Categories
Michezo

Droo ya robo fainali ya mataji ya Afrika kuandaliwa April 30

Shirikisho la kandanda Afrika limetangaza kuandaa droo ya mechi za kwota fainali kuwania mataji ya ligi ya mabingwa na kombe la shirikisho April 30 mwaka huu.

Kulingana na droo hiyo timu zitakazoibuka za pili zitapangwa dhidi ya wapinzani watakaoongoza  makundi yao.

Mechi za makundi za ligi ya mabingwa zilikamilika wiki iliyopita huku vilabu  vilivyofuzu kwa robo fainali vikiwa Simba ya Tanzania,Al Ahly ya Misri ,Mamelodi Sundowns ya Afrika Kusini,Cr Belouizdad kutoka Algeria,Esperance ya Tunisia,Mc Alger ya Algeria,Kaizer Chiefs kutoka Afrika Kusini na Wydad Casablanca ya Moroko.

Mechi za makundi za kombe la shirikisho zitakamilika tarehe 29 mwezi huu.

Categories
Michezo

Fahamu timu 8 zitakazopiga robo fainali ya ligi ya mabingwa Afrika

Vilabu vinane vitakavyocheza kwota fainali ya ligi ya mabingwa Afrika ,imebainika kufuatia kumalizika kwa mechi za makundi Jumamosi iliyopita.

Timu nane zilizotinga robo fainali ni ;Simba sports Club ya Tanzania,Al Ahly ya Misri za kutoka kundi A,Mamelodi Sundowns ya Afrika Kusini na  CR Belouizdad ya Algeria za kundi B,Wyadad Casablanca kutoka Moroko na Kaizer Chiefs ya Afrika Kusini,Esperance ya Tunia na Mc Alger ya Algeria za kundi D.

Algeria na Afrika Kusini  inawakilishwa na timu 2 kila moja,wakati Tanzania,Tunisia,Moroko na Misri zikiwa na timu moja kila moja.

MC Alger-ilibuniwa mwaka 1962 ikiwa timu ya kwanza ya dini ya Kiislamu nchini Algeria

Inafunzwa na kocha Abdelkadir Amrani na itakuwa ikishiriki hatua ya robo fainali kwa mara ya nne  na ya kwanza tangu mwaka 1980 na kwa jumla watakuwa wakicheza kwota fainali kwa mara ya 8 ,miaka ya 1976 walipoibuka mabingwa,1977,1979,1980,2000,2011 na 2018.

CR Belouizdad  au Chabab Riadhi de Belouizdad  ni timu ya Algeria iliyobuniwa mwaka 1962  na itakuwa ikishiriki kombe la ligi ya mabingwa kwa mara ya  4 na ya kwanza tangu mwaka  2001 ingawa ni mara ya kwanza kucheza robo fainali.

Belouizdad wameshiriki kombe hilo miaka ya 1970,2001 na 2002 huku wakibanduliwa katika raundi ya kwanza kwenye makala yote.

Wydad Athletic  Club  au maarufu Wydad Casablanca ni timu ya Moroko  iliyobuniwa mwaka 1937 na inaongozwa na kocha Faouzi Benzarti.

WAC inashiriki ligi ya mabingwa kwa mara ya 12 mwaka msimu huu na wametawazwa mbaingwa mwaka wa 1992 na 2017 na pia walicheza hadi robo fainali msimu wa mwaka 2019-2020.

Al Ahly ni timu ya Misri iliyobuniwa mwaka 1907 na ni miongoni mwa timu kongwe zaidi Afrika.

Ahly maarufu kama Red Devils ndio timu iliyoshinda kombe la ligi ya mabingwa Afrika mara nyingi zaidi ikiwa mara 9 na inaongozwa na kocha Pitso Mosimane.

Ahly wanatetea kombe hilo msimu huu .

Mamelodi Sundowns ukipenda Masandawana au the Brazzillians ni klabu ya Afrika Kusini iliyobuniwa mwaka 1970 na wanashiriki ligi ya mabingwa Afrika kwa mara ya 14 wakitawazwa mabingwa mwaka 2016 na watakuwa wakicheza kwota fainali kwa mara ya 6.

Kaizer Chiefs ukipenda  Amakhosi  na ilibuniwa mwaka 1970  na inafunzwa na kocha Gavin Hunt.

Chiefs wamefuzu kwa robo fainali ya ligi ya mabingwa Afrika kwa mara ya kwanza .

Esperance sportive du Tunis  ni klabu ya Tunisia  inashiriki kombe la ligi ya mabingwa msimu huu kwa mara ya 19  na kuibuka mabingwa mara 4 mwaka 1994,2011,2018  na 2019  .

Simba sports club ndio mwakilishi pekee wa Afrika mashariki na ukanda wa Cecafa aliyefuzu kwa robo fainali ya mwaka huu ikiwa pia mara ya kwanza katika historia ya ligi ya mabingwa Afrika.

Timu nane zilizofuzu kwa hatua ya robo fainali zimegawanywa katika makundi mawili ,viongozi wa makundi na timu zilizonyakua nafasi za pili.

Katika kwota fainali timu zilizoongoza makundi zimetanganishwa na zitapangwa dhidi ya wapinzani waliomaliza nafasi ya pili lakini timu zilikuwa kundi moja hazipangwa pamoja .

Hata hivyo hali itabadilika wakati wa droo ya semi fainali ambapo timu yoyote itapangwa na mpinzani yeyote.

Mabingwa wa kombe hilo watafuzu kuhsiriki kombe la dunia baina ya vilabu.

 

 

 

 

Categories
Michezo

Mechi za makundi za ligi ya mabingwa kukamilika Jumamosi

Michuano ya makundi kuwania kombe la ligi ya mabingwa Afrika itakamilika Jumamosi huku orodha ya timu 8 zitakazocheza kwota fainali ikibainika.

Hata  hivyo tayari timu 6 kati 8 zitakazocheza robo fainali zimebainika ambapo kundi A Simba ya Tanzania iliongoza kwa alama 13 licha ya kushindwa  bao 1-0 dhidi ya Ahly  ya Misri  Ijumaa usiku kikiwa kipigo cha kwanza huku timu zote mbili zikifuzu kwa awamu ya nane bora.

Mamelodi Sundowns ya Afrika Kusini iliongoza kundi B kwa alama 13 licha ya kushindwa pia kwa mara ya kwanza walipocharazwa mabao 2-0 na CR Belouizdad ya Algeria Ijumaa huku wote wawili wakitinga kwota fainali.

Viongozi wa kundi C Wydad Casablanca ya Moroko ambao tayari wamefuzu kwa robo fainali wataawalika  Petro Atletico ya Angola Jumamosi wakati Horoya ya Guinea ikiwa nyumbani kupimana na nguvu na Kaizer Chiefs ya Afrika Kusini huku pande zote zikiwania nafasi moja iliyosalia kundini ya kufuzu.

Katika kundi D mabingwa wa zamani Esperance watawaalika Mc Alger kutoka Algeria,wageni wakihitaji ushindi ili kuongoza kundi hilo au sare ili kujikatia tiketi kwa robo fainali.

Zamalek ya Misri wako nyumbani dhidi ya mabingwa wa Senegal Tengueth katika mchuano ambao wenyeji sharti washinde ili kuwa na fursa ya kufuzu kwa robo fainali.

Categories
Michezo

Ratiba ya mechi za robo fainali kuwania kombe la ligi ya mabingwa Afrika kubainika

Mechi za makundi kuwania kombe la ligi ya mabingwa Afrika zitaingia raundi ya 5 Jumamosi huku ratiba timu zitakazapiga robo fainali zikitarajiwa kubainika.

Al Merrikh ya Sudan ambayo tayari imebanduliwa itakuwa nyumbani kuwaalika mabingwa watetezi Al Ahly wanaohitaji ushindi ili kujiongezea matumaini ya kuongoza kundi A,wakati Simba SC ya Tanzania ikiwa nyumbani uga wa Benjamin Mkapa dhidi ya AS Vita ya DRC.

Simba wanaongoza kundi hilo kwa pointi 10,tatu zaidi ya Ahly ,huku vijana hao wa Tanzania wakihitaji tu sare kufuzu kwa robo fainali kwa mara ya kwanza,wakati Vita waki hawana budi kushinda ili kufufua matumaini ya kutinga kwota fainali .

Wydad Casablnca ya Moroko ambayo tayari imefuzu kwa robo fainali itawazuru Kaizer Chiefs ya Afrika Kusini,wakati Petro Atletico ya Angola ikiwa nyumbani Luanda dhidi ya Horoya AC ya Guinea.

Esperance ya Tunisia itakuwa ziarani dhidi ya mabingwa wa Senegal Tengueth wakati Zamalek wakipambana na MC Alger ya Algeria.

Kufikia sasa timu za Mamelodi Sundowns ya Afrika Kusini,Wydad Casablanca kutoka Moroko na Esperance ya Tunisia zimejikatia tiketi kwa kwota fainali.

 

 

Categories
Michezo

Mamelodi na Esperance watinga robo fainali ya ligi ya mabingwa Afrika

Mamelodi Sundowns na Esperance ndizo timu mbili za kwanza kutinga kwota fainali ya ligi ya mabingwa Afrika baina ya vilabu vya Afrika , baada ya kushinda mechi zao za Jumanne usiku .

Hamdou El Houni alipachika bao la pekee na kuwawezesha mabingwa mara 4 Esperance kutoka Tunisia  kupata ushindi wa goli 1 kwa bila ugenini dhidi ya Zamalek ya Misri  na kuongoza kundi D kwa pointi 10 nao MC Alger kutoka Algeria wakawalemea mabingwa wa Senegal Tengueth  bao 1 kwa nunge na kuweka hai matumaini ya kufuzu robo faiali.

Esperance wakichuana na Zamalek

Alger ini ya pili kwa alama 8 ikifuatwa na Zamalek  kwa alama 2 huku Tengueth  wakishika mkia kwa pointi 1.

Mamelodi Sundowns ya Afrika Kusini ikicheza nyumbani iliwacharaza Toupiza Mazembe ya Jamhuri ya Demokrasia ya Congo bao 1 kwa bila na kufuzu kwa robo fainali ikiwa timu pekee iliyoshinda mechi zote 4  za ufunguzi.

Bao la Masandawana lilipachikwa kimiani na Lebohang Maboe dakika ya 28 .

Katika mechi nyingine ya kundi B CR Belouizdad ya Algeria ilitoka sare tasa dhidi ya Al Hilal Omdurman ya Sudan.

Mamelodi wanaongoza kundi B  kwa alama 12 wakifuatwa kwa umbali na Belouizdad na Hilal kwa alama 3 kila moja huku  Mazembe ikishika nanga kwa alama 2.

Mamelodi wakipiga dhidi ya Mazembe

Mabingwa mara mbili wa kombe hilo Wydad Casablanca kutoka Moroko waliambulia sare tasa ugeninini dhidi ya Horoya katika kundi C  wakati Kaizer Chiefs na Petro Atletico ya Angola pia zikitoka sare ya 0-0 .

Casablanca wanaongoza kundi hilo kwa alama 10,wakifuatwa na Horoya na Kaizer kwa pointi 5 kila moja wakti Atletico ikiwa na alama 1.

Simba ya Tanzania inaongoza kundi A kwa alama  10 ikifuatwa na Ahly kwa alama 7 huku Vita Club ikiwa ya tatu kwa alama 4 nayo Merreikh ina pointi 1.

Mechi za raundi ya tano zitachezwa tarehe 2 mwezi ujao huku zile za awamu ya 6 na ya mwisho zikisakatwa April 9.

 

Categories
Michezo

Simba yanusia robo fainali ya ligi mabingwa baada ya kumng’ata mwarabu mweusi 3-0

Miamba wa soka Afrika mashariki Simba SC imeendelea kuongoza kundi A la michuano kuwania kombe la ligi ya mabingwa Afrika na kujiweka katika hali nzuri ya kutinga kwota fainali kwa mara ya kwanza baada ya kuifyatua Al Merreikh ya Sudan magoli 3-0 katika mechi iliyosakatwa uwanja wa Benjamin Mkapa jijini Daresalaam Tanzania Jumanne alasiri.

Luis Miquissone aliyepachika bao lilomwadhibu mwarabu wa Misri,alifungua ukurasa wa magoli kwa bao la dakika ya 18 kabla ya Mohamed Hussien kuongeza la pili dakika ya 38 huku vijana wa msimbazi wakiongoza 2-0 kufikia mapumzikoni.

Kipindi cha pili Mnyama aliendelea na gonga gonga zake na kubisha mlango wa wakwasi wa mafuta ,Merreikh na dakika ya 49 Chris kope Mugalu akacheka na nyavu kwa bao la tatu na kutoka hapo wajukuu wa Mkapa wakaendelea na mazoezi hadi kipenga cha mwisho wakipata alama tatu muhimu na magoli matatu bila jawabu.

Ushindi huo unaiweka Simba mguu mmoja ndani ya robo fainali ya kombe hilo kwa mara ya kwanza wakihitaji pointi moja pekee kutokana na mechi zilizosalia mbili wakiwaalika AS Vita Club ya Jamhuri ya demokrasia ya Congo na mwaliko mjini Cairo dhidi ya mabingwa mara 9 Al Ahly April 9.

Ahly pia wamesajili ushindi wa pili baada ya kuwanyuka Vita 3-0 katika mji wa Kinsasha na kufufua matumaini yao ya kufuzu kwa robo fainali.

Simba wanaongoza kundi A kwa pointi 10 ,3 zaidi ya Ahly huku Vita ikiwa na alama 4 nayo Merreikh inashika nanga kwa alama 1

Categories
Michezo

Mechi za CAF Champions League kuingia raundi ya nne Jumanne

Michuano ya kuwania kombe la ligi ya mabingwa baina ya vilabu vya Afrika itaingia raundi ya 4 hatua ya makundi Jumanne huku timu za kwanza kutinga robo fainali zikitarajiwa kuanza kubainika.

Simba Sc ya Tanzania inayoongoza kundi A kwa alama 7 itakuwa nyumbani Daresalaam katika uwanja wa Benjamin Mkapa kuwaalika Al Merreikh ya Sudan saa kumi alasiri wakati mabingwa watetezi Al Ahly kutoka Misri wakiwa Kinsasha dhidi ya AS Vita Club.

Msimamo kundi A

1.Simba–alama 7

2.AS Vita—alama 4

3.Al Ahly —alama 4

4.Al Merreikh–alama 1

Katika kundi B Mamelodi Sundowns ya Afrika Kusini watakuwa nyumbani kuwaalika mabingwa wa zamani TP Mazembe ya Demokrasia ya Congo,wenyeji wakihitaji ushindi ili kutinga robo ,wakati Mazembe wakiwinda ushindi wa kwanza.

Katika pambano jingine kundi hilo Al Hila Omdurman ya Sudan itawakaribisha mabingwa wa Algeria CR Belouizdad.

Msimamo wa kundi B

1.Mamelodi—-alama 9

2.Al Hilal——-alama 2

3.Mazembe —alama 2

4.Belouizdad—-alama 2

Vigogo wa Moroko Wydad Casablanca watazuru  Conakry kuvaana ba Horoya AC ,Casablanca wahitaji ushindi pia kufuzu kujihakikishia nafasi ya kwanza na kutinga kwota fainali.

Kaizer Chiefs ya Afrika Kusini itawaandaa  Petro Atletico ya Angola katika mechi nyingine ya kundi C.

Msimamo wa kundi C

1.Wydad —-alama 9

2.Horoya—–alama 4

3.Kaizer—–alama 4

4.Petro—-alama 0

Katika kundi D Esperance watakuwa Misri kukabana koo na Zamalek wakati Mc Alger ya Algeria ikiwaalika mabingwa wa Senegal Tengueth.

Msimamo wa kundi D

1.Esperance —alama 7

2.Alger——-alama 5

3.Zamalek —-alama 2

4.Tengueth —-alama 1

Timu mbili bora kutoka kila kundi zitafuzu kucheza robo fainali ya kombe hilo ambalo mabingwa hutuzwa zawadi nono ya dola milioni 2.5 za Marekani na kufuzu kucheza kombe la dunia baina ya vilabu.

 

Categories
Michezo

Simba yaitafuna Vita hadharani

Miamba wa soka nchini Tanzania,klabu ya Simba Sports club walianza vyema mechi za makundi za kuwania kombe la ligi ya mabingwa Afrika baada ya kuwaangusha AS Vita Club ya Jamhuri ya Demokrasia ya Congo bao 1 bila jawabu katika pambano la kundi A lililopigwa Ijumaa usiku katika uwanja wa Kinsasha.

Bao la mnyama Simba lilitiwa kimiani na mshambulizi Mutshimba Lugalu kupitia mkwaju wa penati  kunako dakika ya 60 na kudumu hadi kipenga cha mwisho.

beki kisi wa Kenya Joash Onyango alipiga dakika zote 90 huku kiungo Francis Kahata akiingia uwanjani kipindi cha pili.

Simba wanaongoza kundi hilo kwa alama 3 ,wakishiriki hatua ya makundi  kwa mara ya pili na ya kwanza  tangu mwaka 2013.

Wekundu wa msimbazi Simba watarejea Dar kujiandaa kwa mkwangurano wa pili watakapowaalika mabingwa watetezi na washindi mara 9 wa kombe hilo Al Ahly  kutoka Misri Februari 23.

Katika pambano la kundi D lililochezwa Cairo,Zamalek walilazimishwa kutoka sare kapa nyumbani dhidi ya MC Alger kutoka Algeria.

Categories
Michezo

Simba SC tayari kumvaa Vita Club huko Kinsasha

Mabingwa wa ligi kuu ya Tanzania bara Simba Sc wameanza mazoezi mjini Kinsasha  Alhamisi jioni  katika jamhuri ya Demokrasia ya Congo kujitayarisha kwa mechi ya kwanza ya makundi kuwania kombe la ligi ya mabingwa Afrika Ijumaa hii dhidi ya wenyeji As Vita Club.

Wekundu wa Msimbazi ambao ni mabingwa mara 21 wa ligi kuu ya kwao wamefuzu kucheza hatua ya makundi ya kombe hilo kwa mara ya pili katika historia na mara ya kwanza tangu mwaka 2003.

Kikosi cha Simba kilicho DRC kinawajumuisha wakenya Francis Kahata na beki kisiki Joash Onyango huku timu hiyo ikiwa ya pekee kutoka ukanda wa East Afrika iliyotinga hatua ya makundi katika kombe hilo .

Baadae tarehe 23 mwezi huu Simba watawaalika mabingwa watetzi na mabingwa mara 9 wa kombe hilo Al Ahly ya Misri,kabla ya kuzuru sudan Machi  5 kuvaana na Al Merreikh na kurudiana nao jijini daresalaam tarehe 16 mwezi uja.

Michuano ya ufunguzi hatua ya nakundi kuwania kombe la ligi ya mabingwa kusakatwa kati ya Ijumaa na Jumamosi.

Categories
Michezo

Ahly kuanza kutetea kombe la ligi ya mabingwa dhidi ya El Merreikh

Washindi mara 9  wa kombe la ligi ya mabingwa Afrika Al Ahly wamejumuishwa kundi A katika droo ya makundi iliyoandaliwa Ijumaa  mjini Cairo pamoja na El Merreikh ya Sudan ,Simba Sc kutoka Tanzania,na As Vita Club ya Drc.

Ahly wataanza ratiba dhidi ya El Merreikh mjini Cairo nao Simba waanzie ugenini dhidi ya Vita Club.

Kundi B linajumuisha Mamelodi Sundowns ya Afrika Kusini,mabingwa mara tano TP Mazembe kutoka Drc,El Hilal ya Sudan na CR  Belouizdad ya Algeria.

Waydad Casablanca ya Moroko wamejumuishwa kundi C pamoja na Horoya AC ya Guinea,Petro Atletico ya Angola na Kaizer Chiefs kutoka Afrika Kusini huku kundi D likisheheni mabingwa mara 4 Esperance ya Tunisia,mabingwa mara 5 Zamalek ,Mc Alger na Teungueth ya Senegal inayoshiriki kwa mara ya kwanza.

Mechi za raundi ya kwanza hatua ya makundi zitachezwa kati ya Februari 12 na 13 mwaka huu.