Categories
Michezo

Olunga apiga dakika 46 huku ndoto yake ya kucheza na Bayern Munich ikizimwa na Al Ahly

Mshambulizi wa Harambee Stars Michael Olunga alicheza dakika 46 kabla ya kuondolewa uwanjani katika ushinde wa timu yake  ya Al Duhail Sc wa bao  1 na mabingwa wa Afrika Al Ahly katika kwota fainali ya kombe la dunia baina ya vilabu  katika uwanja wa Education City Stadium mjini  Al Rayyan nchini Qatar Alhamisi usiku.

Ilikuwa mechi ya kwanza kwa Olunga kucheza katika fainali hizo za kombe la dunia akiwakilisha mabingwa hao watetezi wa ligi kuu nchini Qatar tangu ajiunge  nao mwezi uliopita kutoka kashiwa Reysol ya Japan.

Tobwe la Hussein El Shahat kunako dakika ya 30 liliotosha kuwapa Ahly maarufu Red Devils kutoka Misri ushindi huo ambao uliwafuzisha kwa nusu fainali watakapochuana na mabingwa wa ulaya Bayern Munich Februari 8 wakilenga kuwa timu ya pili ya Afrika kucheza fainali ya kombe hilo baada ya TP Mazembe ya Jamhuri ya demokrasia ya Congo.

Katika mechi nyingi ya robo fainali mabingwa wa Marekani Kaskazini  Tigres UNL ya Mexico waliibandua Ulsan Hyundai ya Korea Kusini mabao 2-1 na kufuzu kwa nusu fainali kuchuana na mabingwa wa Amerika Kusini  Palmeiras ya Brazil .

Al Duhail watarejea uwanjani dhidi ya mabingwa wa Asia Ulsan kuwania nafasi ya 5 na 6 tarehe 7 kabla ya fainali ya tarehe  11 mwezi huu.

Mashindano hayo hushirikisha  mabingwa wa kila bara na huandaliwa kila mwaka .

 

Categories
Michezo

Olunga alenga kuandikisha historia kucheza FIFA World Cup

Mshambulizi  wa Harambee Stars Michale Olunga anatarajiwa kuingia kwenye madaftari ya kumbukumbu kuwa Mkenya wa kwanza kucheza mashindano ya kombe la dunia baina ya vilabu yatakayoanza  Alhamisi hii nchini Qatar.

Olunga aliye na umri wa miaka 26 amejumuishwa kwenye kikosi cha klabu ya Al Duhail Sc  huku wakicheza mchuano wa ufunguzi Alhamisi Februari 4 dhidi ya mabingwa wa Afrika Al Ahly kutoka Misri.

Awali Mc Donald Mariga alikuwa kwenye kikosi cha Inter Milan ya Italia kilichonyakua kombe la dunia mwaka 2010 katika muungano wa Milki za kiarabu.

Olunga ambaye aliibuka mfungaji na mchezaji bora katika ligi kuu ya Japan mwaka jana akiwa na klabu ya Kashiwa Reysol alijiunga na mabingwa hao wa Qatar kwa kima cha shilingi milioni 933 ambapo anakisiwa kulipwa mara dufu ya mshahara aliokuwa akilipwa akiwa Japan .

Mshambulizi huyo wa Kenya anatarajiwa kuichezea Al Duhail katika mechi ya robo fainali ya kombe la dunia Alhamisi dhidi ya mabingwa mara 9 wa Afrika Al Ahly baada ya kujumuishwa kwenye kikosi cha wanandinga 23 wa mabingwa hao watetezi wa ligi kuu Qatar zamani wakifahamika kama Lakhwiya.

Katika mechi nyingine ya robo fainali ya Alhamisi mabingwa wa Marekani kaskazini Tigres UNL  ya Mexico itapambana na mabingwa wa bara Asia Ulsan Hyundai.

Mashindano ya kombe la dunia kati ya vilabu yanajumuisha mabingwa wa kila bara ,Ulaya ikiwakilishwa na Bayern munich na Palmeiras wakiwakilisha Marekani Kusini  huku fainali yake ikisakatwa Februari 11.

 

 

 

Categories
Michezo

Olunga afungua akaunti za magoli Qatar kwa Hatrick

Mshambulizi wa Harambee Stars Michael Olunga alifungua ukurasa wa kupachika mabao katika klabu yake mpya ya Al Duhail Sc   Jumatatu usiku nchini Qatar alipopiga magoli matatu na kuipa timu yake ushindi wa mabao 6-0  na kufuzu kwa kwota fainali ya kombe la Amir.

Olunga aliyejiunga  na klabu hiyo mapem mwezi akitokea Kashiwa Reysol ya Japan alipachika mabao 2 kunako kipindi cha kwanza ,dakika ya 6 kupitia mkwaju wa penati  baada ya mshambulizi Dudu kutoka Brazil kuangushwa katika eneo la hatari.

Edmilson alimpokeza Olunga pasi ya dakika ya 43  akiunganisha kwa kichwa mkwaju wa kona na kupiga goli la 2 .

Olunga alipachika goli la tatu dakika  ya  69  huku timu yake ikisajili ushindi wa jumla wa mabao 37-7 katika mechi hiyo ya mikondo miwili na kufuzu wka robo fainali.

Mshambulizi huyo aliibuka mfungaji bora katika ligi kuu ya Japan msimu jana pamoja na kutawazwa mchezaji bora kabla ya kuhamia Qatar anakolipwa msahara mara dufu.