Nahodha wa timu ya taifa ya Tanzania Ali Mbwana Samatta alifunga bao lake la tatu katika klabu ya Ferbahce ya Uturuki msimu huu huku akichangia ushindi wa magoli 3-1 nyumbani dhidi ya Ankaragucu Jumatatu usiku.
Sammata alipachika bao hilo kunako dakika ya 34 ya mchezo alipopokea pasi katika eneo la D na kumhadaa kipa .
Likuwa bao la tatu msimu huu kwa Samatta msimu huu ,huku ushindi huo ukiichupisha Fernabahce hadi nafasi ya pili kwenye jedwali kwa alama 38 sawa na Besiktas.
Mshambulizi huyo alijiunga na Ferbahce Septemba mwaka jana kwa mkataba wa miaka minne akitokea Aston Villa kwa kima cha Euro miloni 6 na awali alikuwa na Racing Genk ya Ubelgiji alikosakata mechi 121 na kupachika mabao 76 huku akichangia mengine 20.