SOYA Awards kugharimu bajeti ya shilingi milioni 8 huku wanaspoti 250 wakialikwa

Tuzo za SOYA zitakazoandaliwa katika mkahawa wa Lake Naivasha Resort tarehe 20 mwezi huu  zitagharimu shilingi milioni 8 .

Kulingana na mshirikishi wa tuzo hizo zinazoadhimisha miaka 17 tangu kuasisiwa ,John Kaplich ,sherehe za mwaka huu zitawaleta pamoja wanamichezo 250  walioalikwa , kinyume na awali ikiwa tu hafla ya kutangamana na kujiburudisha na wala sio  kushindana.

“Hafla za SOYA mwaka huu ambao kwa kawaidi huandaliwa mwzi Januari zitandaaliwa katika hoteli ya Lake Naivasha Resort Februari 20 , kuwaburudisha wanaspoti,sio tuzo la kawaida lakini tutaangalia ukakamavu wa wanamichezo ,itakuwa kama holiday kwao ndio maana hatutakuwa na categories 18 ilivyokuwa awali”akasema Kaplich

Tuzo hiyo itaanza kwa mafunzo kwa wanamichezo waalikwa maarufu kama Symposium mapema Februari 20 itakayolenga michezo na jinisa,michezo na ulaji muku,Sports and media branding na sports fame and failure  kabla ya sherehe kuandaliwa usiku.

“Hii haitakua sherehe za kawaida ndio maana pia tutakuwa na symposium kuwafunza wanamichezo waalikwa kuhusu maswala mane makuu ya Sports fame and failure,sports and media branding,sports and gender na sports and Health ,kisha jioni tuwe na awards ambapo tutakuwa na vitengo 6 pekee vya kushindaniwa”akaongeza Kaplich

Mshikilizi wa rekodi tya dunia ambaye pia ndiye bingwa wa Olimpiki katika mbio za marathon Eliud Kipchoge na bingwa wa dunia katika mita 5000 Hellen Obiri  walitawazwa wanaspoti bora wa kiume na kike kwenye makala ya mwaka 2019 ,sherehe zilizoandaliwa Januari mwaka jana kaunti ya Mombasa.

Tuzo za SOYA zilianzishwa mwaka 2003 na rais wa sasa wa kamati ya Olimpiki Nock Paul Tergat kwa lengo la kuwatambua na kuwatuza wanaspoti wanaofanya vyema.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *