Simba wa Teranga kupimana nguvu na Morocco

Timu ya taifa ya Senegal itacheza mechi mbili za kujipiga msasa dhidi ya Morocco na Mauritania  kujiandaa kwa mechi ya kufuzu kwa fainali za kombe la Afcon mwaka ujao Nchini Cameroon.

Kulingana na shirikisho la kandanda nchini Senegal FSF ,Teranga Lions ijulikanavyo timu hiyo, itachuana na Atlas Lions ya Morocco Oktoba 9 mwaka huu mjini Rabat kabla ya kuwaalika  Mauratania Oktoba 13 mjini Thies.

Simba Teranga wanaongoza kundi I la mechi za kufuzu kwa dimba la Afcon mwaka ujao nchini Cameroon kwa pointi 6 baada ya kuwashinda Eswatini mabao 4-1 na Congo Brazaville mabao 2-0 katika mechi za ufunguzi.

 

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *