Categories
Michezo

Chelsea na PSG zafuzu nusu fainali ya ligi ya mabingwa ulaya licha ya kushindwa

Paris St Germain ya Ufaransa  na Chelsea ya Uingereza zimetinga nusu fainali ya kombe la ligi ya mabingwa barani ulaya licha ya kupoteza mechi za marudio  za robo fainali Jumanne usiku.

Mabingwa wa Ufaransa PSG kwa walilipiza kisasi cha kushindwa na Bayern Munich kwenye fainali ya mwaka jana ,na kuwatimua katika kwota  fainali kwa magoli ya ugenini ,baada ya mechi kumalizikia sare ya 3-3.

Munich walipata ushindi wa bao 1-0 ugenini Parc De Princess Jumanne usiku  kupitia wa Maxim Chuopo Moting lakini  matumaini ya kupata bao la pili ambalo lingewafuzisha yakazamishwa huku wenyeji wakisaidiwa na ushindi wa magoli 3-2 katika mkumbo wa kwanza ugani Allienz Arena.

Psg watakuwa wakipiga nusu fainali ya kombe hilo la kifahari kwa mara ya pili mtawalia ,baada ya kucheza hatua hiyo msimu uliopita.

Psg watakutana kwenye semi fainali na mshindi wa kwota fainali  kati ya Manchester City na Borusia Dortmund.

Katika marudio ya kwota fainali iliyosakatwa mjini Seville Uhispani,Chelsea waliokuwa wameishinda FC Porto ya Ureno magoli 2-0 katika mkumbo wa kwanza magoli waliangushwa bao 1-0 .

Porto walipata bao hilo la ushindi dakika ya nne ya ziada katika kipindi cha pili kupitia kwa  Mehdi Taremi,huku  Chelsea wakifuzu kupiga nusu fainali ya kombe hilo kwa mara  ya  8 ikiwa timu pekee ya Uingereza kufuzu kwa hatua hiyo mara nyingi zaidi  , pia ikiwa semi fainali ya kwanza kwa vijana wa Thomas Tuchel tangu mwaka 2014.

The Blues watachuana katika nusu fainali  baina ya mwisho wa mwezi huu na mwanzoni mwa mwezi ujao  na mshindi wa robo fainali ya Jumatato baina ya Liverpool na Real Madrid,Los Blancos wakizuru Anfield wakijivunia uongozi wa 3-1.

 

Categories
Michezo

David Alaba kugura Munich mwisho wa msimu huu

Beki wa Bayern Munich David Alaba ametangaza kuigura timu hiyo ifikiapo mwishoni mwa msimu huu kwa uhamisho usio wa malipo.

Alaba amabye amenyakua mataji 9 ya ligi kuu Ujerumani Bundesliga ,na mawili ya Champions League akiwa Allianz Arena amedokezwa kuhamia Real Madrid,Manchester City,Liverpool au Chelsea ingawa mwenyewe hajafichua atakakoelekea.

“Nimesalia na miaka 6 au 7 katika amali yangu ya soka ndio maana nataka kujaribu kitu kipya,sio siri wasimamizi wangu wanafanya mazungumzo na klabu kadhaa”akasema Alaba

Mwanandinga huyo aliye na umri wa miaka 28 kutoka Austria alinyakua mataji 6 ya kombe la Ujerumani,Mawili ya Supercup Ujerumani na mawili ya Uefa Supercup tangu ajiunge na Munich mwaka 2008 na hadi wa leo amepiga mechi 415 na pia mechi nyingine 76 kwa timu yake ya taifa.

Categories
Michezo

Bayern Munich watwaa kombe la dunia baada ya kuwazidia maarifa Tigres

Bayern Munich ndio mabingwa wa dunia baina ya vilabu baada ya kuwalemea Tigres UANL kutoka Mexico bao 1-0 katika mechi  fainali iliyosakatwa uwanjani Education City nchini Qatar.

Bao la pekee na la ushindi kwa Munch maarufu kama Bavarians lilipachikwa kimiani na Benjamin Pavard kunako dakika ya 59  .

Kombe hilo lililkuwa la 6 kwa Munich na la pili la dunia  na kusawazisha rekodi ya Pep Guardiola aliyetwaa mataji 6 na Baverians msimu wa mwaka 2009/2010.

Mabingwa wa Afrika Al Ahly walinyakua nishani ya shaba baada ya kuwalemea mabingwa wa Marekani Kusini Palmeiras kutoka Brazil mabao 3-2 kupitia mikiki ya penati kufuatia sare tasa dakika 90.

Categories
Michezo

Bayern Munich waanza msimu kwa makeke huku vigogo Madirid wakiduwazwa

Mabingwa watetezi wa ligi ya mabingwa barani ulaya Bayern Munich walitoa onyo kali walipowaadhibu Atletico Madrid  mabao 4-0 katika mechi ya kundi A iliyosakwa Jumatano usiku ugani Alienz Arena.

Kinsley Coman na Leon Goretzka waliwaweka wenyeji kifua mbele kufikia mwishoni mwa kipindi cha kwanza kabla ya kiungo Corentin Tolisco na Coman kuongeza mengina mawili katika kipindi cha pili.

Katika pambano jingine Real Madrid waliambulia kichapo cha mabao 3-2  nyumbani kutoka kwa Shaktar Donestk  ya Ukraine ambayo iliwajumuisha chupukizi 11 kuchukua nafasi za wachezaji wa kikosi cha kwanza waliotengwa baada ya kupatikana na homa ya Korona.

Nicolas Tagliafico alijifunga na kuwazadi Liverpool ushindi wa bao 1 -0 mjini Ajax wakati Intermilan wakihitaji bao la dakika za mwisho kutoka kwa mshambulizi Romelu Lukaku ili kulazimisha sare ya 2-2 dhidi ya Borusia Monchegladbach ya Ujerumani wakati Machester City ikiwaangusha Fc  Porto  ya Ureno  mabao 3-1.

Categories
Michezo

Mabingwa wa Ulaya Bayern Munich waduwazwa

Mabingwa watetezi wa ligi kuu nchini Ujerumani Bayern Munich  waligutushwa Jumapili jioni walipoambulia kichapo cha mabao 4-1 ugenini kwa Tsg Hoffenheim ,kikiwa kichapo cha kwanza kwa  meneja Hansi Flick.

Ermin Bicakcic alifungua  ukurasa wa mabao kwa wenyeji kunako dakika ya 16 kabla ya Mu’nas Dunbbar kuongeza la pili dakika 8 baadae.

Joshua Kimmich alikomboa bao moja kwa  Munich katika dakika ya 36 lakini  Andrej Kramaric  akapanua uongozi wa  Hoffenheim kwa bao la tatu dakika ya  77 na kuongeza la nne kupitia penati ya dakika ya mwisho.

Munich walionekana kupoteza pambano la Jumapili kutokana na uchovu baada ya kucheza hadi muda wa ziada kabla ya kuishinda Sevilla kupitia muda wa ziad na kushinda kombe la Eufa Super katikati ya wiki.

Tayari Munich walikuwa wamenyakua taji la  Bundesliga,kombe la Ujerumani,Ligi ya mabingwa Ulaya na Eufa Super Cup kabla ya kipigo cha Jumapili.

Categories
Michezo

Thiago Alcântara akubali kujiunga na Liverpool kwa pauni milioni 27 nukta 3

Kiungo wa Uhispania Thiago Alcantara ameafikiana kujiunga na mabingwa wa Uingereza Liverpool kwa ada ya pauni milioni 27 nukta 3 akitokea Bayern Munich .

Mspanyola huyo anatazamiwa kuandikisha kandarasi ya miaka minne .

Liverpool wamekuwa wakisitasita kumsajili Alcantara aliye na umri wa miaka 29 ,akiwa amesalia na mwaka mmoja katika mkataba wake na Munich  huku pia Manchester United ikiwinda huduma zake.

Yamkini Thiago amefurahia kujiunga na the reds ,licha ya tamaa ya Manchester United inayowinda huduma zake pia.

Thiago, ambaye ni mwanawe mshindi wa kombe la dunia Brazil mwaka 1994  Mazinho, alijiunga na Municha mwaka 2013 kutoka Bercelona na amesekata michuano   233 kwa mabingwa hao wa ujerumani.

Kakake mdogo , Rafinha, angali katika timu ya Bercelona.