Categories
Michezo

Mshambulizi wa Bandari Fc William Wadri aibuka mchezaji bora ligi kuu FKF

Mshambulizi  wa Bandari Fc William Wadri ametawazwa mchezaji bora katika ligi kuu ya Kenya FKF mwezi Februari .

Wadri, alikuwa nguzo muhimu na kuchangia timu yake kushinda mechi zote za mwezi Februari na amemshinda  Lawrence Juma wa Sofapaka,Jackson Macharia wa Tusker Fc na  Eric Gichimu kutoka Bidco United .

Wadri akiwa na kocha wake Andre Casa Mbungo

Wadri alikuwa katika ubora wake mwezi Februari akipachika mabao matatu na kuchangia jingine moja kwa timu yake ya Bandari .

Mshambulizi huyo amepokea  tuzo pamoja na shilingi elfu 50 ,na kuwa mwanandinga wa tatu kupokea tuzo hiyo ,baada ya  Elvis Rupia wa AFC Leopards  aliyebuka mshindi mwezi Disemba mwaka jana na Henry Meja wa Tusker FC aliyeshinda tuzo  hiyo mwezi Januari.

Categories
Michezo

Casa Mbungo wa Bandariu FC atawazwa kocha bora ligi kuu mwezi Februari

Kocha wa klabu ya Bandari FC Andre Casa Mbungo ndiye kocha bora wa ligi kuu FKFPL katika mwezi Februari katika tuzo za kila mwezi.

Mbungo aliongoza Bandari kushinda mechi nne mwezi Februari huku akimpiku Anthony Akhulia wa Bidco United.

Bandari walisajili ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Kariobangi Sharks katika mechi ya kwanza mwezi Februari, kabla ya kuwaumbua
AFC Leopards 2-1 na kuimenya Vihiga United mabao 5 kwa ombwe na kuwacharaza wanajeshi Ulinzi Stars 2-0 katika mechi ya kufunga mwezi.

Mbungo ndiye mshindi wa tatu wa tuzo hiyo baada ya Zedekiah Zico Otieono wa KCB na Francis Kimanzi wa Wazito FC walioshinda miezi ya Disemba na Januari mtawalia.

Mnyarwanda huyo amepokea tuzo na zawadi ya shilingi 50,000.

Categories
Michezo

Ingwe waikwaruza Homeboyz ligi kuu FKF

Miamba wa soka Kenya Afc Leopards walisajili ushindi wa pili mtawalia kwenye ligi kuu FKF chini ya kocha mpya Patrick Auseems kutoka Ubelgiji walipowaadhibu Kakamega Homeboyz magoli 2-1 katika pambano la Jumapili uwanjani Bukhungu ukiwa ushindi wa kwanza kwa Leopards katika uga huo.

Clyde Senaji aliwaweka wageni Ingwe uongozini kwa goli la kwanza dakika ya 10, kabla ya lvis Rupia kuongeza la pili huku wakiongoza 2-0 kufikia mapumzikoni.

Allan Wanga alifunga bao la kufuta machozi kwa wenyeji na mechi kumalizika kwa ushindi wa Leopards 2-1.

Katika michuano mingine Bandari Fc pia walizidisha makali yao kwa kuinyoa Ulinzi Stars mabao 2-0 katika uwanja wa Kericho Green,Sofapaka wakasajili ushindi wa mabao 2-1 ugenini kwa Posta Rangers nao Kariobangi Sharks wakawafilisi KCB kwa kuwazabua mabao 3-0.

Tusker Fc waliolimwa na Bidco United Jumamosi wangali kushikilia kukutu uongozi wa ligi hiyo kw alama 32 baada ya mechi 14,wakifuatwa na KCB kwa pointi 26,pointi moja zaidi Bandari Fc iliyo ya tatu na AFC Leopards katika nafasi ya 4 wakati Kariobangi Sharks wakihitimisha tano boar kwa alama 24.

Categories
Michezo

Casa Mbungo atua Bandarini kupiga ukufunzi kwa miaka miwili

Andre Cassa Mbungo ameteuliwa  kuwa kocha mpya wa kilabu cha Bandari FC chenye makaoa yake pwani ya Kenya kwa kandarasi ya miaka miwili .

Mnyarwanda huyo  mwenye umri wa miaka 51 na ambaye msimu jana aliifunza  AFC Leopards atasaidiwa  na aliyekuwa kocha msaidizi wa  Gor Mahia Patrick Odhiambo katika majukumu yake mapya.

Kibarua cha kwanza cha Mbungo kitakuwa kuiongoza Bandari dhidi ya washindi mara 11 wa ligi kuu  humu nchini Tusker Fc katika pambano la ligi kuu FKF.

Kocha huyo amesema lengo lake Bandarini ni kunyakua mataji .

 

CEO wa Bandari   Edward Oduor

Mabingwa watetezi wa ligi Gor Mahia pia wamekuwa wakinyemelea huduma za kocha huyo lakini mwenyewe akaamua kutua Bandari

“Ulikuwa uamuzu rahisi kwangu baada ya Bandari kunionyesha kuwa wanahitaji huduma zangu na niwapa kipa umbele badala ya Gor Mahia”akasema Mbungo

Bandari  inashikilia nafasi ya sita ligini kwa alama nane baada ya kucheza mechi sita.

Baada ya kuigura Ingwe mwaka 2019 Mbungo alirejea nyumbani Rwanda na kuifunza  Gasogi United kabla ya kuhamia Rayon Sports .

Mbungo aliigura Ingwe Disemba mwaka 2019 kwa kutolipwa mshahara wake.