Categories
Vipindi

Mahojiano na Rais Uhuru Kenyatta kuhusu Covid-19

Leo asubuhi Rais Uhuru Kenyatta alifanya mahojiano na waandishi wa habari akiwemo Bonnie Musambi wa Radio Taifa kuhusu mikakati ya serikali kukabiliana na janga la virusi vya Covid-19.

Akizungumza kutoka Ikulu ya Nairobi, Rais Kenyatta alidhibitisha waliotoroka kutoka maeneo maalum walikokuwa wametengwa ili kukabiliana na kusambaa kwa virusi vya Covid-19 watasakwa, kukamatwa na kurejeshwa katika vituo hivyo na kutengwa kwa siku 14 zaidi.

Kuhusu swala la kulipa kodi, Rais alisema hatawalazimisha wamiliki wa nyumba kukosa kulipisha kodi huku akiwapongeza wale ambao wamewaruhusu wapangaji kutolipa kodi ya nyumba.

Kenyatta alisema serikali inatafakari kufunguliwa kwa shule baada ya athari ya virusi vya janga la Corona. Aliongeza kuwa serikali itahakikisha kuwa watahiniwa wa mitihani ya KCPE na KCSE wanafanya mitihani yao kama ilivyopangwa.

Rais alisisitiza kuwa saa za makataa ya kutotoka nje usiku hazitabadilika.

Sikiza mahojiano hapa…

https://podcasts.kbc.co.ke/wp-content/uploads/2020/04/PRES-UHURU-KENYATTA-INTERVIEW-WITH-JOURNALISTS-AT-STATEHOUSE-22ND-APR-2020.mp3