Categories
Michezo

Safari ya Afrika kwenda kombe la dunia Qatar mwaka ujao yaahirishwa hadi Oktoba

Shirikisho la kandanda Afrika Caf limetangaza kuahirisha  mechi za kufuzu kwa kombe la dunia mwaka ujao nchini Qatar kutoka mwezi Juni hadi  Oktoba.

Caf imesema kuwa imebidi kuahirisha mechi hizo kutokana na changamoto zilizoletwa  na janga la Covid 19 .

Kulingana na kamati kuu ya CAF  mechi hizo sasa zitaanza Oktoba na kumalizika Machi mwaka 2022.

Habari hizo ni afueni kwa timu nyingi ambazo zilikuwa hazijajiandaa vyema haswa baada ya kukamilisha mechi za kufuzu kwa kombe la AFCON mwezi Machi mwaka huu.

Harambee stars imejumuishwa kundi E la safari ya kwenda Qatar pamoja na The Flying Eagles ya Mali,Uganda Cranes na Amavubi ya Rwanda na waatanza harakati za kufuzu dhidi ya Uganda Cranes jijini Nairobi kabla ya kuzuru Kigali dhidi ya Rwanda.

Timu bora kutoka kila kundi itafuzu kwa raundi ya pili na ya mwisho ambapo washindi watano watawakilisha Afrika katika fainali za kombe la dunia kati ya Novemba 21 na Disemba 18 nchini Qatar mwaka ujao.

 

 

Categories
Michezo

Zoo Fc yaondolewa ligi KUU FKF na kushushwa hadi ligi ya daraja ya kwanza kwa kupanga matokeo

Shiriksisho la soka ulimwenguni  Fifa  mapema Jumanne limetangaza kuishusha klabu ya Zoo Fc  kutoka ligi kuu ya FKF hadi ligi ya National super league  kwa koas la kupanga matokeo ya mechi .

Kulingana na barua  iliyoandikwa na mwenyekiti wa kamati ya nidhamu ya FIFA  Alejandro Piera Zoo Fc yenye makao yake kaunti ya Kericho  imepatikana na makosa  ya kupanga matokeo ya mechi zake  na imeondolewa kwenye ligi kuu kwa msimu mmoja.

Ni Januari mwaka uliopita ambapo kocha wa  Zoo  Herman Iswekha  alikiri kuwa wachezaji wake watatu  walikuwa wakipanga matokeo ambao baadae waliruhusiwa kuondoka .

Kufurushwa kwa Zoo  kutoka ligi kuu kwa makosa ya kupanga matokeo kuanjiri miaka miwili baada ya wachezaji  wane  kuhusishwa kupanga matokeo katika ligi kuu msimu wa mwaka 2019 na pia ni mapema mwaka jana ambapo Mganda Ronald Mugisha alitiwa mabroni katika hoteli moja mjini Kisumu kwa kuhisika kupanga matokeo ya mechi kati ya KCB na Western Stima lakini aachiliwa huru baadae kufuatia mwenyekiti wa Stima Laban Jobita kuondoa kesi mahakamani.

Categories
Michezo

CAF yaidhinisha uwanja wa Nyayo kuandaa mechi ya Harambee stars kufuzu kwa kombe la dunia dhidi ya Uganda

Categories
Michezo

Mabingwa watetezi Al Ahly kumenyana na Mamelodi Sundowns robo fainali ya ligi ya mabingwa Afrika

Mabingwa watetezi wa ligi ya mabingwa Afrika Caf,Al Ahly kutoka Misri watapambana na Mamelodi Sundowns ya Afrika Kusini katika kwota fainali ya kombe hilo.

Ahly ambao ni washindi mara 9 wa kombe hilo  na wanaofunzwa na kocha wa zamani wa Mamelodi  Pitso Mosimane ,wataanzia nyumbani  kati ya Mei 14 na 15 huku marudio yakiwa Afrika Kusini wiki moja baadae.

Mc Alger ya Algeria itachuana na Wydad Casablanca kutoka Moroko,Esperance ya Tunisia imenyane na Cr Belouizdad ya Algeria wakati waakilishi pekee wa Afrika mashariki Simba Sports club kutoka Tanzania wakimaliza udhia na Kaizer Chiefs ya Afrika Kusini.

Mshindi wa robo fainali kati ya Ahly na Mamelodi  akicheza nusu fainali dhidi ya atakayeshinda kati ya Belouizdad na  Esperance huku mshindi kati ya Simba na Kaizer Chiefs akipimana nguvu na mshindi kati ya MC Alger na  Wydad Casablanca.

Mshindi wa kombe hilo atafuzu kuwakilisha Afrika katika mashindano ya kombe la dunia baina ya vilabu mwishoni mwa mwaka huu.
Categories
Michezo

Droo ya kwota fainali ya kombe la shirikisho yatangazwa

Droo ya kwota fainali ya kombe la shirikisho la soka Afrika imeandaliwa  Ijumaa mjini Cairo Misri huku mkondo wa kwanza ukipigwa Mei 16 na mechi za marudio zichezwe Mei 23.

Kulingana na droo hiyo Raja Casablanca ya Moroko  itachuana na Orlando Pirates ya Afrika Kusini,Pyramids ya Misri waliocheza  hadi fainali ya mwaka jana ipambane na Enyima kutoka Nigeria wakati CS Sfaxien ya Tunisia ikiwa na miadi dhidi ya Js Kabelyie ya Algeria huku  Cotton Sport ya Cameroon wakimaliza udhia na As Jaraaf ya Senegal.

Mshindi wa robo fainali kati ya Orlando Pirates na Raja Casablanca atamenyana na mshindi  baina ya Pyramids  na Enyimba kwenye nusu fainali ya kwanza huku mshindi kati ya Faxien na Kabyilie  akiwema miadi dhidi ya atakayeshinda kati ya Jaraaf na  Cotton Sport katika nusu fainali ya pili.

Duru ya kwanza ya  semi fainali itasakatwa baina ya Juni 18 na 20  huku marudio yakiwa kati ya Juni 25 na 27 nayo fainali iandaliwe Julai 10.

 

Categories
Uncategorised

Ratiba ya kwota fainali kombe la shirikisho Afrika CAF yakamilika

Ratiba ya timu 8 zitakazocheza kwota fainali ya kombe la shirikisho la soka Afrika imebainika baada ya kukamilika kwa mechi za kundi Jumatano usiku.

Timu zilizotinga robo fainali ni pamoja na :-

Enyimba ya Nigeria -ni mabingwa mara mbili wa ligi ya mabingwa.

Orlando Pirates ya Afrika Kusini -wameshinda ligi ya mabingwa mwaka 1995 na kuibuka wa pili katika kombe la shirikisho mwaka 2015.

Js Kabyelie kutoka Algeria – walishinda kombe la CAF  Cup mara tatu.

Cotton Sport ya Cameroon- walimaliza wa pili katika ligi ya mabingwa mwaka 2008.

ASC Les Jaraaf Des Dakar kutoka Senegal – wamefuzu kwa mara ya kwanza kwa robo fainali.

CS Sfaxien ya Tunisia  -walionyakua kombe la  shirikisho mara tatu.

Raja Club  Athletic ya Moroko  – ni washindi wa kombe hilo mwaka 2018 na washindi wa ligi ya mabingwa mara 3.

Pyramids ya Misri – ilimaliza ya pili mwaka jana katika kombe la shirikisho.

Vilabu hivyo vinane vitabaini wapinzani wao kwenye droo itakayoandaliwa jijini Cairo Misri Ijumaa  ya April  30  ambapo timu zilizoongoza makundi yao zitapangwa dhidi ya zile zilizomaliza za pili kwenye makundi yao.

Timu zilizoongoza makundi ni Enyimba ,JS Kabylie,Jaraaf  na Raja Casablanca.

 

 

 

Categories
Michezo

Droo ya soka kuwania taji ya Olimpiki mjini Tokyo Japan yazumiza timu za Afrika

Droo ya soka kwa wanaume na wanawake katika makala ya 32 ya michezo ya Olimpiki mwaka huu mjini Tokyo Japan imetangazwa huku timu za Afrika zikijumuishwa makundi magumu.

Kwa mjibu wa droo hiyo iliyoandaliwa mjini Zurich Uswizi ,mataifa 28 yaliyofuzu kwa wanaume na wanawake yametengwa katika makundi 7 ya timu nne nne kila moja .

Bafana Bafana ya Afrika Kusini imejumuishwa kundi A katika soka ya wanaume pamoja na wenyeji Japan,Mexico na Ufaransa huku waakilishi wengine wa bara hili  Misri wakiwa kundi C pamoja na Uhispania,Argentina na Australia wakati Ivory Coast wakiangukia kundi D pamoja na  mabingwa watetezi Brazil,Ujerumani iliyoibuka ya pili mwaka 2016  na Saudi Arabia.

Droo ya Soka ya wanaume

Kundi  A: Japan, South Africa, Mexico, France.

Kundi B: New Zealand, Korea Republic, Honduras, Romania.

Kundi C: Egypt, Spain, Argentina, Australia.

Kundi D: Brazil, Germany, Côte d’Ivoire, Saudi Arabia.

Waakilishi pekee  wa Afrika Zambia maarufu kama Shipolopolo wamo  kundi moja na China,Brazil na Uholanzi

Makundi ya soka ya wanawake

Kundi E: Japan, Canada, Great Britain, Chile.

Kundi F: China PR, Brazil, Zambia, Netherlands.

Kundi  G: Sweden, USA, Australia, New Zealand.

Mashindano hayo yataanzia hatua ya makundi kabla ya kuingia mchujo wa robo fainali,nusu fainali  mechi ya medali ya shaba na hatimaye fainali.

 

Categories
Michezo

Kocha wa Uganda Cranes Jonathan Mckinstry atimuliwa

Shirikisho la soka nchini Uganda FUFA limetamatisha kanadarasi ya kocha wa timu ya taifa The Cranes Jonathan Mckinstry kwa maafikiano.

Makinstry amekuwa akiiongoza Uganda kwa kipindi cha miezi 18 iliyopita kwenye mkataba wake wa miaka mitatu , huku akiwasaidia kutwaa kombe la CECAFA mwaka 2019.

Hata hivyo mambo yamemwendea tenge Mwingereza huyo wa Ireland Kaskazini  ,huku akipigwa marufuku katika mechi mbili za mwisho za Uganda kufuzu kwa kombe la AFCON mwakani dhidi ya Burkina Faso na Malawi, huku wakikosa kufuzu kwa kuibuka nafasi ya tatu.

Mckinstry awali amezinoa timu za Rwanda na Sierra Leona na FUFA inatarajiwa kutangaza mkufunzi mpya kabla ya kuanza kwa mechi za kufuzu kwa kombe la dunia mwezi Juni mwaka huu,timu hiyo ikiwa kundi moja na Kenya,Rwanda na Mali.

Categories
Michezo

Nahodha wa Uganda Dennis Onyango astaafu soka kimataifa

Nahodha wa muda mrefu wa timu taifa ya Uganda Dennis Onyango amestaafu soka ya kimataifa.

Onyango ambaye amekuwa kipa chaguo la kwanza wa Uganda Cranes aliandika waraka kwa shirikisho la Uganda FUFA  kustaafu akitaja kuwa aliafikia uamuzi huo mgumu kufuatia ushauri wa familia yake.

“Nimechukua uamuzi huu mgumu baada ya kushauriwa na familia yangu ,nichukue fursa hii kuishukuru familia yangu,meneja wangu na wote waliochangia ufanisi wangu”akasema Onyango

Kwa jumla Onyango ambaye pia anaichezea klabu ya Mamelodi Sundowns ya Afrika Kusini, aliichezea Cranes mechi 79  za kimataifa tangu mwaka  2005 dhidi ya Cape Verde.

Kustaafu kwa Onyango aliye na umri wa miaka 35 kunatokea wiki moja baada ya kiungo  Hassan Waswa pia kutangaza kustaafu soka ya kimataifa.

 

Categories
Michezo

Kocha wa Togo Claude Le Roy ang’atuka baada ya kuwa usukani kwa miaka mitano

Kocha wa Togo Claude Le Roy amejiuzulu baada ya kuiongoza timu hiyo kwa miaka mitano huku akishindwa  kuifuzisha kwa fainali za mwaka ujao za kombe la AFCON.

Mfaransa huyo aliye na umri wa miaka 73 alishika hatamu za kuinoa Togo maarufu kama the Hawks mwaka 2016 huku akiwafuzisha kwa fainali za AFCON mwaka 2017 nchini Gabon lakini ikashindwa kufuzu mwaka 2019 na pia mwaka ujao nchini Cameroon.

Claude Le roy

Kwa Jumla Le Roy ameiongoza Togo kwa mechi 35 za kimataifa akishinda 9 kutoka sare 12 na kupoteza 14, hivi punde  ikiwa kichapo cha nyumbani dhidi ya Kenya katika mchuano wa kufuzu kwa fainali za mwakani za AFCON.

Le Roy amejiuzulu kwa maafikiano na shirikisho la soka nchini Togo FTF na waziri wa michezo Dkt Bessi Lidi Kama na sasa wataanza sakasaka za mkufunzi mpya kabla ya mechi za kufuzu kombe la dunia mwaka ujao nchini Qatar mechi zitakazoanza Juni mwaka huu ,Togo ikijumuishwa kundi  H pamoja na Senegal,Congo na Namibia.