alhamisi usiku walipoibwaga Burkina Faso penati 5-4 na kufuzu kwa nusu fainali ya kombe la bara Afrika kwa chipukizi wasiozidi umri wa miaka 20 mjini Nouakchott Mauritania.

Burkina Faso maarufu kama Young Stallions walianza vyema mechi kwa mashambulizi mengi lakini kipa wa Uganda Komakach alikuwa mwiba na kupangua matobwe yote.
Ugand pia walishuhudia mikwaju yao kupitia kwa Steven Sserwadda ,Ivan Bogere na Isma Mugulusi ikipanguliwa.

Mechi ilimalizikia kwa sare tasa baada ya dakika 120 na kuamuliwa kupitia matuta ya penati Uganda wakiunganisha zote 5 huku kipa wa Hippos Komakach akipangua

penati ya kwanza iliyochongwa na Naser Djiga Yacouba .

Uganda wanaoshiriki michuano hiyo kwa mara ya kwanza watacheza nusu fainali na mshindi kati ya Tunisia na Moroko watakaomenyana kwenye robo fainali ya Ijumaa.

Ghana wakimenyana na Cameroon

Ghana waliibandua Cameroon pia kupitia penati 5-3 kufuatia sare tasa dakika 120 katika kwota fainali ya kwanza.

Ghana ukipenda Black Satelites watamenyana na mshindi wa robo fainali ya Ijumaa baina ya Afrika ya kati na Gambia katika hatua ya nusu fainali.

Categories
Michezo

Wenyeji Mauritania waadhibiwa na Cameroon AFCON U 20

Wenyeji Mauritania waliishia kujutia kosa moja lililofanywa mwishoni mwa kipindi cha pili na kaumbulia kichapo cha bao 1-0 dhidi ya Cameroon katika mechi ya ufunguzi kuwania kombe la AFCON kwa chipukizi wasiozidi umri wa miaka 20 katika uwanja wa Olimpiki mjini   Nouakchott Jumapili usiku.

Junior Sunday Jang  aliwafungia Cameroon bao la pekee na la ushindi katika   dakika ya 81  akitumia makosa ya mlinzi wa Mauritania aliyepiga pasi kwa kipa wake lakini ikawa fupi na kutwaliwa na mshambulizi huyo aliyepachika bao .

Mauritania wanaoshiriki kwa mara ya w kwanza walidhihirisha mchezo wa hali ya juu huku wakikosa nafasi za wazi za kupitia kwa Oumar Mbareck na  Adama Diop .

Pasi ya difenda Alioum Moubarak wa Mauritania kwa kipa wake ikikatwa na  Sunday Junior  aliyeipa Cameroon inayoshiriki michuano hiyo kwa mara ya 10 ushindi huo muhimu.

Cameroon watarejea uwanjani tarehe 17 dhidi ya Uganda wakati Mauritania wakichuana na Msumbiji.

Mashindano hayo yanayoshirikisha mataifa 12 yataingia siku ya pili Jumatatu kwa jumla ya mikwangurano  mitatu,Uganda wakifungau kazi dhidi ya Musmbiji kuanzia saa kumi alasiri katika kundi A ,kabla ya Burkina Faso kukabiliana na Tunisia saa moja usiku kundini B nao  Namibia wamenyane na Jamhuri ya Afrika ya kati.

Categories
Michezo

Cameroon, Guinea walenga Shaba CHAN 2020

Wenyeji Cameron na Guinea watashuka uwanjani Re unification mjiniu Douala Jumamosi usiku katika mechi ya kufuta machozi kuwania nishani ya shaba au ukipenda nafasi ya tatu nne kwenye makala ya 6 ya kipute cha CHAN.

Timu zote zililenga kufika fainali ya Jumapili na kunyakua kombe lakini ghafla bin vuu ndoto hiyo ikazimwa zilipoambulia vichapo katika nusu fainali.

Guinea maarufu kama Syli Nationale  walianza harakati za kundi D kwa ushindi wa magoli 3-0 dhidi ya Namibia kabla ya kutoka sare ya bao 1 dhidi ya Zambia na sare ya mabao 2 dhidi ya Tanzania na kuongoza kundi hilo kwa pointi 5.

Upanda wao Indomitable Lions walianza safari ya kundi A kwa ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Zimbabwe kabla ya kwenda sare ya goli 1 dhidi ya Mali na sare tasa dhidi ya Burkina Fasso wakiibuka wapili kundini kwa alama 5.

Katika hatua ya kwota fainali Guinea iliwatema Rwanda bao 1-0 nao Cameroon wakaizabua DR Congo mabao 2-1 kwenye robo  fainali.

Hata hivyo masaibu kwa timu zote yaliingia katika nusu fainali Guinea walizidiwa maarifa na Mali magoli 5-4 kupitia penati wakati Cameroon wakidhalilishwa mabao 4-0 na Moroko.

Guinea wanaoongozwa  na kocha Mohammed Bangoura  watalenga kuboresha matokeo ya mwaka 2016 nchini Rwanda walipocheza mchuano sawia na huo na kumaliza katika nafasi ya nne  walipoteza kwa Ivory Coast na wanajivunia mfungaji wa pili bora Yakhouba Barry aliyepachika mabao 3 hadi sasa huku pia wakijivunia kwamba wamefika hadi hatua ya timu nne bora licha ya kuwa na kikosi hafifu na kilichobezwa mwanzoni mwa mashindano.

Cameroon chini ya mwalimu marti Mpile watakuwa na kila sababu ya kuwafurahisha mashabiki baada ya fedheha ya semi fainali na Moroko ingawa ni mara ya kwanza kwa timu hiyo kufika umbali huu.

Nahodha wa Cameroon Salomon Banga Bindjeme 2 amefunga mabao 2 sawa na Victor Kantabadouno na Morlaye Syla wote wa Guinea.

Wachezaji Serge Anduolo na kapteni Salomon Banga Bindjeme 2 ni miongoni mwa wanandinga wenye tajriba baada ya kushiriki CHAN ya mwaka 2018 nchini Moroko  wakati Guinea wakijivunia kipa  Abdoulaye Camara ambaye alikuwa kikosini mwaka 2018 nchini Moroko.

Kufikia sasa mechi 30 zimepigwa na magoli 58 kufungwa wastaniu wa bao 1 nukta 93 huku Soufiane Rahimi wa Moroko akiongoza kwa mabao 5.

Categories
Michezo

Moroko wafuzu fainali ya CHAN baada ya kuwadhalilisha wenyeji Cameroon mbele ya umma

Sofiane Rahimi alipachika mabao 2 na kuwasaidia Atlas Lions ya Moroko kufuzu kwa fainali ya kombe la CHAN baada ya kuititiga Cameroon mabao 4-0 katika nusu fainali ya pili iliyosakatwa Jumatano usiku katika uwanja wa Limbe Omnisport.

Soufiane Bouftini na Soufiane Rahimi walifunga bao moja kila mmoja katika dakika ya 28 na dakika ya 40  huku Moroko wakiongoza mabao 2-0 kufikia mapumzikoni  katika kipindi ambacho wenyeji walizidiwa nguvu.

Kipindi cha pili Indomitable Lions walijizatiti na kuanza kufanya mashambulizi ya hali na mali lakini mabeki wa Moroko walikua macho na kuzima mashambulizi yote.

Omar Namsaoui alichezewa rafu na kipa  Haschou Kerrido huku mkwaju wa adhabu uliochongwa ukiunganishwa na Bouftini kwa bao la kwanza .

Rahimi alitumia vyema mkanganyiko baina ya mabeki wa Cameroon na kipa wao na kupachika bao la tatu dakika ya 74 huku Mohammed Ali Bemammer akifunga kazi kwa goli la nne dakika ya 82.

Wenyeji wangeadhibiwa zaidi endapo kipa kerrido na safu ya ulinzi haingekuwa macho .

Moroko wanalenga kuwa taifa la kwanza kuhifadhi kombe hilo watakaposhuka katika uwanja wa Ahmadou Ahidjo  Jumapili usiku kwa fainali dhidi ya Eagles ya Mali iliyowabandua  Guinea mabao 5-4 kupitia mikiki ya penati kufuatia sare tasa baada ya dakika 120.

Upande wao Guinea watapambana  na Cameroon  Jumamosi usiku katika mkwangurano wa kuwania nafasi ya tatu na nne.

Moroko walinyakua kombe hilo mwaka 2018 wakiwa waandalizi baada ya kuichachafya Nigeria mabao 4-0 katika fainali huku  Mali wakisaka taji hiyo kwa mara ya kwanza.

Categories
Michezo

Cameroon yaitema DR Congo na kuingia nusu fainali ya CHAN kwa mara ya kwanza

Waandalizi Cmaeroon walifuzu kwa nusu fainali ya makala ya 6 ya mashindano ya kuwania kombe la CHAN baada ya kuwazidia maarifa mabingwa mara mbili  DR Congo magoli 2-1 katika kwota fainali ya pili iliyosakatwa ugani Japoma mjini Doula Jumamosi usiku.

Majirani DR Congo maarufu kama leopards walichukua uongozi wa mchuano huo kupitia kwa bao la kichwa lililotingwa na Makabi Lilepo,katika dakika ya 22 na kuwanyamazisha mashabiki wa nyumbani.

Hata hivyo Indomitable Lions waliendelea kujituma na dakika 7 baade mshambulizi mzoevu Yannick Ndjeng akasawazisha  kufuatia makosa ya kipa wa Leopards Ley Matampi.

Dakika 3 kabla ya kukamilika kwa kipindi cha kwanza mshambulizi wa Cameroon Felix Oukine  alivurumisha kombora lililomkanganya beki wa Congo na kumhadaa kipa Matampi na kuwanyanyua mashabiki wa nyumbani kwa goli la pili.

Kipindi cha pili timu zote ziliendelea kuviziana na kucheza kwa tahadhari kuu na hadi kipenga cha mwisho Cameroon wakafuzu nusu fainali ambapo watapambana na mshindi wa kwota fainali ya tatu itakayosakatwa Jumapili kati ya mabingwa watetezi Moroko na Zambia.

 

Categories
Michezo

Cameroon na Mali watoshana nguvu huku Burkina Fasso ikiwatimua Zimbabwe CHAN

Wenyeji Cameroon maarufu kama Indomitable Lions na Flying Eagles ya Mali  zilitoka sare  ya bao 1-1   katika uwanja wa Ahidjo Ahmadou mjini Doula,mchuano  wa kundi A uliochezwa Jumatano usiku .

Cameroon walitangulia kufunga bao katika dakika ya 6  kupitia kwa Salomon Bindjeme 2 kabla ya Issaka Samake kuisawazishia Mali kunako dakika 12 na kipindi cha kwanza kumalizika kwa sare ya 1-1.

Timu zote zilicheza kwa tahadhari kuu huku mchuano ukimalizika kwa sare ya bao 1-1.

Matokeo hayo yanamaanisha kuwa timu zote zina fursa ya kufuzu kwa robo fainali zikiwa na alama 4 kila moja huku wakimaliza mechi zao Jumapili ijayo  ambapo Cameroon watacheza na Burkinafasso huku Mali wakihitimisha ratiba dhidi ya  Zimbabwe.

Katika pambano la pili Jana usiku Zimbabwe inayofunzwa na kocha Zdravko Lugarisic ilikuwa timu ya kwanza kubanduliwa katika mashindano ya mwaka huu baada ya kupoteza mabao 3-1 kwa Burkina Fasso  katika uwanja wa Ahidjo Amadou.

Issouf Sosso alifungua ukurasa wa magoli kwa Burkinafasso katika dakika ya 14 kabla ya Partson Jaure kusawazisha katika dakika ya 23 na kipindi cha kwanza kuishia sare ya 1-1.

Claver Kiendrébéogo aliwarejesha Burkinafasso uongozini kwa bao la pili dakika 53 naye Issiaka Ouédraogo kupachika bao la tatu dakika ya 67.

Cameroon wangali kuongoza kundi hilo kwa pointi 4 sawa na Mali wakifuatwa na Burkina Fasso kwa alama 3 wakati Zimbabwe ikiwa bila alama.

Mechi mbili za kundi B kupigwa Alhamisi Libya wakifungua ratiba dhidi ya Congo DR nao Niger wacheze na Congo Brazaville saa nne usiku.

 

 

Categories
Michezo

Cameroon na Mali zawinda nafasi ya robo fainali

Wenyeji Indomitable Lions ya Cameroon na Flying Eagles ya Mali watakuwa wakiwania tiketi ya kwanza kucheza robo fainali ya makala ya 6 ya kombe la CHAN watakapopambana Jumatano usiku katika mchuano wa kwanza wa raundi ya pili uwanjani Ahidjo Amadou  mjini Yaounde Cameroon.

Timu hizo zitakutana katika mechi ya kundi A ikiwa ni mara ya pili katika historia baada ya Cameroon kuwashinda Mali bao 1-0 katika makala ya CHAN mwaka 2011 nchini Sudan.

Mataifa yote yaliafungua makala ya mwaka huu ya CHAN kwa ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Zimbabwe na Burkinafasso Jumamosi iliyopita huku pia ikisadifu magoli yote kufungwa kuanzia dakika za 70  na 72 .

Kocha wa Mali Nahoum Diane’ ambaye ana uzoefu mkubwa atajaribui kutumia vyema safu yake ya ushmabulizi na mabeki ili kupata matokeo huku Indomitable Lions pia wakijivunia safu imara ya nyuma.

Sare pia itafaidi pande zote na kuwafuzisha robo fainali endapo mchuano wa pili kati ya Burkinafasso na Zimbabwe utaishia sare.

Categories
Michezo

Camerron wakashifiwa kwa ushirikina katika mechi yao CHAN dhidi ya Zimbabwe

Cameroon walishutumiwa  vikali kabla ya mchuano wa ufunguzi wa Chan dhidi ya Zimbabwe Jumamosi kwa madai ya kutumia ushirikina.

Hii ni baada ya popo aliyekufa kupatikana katikati ya uwanja  na kocha wa Zimbabwe Zdravko Lugarisic zamani akiwa Gor Mahia ya Kenya.

Kocha wa Zimbabwe Lugarisic akionyesha popo aliyefia katikatiya uwanja

Cameroon walisajili ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Zimbabwe katika mchuano huo huku wakipoteza nafasi nyingi za kupata magoli zaidi.

Hata hivyo wapo waliosema ni kawaida kwa ndege kama popo kuanguka uwanjani au kufia uwanjani ingawa Lugarisic Raia wa Croatia alikuwa na mtazamo kuwa huo ulikuwa ushirikina na ndio chanzo cha timu yake kupoteza.

 

Categories
Michezo

Wenyeji Cameroon wafungua CHAN kwa ushindi

Wenyeji Indomitable Lions walianza makala ya 6 ya fainali za kombe la CHAN kwa ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Zimbabwe katika mchuano wa kundi A uliosakatwa Jumamosi usiku katika uwanja wa Ahmadou Ahidjo mjini Yaounde.

Baada ya kipindi cha kwanza kumalizika kwa sare tasa Cameroon walirejea kipindi cha pili wakiwa wameimarisha mchezo na kuongeza mashambulizi ndiposa beki  Salomon Banga akapachika bao la tikitataka kunako dakika ya 72 .

Cameroon walipoteza nafasi nyingi za kufunga mabao kuanzia kipindi cha kwanza huku pia kipa wa Zimbabwe Ariel Sibanda akipangua mikwaju kadhaa .

sehemu ya  sherehe za ufunguzi

Mashabiki wa nyumbani walioruhusiwa uwanjani waliipa shime timu yao na kusajili ushindi huo mhimu ambao unawaweka katika nafasi nzuri ya kutinga robo fainali.

Kabla ya mchuano wa ufunguzi kulikuwa na sherehe kabambe za ufunguzi ambapo pia rais wa Fifa Gianni Infantinho alikuwa uwanjani kuhudhuria pambano hilo.

Categories
Michezo

Cameroon kusukumwa na mashabiki wa nyumbani CHAN

Mataifa 16 yako nchini Cameroon kushiriki  mashindano  ya Afrika kwa wachezaji wanaosakata  soka katika ligi za nyumbani maarufu  CHAN  yatang’oa nanga rasmi Jumamosi hii.

Mataifa hayo 16 yametengwa katika makundi manne ya timu 4 kila moja huku mechi hizo 32 zikiandaliwa katika viwanja 4 vilivyo katika miji mitatu  nchini Cameroon .

Tuangazie  Cameroon iliyo  katika kundi A ambalo linajumuishwa wenyeji pia ,Zimbabwe,Mali na Burkinafasso.

Cameroon watacheza pambano la ufunguzi Jumamosi dhidi Zimbabwe  kuanzia saa moja katika kundi A kabla ya kuwapisha Mali watakaomenyana na Burkinafasso saa nne usiku mechi zote zikipigwa katika uwanja wa Limbe.

Cameroon watakuwa wakicheza CHAN kwa mara ya nne wakicheza hadi robo fainali mara mbili mwaka 2011 na 2016 , ingawa walishindwa kutoka kwa kundi lao katika makala ya mwaka 2018 ,  na watakuwa wakiongozwa na Martin Ndtoungou Mpile .

The Indomitable Lions inajivunia wachezaji  beki Banga Bindjeme aliyekuwa CHAN mwaka 2018 na mshambulizi mzoevu Jacques Zoa.

Wenyeji watakuwa na msukumo wa kipekee baada ya serikali na waandalizi wa michuano hiyo kuruhusu mashabiki wa nyumbani pekee kuingia uwanjani.