Sikutumia Diamond kupata umaarufu, nilimpenda kweli, Tanasha Donna

Mwanamziki Tanasha Donna Oketch amekana usemi kwamba aliingia kwenye uhusiano na Diamond mwanamziki maarufu wa Tanzania kwa ajili ya kupata umaarufu.

Donna anasema labda ingechukua muda mrefu kidogo kufika aliko kwa sasa bila Diamond lakini bado angefika tu maanake alikuwa na mpango wa maisha yake kama mwanamziki.

Mama huyo wa mtoto mmoja kwa jina Naseeb Junior anasema wakati wa uhusiano wake na Diamond alimpenda yeye tu na ni jambo ambalo anasema Diamond alilifahamu vyema kwani hata simu yake alikuwa akiidurusu kila mara.

Donna anaamini kwamba ikiwa hangempenda Diamond kikweli hangekuwa mwaminifu kwake na angefanya mengi kisiri na angeshikwa na woga wakati anachukua simu yake.

Binti huyo anakiri kwamba uhusiano wake na Diamond umesaidia pakubwa kuinua kazi yake kama mwanamziki. Amefafanua kwamba alikutana na Diamond akiwa tayari amerekodi nyimbo kadhaa na alikuwa amejua watu wengi kwenye ulimwengu wa sanaa ya mziki.

Tanasha anasema amesonga mbele ila ataendelea kumpenda Diamond kwa sababu ndiye baba ya mtoto wake. Hata baada ya kuachana Diamond na Tanasha walitoa wimbo kwa jina “Gere” kitu ambacho kilisisimua mashabiki wao wakidhani kwamba wamerudiana.

Uhusiano wa Diamond na Tanasha ulikuwa kama wa mwaka mmoja hivi na miezi mitano baadaye Diamond akatangaza kwamba ashapata mwanamke wa kuoa.

 

Mwaka huu pia kwenye harusi ya dadake Esma, Diamond aliuliza waliokuwepo wamuombee ili naye afunge ndoa kabla mwisho wa mwaka huu. Baada ya hapo kulitokea habari kwamba tayari mipango ya ndoa ya Diamond inaendelea na ataoa kutoka familia moja tajiri nchini Rwanda.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *