Categories
Michezo

Yanga yamnyatia kocha Auseems wa Leopards

Miamba wa soka nchini Tanzania  Young Africans   maarufu kama  vijana wa Jangwani  wameanza kumnyemelea  kocha  wa AFC Leopards Patrick Aussems .
Auseems ambaye ni raia wa Ubelgiji angali na kandarasi ya miezi 6 na Leopards  huku ikiyakinika kuwa Yanga wako tayari  kufanya kila juhudi kumsajili  kocha huyo  kutwaa mikoba ya Mrundi Cedric Kae aliyepigwa kalamu Jumapili iliyopita kwa matokeo mabovu.
Endapo ataondoka Ingwe itakuwa mara ya pili kwa Auseems kurejea  Tanzania baada ya awali kuwa na timu ya Simba SC mwaka 2018 hadi 2019.
Yanga ingali kuongoza ligi kuu Tanzania bara kwa  pointi 50 kutoka na michuano 23,pointi tano zaidi ya watani wao Simba SC lakini matokeo yao yamedorora wakiwa wameshinda pambano moja pekee kati ya tano za mwisho.

 

Categories
Michezo

Ingwe waikwaruza Homeboyz ligi kuu FKF

Miamba wa soka Kenya Afc Leopards walisajili ushindi wa pili mtawalia kwenye ligi kuu FKF chini ya kocha mpya Patrick Auseems kutoka Ubelgiji walipowaadhibu Kakamega Homeboyz magoli 2-1 katika pambano la Jumapili uwanjani Bukhungu ukiwa ushindi wa kwanza kwa Leopards katika uga huo.

Clyde Senaji aliwaweka wageni Ingwe uongozini kwa goli la kwanza dakika ya 10, kabla ya lvis Rupia kuongeza la pili huku wakiongoza 2-0 kufikia mapumzikoni.

Allan Wanga alifunga bao la kufuta machozi kwa wenyeji na mechi kumalizika kwa ushindi wa Leopards 2-1.

Katika michuano mingine Bandari Fc pia walizidisha makali yao kwa kuinyoa Ulinzi Stars mabao 2-0 katika uwanja wa Kericho Green,Sofapaka wakasajili ushindi wa mabao 2-1 ugenini kwa Posta Rangers nao Kariobangi Sharks wakawafilisi KCB kwa kuwazabua mabao 3-0.

Tusker Fc waliolimwa na Bidco United Jumamosi wangali kushikilia kukutu uongozi wa ligi hiyo kw alama 32 baada ya mechi 14,wakifuatwa na KCB kwa pointi 26,pointi moja zaidi Bandari Fc iliyo ya tatu na AFC Leopards katika nafasi ya 4 wakati Kariobangi Sharks wakihitimisha tano boar kwa alama 24.

Categories
Michezo

Rupia aubuka mchezaji bora ligi kuu FKF Disemba

Mshambulizi wa AFC Leopards  Elvis Rupia ametawazwa mwanasoka bora kwenye ligi kuu ya  FKF Kenya mwezi Disemba mwaka jana .

Rupia aliwapiku kipa wa KCB Joseph Okoth na mshambulizi wa Kariobangi Sharks  Eric Kapaito  na kuwa mshindi wa kwanza wa tuzo hiyo inayoandamana na shilingi 50,000.

Mshambulizi huyo alikuwa na msimu bomba akipachika wavuni maboa 6 katika mechi 4 za ufunguzi kufikia Disemba akifunga bao moja katika ushindi wa Leopards wa   mabao 2-1 dhidi ya  Tusker FC,na kufunga mengine mawili dhidi ya Bidco United kabla ya kufunga magoli 3 dhidi ya Sofapaka .

Tuzo hiyo itakuwa ikitolewa kila mwezi ikiwashirikisha kocha na mchezaji bora.

Categories
Michezo

Kocha Auseems ahudhuria mazoezi ya kwanza ya Ingwe

Kocha mpya wa AFC Leopards Patrick Auseems alihudhuria mazoezi ya  kwanza  ya timu hiyo Jumanne asubuhi saa chache baada ya kusaini mkataba wa kuifunza timu hiyo .

Mbelgiji huyo ambaye zamani alitwaa ubingwa wa ligi kuu  Tanzania akiwa  na  Simba SC  msimu wa mwaka 2018/2019  na  kufikia robo fainali ya ligi ya mabingwa Afrika ,ana leseni ya  EUFA PRO na anatwaa mikoba  ya ukufunzi kutoka kwa  Antony Kimani.

Kocha huyo aliye na umri wa miaka 55 pia amewahizifunza timu za Al Hilal ya Sudan akishinda kombe la Super na kunyakua ligi kuu nchini Congo na AC Leopards mwaka 2014 na amefanya ukufunzi kwa miaka 30 barani ualaua na Afrika.

Kocha Patrick Auseems akiongoza mazoezi ya AFC Leopards

Kibarua cha kwanza kwa kocha huyo akiwa usukani ni mechi ya raundi ya 64 bora kuwania kombe la FKF Jumapili ijayo mjini Wundanyi dhidi ya Taita Taveta Stars.

Auseems alikuwa difenda wa zamani wa klabu cha Stadard Liege nchini Ubelgiji.

 

Categories
Michezo

Mashemeji waogopana ligi kuu FKF

Derby iliyokuwa ikisubiriwa kwa hamu na ghamu baina ya  AFC Leopards na Gor Mahia haikuwa na chochote muhimu baada ya timu zote kutoka sare tasa katika pambano la ligi kuu Jumapili alasiri katika uwanja wa Kasarani.

Leopards watajilaumu baada ya kukosa nafasi chungu nzima za kupachika magoli hususan kipindi cha kwanza wakati Kogalo wakicheza kwa tahadhari kuu na kupata pointi hiyo muhimu.

Leopards walikuwa wakisaka ushindi wa kwanza dhidi ya Gor kwenye ligi kuu tangu mwaka 2016 lakini watalazimika kusubiri zaidi.

Pointi hiyo moja inawaweka  Leopards katika nafasi ya 4 kwa alama 19  nao Gor Mahia  wakiwa katika nafasi ya 6 kwa alama 16 kutokana na mechi 9.

Katika mchuano mwingine wa Jumapili Bidco United ilisajili ushindi wa 2-0 dhidi ya Zoo Fc.

Categories
Michezo

Mashemeji Derby Kasarani bila mashabiki Jumapili

Mabingwa watetezi wa ligi kuu ya Kenya Gor Mahia watashuka uwanjani Kasarani Jumapili  Februari 7  kwa mechi ya ligi kuu maarufu kama Mashemeji Derby huku kwa mara ya kwanza mechi ya hiyo ya ubabe na utani mkubwa ikichezwa bila mashabiki uwanjani kutoka na ugonjwa wa Covid 19.

Timu zote zililkuwa zimeiomba wizara ya afya  kuruhusu angaa mashabiki 5,000 ombi lililokataliwa na  kuwalazimu mashabiki kusalia nyumbani wakati wa mchuano huo siku ya  Jumapili .

Katibu mkuu wa Gor Mahia Sam Ochola amesema wamejiandaa vyema huku wakilenga kuzoa alama zote tatu ili kuwakaribia Leopards kwenye jedwali.

“Kikosi chetu kiko  sawa tunatafuta pointi zote tatu ili tuwakaribie Leopards”akasema Ochola

Kwa upande wake mwenyekiti wa Leopards Dan Shikanda ana imani ya kusajili matokeo bora mchuano huo huku akilalama kuhusu kufungiwa nje kwa mashabiki.

“Tulitarajia kuwa by the time tunacheza hii mechi serikali itaruhusu mashabiki lakini kwa sasa tutacheza tu bila mashabiki lakini tunalenga kupata matokeo mazuri”akasema Shikanda

Leopards ni ya 4 ligini kwa pointi 18 wakati Gor Mahia ikishikilia nafasi ya 6 kwa alama 15.

Categories
Michezo

Ingwe yaichuna Sharks huku KCB wakiwazima Western Stima

AFC Leopards waliwakwaruza Kariobangi Sharks mabao 2-0 katika mchuano wa ligi kuu uliopigwa Jumapili alasiri  katika uwanja wa Kasarani.

Elvis Rupia alipachika bao la kwanza dakika ya 11 huku wakiongoza kwa goli hilo kufikia mapumziko.

Kipindi cha pili pande zote zilicheza kwa tahadhari huku wageni Ingwe wakilazimika kumaliza mechi na wachezaji 10 uwnajani kufuatia kupigwa kadi nyekundu kwa Fabrice Mugheni  dakika ya 89.

Kadi hiyo nyekundu haikuwatamausha Leopards walioongeza mashambulizi na  Jefari Odeny akaongeza bao la pili kunako dakika ya 92  ukiwa ushinde wa pili kwa Sharks msimu huu.

Katika mikwangurano mingine  Kakamega Hombeboyz wakiwa nyumbani Bukhungu waliikung’uta Bidco United magoli 2-0 Ali Bhai na Moses Mudavadi wakipachika  mabao yote katika kipindi cha kwanza wakati KCB wakiiparuza Western Stima mabao 3-1 katika uga Moi kaunti ya Kisumu.

Kcb wangali kushikilia kukutu uongozi wa ligi hiyo kwa pointi 21 baada ya michuano 8 wakifuatwa na Tusker Fc kwa alama 20 huku Wazito Fc wakifunga orodha ya tatu bora kwa alama 17.

 

 

Categories
Michezo

Chui watoa kucha ligini na kudumisha rekodi ya 100%

Miamba wa soka nchini Kenya Afc Leopards waliendeleza msururu wa matokeo mazuri kwa kulilaza Bidco United mabao 2-0 katika mechi ya ligi kuu iliyosakatwa Jumapili Jioni katika uwanja wa Kasarani.

Leopards walihitaji mabao 2 ya mshambulizi Elvis Rupia kunako kipindi cha pili ili kuwatema Bidco waliopandishwa ngazi ligini msimu huu na kudumisha rekodi ya asilimia 100 baada ya michuano miwili kwani pia wakikuwa wameilaza Tusker Fc mabao 2-1 katika pambano la ufunguzi.

Sofapaka wakiwa Kilifi waliwateketeza Western Stima mabao 3-1 ,Ellie Asieche akicheka na nyavu mara mbili ,moja kila kipindi huku naye Kepha Aswani akafunga kazi kwa  Batoto Ba Mungu kwa goli la 3 huku lile la maliwazo kwa wageni Stima likifungwa na Samuel Odhiambo.

Huo ulikuwa ushindi wa kwanza kwa Sofapaka waliopoteza pambano la ufunguzi  bao 1-0 ugenini kwa Bandari Fc.

Kwenye  matokeo mengine wana Mvinyo Tusker watazidi kusubiri ushindi wa kwanza ligi, baada ya kukabwa koo na Bandari Fc kwa kutoka sare kapa huku Kakamega Homeboyz wakishindwa kutamba nyumbani na kutoka sare ya 1-1 dhidi ya Posta Rangers.

Leopards wanaongoza jedwali kwa pointi 6  sawia na KCB baada ya mechi mbili .

Categories
Michezo

Muyoti atwaa mikoba ya kuinoa Wazito FC

Nicholas Muyoti ameteuliwa kuwa kocha mpya wa kilabu cha  Wazito Fc kinachoshiriki ligi kuu ya soka humu nchini.

Hadi uteuzi wake Muyoti amekuwa kocha wa Kakamega Homeboyz alikosajili matokeo mazuri huku akiwa na imani kuendeleza matokeo  hayo katika timu ya  Wazito Fc.

Katika majukumu yake ya ukufunzi Muyoti atasaidiwa na aliyekuwa kocha wa Muhoroni Youth  Jeff Odongo huku kipa mstaafu Mathews Ottomax akiwa mkufunzi wa makipa  .

Baadhi    ya       wachezaji        wa         Wazito Fc

Muyoti anachukua jukumu la kuwanoa Wazito Fc kutoka kwa Fred Ambani ambaye alitimuliwa Jumatatu pamoja na wasaidizi wake wote akiwemo msaidizi wake Salim Babu na mkufunzi wa makipa Elias Otieno.

Timu hiyo ya Wazito ambayo zamani ilikuwa ya chuo kikuu cha Nairobi imekuwa na hulka ya kuwapiga kalamu makocha na wachezaji mara kwa mara na halieweki chanzo cha kufurushwa kwa  Ambani na wasaidizi wake.

Categories
Michezo

Gor Mahia walikuwa ‘Bize’ Sokoni huku dirisha la uhamisho wachezaji likifungwa

Mabingwa watetezi wa ligi kuu ya Kenya Gor Mahia ndio timu iliyokuwa bize sana katika dirisha la uhamisho wachezaji kwenye ligi kuu Kenya lililokamilika  Novemba 6 mwaka huu ,huku ikiwasajili wanandinga 17 wapya na kuwaachilia wengine 15 kuondoka kusaka lishe bora.

Western Stima pia iliwasajili wachezaji wengi wakiwa 16 na kuwaruhusu wengine 20 kugura wakati wanajeshi Ulinzi Stars wakiwam miongoni mwa timu ambazo zilisajili wachezaji wachache mno wakiwa wane.

Katika uhamisho AFC Leopards iliwasajili wachezaji  13 wapya pamoja na kocha Tomas Truch huku ikiwaachilia wachezaji wanane,Bandari Fc ikiwasajili wachezaji watano pekee wengi wao kutoka timu ya mwambao Coast Stima Fc nao wane wakaondoka .

Bidco United ilisajili wachezaji 11na kuwaruhusu 9 kuondoka nao Kakamega Homeboyz wakasajili wanandinga 9 huku 7 wakiondoka,kisha Sofapa ikanasa wachezaji 9 nao 12 wakagura.

Ifuatayo ni orodha kamili ya usajili wachezaji katika ligi kuu ya FKF .

https://footballkenya.org/fkf-pl-transfers-club-by-club-guide-to-all-confirmed-deals/

 

Msimu mpya wa ligi kuu unatazamiwa kuanza Novemba 20 mwaka huu na kukamilika Mei mwakani.