Super Unfair! Babu Tale azomewa na mwanawe.

Mheshimiwa Hamisi Shaban Tale Tale alijipata pale alipozomewa na mtoto wake wa kiume kwa kosa la kuondoka nyumbani usiku.

Mbunge huyo wa eneo bunge la Morogoro Kusini nchini Tanzania, ambaye pia ni meneja wa mwanamuziki Diamond Platnumz, alirekodi kisa hicho na kupachika video hiyo kwenye akaunti yake ya Instagram.

Mtoto wake wa kiume anasikika akimwambia kwamba sio vizuri kwake kuondoka nyumbani usiku na kuwaacha, na hapo inabidi Babu Tale ajieleze kwamba anakwenda kazini.

Anaendelea kumwambia kwamba ikiwa anataka aishi maisha mazuri, apate nafasi ya kwenda shule nzuri na mambo mengine mazuri lazima babake afanye kazi usiku na mchana.

Wanapoendelea kuzungumza, anaingia binti yake mdogo ambaye anamwambia babake kwamba wanastahili kwenda kulala kwani ni usiku kisha video inakatika.

Babu Tale alifiwa na mke wake kwa jina Shamsa mwisho wa mwezi Juni mwaka 2020 na alimwachia watoto watatu na kitinda mimba alikuwa hata hajafikisha umri wa miaka mitatu wakati huo.

Kulikuwa na tetesi kwamba meneja huyo wa Diamond alimtoa kafara mke wake ili ashinde kiti cha ubunge swala ambalo amelikanusha.

Mheshimiwa Tale amelazimika kujukumika katika malezi ya wanawe moja kwa moja na amesikika mara kwa mara akisema kwamba hataoa tena.

Hata hivyo anaonekana kufurahia kutangamana na wanawe kwa karibu huku akitimiza kazi ya ubunge na ile ya kumsimamia msanii Diamond Platnumz.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *