Categories
Kimataifa

Marekani yatilia shaka matokeo ya uchaguzi nchini Guinea

Marekani imeibua wasiwasi kuhusiana na kutofautiana kwa matokeo ya awali ya uchaguzi wa urais nchini Guinea.

Kwenye taarifa ubalozi wa marekani umesema hakuna uwazi katika ujumlishaji wa kura na pia tofauti katika matokeo yanayotangazwa na yale ya  hati zinazowasilishwa kutoka kwa vituo vya kupigia kura.

Kiongozi wa Guinea mwenye umri wa miaka  82 Alpha Condé alishinda kipindi cha tatu uongozini kwa njia tata kulingana na matokeo ya awali huku maandamano yakizuka kote nchini humo.

Marekani imehimiza pande zote kusuluhisha kwa amani mizozo ya kiuchaguzi kupitia taasisi husika.

Marekani ilisema  imeunga mkono juhudi za kidiplomasia zinazotekelezwa na jumuia ya Ecowas,muungano wa Afrika pamoja na umoja wa mataifa wa kurejesha amani katika taifa hilo.

Kinara mkuu wa upinzani Cellou Dalein Diallo alijitangaza kuwa mshindi kwenye uchaguzi huo na alizuiwa kuondoka kwenye nyumba yake hadi Jumatano wakati ambapo alisema maafisa wa usalama waliokuwa nje ya nyumba yake waliondolewa.

Categories
Kimataifa

Wananchi wa Guinea wapiga kura kumchagua rais

Raia wa Guinea wanapiga kura kwenye uchaguzi wa urais leo huku Rais Alpha Condé mwenye umri wa miaka 82 akitaka awamu ya tatu.

Muda wa kampeni ulikamilika Ijumaa usiku wa manane katika nchi hiyo huku kukiwa na wasi wasi wa kuzuka kwa vita baada ya kundi la watu wasiojulikana kuvamia kambi ya kijeshi nchini humo na kumwua kwa kumpiga risasi afisa mkuu wa kijeshi.

Rais Condé alishinikiza kupitishwa kwa katiba mpya mwezi Machi akisema katiba hiyo itaboresha nchi hiyo, hatua ambayo pia ilimwezesha kukwepa sharti la rais kuhudumu kwa hatamu mbili.

Baada ya kuwa mwanaharakati wa upinzani kwa miongo kadhaa , Condé aliibuka kuwa rais wa kwanza  Guinea kuchaguliwa kwa njia ya kidemokrasia mwaka 2010 na akashinda uchaguzi mwingine ulioandaliwa mwaka  2015.

Makundi ya kutetea haki za binadamu yamekuwa yakimkosoa rais huyo huku wakimtuhumu kwa kuwa dikteta.

Condé anakabiliana na mpinzani wake wa muda mrefu Cellou Dalein Diallo, ambaye tayari amemshinda katika chaguzi mbili.

Diallo, mwenye umri wa miaka 68, ambaye sasa ndiye kiongozi wa upinzani nchini  Guinea alikuwa waziri mkuu chini ya aliyekuwa kiongozi wa nchi hiyo Lansana Conté.

Takriban wapiga kura mlioni 5.4 wanashiriki katika zoezi hilo huku matokeo yakitarajiwa kutangazwa baada ya siku chache.

Ili kushinda urais moja kwa moja, mgombea anatakiwa kupata zaidi ya nusu ya kura hizo, vyenginevyo kutakuwa na awamu ya pili ya kura ya urais mnamo tarehe 24 Nonvemba mwaka huu.

Categories
Kimataifa

Mauaji ya afisa mkuu wa kijeshi yazua taharuki nchini Guinea

Taharuki imetanda nchini Guinea, kufuatia mauaji ya afisa mkuu wa kijeshi Kanali mamady Conde.

Mauaji haya yanajiri siku mbili kabla ya uchaguzi wa urais ambapo rais Alpha Conde anawania muhula tata wa tatu.

Watu waliokuwa na bunduki walimuuwa kwa kumpiga risasi kanali Conde mapema leo katika kambi ya kijeshi huko Kindia, kilomita 130 kaskazini mashariki mwa mji mkuu wa Conakry.

Wakazi wa mtaa ulioko karibu walisikia milio ya risasi mwendo wa saa nane usiku na kasha ufyatulianaji mkali wa risasi ukaendelea kwa saa tano.

Kulikuwa na habari kuhusu jaribio la maasi ya kijeshi na kwamba wanajeshi walikuwa wamechukua silaha ili kuwaokoa baadhi ya wenzao ambao wanazuiliwa.

Hali hiyo sasa imedhibitiwa na msako umeanza wa wanajeshi husika.