Stade Malien wahifadhi taji ya ligi kuu ya Mali

Kilabu ya Stade Malien ya Mali ndio mabingwa wa ligi kuu ya soka nchini Mali msimu wa mwaka 2019/2020 baada ya kuwabwaga Yeleen Olympique mabao 3-0  katika mechi ya kufunga msimu wikendi iliyopita.

Taji hiyo ilikuwa ya 19 ya ligi kuu kunyakuliwa na Malien na la tano mtawalia.

Stade Malien watashuka uwanjani leo jioni kwa mechi yao ya 4 na ya mwisho katika kundi la kuwani ubingwa huo dhidi ya Real Bamako ikiwa ni pambano tu la kufunga ratiba.

Kikosi cha kwanza cha Stade Malien

Stade Malien sasa wataiwakilisha Mali katika  mashindano ya kombe la ligi ya mabingwa Afrika huku Yeelen  na  Real  wakiwania nafasi ya  pili ili kushiriki kombe la shirikisho.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *