Categories
Michezo

Simba amrarua mwarabu na kuongoza kundi A ligi ya mabingwa

Simba Sports club wameweka hai matumaini ya kutinga robo fainali ya kombe la ligi ya mabingwa Afrika baada ya kuwachuna mabingwa watetzi Al Ahly bao 1-0 katika mkwangurano uliosakatwa Jumanne alasiri katika uwanja wa Benjamin Mkapa jijini Daresalaam Tanzania.

Bao la pekee na la ushindi kwa mnyama simba lilipachikwa kimiani na kiungo wa Msumbiji Luis Muquissone kunako dakika ya 39 na kudumu hadi kipenga cha mwisho.

Kichapo cha Al Ahly kilikuwa cha kwanza katika ligi ya mabingwa Afrika baada ya zaidi ya msimu mmoja .

Uwanja wa Mkapa ulifurika hadi pomoni wakati wa mechi hiyo baada ya tiketi zote za mechi kuuzwa .

Ushindi huo unaweweka Simba uongozini pa kundi A kwa alama 6 baada ya mechi 2 kufuatia ushindi wa goli 1-0 ugenini mjini Kinsasha dhidi ya As Vita katika pambano la ufunguzi .

Mnyama Simba ataanza matayarisho kwa ziara ya Khartoum mwishoni mwa juma hili dhidi ya El Merreikh ya Sudan huku wakihitaji angaa ushindi katika mechi mbili kati ya 4 zilisozalia ili kutinga kwota fainali kwa mara ya kwanza.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *