Categories
Michezo

Gambia yawagutusha Ghana huku Tanzania wakitimuliwa AFCON U 20

Gambia ilitoka nyuma na kuwabwaga Ghana magoli 2-1 katika mchuano wa kundi C uliosakatwa Jumatatu usiku nchini Mauritania.
Abdul Fatawualikuwa ameiweka Ghana uongozini baada ya dakika 8 za mchezo ,kabla ya Kajally Drammeh na Lamarana Jallow kuwafungia Young Scorpions magoli 2 na kuwaweka Limbukeni Gambia uongozini kufikia mapumzikoni .

Licha ya kupewa kadi nyekundu Gambia walijizatiti na kutwaa ushindi huo mhimu uliowafuzisha kwa robo fainali wakimaliza wa pili kwa alama 4.

Katika mechi nyingine Moroko waliikomoa Tanzania mabao 3-0 na kuongoza kundi hilo la C El Mehdi El Moubarik, Mohammed Amine Essahel na Ayoub Mouloua wakipachika magoli ya Moroko katika kipindi cha kwanza na kuongoza kundi kwa pointi 7.

Categories
Michezo

Burkina Faso na Tunisia wasajili ushindi AFCON U 20

Timu za Burkina Faso na Tunisia zilisajili ushindi wa kwanza  katika kundi B  katika mashindano ya kuwnaia kombe la Afrika kwa chipukizi walio chini ya umri wa miaka 20 yanayoendelea nchini Mauritania.

Tunisia walisajili ushindi wa mabao 2-0  dhidi ya Namibia katika mechi ya kwanza uwanjani Cheikh Ould Boidiya   mjini Nouakchott Mauritania na kuweka hai matumaini ya kufuzu hatua ya mwondoano  .

Marc Martin Lamti na Hassan Ayari walipachika mabao yote moja kila kipindi  na kuiweka Tunisia katika nafasi nzuri ya kutinga robo fainali  wakiwa wamezoa pointi 4 kutokan an mechi 2 nao Namibia wananing’inia kubanduliwa wakiwa na alama 1.

Katika mkwangurano mwingine  wa pili kundini B ,Burkina Faso walitoka nyuma na kulazimisha ushindi wa magoli 3-1 dhidi ya Jamhuri ya Afrika ya Kati .

Isaac Ngoma aliwaweka Afrika ya kati uongozini kufutia kosa la  dakika ya 32 ,lakini Burkina Faso wakarejea mchezoni kwa goli la dakika ya 2 ya ziada ya Joefrey  Bazie na timu zote kwenda mapumzikoni wakiwa sara ya 1-1.

Eric Chardey aliongeza bao la pili kwa  Burkina Faso dakika ya 52  naye Pindwinde Beleme  akakongomelea msumari wa mwisho kwa jahazi la Afrika ya Kati kwa goli la 3.

Burkina Faso wamezoa pointi 4 baad ya mechi 2  sawa na Tunisia huku Afrika ya kati na Namibia wakiwa na alama 1 kila moja.

Kipute hicho kuendelea Ijumaa jioni kwa mechi za kundi C ,Tanzania waliopoteza mechi ya kwanza wakikabiliana na Gambia saa moja usiku ,kabla ya Ghana kumaliza udhia na Moroko saa nne usiku.

Categories
Michezo

Tanzania yapigwa kumbo huku Moroko walilazimisha ushindi AFCON U 20

Timu ya Ghana kwa wanaume wasiozidi umri wa miaka 20 illinyuka Tanzania maarufu kama ngorongoro Heroes  mabao 4-0 katika mkwangurano wa kundi C kuwania kombe la AFCON kwa chipukizi wasiozidi umri wa miaka 20 mjini Noukchot nchini Mauritania Jumanne usiku.

Precious Boah alipachika mabao mawili kwa Ghana maarufu kama  Black Satellites  ,kabla ya Abdul Fatawu na Joselpho Barnes  kuongeza mengine mawili.

Katika pambano jingine  Moroko walihitaji penati tatanishi kunako kipindi cha kwanza ili kuwashinda Gambia bao 1-0 .

Mashindano hayo kuendelea Jumatano kwa mechi mbili za kundi A  Cameroon na Uganda wakimenyana katika mechi ya kwanza saa moja usiku huku atakayeshinda akifuzu kwa kwota fainali na pia sare itatosha kuvusha timu zote mbili kwa robo fainali baada ya kushinda mechi zao za ufunguzi.

Katika mechi ya pili kundini humo Msumbiji watachuana na wenyeji Mauritania saa nne usiku huku atakayeshindwa akiyaaga mashindano ,hususan baada ya wote wawili kupoteza mechi za ufunguzi.

 

 

 

 

 

Categories
Michezo

Limbukeni Afrika ya kati na Namibia watoshana nguvu

Namibia na Jamhuri ya  Afrika ya kati zilitoka sare ya bao 1 katika mchuano wa mwisho wa kundi B  wa mashindano ya kombe la AFCON kwa chipukizi wasiozidi umri wa miaka 20 , uliopigwa katika uwanja wa Cheikha Boudiya Noukchot  nchini Mauritania.

Flory Jean Michael Yangao aliiweka Afrika ya kati  dakika 8 baada ya mapumziko kabla ya  Penuua Kandjii  kusawazisha kwa Namibia  mwishoni mwa mechi na kusajili sare ya pili katika kundi hilo ,baada ya Tunisia na Burkina Faso kucheza sare tasa.

Mashindano hayo kuingia siku ya tatu Jumanne  kwa mikwangurano ya kundi C  ,mabingwa mara tatu Ghana watafungua dimba saa moja usiku dhidi Tanzania wanaoshiriki kwa mara ya kwanza nao Gambia wakumbane na Moroko saa nne usiku.

Mataifa 12 yanashiriki mashindano hayo .

 

Categories
Michezo

Uganda yaipakata Msumbiji AFCON U 20

Timu ya Uganda maarufu kama Hippos imeanza vyema mechi za kundi A katika mashindano ya kuwania kombe la AFCON kwa chipukizi walio chini ya umri wa miaka 20 baada ya kuwacharaza Msumbiji mabao 2-0 katika mechi iliyochezwa Jumatatu alasiri nchini Mauritania .

Mshambulizi wa klabu ya Police Derrick Kakooza alipachika bao la kwanza dakika ya 57 kupitia penati kabla ya kiungo wa KCCA Steven Serrwada dakika 4 kabla ya kipenga cha mwisho huku ushindi huo ukiwaweka katika nafais nzuri ya kutinga robo fainali wakiongoza kundi hilo kwa alama 3 sawa na Cameroon kuelekea kwa mechi kati ya timu hizo mbili Jumatano hiii.

Mashindano hayo yanashirikisha mataifa 12 huku fainali yake ikipigwa tarehe 6 mwezi ujao.

 

Categories
Michezo

Wenyeji Mauritania waadhibiwa na Cameroon AFCON U 20

Wenyeji Mauritania waliishia kujutia kosa moja lililofanywa mwishoni mwa kipindi cha pili na kaumbulia kichapo cha bao 1-0 dhidi ya Cameroon katika mechi ya ufunguzi kuwania kombe la AFCON kwa chipukizi wasiozidi umri wa miaka 20 katika uwanja wa Olimpiki mjini   Nouakchott Jumapili usiku.

Junior Sunday Jang  aliwafungia Cameroon bao la pekee na la ushindi katika   dakika ya 81  akitumia makosa ya mlinzi wa Mauritania aliyepiga pasi kwa kipa wake lakini ikawa fupi na kutwaliwa na mshambulizi huyo aliyepachika bao .

Mauritania wanaoshiriki kwa mara ya w kwanza walidhihirisha mchezo wa hali ya juu huku wakikosa nafasi za wazi za kupitia kwa Oumar Mbareck na  Adama Diop .

Pasi ya difenda Alioum Moubarak wa Mauritania kwa kipa wake ikikatwa na  Sunday Junior  aliyeipa Cameroon inayoshiriki michuano hiyo kwa mara ya 10 ushindi huo muhimu.

Cameroon watarejea uwanjani tarehe 17 dhidi ya Uganda wakati Mauritania wakichuana na Msumbiji.

Mashindano hayo yanayoshirikisha mataifa 12 yataingia siku ya pili Jumatatu kwa jumla ya mikwangurano  mitatu,Uganda wakifungau kazi dhidi ya Musmbiji kuanzia saa kumi alasiri katika kundi A ,kabla ya Burkina Faso kukabiliana na Tunisia saa moja usiku kundini B nao  Namibia wamenyane na Jamhuri ya Afrika ya kati.

Categories
Michezo

Dimba la AFCON kwa chipukizi chini ya miaka 20 kuanza Jumapili Mauritania

Makala ya 16 ya michuano ya AFCON kwa vijana walio chini ya umri wa miaka 20 yataanza kutimua vumbi nchini Mauritania Jumapili usiku kwa mkwangurano wa ufunguzi wa kundi A baina ya wenyeji dhidi ya Cameroon kuanzia saa tano katika kundi A  .

Uganda watashuka uwanjani  Jumatatu kuwajulia hali  Msumbiji katika pambano la kundi A ,kabla ya Burkina Faso kufungua ratiba ya kundi B pia Jumatatu dhidi ya Tunisia nao Namibia wakwangurane na Jamhuri ya Afrika ya kati.

Mabingwa mara tatu Ghana ndio walioshiriki kipute hicho mara nyingi ikiwa mara 12 wakifuatwa na Cameroon  ambao ni mabingwa wa mwaka 1995 walioshiriki mara 10  ,nao  Moroko wanashiriki kwa mara ya 5 huku Burkina Faso ikishiriki kwa mara ya 4.

Hata hivyo mataifa 7 yanashiriki michuano hiyo mwaka huu kwa mara ya kwanza yakiwa:wenyeji Mauritania,Tanzania,Uganda,Namibia,Msumbiji,Jamhuri ya Afrika ya kati na Tunisia .

Mashindano hayo yatakayokamilika tarehe 6 mwezi ujao yanashirikisha mataifa 12  huku Afrika Mashariki ikiwakilishwa na Uganda na Tanzania waliofuzu kupitia michuano ya CECAFA mwaka uliopita nchini Tanzania.

Mali ambao hawakufuzu kwa mashindano ya mwaka huu walinyakua kombe hilo katika makala ya mwaka 2019 walipoishinda Senegal penati 3-2 kufuatia sare ya bao 1-1 katika dakika 120 .

Michuano yote ya kipute hicho itarushwa mbashara kupitia KBC Channel one .

 

Categories
Michezo

Viboko wa Uganda waitafuna Tanzania na kunyakua kombe la CECAFA 2020

Timu ya Uganda kwa Chipukizi walio chini ya umri wa miaka 20 maarufu kama Hippos ,ndio mabingwa wa mwaka huu wa kombe la Cecafa  baada ya kuwadhalilisha wenyeji Tanzania mabao 4-1 katika fainali iliyosakatwa Jumatano jioni katika uwanja wa Black Rhino Academy eneo la Karatu mjini Arusha Tanzania.

Richard Basangwa, Steven Sserwadda,  Ivan Bogere na  Kenneth Semakula waliiwajibikia Uganda kwa bao moja kila mmoja ,huku Abdul Suleiman akifunga bao la maliwazo kwa Ngorongoro Heroes kupitia penati.

Viboko hao wa Uganda wangeongoza mabao 3-1 kufikai mapumziko lakini mshmabulizi mwiba Ivan Bogere  akapaishia penati ya dakika ya 45 .

Ilikuwa  mechi ya kulipiza baada ya Tanzania kunyakua kombe la Cecafa mwaka jana ,michuano hiyo ilipoandaliwa nchini Uganda.

Hata Hivyo  timu zote mbili za Uganda na Tanzania zimejikatia tiketi kucheza fainali za Afcon mwaka ujao nchini Mauritania katika mala ya 15.

Kuelekea fainali Uganda iliikomoa Kenya mabao 3-1 katika semi fainali wakati Tanzania wakiwaadhibu Sudan Kusini magoli 2-1 pia katika nusu fainali.

Iilikuwa kombe la 4 la Cecafa kwa uganda tangu mashindano hayo yatangulizwe mwaka 1971,wakiibuka mabingwa miaka ya 1973,2006,2010 na 2020 na kuwa taifa lenye ufanisi mkubwa katika michuano hiyo.

Uganda pia kwa mara ya kwanza wanashikilia vyokombe vyote vya Cecafa kwa wakati mmoja vikiwa nia:-Cecafa kwa wavulana wasiozidi umri wa miaka 15 ,Wasichana walio chini ya umri wa miaka 17,Wavulana walio chuini ya miaka 17 ,wanaume walio chini ya umri wa miaka 20,kombe la Cecafa Kagame linaloshikiliwa na KCCA na kombe la Cecafa senior challenge cup wanaloshikilia Ugand Cranes.

 

 

 

 

Categories
Michezo

Viboko wa Uganda kukabiliana na Ngorongoro Heroes ya Tanzania fainali ya CECAFA

Fainali ya kuwania  kombe la Cecafa kwa vijana  chipukizi wasiozidi umri wa miaka 20 itapigwa Jumatano  alasiri baina ya mabingwa watetezi Tanzania dhidi ya Uganda katika uwanja wa Black Rhino Academy eneo la Karatu mjini Arusha Tanzania.

Wenyeji Tanzania maarufu kama Ngorongoro Heroes  walianza safari ya michuano  hiyo katika kundi A  kwa kuipakata  Djibouti magoli 6-1 ,kabla ya kuimenya Somalia mabao 8-1 katika pambano la mwisho na hatimaye  kuibandua Sudan Kusini bao 1-0 kwenye nusu fainali.

Upande mwingine  Viboko wa Uganda au Hippos walianza kundi B kwa kutoka sare tasa dhidi ya Sudan Kusini kabla ya kuigaragaza  Burundi mabao 6-1 katika mechi ya mwisho na kuitema kenya mabao 3-1 kwenye nusu fainali.

Uganda na Tanzania tayari zimejikatia tiketi kupiga fainali za 15 za kuwania kombe la Afcon mwaka ujao nchini Mauritania kwa kufika fainali.

Tanzania wakipiga fainali ya mwaka jana dhidi ya Kenya

Fainali ya Jumatano  itashuhudia Tanzania wakilenga kuhifadhi ubingwa wa mwaka uliopita wakati Waganda pia wakipania kulipiza kisasi kwa kukosa kunyakua kombe hilo wakiwa nyumbani mwaka uliopita.

Kenya na Sudan Kusini zitamenyana kuanzia saa sita adhuhuri katika mechi ya kuwania nafasi ya tatu na nne katika uwanja wa Black Rhino Academy eneo la Karatu mjini Arusha.

 

 

Categories
Michezo

Kenya kupambana na Uganda nusu fainali ya CECAFA Jumatatu

Chipukizi wa Kenya walio chini ya umri wa miaka 20 watashuka uwanjani Black Rhino Academy sports Complex Jumatatu Novemba 30  kuanzia saa sita adhuhuri kupambana na majirani Uganda katika nusu fainali ya kwanza ya michuano ya kombe la Cecafa mjini Arusha Tanzania.

Kenya ijulikanayo kama Rising Stars iliongoaza kundi  C kwa alama 6 baada ya kuwalemea  Ethiopia mabao 3-0 katika mechi ya  kwanza kabla ya kuilaza Sudan mabao 2-1 katika mechi ya mwisho .

KENYA RISING STARS

Kwa upande wao Uganda waliongoza pia kundi B kwa pointi 4 baada ya  kwenda sara tasa dhidi ya Sudan Kusini, kabla ya kuiparamia Burundi mabao  6-1 katika mechi ya mwisho .

Nusu fainali ya mwisho itang’oa nanga mida ya saa tisa unusu katika uwanja uo huo kati ya mabingwa watetezi na wenyeji Tanzania dhidi ya Sudan Kuisini.

UGANDA HIPPOS

Tanzania maarufu kama Ngorongoro Heroes walianza kwa ushindi wa mabao 6-1 dhidi ya Djibouti katika mechi ya ufunguzi ya kundi A ,kabla ya kuisasambua Somalia mabao 8-1 katika mechi ya pili na kuongoza kundi kwa alama 6.

TANZANIA NGORONGORO HEROES

Sudan Kusini nao waliibuka wa pili kundi B kwa alama 4 wakienda sare kapa dhidi ya Uganda na kuipiku Burundi magoli 4-0 katika mechi ya mwisho.

Washindi wa nusu fainali za Jumatatu watafuzu kushiriki mashindano ya kombe la Afcon mwaka ujao nchini Mauritania pamoja na kumenyana kwenye fainali ya Disemba 2 kubaini mabingwa.

SOUTH SUDAN

Tanzania walitwaa kombe hilo mwaka jana nchini Uganda baad ya kuipiga Kenya fainalini.